Thursday, May 2, 2013

MATOKEO YA YANGA VS COASTAL UNION MAY 1 2013.

 

SHANGWE ZA BAYERN MUNICH DHIDI YA BARCA, NA ZA MECHI PIA.

 Thomas Muller akiongoza shangwe za ushindi dhidi ya Barcelona, hapa ilikua ni mbele ya mashabiki wa Bayern waliosafiri kutoka Ujerumani mpaka Hispania.

Magazeti ya leo Alhamisi ya 2nd May 2013





KATIKA SIKU YA MEI MOSI SERIKALI YATANGAZA KUPUNGUZA KODI KATIKA MISHAHARA

 Rais Jakaya Kikwete (katikati) akishikana mikono na viongozi wengine kuimba wimbo wa Mshikamano Daima wakati wa maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani iliyofanyika kitaifa mkoani Mbeya jana.
         
Wafanyakazi nchini watapata nafuu kimapato, pale Serikali itakapoanza kutekeleza azma yake ya kupunguza kodi kwenye mishahara (PAYE) wiki mbili zijazo.

Rais Jakaya Kikwete, jana aliashiria hivyo baada ya kutangaza punguzo la PAYE, kwa lengo la kupunguza mzigo wa ugumu wa maisha kwa mfanyakazi.

Alitangaza hatua hiyo alipohutubia wananchi jana katika maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi, yaliyofanyika kitaifa kwenye Uwanja wa Sokoine, Mbeya na kutangazwa moja kwa moja na vyombo vya habari.

“Tangu mwaka 2007 baada ya kilio cha wafanyakazi, tulipunguza kodi kutoka asilimia 18 hadi 15, na kwa mwaka 2010/11 tulipunguza hadi asilimia 14.

CCM WAMVAA MKUU WA MKOA WA ARUSHA.....WANADAI AMEMUONGEZEA UMAARUFU GODBLESS LEMA

 VIGOGO wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wakiwemo wabunge, wamemjia juu Mkuu wa Mkoa (RC) wa Arusha, Magessa Mulongo kwa jinsi alivyoshughulikia kesi ya Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema (CHADEMA).

Wabunge hao waliliambia gazeti hili mjini Dodoma kuwa kesi ya uchochezi iliyofunguliwa na serikali dhidi ya Lema kwa shinikizo la mkuu huyo, itaiathiri kwa kiasi kikubwa CCM.

Mbunge wa Mwibara, Kangi Lugola alisema kuwa amefuatilia kwa makini chanzo cha kesi ya Lema na hatimaye kukamatwa na polisi mithili ya gaidi, na kubaini kuwa hulka
za utendaji kazi wa baadhi ya viongozi wa serikali zinawapa sifa na umaarufu zaidi CHADEMA.

“Mimi sitaki kuingilia kesi, lakini ukiangalia kuanzia ile inayoitwa video ya vurugu za Chuo cha Uhasibu Arusha na jinsi Mkuu wa Mkoa alivyofika eneo la tukio na kuondoka, utabaini udhaifu mkubwa wa kiongozi huyo ambao leo unamfanya Lema aonekane shujaa.
“Leo tunaingia kwenye uchaguzi mdogo wa madiwani pale Arusha, tunaweza tukashinda, lakini tutafanya kazi ya ziada kwa sababu tu ya udhaifu wa Mkuu wa Mkoa wa Arusha,” alisema Lugola.

"SIJAJA BONGO KUFUATA PENZI LA DIAMOND"...AVRIL

Jana ilikuwa ni birthday ya msanii wa Ogopa Djs ya Kenya, Judith Nyambura Mwangi a.k.a Avril ambaye alitua jijini dar es salaam juzi na sababu ya ujio wake ilikuwa ni vitu vikubwa viwili.

Akihojiwa katika kipindi cha XXL kupitia Clouds fm Avril amesema ujio wake hapa bongo kwanza ni ku-celebrate birthday yake na fans wa Tanzania, na pili ni ku-launch single yake mpya aliomshirikisha Ommy Dimpoz ambaye kwa sasa yuko ziarani barani Ulaya, party ilifanyika usiku wa kuamkia jana (April 30) pale Elements club.

Kuhusiana na maneno ambayo yamekuwa yakisemwa juu ya tetesi za kuwepo kwa mahusiano baina yake na Diamond Platnumz ambaye alimshirikisha Avril katika video ya Kesho, Avril amekana kuwepo kwa uhusiano wowote zaidi ya kuwa marafiki wa kawaida na wa kikazi. "Hakuna kitu chochote kati yangu na diamond  na  sijaja  Tanzania  kufuata  penzi  lake... we are just friends na relationship yetu ni proffesional relationship katika muziki", alisema Avril.

Hii ndo birthday party ya kwanza kwa Avril kufanya, birthdays zake zote zilizopita alikua anasheherekea kwa kuchill tu nyumbani na familia yake.

WABUNGE WATWANGANA NGUMI NDANI YA BUNGE...

                                                               Bunge la Venezuela.
Makonde yameibuka bungeni na baadhi ya wabunge kujeruhiwa katika sintofahamu, kutokana na mjadala kuhusu uchaguzi wa hivi karibuni unaobishaniwa.

Upande wa upinzani ulisema juzi kwamba wabunge wao saba, walishambuliwa na kujeruhiwa wakati wakipinga hatua ya kuwazuia kuzungumza katika Bunge hilo, kutokana na kukataa kwao kutambua ushindi wa Rais Nicolas Maduro uliofanyika Aprili 14.

Wabunge wa chama tawala walilaumu wapinzani wao hao na kuwaita mafashisti kwa kuanzisha vurugu, hali iliyoonesha siasa tete katika Taifa hili mwanachama wa OPEC baada ya kifo cha Msoshalisti, Hugo Chavez mwezi jana.

"SIKU NIKIFA RUGE MUTAHABA NA KUSAGA WASIHUDHURIE MAZISHI YANGU"....LADY JAYDEE

Watu wanashtuka mtu akiongelea kifo, Utafikiri hawafahamu fika kuwa kila nafsi itakionja, Kwenye maisha yangu nimepitia mambo mengi, magumu na mepesi
Na bado naendelea ku experience mambo magumu zaidi kadri ninavyozidi kuwa mkubwa.

Siku za karibuni nimekuwa nikipigwa vita sana na watu wenye uwezo mkubwa kifedha , ki umri na hata wenye ukubwa wa connection katika hii industry ya muziki. Wanaomiliki chombo cha habari.

Nasimama na kusema kuwa sitokata tamaa, kwani lengo lao kubwa ni kuona na kuhakikisha nimeanguka kabisa na sipo katika ramani ya muziki.