Wednesday, March 27, 2013

RAIS KIKWETE AZINDUA TAARIFA YA UTAFITI WA VISAHIRIA VYA UKIMWI NA MALARIA MWAKA 2012

 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akikata ukanda kuzindua rasmi taarifa ya utafiti wa viashiria vya ukimwei na malaria mwaka 2012 leo Machi 27, 2013 katika ukumbi wa Karimjee jijini Dar es salaam.

Kulia kwake ni Waziri Mkuu Mhe Mizengo Pinda na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe Saidi Meck Sadiki. Kushoto kwake ni Mkurugenzi wa Tume ya Kudhibiri Ukimwi (TACAIDS) Mama Fatma Mrisho na

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge), Mhe William Lukuvi.

KITABU CHA KIFO NI HAKI YANGU CHAZINDULIWA RASMI


 Mtunzi mashuhuri wa vitabu kutoka kampuni ya Mkuki na Nyota, Mzee Walter Bgoya, akikata utepe pamoja na mtunzi wa kitabu cha ‘Kifo ni Haki Yangu’, Eric James Shigongo (kulia) wakati wa uzinduzi wa kitabu hicho uliofanyika katika duka la vitabu la Tanzania Publishing House lililopo mtaa wa Samora jijini Dar es Salaam.
 Mtunzi Eric Shigongo akimpatia kitabu mtunzi mwenziye, mzee Walter Bgoya.

ALICHOKIANDIKA ZITTO KABWE KUHUSU HABARI ZA NJAMA ZA KUMUUA

BINTI ABAKWA MPAKA KUFA...ALIKUWA ANATOKA NACHINGWEA RESORT

Bint aliyejulikana Mariam amekutwa na mauti  baada ya kubakwa mpaka kufa....

Vijana hao waliokosa utu na kushindwa kumuogopa Mungu walifanya kitendo hicho mbele ya eneo la kanisa(Voda st)Nachingwea Lindi.

Marehemu alikuwa  na  mkasa   huo wakati akitoka Nachingwea Resort(NR) katika muziki siku ya ijumaa.Inasadikika marehemu amelewa  na wabakaji  alitoka nao muziki.

MSANII RADO ANUSURIKA KIFO BAADA YA KUPOKEA KICHAPO KIKALI MWANANYAMALA

 MSANII wa muziki na filamu Bongo, Saimon Mwapagata ‘Rado’ amenusurika kifo kutoka kwa vijana waliofunga njia maeneo ya Mwananyamala, jijini Dar Jumapili iliyopita.

Kwa mujibu wa rafiki wa Rado ambaye pia ni msanii wa filamu, Deogratius Shija, tukio hilo lilitokea usiku wakati Rado alipokuwa akirudi nyumbani kwake..

“Alikuta njia imefungwa na vijana watatu, alijaribu kuwapigia honi lakini hawakufungua njia.

“Rado alishuka kwenye gari na kuwauliza kwa nini wamefunga njia wakamjibu kwamba mmoja wao ameibiwa simu, hivyo wanamtafuta mwizi wao.
Shija alisema kwamba ghafla vijana wale walimvamia Rado  na kumshushia kipigo cha haja wakiwa na mapanga na marungu na kumjeruhi hadi akapoteza fahamu.

 “Nilipigiwa simu na msamaria  na kuambiwa kuwa Rado hajiwezi, sababu kuna watu wanaomjua maeneo yale alipelekwa Oysterbay Polisi kisha kukimbizwa Hospitali ya Mwananyamala ambako alishonwa, kifuani na mguuni,”

YULE MTOTO WA MIAKA 8 ALIYEOA BIBI WA MAIAKA 61 ADAI KUFURAHIA FURAHA KUITWA BABA

 KUSHOTO: Sanele akibusiana na mkewe, Helen siku ya harusi yao wiki mbili zilizopita. KULIA: Sanele na Helen walipata chakula cha usiku pamoja nyumbani kwa mkewe huyo.

Huku miguu yake ikining'inia juu ya sakafu na sehemu yake ya chakula cha mtoto, inaonekana kama anakula chakula cha usiku na bibi yake.Ukweli ni kwamba Sanele Masilela, mwenye miaka 8, anafurahia chakula cha usiku na mke wake, baada ya kumuoa wiki mbili zilizopita, na inasemekana kwa sasa ameanza kujisikia kama mume kamili.

Magazeti ya leo Jumatano ya 27th March 2013