Monday, November 5, 2012

Huyu ndio Miss Tanzania 2012





Mshindi wa Miss Tanzania 2012 Brigitte Alfred (katikati)katika picha ya pamoja na mshindi wa Pili Eugene Fabian (kushoto) na Mshindi wa Tatu, Edda Sylvester, Brigitte anatokea Kitongoji cha Sinza na Kanda ya Kinondoni wakati, Eugene Mkoa wa Mara na Kanda ya Ziwa, Edda ni Miss Kigamboni na Kanda ya Temeke.










Hongera Brain

    Napenda kutoa pongezi kwa kijana wangu Brain kwa kumaliza kidato cha nne katika shule ya Tengeru Boys Arusha,Hongera sana Brain na mwenyenzi mungu akutangulie. your Aunty Faustina (Mama wa aSilialive)

Bodi Ya Utalii Washuhudia Matangazo Yao Uingereza

 Mkurugenzi wa Masoko wa Bodi ya Utalii Tanzania TTB Devotha Mdachi akizungumza na Waziri wa mambo ya nje wa zamani wa Uingereza na Mbunge wa Jimbo la South Shields Mh.David Miliband wakati ujumbe wa TTB ulipotembelea Uwanja wa Sunderland FC na kushuhudia mchezo wa ligi kuu ya Uingereza kati ya timu hiyo na timu ya Aston Villa uliofanyika siku ya jumamosi nchini Uingereza, Bodi ya utalii Tanzania inatangaza matangazo ya utalii wa Tanzania katika viwanja sita vinavyotumika kuchezea ligi kuu ya Uingereza (Premier Liegue) kikiwemo kiwanja cha Sunderland FC, katika picha katikati ni Edmund Hazal Mkurugenzi wa Kampuni ya Lantech Services inayoratibu matangazo hayo,Bw. David Miliband pia ni mwenyekti wa klabu ya Sunderland.
 Waziri wa mambo ya nje wa zamani wa Uingereza na Mbunge wa Jimbo la South Shields Mh.David Miliband  akiwa katika picha ya pamoja na Meneja Masoko wa Bodi ya Utalii Tanzania TTB Bw. Geofrey Meena kushoto mara baada ya kumalizika kwa mchezo wa ligi kuu ya Uingereza kati ya Suderland na Aston Villa, David Miliband pia ni mwenyekiti wa klabu ya Suderland
 Mkurugenzi wa Masoko wa Bodi ya UtaliiTanzania TTB Devotha Mdachi akiwa katika picha ya pamoja na wachezaji wa zamani na maafisa wa timu ya Sunderland FC baada ya kukabidhiwa zawadi ya saa kutoka kulia ni Balozi wa Sunderland na Golikipa wa zamani Jimmy Montgomery, Gary Mutchinson Mkurugenzi wa Biashara na Kevin Ball Nahodha wa zamani wa timu hiyo
Ujumbe wa Bodi ya Utalii na maafisa wa taasisi mbalimbali wakipiga picha ya pamoja nje ya uwanja huo kutoka kulia ni Bw. Manase kutoka Ngorongoro, Bw. Mukhtar kutoka Jumuiya ya Afrika Mashariki , Mkurugenzi wa Masoko TTB Devotha Mdachi, Geofrey Meena Meneja Masoko TTB na Edmond Hazal Mkurugenzi wa kampuni ya Lantech Services inayoratibu matangazo hayo katika viwanja vya ligi kuu Uingereza.
Picha kwa hisani ya Fullshangweblog

Magazeti ya leo Jumatatu 5th November 2012