Friday, December 7, 2012

Tanzania Kusimamia Wanajeshi Wa Pamoja DRC

Jumla ya nchi kumi katika eneo la Maziwa makuu zimekubaliana kuunda jeshi la pamoja litakalokuwa na jumla ya askari 4,000 katika kukabiliana na ghasia na vita vya mara kwa mara mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo.

Waziri wa Ulinzi wa DR Congo, Dakta Crispus Kiyonga amethibitisha uundwaji wa jeshi hilo, akisema litafanya kazi chini ya usimamizi wa Tanzania.

Mapigano ya hivi sasa mashariki mwa Congo yalizuka mwezi Aprili mwaka huu wakati waasi wa M23 walipoliasi jeshi la nchi hiyo na kusababisha watu laki tano kuyakimbia makaazi yao wakihofia usalama wao.
Wakati huohuo, viongozi wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini Mwa Afrika, SADC, wameanza mkutano wao wa dharura jijini Dar es salaam nchini Tanzania.

Wameanza kwa kufanya kikao cha Asasi ya Ulinzi, Siasa na Usalama ya SADC inayojulikana kama TROIKA chini ya Mwenyekiti wake Rais Jakaya Kikwete wa Tanzania.

Kwa mujibu wa Waziri wa Mambo ya nchi za Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wa Tanzania, Bernard Membe, kikao hicho cha TROIKA kimewakutanisha marais Jakaya Kikwete, Hifikepunye Phohamba wa Namibia na Jacob Zuma wa Afrika Kusini.
Amesema mara baada ya kikao hicho cha TROIKA viongozi hao watajumuika na Rais Yoweri Museveni wa Uganda ambaye pia ni mwenyekiti wa mkutano wa kimataifa wa nchi za Ukanda wa Maziwa Makuu, pamoja na Rais Armando Guebuza wa Msumbiji ambaye ni Mwenyekiti wa sasa SADC.

Viongozi hao kwa pamoja watajadiliana kwa kina matatizo ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Madagascar na Zimbabwe ambapo watawasilisha mapendekezo yao katika mkutano mkuu wa viongozi wote 14 wa SADC utakaofanyika kesho.

Chanzo:  http://www.bbc.co.uk/swahili

UDASA- TAARIFA KWA UMMA


UNIVERSITY OF DAR ES SALAAM Academic Staff Assembly

TAARIFA KWA UMMA

Hii ni kuitaarifu jumuiya ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na umma kwa ujumla kuwa, katika kusheherekea uhuru wa Tanzania Bara, Jumuiya ya Wanataaluma wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDASA) kwa ushirikiano na IPP Media wameandaa Kongamano la Uhuru litakalofanyika siku ya Jumapili tarehe 9 Desemba 2012 katika Ukumbi wa Nkrumah kuanzia saa 8 alasiri hadi saa 12 jioni.

Mada kuu ya Kongamano ni, “Uhuru wetu na Mustakabali wa Taifa kwa Miaka 50 Ijayo”. Kongamano hilo litajikita katika vipengele vifuatavyo:-

a) Amani na Utulivu wa Taifa letu kwa Miaka 50 Ijayo;

b) Elimu na Maendeleo ya Taifa kwa Miaka 50 Ijayo;

c) Rasilimali zetu kwa Maendeleo ya Kiuchumi ya Taifa.

 Kongamano hilo litarushwa moja kwa moja na ITV, Radio One na Capital Radio ili wananchi wote waweze kufuatilia kongamano hilo muhimu. Watakaongoza mjadala ni Prof. Gaudence Mpangala, Dkt Martha Qorro, Dkt Haji Semboja, Dkt. Kitila Mkumbo, Bw. Maggid Mjengwa na Mhandisi Joshwa Raya. Watakuwepo pia wazungumzaji waalikwa kama vile: Mzee Joseph Butiku, Dkt Aldin Mutembei, Mh. January Makamba (Mb), Julius Mtatiro, Usu Mallya na Esther Wassira. Kongamano linategemewa kufungwa na Mh. Bernard Membe (Mb), Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.

 Wote mnakaribishwa..

Limetolewa na Uongozi wa UDASA

Tanzania Kuadhimisha Miaka 51 Ya Uhuru

Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Saidi Meck Sadiki amewaomba wakazi wa jiji la Dar es salaam kujitokeza kwa wingi kuhudhuria sherehe za maadhimisho ya miaka 51 ya Uhuru wa Tanganyika zitakazofanyika katika Uwanja wa Uhuru jiji Dar es salaam.
azimishishwa mfumo wa aina yake na kuhudhuriwa na viongozi wengi wa ndani na nje ya nchi.

Akitoa ufafanuzi wa kukamilika kwa maandalizi ya sherehe hizo leo jijini Dar es salaam Bw. Saidi Meck Sadiki amesema kuwa maadhimisho ya mwaka huu yatahudhuriwa na viongozi mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi na mwaka huu mkoa wa Dar es salaam umepewa heshima ya kuandaa sherehe za kutimiza miaka 51 ya uhuru.
Amesema katika kipindi cha miaka 51 ya uhuru Tanzania imepata mafanikio makubwa katika nyanja mbalimbali za uchumi, ulinzi na usalama pamoja na uhusiano wa kimataifa.

Amefafanua kuwa mgeni rasmi katika maadhimisho hayo atakuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Jakaya Kikwete na kuongeza kuwa yataongozwa na kauli mbiu isemayo Uwajibikaji, Uadilifu na Uzalendo ni nguzo ya Maendeleo ya Taifa letu.

Aidha amefafanua kuwa sherehe za mwaka huu zitahudhuriwa na ugeni wa marais kutoka Jumuiya ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) na kupambwa na gwaride maalum lililoandaliwa na vikosi vya ulinzi na usalama vya Tanzania , halaiki maalum, vikundi mbalimbali vya burudani vya ngoma za asili vya hapa Tanzania hususani kutoka maeneo ya Ukerewe, Dodoma na Zanzibar.

Vikundi vingine vitakavyopamba sherehe hizo ni kundi la Taifa la sanaa kutoka nchini Rwanda (Rwanda National Ballet).

JK Aongoza Kikao Cha Kamati Ya Ulinzi Ya SADC Jijini Dar es Salaam

 Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya nchi za Jumuiya uchumi na maendeleo ya Kusini (SADC) Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimkaribisha ikulu Rais Jackob Zuma wa Afrika ya Kusini ili kushiriki kikao cha kamati hiyo.Pembeni ni Katibu Mkuu wa SADC Dr.Tomaz Salomao.
 Mwenyekiti wa Kamati ya ulinzi na Usalama ya SADC Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete(watatu kushoto) akiongoza kikao cha kamati hiyo kilichofanyika ikulu jijini Dar es Salaam leo.Wengine katika picha kutoka kushoto ni Rais Wa Namibia Hifikepunye Pohamba, Rais Jackob Zuma wa Afrika ya kusini(kulia) na wapili kushoto ni Katibu Mkuu wa SADC Dr.Tomaz Salomao
Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya SADC Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete( Wanne Kushoto) akiwa na viongozi SADC waliopo katika kamati hiyo.Wengine katika picha ni Rais Wa Afrika ya Kusini Jackob Zuma(Watatu kushoto), Rais Hifikepunye Pohamba wa Namibia(kulia),Rais Mstaafu wa Msumbiji ambaye pia ni msuluhishi wa SADC kwenye mgogoro wa Madagaska, Joachim Chissano(wapili kushoto) na kushoto ni Katibu mkuu wa SADC Dkt.Tomaz Salomao

(Picha na Freddy Maro).

Mnyika Mbunge Rasmi Ubungo

Mbunge wa Ubungo John Mnyika sasa ni mbunge rasmi wa Ubungo,baada ya Hawa Ng'umbi Kufuta rufani yake bila gharama.

Picha Ya Fullshangwe

CCM Iringa Wajitabiria Ugumu Uchaguzi Ujao

CHAMA Cha Mapinduzi mkoani Iringa, kimeshitshwa na taarifa ya Wakala wa Barabara (Tanroads) mkoani humo kuwa baadhi ya barabara zilizoahidiwa na Rais Jakaya Kikwete kuwa zingetengenezwa kwa kiwango cha lami kama angechaguliwa, hazijatengewa fedha katika bajeti ya mwaka 2012/13.

Katibu wa CCM mkoani humo Emanuel Mteming’ombe, alisema hatua hiyo inakihatarisha chama hicho wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 hasa ikizingatiwa kuwa Rais Kikwete atakakiwa kumnadi mgombea wa urais kupitia chama hicho.

“Hii ni hatari kama barabara hizo hazitatengenezwa na kukamilika, jambo hili litatusumbua kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 kwa sababu Rais atatakiwa kumnadi mgombea wetu na wananchi watauliza maswali hayo ya ahadi za barabara, ”alisema Mteming’ombe.

Hata hivyo Mteming’ombe alimpongeza Meneja wa Tanroads mkoani humo, Mhandisi Paul Lyakurwa kwa jitahadi za kuhakikisha kuwa barabara hizo zinatengenezwa.
Pia aliishauri Bodi ya Barabara ya Mkoa wa Iringa iliyoketi chini ya mwenyekiti wake Dk Chritine Ishengoma akuihimiza Serikali kutekeleza ahadi hizo.

Akitoa taarifa ya utekeleza wa ahadi za Rais Kikwete katika kikao hicho, Lyakurwa alisema barabara kadhaa ambazo ujenzi wake uliandaliwa mwaka wa fedha wa 2011/13 umesimama kutokana na kutotengewa fedha katika bajeti ya mwaka 2012/13.

Alizitaja barabara hizo kuwa ni ya Rujewa, Madibira Mafinga yenye urefu wa kilometa 151 ambayo alisema upembezi yakiniufu ulishakamilika na kinachosubilrwa ni kupata mkandarasi.Mhandis Lwakurwa alizitaja barabara nyingine kuwa ni ya Ipogolo- Kilolo.

Chanzo:  http://www.mwananchi.co.tz/habari

Wakili: Korti Ilikosea Kumvua Lema Ubunge

WAKILI wa Serikali Mkuu Timon amedai kuwa Mahakama Kuu Kanda ya Arusha ilikosea kutengua ubunge wa aliyekuwa Mbunge wa Arusha mjini, Godbless Lema, kwa madai ya kutumia lugha za matusi kwa kuwa Bunge limeruhusu wanasiasa kutukanana kwenye kampeni.

Wakili Vitalis alitoa madai hayo jana, wakati wa usikilizwaji wa rufaa ya Lema, aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema),katika Mahakama ya Rufani jijini  Dar es Salaam.

Wakati wakili huyo wa serikali akitoa madai hayo, Wakili wa wajibu rufaa, ambao walishinda katika kesi ya msingi, Alute Mughway, naye alidai kuwa Mahakama Kuu, Arusha ilikosea katika uamuzi wake, pamoja na mambo mengine, kwa kukataa baadhi ya madai yao.

Lema alivuliwa ubunge April 5, 2012, katika hukumu iliyotolewa na Jaji Gabriel Rwakibalia, kufuatia kesi iliuyofunguliwa makada watatu wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Mussa Mkanga, Happy Kivuyo na Agnes Mollel, wakipinga ushindi wake katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2010.

Lema kupitia kwa Wakili wake Method Kimomogoro alikata rufaa Mahakama ya Rufani, lakini Novemba 8, 2012 mahakama ilitupilia mbali rufaa hiyo baada ya kuini kuwepo kwa dosari za kisheria, kutokana na pingamizi lililowekwa na upande  wa wajibu rufaa.

Hata hivyo mahakama hiyo ilimpa nafasi nyingine ya  kukata rufaa tena baada ya kumpa siku 14 kufanya marekebisho ya dosari hizo za kisheria na kuiwasilisha mahakamani ndani ya muda huo, amri ambayo aliitekeleaza.

Wakati Lema akikata rufaa kupinga hukumu ya Mahakama Kuu kumvua ubunge, wajibu rufaa nao walikata rufaa (Cross Appeal) kupinga uamuzi wa mahakama hiyo, huku wakibainisha hoja nne.

Katika hoja ya kwanza hadi ya tatu walidai kuwa Jaji alikosea katika hukumu yake kwa kuchanganya vituo vilivyotolewa ushahidi na mashahidi wanne na hatimaye akakataa ushahidi wapo, pamoja na tarehe za ratiba ya kampeni ya CCM nay a Chadema.

Hoja ya nne walidai kuwa Jaji alikosea kwa kuamua kuwa hata kama Lema kwenye kampeni zake alidai kuwa Dk. Buriani ni mkazi wa Zanzibar hatafaa, wakidai kuwa ukazi si sifa ya kuchaguliwa kuwa mbunge.

Hatimaye rufaa hizo zilisikilizwa jana na jopo la   Majaji watatu wa Mahakama ya Rufani, lililoundwa na Jaji Salum Massati, Jaji Bernard Luanda, chini ya uongozi wa  Jaji Nathalia Kimaro.

Wakati wa usikilizwaji wa rufaa hiyo, mawakili wawili ambao ni ndugu, Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lisu na kaka yake Mghway, walipambana vikali kwa hoja za kisheria.

Lisu, Kada wa Chadema ambaye pia ni Mnadhimu wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, alikuwa akimtetea Lema mrufani (Lema), akisaidiana na Wakili  Method Kimomogolo, huku Mughway akiwatetea wajibu rufani ambao ni makada wa CCM.

Familia Ya Sharo Yaibua Mazito

FAMILIA ya msanii Hussein Ramadhani Mkiety (Sharo Milionea) aliyekufa katika ajali wilayani Muheza wiki
iliyopita imedai kuwa haiamini kwamba kifo cha mtoto huyo kilitokana na ajali, hivyo kulitaka Jeshi la Polisi kufanya uchunguzi wa kina kubaini ukweli.

Mjomba wa marehemu , Mohamed Msenga alisema jana kwamba familia imekuwa na shaka juu ya mazingira ya kifo hicho baada ya kurejeshewa nguo za msanii huyo zilizokuwa zimeibwa baada ya ajali lakini hazikuwa na damu.

Msenga alisema muda mfupi baada ya mama mzazi wa Marehemu Zaina Mwaimu Mkiety (54), kuitwa polisi na kukabidhiwa  vitu mbalimbali zikiwamo nguo ambazo marehemu alikuwa amevaa siku ya ajali hawakuona hata alama ya damu jambo ambalo liliwashangaza.
Alisema shaka hiyo ilianzia katika eneo ambalo ajali hiyo ilitokea akisema walipofika na kuonyeshwa mahala alipokuwa ameangukia, hawakuona damu jambo ambalo liliwatia shaka.
Alisema begi la nguo za msanii huyo lilikuwa na udongo mwingi likionyesha kwamba walioiba walikuwa wamelifukia kabla ya kusalimisha lakini hakuna damu zilizoonekana.

Kaimu Mganga Mkuu wa Hospitali ya Teule Muheza, Dk Julius Mjema aliyeufanyia uchunguzi mwili wa Sharo Milionea alisema sababu ya kifo chake ni kichwa kupondeka.
“Mimi ndiye niliyefanyia ‘postmoterm’ (uchunguzi), mwili wa Sharo Milionea, ni kwamba kichwa kilikuwa kimepondeka huku mifupa ya kichwa ikiwa imepondeka pia,” alisema Dk Mjema.

Kuhusu madai ya nguo kutokuwa na damu, alisema marehemu alipata mpasuko wa ndani kwa ndani na siyo wa  nje, ndiyo maana alipofikishwa chumba cha maiti damu zilionekana zikiwa zimeganda masikioni.

Hata hivyo, Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Tanga, Constantine Massawe alipoulizwa kuhusu madai hayo ya familia  alisema: “Hiyo ni taarifa ambayo jeshi la polisi litaifanyia kazi kwa kuingia kwa kina katika kuchunguza ili kuridhisha pande zote.”


Mama yake alia kukosa mjukuu
Katika hatua nyingine, mama mzazi wa msanii huyo amesema kutoachiwa mjukuu na tarehe za mwisho wa mwezi ni alama ambazo zitasababisha awe akimkumbuka mwanaye huyo milele.
Akizungumza nyumbani kwake, katika Kitongoji cha Jibandeni Kijiji cha Lusanga wilayani hapa alisema kila ulipokuwa ukifikia mwisho wa mwezi ulikuwa ni muda wake wa neema kwani Sharo Milionea alimtumia fedha za matumizi yake binafsi pamoja na familia nzima nyumbani hapo.


“Pamoja na kwamba kila mara alikuwa akinitumia fedha za kutatua shida zangu mbalimbali nilizokuwa nikimweleza lakini kila mwisho wa mwezi alikuwa akihakikisha anatuma fungu la matumizi yangu na ndugu zake hapa nyumbani,” alisema mama huyo.
Alisema mwisho wa mwezi itakuwa ni alama ya kudumu ya kumbukumbu ya mwanawe kwa sababu ni wakati ambao alikuwa akimtumia fedha za matumizi yake pamoja na
familia nzima.

Kuhusu mjukuu alisema: “Sharo ni mwanangu wa pekee wa kiume, amekufa bila kuniachia mjukuu.. hii inaniuma sana lakini namshukuru Mungu kwani amechukua kiumbe chake na ndiye ajuaye siri iliyofichika mbele yangu,” alisema.

Alisema hadi alipofariki hakuwahi kumdokeza juu ya kuwa na mtoto wala kumpa mimba msichana yeyote... “Unajua Sharo Milionea alizaliwa pacha na mwenzake Hassan lakini mwenzake alifariki dunia siku tano baada ya kuzaliwa kwa hiyo katika kizazi changu mwanangu pekee wa kiume alikuwa Sharo Milionea ambaye nilitumaini kwamba angeniletea wajukuu,” alisema Zaina.

Na: Burhani Yakub, Muheza

BABA ANAETUHUMIWA KUZINI NA KUZAA NA MWANAE WA KUMZAA ATINGA MAHAKAMANI BAADA YA KESI KUAIRISHWA AZOMEWA NA KINA MAMA NA KUKIMBIA KAMERA ZA WANDISHI WA HABARI

Mkazi wa Mtaa wa Mbete,Kata ya Isanga Jijini Mbeya Bwana Yussuf Hamad(39),anatuhumiwa kumpa mimba binti yake wa kumzaa(16) jina lake limehifadhiwa. akiingia mahakamani leo mbele yake ni mke wake na mtoto wake aliyezaanae ambao sura zao tumefunika


Bwana Yussuf Hamad anaetuhumiwa kuzaa na bintie akitaka kumpokonya kamera  mwandishi wa gazeti la majira Rashid Mkwinda ili asimpige picha
Jamaa kuona amezidiwa akaamua kujifunika na shati lake huku akitoa maneno makali kuwa nyie waandishi mmekosa cha kuandika mmeona hii ndiyo habari hakuna habari nyingine? alihoji mtuhumiwa huyo
                                                  Huyoooo anatoka nje ya mahakama

                     Sasa anavaa kofia yake ili watu wasimtambue huku akisema nifuateni niwaonyeshe kazi
                                                        Njooni sasa huku kashika jiwe

Akina mama wanamsindikiza kwa kumzomea mtuhumiwa huyo


 Mkazi wa Mtaa wa Mbete,Kata ya Isanga Jijini Mbeya Bwana Yussuf Hamad(39),anatuhumiwa kumpa mimba binti yake wa kumzaa(15) jina lake limehifadhiwa.

Hayo yamethibitishwa na Mama mzazi wa binti huyo Bi, Regina Simon(35) baada ya kupata taarifa Mei 11 mwaka huu kuwa binti yake ana ujauzito wa miezi minne,na kuamua kutoa taarifa kwa Balozi  wa mtaa huo Bwana Steven Ovaova ambaye naye alitoa taarifa kwa Mwenyekiti wa Kitongoji Bwana Angelo Sanga.

Viongozi hao wa mtaa walimuita  mtuhumiwa na ili kupata ukweli wa tukio hilo,lakini mtuhumiwa alikanusha ingawa binti yake alithibitisha kutendewa ukatili huo na kwamba alikuwa akitishiwa kwa mapanga kila alipokuwa akifanya naye tendo la ndoa.

Baada ya uongozi kupata maelezo kutoka kwa binti huyo na mzazi kukataa waliamua kuipeleka kesi hiyo Polisi,ambapo walitoa PF3 iliyomwezesha binti huyo kupelekwa kwa
daktari ambaye alithibitisha kuwa binti huyo ana ujauzito.

 Binti huyo amejifungua mtoto wa kike ambae sasa anamiezi mitatu mtoto huyo kaletwa leo mahakamani kama ushahidi kesi hiyo imeairishwa mapaka tarehe 12/12 mwaka huu,

http://mbeyayetu.blogspot.com/

Magazeti ya leo Ijumaa ya 7th December 2012