Friday, January 4, 2013

INASIKITISHA BALI TUNASEMA WAPUMZIKE KWA AMANI.

         
 AJUAYE uchungu wa mtoto ni mzazi! Ukiwatazama akina mama watatu wa wasanii wa Tanzania waliofariki dunia kwa nyakati na sababu tofauti hivi karibuni wakilia kwa uchungu, unaweza ukadhani wazazi hao ni ndugu kwa namna nyuso zao zinavyoonekana kuwa na majonzi mazito,

Risasi Jumamosi linakuchambulia.

Makabrasha ya gazeti hili yanawaonesha mama wa marehemu Steven Kanumba, Flora Mtegoa, mama wa marehemu Hussein Mkiety ‘Sharo Milionea’, Zaina Mkiety na mama wa marehemu Juma Kilowoko ‘Sajuki’, Zaituni Mzena wakilia kwa uchungu.
Wazazi hao walionekana wenye majonzi kupita maelezo kwani kila mmoja alimbeba mwanaye tumboni kwa miezi tisa, akamlea, akamtunza kwa tabu hadi akakua lakini baada ya kuanza kufaidi matunda yao tu, Mungu akawachukua.

SHELUKINDO : Namuunga mkono lowassa 2015

MBUNGE wa Kilindi (CCM), Beatrice Shelukindo ametangaza kuchukua kile alichokiita uamuzi mgumu ili kuhakikisha kuwa Mbunge wa Monduli (CCM), Edward Lowassa anamrithi Rais Jakaya Kikwete katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015.Shelukindo alitoa kauli hiyo Jumapili wakati akiwasalimia wakazi wa Monduli baada ya kukaribishwa kuchangia ujenzi wa Hosteli ya KKKT katika sherehe za kukaribisha Mwaka Mpya zilizofanyika nyumbani kwa Lowassa ambazo pia zilihudhuriwa na makada kadhaa wa CCM.

Jana alipoulizwa kuhusu kauli hiyo, Shelukindo alisema: “Ni kweli mimi ni muumini wa Lowassa, ila pale (mkutanoni) sikumtaja kwa sababu najua chama kina taratibu zake na muda wa mchakato wa kumpata Rais haujafika.”

SERENGETI FREIGHT YATOA PONGEZI KWA BODI YA UTALII TANZANIA


BAADHI YA PICHA ZA MKUTANO WA CHADEMA IRINGA


TEKELEZENI AHADI MLIZOZITOA WAKATI WA KUOMBA KURA-OLE NANGOLE

 MWENYEKITI wa Chama cha Mapinduzi mkoa wa Arusha(CCM)Bw Onesmo Ole Nangole amewataka Viongozi mbalimbali wa chama hasa wale ambao walitoa ahadi  kwa wananchi kwenye uombaji wa kura kuhakikisha kuwa wanatekeleza ahadi hizo kwa haraka sana kwani wale ambao hawatekelezi ahadi wanachangia sana chama hicho kuelekezewa lawama

 Bw. Nangole aliyasema hayo Juzi wakati akifungua Kata mpya ya Chama hicho ambayo kwa sasa inajulikana kama Kata ya Majengo iliopo Meru Mkoani Arusha.

 Aidha Bw Nangole alisema kuwa tabia ya baadhi ya Viongozi ya kuwa watoa ahadi hasa nyakati za kura na kisha wakishapata kura wanasahau ahadi zao inachangia sana kuunguza Ccm kwenye jamii na kuonekana kuwa ni watoaji ahadi zisizotekelezwa.

 Alisema kuwa Viongozi wote ambao walitoa ahadi mbalimbali kwa wananchi hasa katika Nyakati za Kura wanatakiwa kuhakikisha kuwa watekeleza ahadi zao na kujijengea tabia ya kuwaangalia wapiga kura wao ili kuendelea kulinda uhai wa Chama

 Mbali na hayo aliongeza kuwa Viongozi mbalimbali wa Chama hicho wanatakiwa kuangalia zaidi ilani ya chama hicho kwa kuhakikisha kuwa wanaainisha matatizo ambayo yapo kwenye jamii na kisha kuyatatua kuanzia kwenye Ngazi za Vitongoji na Vijiji.

 Katika hatua nyingine Katibu wa Chama hicho Wilaya ya Meru Bw Langaeli Akyoo alisema kuwa bado Wilaya hiyo inakabiliwa na changamoto mbalimbali ambazo zinatakiwa zitatuliwe kwa haraka sana ingawaje umoja na ushirikiano unaitajika kwa haraka sana

TANAPA WAONGEZA MUDA WA KUWASILISHA KAZI ZA KUSHINDANIWA



Kutokana na changamoto mbalimbali zilizojitokeza na kuibuliwa na wadau wa habari nchini kuhusiana na siku ya mwisho ya kuwasilisha kazi za kushindaniwa, Waandaaji wa TANAPA Media Awards 2012 wamesogeza mbele tarehe ya mwisho ya kuwasilisha kazi hizo kutoka 31.12.2012 na kuwa tarehe ya mwisho sasa itakuwa 31.01.2013.

WASHIRIKI:

Tuzo hizi ziko wazi kwa wanahabari wote nchini kutoka katika Magazeti, Redio na Runinga. Ili uweze kutimiza sifa za ushiriki wako katika tuzo za TANAPA Media Awards 2012, unatakiwa kuwasilisha kazi zote zilizochapwa na kutangazwa katika kipindi cha kuanzia tarehe 01 Januari, 2012 hadi 31 Disemba, 2012.

JINSI YA KUSHIRIKI

Wanahabari wanaweza kushiriki kwa kutuma kazi zao kwa kiwango cha juu cha kazi tatu kwa kila kundi. Wanahabari watakaoshiriki tuzo hizi watapaswa kujaza fomu maalum za ushiriki zinazopatikana katika tovuti ya shirika www.tanzaniaparks.com

MAKUNDI

A     Tuzo ya Utalii wa Ndani katika Hifadhi za Taifa     Redio                 (washindani watatu)
Runinga             (washindani watatu)
Magazeti            (washindani watatu)
B     Tuzo ya Uhifadhi katika Hifadhi za Taifa     Redio                 (washindani watatu)
Runinga             (washindani watatu)
Magazeti            (washindani watatu)

Kazi zinaweza kuwasilishwa katika lugha ya kiingereza au Kiswahili. Tuzo: Washindi kwa kila kundi watapata tuzo zifuatazo:

Mshindi wa Kwanza    

Fedha taslimu Sh. 1,500,000, Ngao, Cheti na Safari ya mafunzo katika moja ya nchi za SADC
Mshindi wa Pili    

Fedha taslimu Sh.1,000,000, Ngao na Cheti
Mshindi wa Tatu    

Fedha taslimu Sh.500,000 na Cheti

Mwisho wa kuwasilisha

Kazi zote zinatakiwa kuwa zimewasilishwa Makao Makuu ya TANAPA hadi kufikia tarehe 31.01.2013.

Anuani ya kuwasilisha kazi:

Mkurugenzi Mkuu

Hifadhi za Taifa Tanzania

AIONE: Meneja Uhusiano- TANAPA Media Awards 2012

SL.P. 3134

Arusha, Tanzania

Au, ziletwe kwa mkono Makao Makuu ya TANAPA, Barabara ya Dodoma, Chumba Namba.32.

Au barua pepe:        prm@tanzaniaparks.comImetolewa na

Pascal Shelutete

MENEJA UHUSIANO

HIFADHI ZA TAIFA TANZANIA

04.01.2013

RAIS KIKWETE AONANA NA MSHAURI WA KIJESHI WA UMOJA WA MATAIFA IKULU DAR ES SALAAM LEO

 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa  na Mshauri Mkuu wa Kijeshi wa Umoja wa Mataifa Luteni Generali Babacar Gaye baada ya kuonana naye Ikulu jijini Dar es salaam leo Januari 4, 2013.Kushoto ni  Mkuu wa Majeshi Tanzania Jenerali Davis Mwamunyange.
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipeana mikono na Mshauri Mkuu wa Kijeshi wa Umoja wa Mataifa Luteni Generali Babacar Gaye baada ya kuonana naye Ikulu jijini Dar es salaam leo Januari 4, 2013.Kushoto Mbele ni Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe Mahadhi Mahadhi Juma Maalim, akifuatiwa na Mkuu wa Majeshi Tanzania  Jenerali Davis Mwamunyange, na wa pili kulia ni Balozi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa Balozi Tuvako Manongi na wengine ni maafisa waandamizi katika JWTZ na Umoja wa mataifa.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete katika picha ya pamoja  na Mshauri Mkuu wa Kijeshi wa Umoja wa Mataifa Luteni Generali Babacar Gaye baada ya kuonana naye Ikulu jijini Dar es salaam leo Januari 4, 2013.Kushoto Mbele ni Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe Mahadhi Juma Maalim, akifuatiwa na Mkuu wa Majeshi Tanzania Jenerali Davis Mwamunyange, na wa pili kulia ni Balozi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa Balozi Tuvako Manongi na wengine ni maafisa waandamizi katika JWTZ na Umoja wa mataifa.


(PICHA NA IKULU)

Rais Kikwete na Mama Salma Kikwete waenda kutoa pole nyumbani kwao Sajuki

 Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiweka saini kitabu cha maombolezo nyumbani kwa msanii wa filamu Marehemu Juma Kilowoko ‘Sajuki’ nyumbani kwao wafiwa Tabata Bima jijjini Dar es salaam leo Januari 4, 2013.
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiweka saini kitabu cha maombolezo nyumbani kwa msanii wa filamu Marehemu Juma Kilowoko ‘Sajuki’ nyumbani kwao wafiwa Tabata Bima jijjini Dar es salaam leo Januari 4, 2013.
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mkewe Mama Salma Kikwete wakiwa nyumbani kwa msanii wa filamu Marehemu Juma Kilowoko ‘Sajuki’ Tabata Bima jijjini Dar es salaam leo ambako walienda kutoa pole leo Januari 4, 2013.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiweka saini kitabu cha maombolezo nyumbani kwa msanii wa filamu Marehemu Juma Kilowoko ‘Sajuki’ nyumbani kwao wafiwa Tabata Bima jijjini Dar es salaam leo Januari 4, 2013.
(PICHA NA IKULU)

RAIS KIKWETE AONGOZA MAMIA KUMZIKA JUMA KILOWOKO 'SAJUKI' JIJINI DAR LEO

 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiweka udongo katika kaburi la marehemu Sadick Juma Kilowoko 'Sajuki' leo.
                  Baba mzazi wa Sajuki, Mzee Kilowoko, akiweka udongo katika kaburi la mwanaye
                                                                   Mazishi ya Sajuki yakiendelea.


                                                   Umati wa watu waliohudhuria mazishi hayo.

MAMIA ya wakazi wa jiji la Dar es Salaam leo wamejitokeza katika makaburi ya Kisutu jijini Dar es Salaam kumpumzisha mpendwa wao Sadick Juma Kilowoko 'Sajuki' aliyefariki dunia alfajiri ya Januari 2, mwaka huu (Jumatano) katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili. Miongoni mwa waliomzika Sajuki ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Jakaya Mrisho Kikwete

HAPA NDIPO ALIPOZIKWA MAREHEMU SAJUKI.


















MAJONZI, VILIO VYATAWALA WAKATI MWILI WA SAJUKI UKIOMBEWA NYUMBANI KWAKE TABATA JIJINI DAR

                                   Mwili wa Sajuki ukipelekwa uwanjani kwa ajili ya kuswaliwa na masheikh.

  Mwili wa Juma Kilowoko 'Sajuki' ukiswaliwa nyumbani kwake Tabata-Bima jijini Dar es Salaam leo kabla ya kwenda kuzikwa.
                                                              Vilio vikitawala msibani hapo.







                    Mama mzazi wa Sajuki akilia kwa uchungu wakati mwili wa mwanaye ukiswaliwa.





(PICHA: GLADNESS MALLYA NA HAMIDA HASSAN / GPL)

NYUMBANI KWA SAJUKI MAHANGA, IDDI AZZAN NA RIDHIWANI KIKWETE WAHANI MSIBA WA SAJUKI JIJINI DAR


Mkurugenzi wa Utamaduni na Maendeleo wa Wizara ya Habari Bw. Herman Mwasoka akitia saini kitabu cha maombolezo nyumbani kwa marehemu Sajuki jijini Dar leo
 Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu nchini Bi. Joyce Fisso akitia saini kitabu cha maombolezo ya Msiba wa Sajuki.
 Mkurugenzi wa Maendeleo na Utamaduni wa Wizara ya Habari Bw. Herman Mwasoka (mwenye suti nyeusi) akimfariji Baba mzazi wa Marehemu Sajuki Mzee Juma Kilowoko alipofika nyumbani kwa marehemu kuhani msiba huo Tabata Bima jijini Dar
 Mchekeshaji maarufu wa The comedy Masanja Mkandamizi akijifuta jasho kwa mbali akielekea msibani nyumbani kwa Marehemu Sajuki. Masanja alikuwa ni mmoja wa wahamishaji katika kuchangia pesa za matibabu ya marehemu Sajuki kwenda nchini India kupitia kipindi cha Luninga cha The Comedy kinachorushwa na Televisheni ya TBC.
 Mzee King Kiki akizungumza jambo na Waheshimiwa Wabunge kwenye msiba wa Sajuki Tabata Bima jijini Dar es Salaam leo.
 Wasanii mbalimbali na wakiendelea kuwasili nyumbani kwa Marehemu Sajuki Tabata Bima jijini Dar es Salaam. Pichani ni Msanii wa muziki Dokii (kushoto) sambamba na Mshiriki wa Shindano la Big Brother Africa Mwisho Mwampamba na wasanii wengine.
 Msanii mkongwe katika tasnia ya muziki wa Dansi na Rhumba Kikumba Mwanza Mpango almaarufu kama King Kiki akitia saini kitabu cha maombolezo nyumbani kwa Marehemu Sajuki Tabata Bima jijini Dar leo.
                           Baadhi ya waombolezaji wakiwa kwenye huzuni kutafakari kifo cha Sajuki.
 VIONGOZI WA SERIKALI WAKIWASILI: Mbunge wa jimbo la Segerea, Dar es Salaam, ambaye pia ni Naibu Waziri wa Kazi na Ajira, Dk. Makongoro Mahanga (wa tatu kushoto) akiwa ameambatana na Mbunge wa jimbo la Kinondoni Mh.Iddi Azzan wakipokelewa na Rais wa Shirikisho la Filamu nchini (TAFF) Bw. Simon Mwakifamba na wasanii wengine wa filamu baada ya kuwasili nyumbani kwa Marehemu Sajuki kwa ajili ya kuhani msiba huo.
 Mkuu wa Itifaki Bw. Simon Simalenga wa Clouds Media akimuongoza Mh.Makongoro Mahanga sehemu maalum kwa ajili ya kutia saini kitabu cha maombolezo.
                 Mbunge wa Kinondoni Mh. Iddi Azzan naye aliangusha saini kwenye kitabu hicho.
 Mbunge wa jimbo la Segerea, Dar es Salaam, ambaye pia ni Naibu Waziri wa Kazi na Ajira, Dk. Makongoro Mahanga akitia saini katika kitabu cha maombolezo nyumbani kwa marehemu Sajuki.
 Mzee King Kiki akizungumza jambo na Waheshimiwa Wabunge kwenye msiba wa Sajuki Tabata Bima jijini Dar es Salaam leo.
 Waheshimiwa wakielekea nyumba ya jirani walikokusanyika baadhi ya waombolezaji na wasanii wa filamu nchini kwa ajili ya kuzungumza machache na kutoa Ubani.
 Katibu wa Fedha msibani hapo mchekeshaji maarufu Steve Nyerere akiwakaribisha waheshimiwa wabunge kuzungumza na hadhira ya waombolezaji (hawapo pichani).
 Pichani Juu na Chini ni Umati wa waombolezaji ukisikiliza nasaha za waheshimiwa Wabunge (hawapo pichani) walipofika nyumbani kwa marehemu Sajuki kuhani msiba huo.


 Kazi ya kuosha vyombo si kina Dada tu, hata kina Kaka wanaweza pia....Pichani ni baadhi ya Watangazaji wa Clouds Radio wakiongozwa na Dina Marios kushiriki kuosha vyombo vilivyotumika katika msiba huo huku wakisaidiana na waombolezaji wengine.
 Mbunge wa jimbo la Kinondoni Mh. Iddi Azzani akielezea kwa majonzi alivyopokea taarifa za msiba wa Sajuki na kuahidi kushirikiana bega kwa bega na Wastara panapomajaliwa ya Mola katika malezi ya mtoto aliyeachwa na marehemu na kuwaasa wadau, ndugu, jamaa na marafiki kumsaidia Wastara kutokana na hali yake na amechangia kiasi cha Shilingi 500,ooo/= kufanikisha shughuli za mazishi ya marehemu Sajuki.
 Mkuu wa Itifaki msibani hapo Bw. Simon Simalenga wa Clouds Media akimpokea Mwenyekiti wa kamati ya Kusaidia timu ya Taifa ya Vijana Serengeti Boys Bw. Ridhiwani Kikwete alipowasili nyumbani kwa marehemu Sajuki kwa ajili ya kuhani maeneo ya Tabata Bima jijini Dar es Salaam.
 Mganga wa Jadi anayefahamika kwa jina la Dokta Manyaunyau (kushoto) sambamba na Msanii wa filamu nchini Cloud wakisikiliza mawaidha ya waheshimiwa wabunge (hawapo pichani).
 Mwenyekiti wa kamati ya Kusaidia timu ya Taifa ya Vijana Serengeti Boys Bw. Ridhiwani Kikwete akitoa pole baada ya kusaili kwa baadhi ya ndugu wa karibu wa marehemu Sajuki msibani hapo.
 Bw. Ridhiwani Kikwete akisalimiana na Baba mzazi wa marehemu Sajuki Mzee Juma Kilowoko nyumbani kwa marehemu Tabata Bima jijini Dar es Salaam.
 Mwenyekiti wa kamati ya Kusaidia timu ya Taifa ya Vijana Serengeti Boys Bw. Ridhiwani Kikwete akitia saini kitabu cha maombolezo nyumbani kwa marehemu Sajuki leo.
 Bw. Ridhiwani Kikwete akimpa maneno ya faraja Baba mzazi wa Marehemu Sajuki Mzee Juma Kilowoko.
 Bw. Ridhiwani Kikwete akitoa mkono wa pole kwa mke wa marehemu Sajuki Bi. Wastara (mwenye buibui).
 Bw. Ridhiwani Kikwete akimfariji mama mzazi wa Marehemu Sajuki alipofika nyumbani hapo kuhani msiba huo.
             Baadhi ya wasanii wa filamu wakisikiliza nasaha za Bw. Ridhiwani Kikwete (hayupo pichani).
                     Katibu wa fedha msibani hapo Steve Nyerere akitetea jambo na Bw. Ridhiwani Kikwete.
 Pichani Juu na Chini ni Baadhi ya wasanii wa filamu wakisikiliza nasaha za Bw. Ridhiwani Kikwete (hayupo pichani).
 Rais wa Shirikisho la Filamu nchini (TAFF) Bw. Simon Mwakifamba akizungumza machache kabla ya kumkaribisha Bw. Ridhiwani Kikwete kuzungumza machache na waombolezaji.
 Mwenyekiti wa kamati ya Kusaidia timu ya Taifa ya Vijana Serengeti Boys Bw. Ridhiwani Kikwete akizungumzia marehemu Sajuki na kuwataka wanawake kuiga mfano wa Maisha ya Sajuki na Wastara jinsi walivyokuwa wakiishi na Upendo mpaka Umauti ulipomkuta marehemu Sajuki na kuwasisitiza kuenzi yale yote mema aliyokuwa akifanya kipindi cha uhai wake na kuwamasisha Umoja na Mshikamano baina yao.

Bw. Ridhiwani Kikwete naye alichangia Shilingi 500,000/= kwa ajili ya kufanikisha mazishi ya Mpendwa wetu Sajuki anayetarajiwa kuzikwa Kesho Ijumaa katika makaburi ya Kisutu jijini Dar es Salaam.
Marehemu Sajuki alikuwa kipenzi cha watoto na wakubwa pia. Pichani ni Umati wa watoto wanaokaa jirani na Nyumba ya Marehemu Sajuki wakiwa wamekusanyika huku wakionyesha majonzi na simanzi tele.

(Picha zote na Mo Blog).