Sunday, December 9, 2012

MATOKEO YA MECHI ZA BARCLAYS DEC 9 2012


Kikundi Cha Akina Dada Wa Precious Group Chazinduliwa Rasmi

 Magreth  Chacha ambaye ni Mkurugenzi wa benki ya wanawake (TWB) akizindua rasmi kikundi cha Precious Groupkwenye ukumbi wa Isumba Lounge jijini Dar es salaam.
 Hapa ikabaki kuwa furaha kwa wote mara baada ya uzinduzi huo.

Magreth  Chacha ambaye ni Mkurugenzi wa benki ya wanawake (TWB) akifurahia jambo na  kikundi cha Precious Groupmara baada ya kukizindua rasmi usiku huu kwenye ukumbi wa Isumba Lounge.
 Magreth  Chacha ambaye ni Mkurugenzi wa benki ya wanawake (TWB) akiwapa nasaha wanakikundi wa Precious Group mara baada ya juzindua kikundi chao.

 Mwenyekiti wa Kikundi cha akina dada cha Precious Group 2012 Agnes Shayo hiza akimkabidhi zawadi ya saa ya ukutani Magreth  Chacha ambaye ni Mkurugenzi wa benki ya wanawake (TWB)aliyekuwa mgeni rasmi katika hafla ya uzinduzi wa kikundi hicho na chakula cha jioni iliyofanyika usiku huu kwenye ukumbi wa Isumba Lounge zamani Jolly Club jijini Dar es salaam, ambapo wageni mbalimbani na wanakikundi wa Precious walijumuika pamoja katika uzinduzi huo.
 Magreth  Chacha ambaye ni Mkurugenzi wa benki ya wanawake (TWB) akijadiliana jambo na Mweka hazina msaidizi wa kikundi hicho katika hafla hiyo, kulia ni Mwenyekiti wa Kikundi cha akina dada cha Precious Group 2012 Agnes Shayo

Happy Birthday Aminah Seif 1yrs

Zaidi Ya Nyumba 50 Zaezuliwa Na Kimbunga

   Paa la nyumba lililoezuliwa
 Nguzo za umeme zilizoanguka
 Mkuu wa Wilaya ya Iringa Letisia Warioba akikabidhi mifuko ya unga wa ugali, kama ni moja ya msaada kwa waathirika wa mvua hizo.
Meneja wa Tanesco moa wa Iringa Donart Makingi akipita kati ya nguzo zilizodondoshwa na mvua za upepo, katika eneo la Migori.

MVUA kubwa zilizoambatana na upepo mkali, zimevunja nyumba zaidi ya 50 na kuezua paa katika Kata ya Migoli na Nyang’olo, katika Tarafa ya Isimani Wilaya ya Iringa, na kusababisha hasara kubwa kwa wananchi.

Wakizungumzia tukio hilo, wananchi walisema mvua hiyo ilianza kunyesha majira ya saa kumi jioni, ambapo baadhi yao walikuwa katika mkutano wa mkuu wa mkoa, ambapo mvua hiyo pia ilisambaratisha mkutano huo.

Maneno Kalinga mkazi wa Nyang’olo alisema mvua hizo ziliambatana na upepo mkali na hivyo kuezua paa la nyumba yake yote, na kudondosha kuta mbili za nyumba yake, huku watoto waliokuwemo ndani ya nyumba wakipata madhara.

Kalinga alisema kijana wake aitwaye Fadhili kalinga aliyekuwa amelala nadani ya nyumba hiyo, aliangukiwa na ukuta na kuumizwa maeneo ya mgongo na kumsaidia kumuondoa katika kifusi na kumuwahisha katika Zahanati ya Nyang’olo.

“Baada ya kupiga kelele majira walikuja kumusaidia kijana wangu, na walipofanikiwa kumtoa katika kifusi, tulimpeleka Zahanati kwa ajili ya kupata matibabu, na hasara nyingine nilizozipata ni kubwa kwani vitu vyote vimelowa na kuharibika, “ Alisema Kalinga.

Estwina Ngobola mkazi wa Migori alisema mali zake ziliharibiwa ikiwemo mifuko ya Sukari kilo 25, unga wa ugali, unga wa ngano, godolo, huku vitanda na kochi vikivunjika baada ya kuangukiwa na tofali

Alisema “Niliingia chumbani ili nifunge dirisha upepo usiingie, kwani mvua ilikuwa na upepo, nikawa ninahofu mji yataingilia dirishani, lakini nilipotaka kufunga dirisha ulikuja upepo mkali nikaona nyumba inatikisika, nikakimbilia nje na baadaye paa lote likatolewa na kutupwa pale, kuta zikadondoka, kama unavyoona hivi,” Alisema Estwina.

Estwina alisema kutokana na hali hiyo ameomba majirani wamuhifadhie vitu vyake, huku yeye akiwa anaishi katika nyumba ya wageni, licha ya kutokuwa na fedha ya kulipa kwani hana ndugu katika mkoa wa Iringa, kwani yeye ni mwenyeji wa Mbeya.

Lucia Magidanga (98) mkazi wa Migori alisema hana mahala pa kuishi baada ya nyumba yake kuezuliwa, huku akiwa hana msaada wowote wa kufanya ukatrabati wa nyumba yake, kutokana na watoto wake wote kufariki.

Naye Mwajuma Nzalamalenga alisema hasara aliyoipata kutokana na janga hilo ni kubwa kwani mali zake zote zimeharibiwa vibaya, yakiwemo Magodoro, unga, Sukari, Maharage, na nyumba ya mma yake ikiwa imeezuliwa yote.
Mwajuama alisema hana mahala pa kuishi yeye na afamilia yake, na hata mvua ikianza tena kunyesha haelewi hali halisi itakuwaje.

Aidha mvua hizo pia zimeangusha nguzo 19 za Tanesco na hivyo eneo hilo kukosa nishati ya umeme, ambapo meneja wa Tanesco mkoa wa Iringa Injinia Donart Makingi alisema eneo hilo halina umeme kutokana na kuanguka kwa nguzo hizo.

Injinia Makingi alisema tayari wanapeleka nguzo za umeme ili kurejesha nishati hiyo na kuwa bado hajapata thamani halisi ya hasara itokanayo na janga hilo la mvua zilizoambatana na upepo mkali.

Hatua hiyo iliulazimu uongozi wa Mkoa kufika katika eneo la tukio kufanya tathimini ya uharibifu uliotokea, huku waathjirika wakipatiwa baadhi ya misaada ya chakula ili kuwasaidia wananchi hao.

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa Pudensiana Kisaka alisema wanafanya tathmini ili kutambua kiwango cha hasara kilichopatikana kwa lengo la kuwasaidia wananchi hao, huku akikabidhi Unga kilo 750 na Maharage kilo 300 kwa waathirika.

Kisaka aliwata wananchi hao kupanda miti kwa kiasi kikubwa msimu huu wa mvua ili kuepukana na upepo mkali unaosababisha madhara makubwa kama ya kuezuliwa nyumba zao na kupata hasara.

Mkuu wa Wilaya ya Iringa Letisia Warioba alisema mkoa kupitia mfuko wa maafa imeunda kamati ya muda ya kutathimini madhara hayo ili kuweza kuwafidia wananchi waliokumbwa na janga

 NA: OLIVER RICHARD - IRINGA

JK: Aongoza Maadhimisho Ya Miaka 51 Ya Tanzania Bara

 Mama Maria Nyerere akiwasili kwenye uwanja wa Uhuru kwa ajili ya kuhudhuria maadhimisho ya miaka 51 ya uhuru wa Tanzania.
 Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Mh. Joseph Kabila akipokewa  na Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Mh Said Meck Sadik mara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa Uhuru asubuhi                                       
 Rais wa Msumbiji Mh. Armando Guebuza akipokewa  na Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Mh Said Meck Sadik mara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa Taifa.                                    
 Mzee Ali Hassan Mwinyi akiwasili kwenye uwanja wa Uhuru kwa ajili ya kuhudhuria maadhimisho hayo.                                 
 Makamu wa Rais Dk. Gharib Bilal akisalimiana na Mama Fatma Karume mara baada ya kuwasili uwanjani hapo, katikati ni Waziri Mkuu Mh. Mizengo Pinda.     
 Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Mh. Mizengo Pinda akiwasili kwenye uwanja wa Uhuru kuhudhuria maadhimisho hayo huku akisindikizwa na Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Mh. Said Meck Sadik.

 Viongozi mbalimbali wakiwa katika maadhimisha hayo kutoka kulia ni Rais Joseph Kabila wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Mama Maria Nyerere, Rais wa Msumbiji Mh. Armando Guebuza,Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Dk. Gharib Bilal na Mzee Ali Hassan Mwinyi rais Mstaafu wa awamu ya pili

 Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania na Amiri Jeshi mkuu Dk.Jakaya Kikwete akiwasili katika gari maalum la Kijeshi na Mkuu wa majeshi Jenerali Davis Mwamunyange kwenye uwanja wa uhuru kwa ajili ya  maadhimisho ya miaka 51 Uhuru wa Tanzania Bara 2012 yanayofanyika kila mwaka Desemba 9, Kauli Mbiu ya Maadhimisho ya Mwaka huu ni “Uwajibikaji, Uadilifu na Uzalendo ni nguzo ya Maendeleo ya Taifa letu”
 Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya muungano ya Tanzania Dk. Jakaya Kikwete akikagua gwaride la vikosi vya Ulinzi na usalaama katika maadhimisho hayo.
 Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya muungano ya Tanzania Dk. Jakaya Kikwete akikagua gwaride la vikosi vya Ulinzi na usalaama katika maadhimisho hayo

 Rais Jakaya Kikwete akipokea gwaride la heshima wakati wa maadhimisho ya miaka 51 ya uhuru wa Tanzania Bara yanayofanyika kwenye uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam akiwa pamoja na viongozi mbalimbali kutoka nje na ndani ya nchi
 Kikosi cha Brass Band cha majeshi ya Ulinzi na usalama  kikitumbuiza katika maadhimisho hayo
Rais Dk. Jakaya Kikwete kulia akipokea Gwaride la Heshima lililpokuwa likipita mbele yake wanaofuatia katika picha ni Rais wa Zanzibar Dk. Mohamed Shein, Rais wa Namibia Mh. Ifikepunye Pohamba na Mke wa Rais Mama Salma Kikwete wakiwa katika maadhimisho hayo

 Vikosi vya Ulinzi na Usalama vikiwa vimejipanga tayari kwa gwaride  la utii na heshima mbele ya Amiri jeshi Mkuu na Rais Jamhuri ya muungano ya Tanzania Dk. Jakaya Kikwete.
 Vijana wa chipukizi wakionyesha michezo na ujumbe mbalimbali wakati wa maadhimisho hayo.Hapa wakionyesha ukakamavu wao huku wakiwa wameshika silaha.
 Kikosi cha wanaanga Jeshi la wananchi JWTZ kikitoa heshima kwa gwaride kali mbele ya Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jakmhuri ya Muungano ya Tanzania Dk. Jakaya Kikwete
  Kikosi cha ardhini Jeshi la wananchi la Tanzania JWTZ kipita kwa gwaride la heshima mbele ya Rais Dk. Jakaya Kikwete