Tuesday, May 14, 2013

Mashabiki Barca wamiminika mitaani kushangilia ubingwa la liga


                                                                            Mashabiki wa Barca

Magazeti ya Leo Jumanne ya 14th May 2013





WENYE MABASI WATAKA NAULI IPANDE TENA

BAADHI ya wamiliki wa mabasi mkoani Shinyanga, wamesema asilimia 24.46 iliyoongezwa katika nauli haitoshi.

Wamiliki hao wameyasema hayo ikiwa ni takriban mwezi mmoja tangu kuanza kutumika kwa nauli mpya za usafiri wa barabara, reli na kupandishwa kwa tozo za huduma za meli bandarini. Hatua hiyo ilichukuliwa na Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (SUMATRA), Aprili 3 mwaka huu.

Wakizungumza na Mtanzania kwa nyakati tofauti mjini Shinyanga, baadhi ya wamiliki wa mabasi na wadau wa sekta ya usafirishaji nchi kavu, walisema awali wao waliwasilisha mapendekezo yao kwa SUMATRA wakiomba kupandishwa kwa nauli kwa asilimia 149.

Mmoja wa wamiliki wa mabasi ambaye hakuwa tayari kutajwa jina lake , alisema kutokana na kupanda kwa bei ya spea za magari na gharama za uendeshaji, kampuni nyingi kwa sasa zinashindwa kufanya matengenezo ya mabasi yao.

Alisema katika mwaka mmoja uliopita, tairi ya gari kubwa ilikuwa ikiuzwa Sh 400,000 lakini kwa sasa inauzwa Sh 650,000. Wakati huo bima ilikuwa Sh 450,000 lakini sasa imepanda hadi Sh 1,000,000, alisema.

Alitaja gharama nyingine kuwa ni kodi zinazotozwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), ushuru wa kituo cha mabasi Sh 2,000 na ada ya Chama cha Madereva Sh 5,000 ambazo hutozwa kwa kila basi linaloingia katika kituo cha mabasi.

MAJINA YA WATUHUMIWA WALIOACHIWA HURU PAMOJA NA RIPOTI YA POLISI KUHUSU BOMU LA ARUSHA

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI KUHUSIANA NA MAENDELEO YA UPELELEZI WA TUKIO LA MLIPUKO WA BOMU KATIKA KANISA LA MT. JOSEPH – OLASITI JIJINI ARUSHA LILILOTOKEA TAREHE 05/05/2013

Ndugu wanahabari, mtakumbuka kwamba mara ya mwisho nilipokutana nanyi niliwaahidi kwamba nitaendelea kuwapa mara kwa mara taarifa juu ta maendeleo ya upelelezi wa tukio la mlipuko wa bomu lililotokea katika kanisa katoliki la mtakatifu joseph mfanyakazi parokia ya olasiti tarehe 05/05/2013 na kusababisha vifo vya watu watatu(3) na wengine kudhaa kujeruhiwa.

Kama nilivyowaeleza hapo awali, baada ya tukio hilo jumla ya watuhumiwa tisa(9) walikamatwa na kuhojiwa kuhusiana na tukio hilo la mlipuko wa bomu kanisani. Watuhumiwa haoa ni victor Ambros Kalist, (20), dereva wa bodaboda na mkazi wa kwa Morombo; Yusuph Lomayani Josee (18) mwendesha bodaboda mkazi wa kwa Morombo na George Bathlomeo Silayo (23) mfanyabiashara na mkazi wa Olasiti.

Watuhumiwa wengine waliokamatwa ni raia watatu toka nchi za falme za kiaruabu (UAE) Abdul Aziz Mubrak (30) mfanyakazi wa mamlaka ya mapato katika falme za kiarabu, Fouad Saleem Ahmed Al Hareez Al Mahri (29) mfanyakazi wa kikosi cha zimamoto katika Falme za Kiarabu, Saeed Abdulla Saad (28) askali polisikitengo cha traffic katika falme za Kiarabu, pamoja na raia mmoja wa Saudi Arabia Al-Mahri Saeed Mohseens (29)

MTUHUMIWA NAMBA MOJA WA BOMU LA ARUSHA AMEFIKISHWA MAHAKAMANI NA KUSOMEWA MASHITAKA 21

 Mtuhumiwa mmoja kati ya tisa waliotiwa mbaroni na jeshi la polisi baada ya kutokea mlipuko wa bomu katika Kanisa la Mtakatifu Joseph Mfanyakazi amefikishwa mahakamani na kusomewa mashtaka 21 ya mauaji na kujaribu kuua.

Victor Ambrose Calist (20) ambaye ni dereva wa bodaboda na mkazi wa eneo la Kwa Mromboo jijini Arushai amesomewa mashtaka yake mbele ya Hakimu mkazi, Devotha Kamuzora.

Mtuhumiwa huyo anakabiliwa na mashtaka matatu ya mauaji ya watu watatu waliofariki dunia katika tukio ambalo lililotokea Mei 5, mwaka huu.

Mawakili wa serikali, Haruna Matagane na Zachariah Elisaria wanadai Calist pia anatuhumiwa kwa makosa 18 ya kujaribu kuua. Hata hivyo makosa mengine bado hayajatajwa..

Pia polisi imewaachia huru raia wanne wa kigeni waliokuwa wakishikiliwa kwa tuhuma za kuhusika katika tukio hilo baada ya uchunguzi uliofanywa na jeshi hilo kwa kushirikiana na FBI na polisi wa kimataifa (Interpol), kubaini hawakuhusika kurusha bomu katika kanisa hilo.

IKULU YAMJIBU DR. SLAA KUHUSU KASHFA YA UDINI WA RAISI KIKWETE ALIZOZITOA

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

KATIBU Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mheshimiwa Wilbroad Slaa, leo, Jumatatu, Mei 13, 2013, amekaririwa na gazeti moja akidai kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete na timu yake ya kampeni, “ilikuwa ikisaka kura kwenye nyumba za ibada na kumwaga sumu mbaya ya udini ambayo sasa inaitesa Serikali nataifa” kwenye Kampeni za Uchaguzi Mkuu wa 2010.

Aidha, katika habari hiyo iliyoandikwa chini ya kichwa cha habari, “Dk. Slaa amlipua JK” kwenye gazeti linalounga mkono CHADEMA la Tanzania Daima,Mheshimiwa Slaa anadai kuwa migogoro ya sasa ya kidini “inajengwa au kutengenezwa na Serikali iliyojikita kusambaza sumu ya udini katika misikiti wakati wa kampeni za Urais mwaka 2010”.

Kwa hakika, hakuna namna nyingine ama namna bora zaidi ya kuielezea kauli hii ya Mheshimiwa Slaa isipokuwa kwamba kauli hiyo ni riwaya nyingine isiyokuwa na mshiko. Ni uongo mtupu. Yake Mheshimiwa Slaa ni maneno yasiyokuwa na ukweli wowote.