Thursday, March 14, 2013

POLISI WAMEMKAMATA KIONGOZI WA CHADEMA, LWAKATARE NA KUMPELEKA MAKAO MAKUU KWA MAHOJIANO

Wilfred Lwakatare ameitwa Makao Makuu ya Polisi sasa hivi kwa mahojiano na jeshi hilo kufuatia video clip iliyowekwa mitandaoni ikionesha  jinsi  alivyokuwa  akipanga  mbinu  za  utekaji....

WILLIFRED LWAKATARE  NI MKURUGENZI WA ULINZI NA USALAMA WA CHADEMA...

Kwa taarifa ni kuwa atawakilishwa na wakili Nyaronyo Kicheere na baadaye kama watafungua kesi watakuwa na Mabere Marando.
Je, hii sio double standard ndani ya taifa?
Mbona Mwigulu hajakamatwa baada ya kusema ana mkanda wa njama za kufanya mauaji?

MAELEZO YOTE NI KWA HISANI YA JAMII FORUM

HATIMAYE PAPA MPYA APATIKANA HUKO VATICAN

  Jorge Mario Bergoglio(Pope Francis) akipewa salamu na Papa aliyejiuzuru Benedict 16

Kadinali Bergoglio anakuwa mtu wa kwanza kutoka Amerika kusini kuchaguliwa kuwa Papa. Mara tu baada ya kuchaguliwa alichagua jina la Papa Francis I. Awali moshi mweupe ulishuhudiwa ukifuka kutoka bomba la kutolea moshi katika kanisa la Sistine Chapel na kufuatiwa na kengele kupigwa.

 Hii ilikuwa ni ishara kwa walimwengu kuwa makadinali ambao walianza mchakato wa kumchagua Papa mpya hatimae walikuwa wamefaulu katika kazi yao. Kadinali Bergoglio anachukuwa mahali pa Papa Benedict XVI, ambaye alijiuzulu mwezi uliopita akisema hana nguvu na uwezo wa kuendelea kuliongoza Kanisa Katoliki. Makadinali 115 wamekuwa faraghani tangu siku ya Jumanne alasiri na wakaanza mchakato wao kwa kupiga kura mara nne kwa siku.

Ilikuwa inahitajika kuwa angalau Makadinali 77 yaani theluthi-mbili wangeliweza kumpigia kura mmoja wao ili aweze kutangazwa kuwa Papa mpya. Na kabla ya mchakato huo kuanza kulikuwa hakuna dalili za kuonyesha nani angelichaguliwa.

Maelfu ya watu kutoka sehemu mbali mbali duniani walikuwa wamekusanyika katika ukumbi wa Kanisa la St Peter tangu siku ya Jumanne. Muda mfupi kabla ya Kadinali Bergoglio kujitokeza , maelfu ya watu walionekana wakikimbia kuelekea ukumbi wa St Peters ili kuweza kumshuhudia Papa mpya akitangazwa

Magazeti ya Leo Alhamisi ya 14th March 2013