Saturday, June 23, 2012

Airtel Yatoa Msaada Vifaa Vya Michezo Shule Za Msingi Gongolamboto


Afisa uhusiano wa Airtel, Jane Matinde akikabidhi jezi za mpira kwa Mwalimu mkuu wa shule ya msingi ya Maarifa, Marietha Mulyalya wakati Airtel ilipotembelea shule za Mwangaza, Maarifa na Gongolamboto Jaika Gongolamboto na kukabidhi vifaa vya michezo hapo Jana

Afisa uhusiano wa Airtel, Jane Matinde akikabidhi jezi za mpira kwa Mwalimu wa Taaluma na michezo wa shule ya msingi ya Gongolamboto Jaika, Almasi Shemdoe wakati Airtel ilipotembelea shule za msingi za Gongolamboto za Mwangaza, Maarifa na Gongolamboto Jaika na kugawa vifaa vya michezo.
Afisa uhusiano wa Airtel, Jane Matinde akikabidhi jezi za mpira kwa  Mwalimu wa Taaluma na michezo wa shule msingi ya Mwangaza, Abdul Mwarami wakati Airtel ilipotembelea shule za  Mwangaza, Maarifa na Gongolamboto Jaika na kukabidhi vifaa vya michezo. Chanzo: www.fullshangweblog.com

Mwili Wa Marehemu Willy Edward Utawekwa Kwenye Nyumba Yake Ya Milele Leo Saa 9 Alasiri


MWILI wa aliyekuwa Mhariri Mkuu wa gazeti la Jambo Leo, marehemu Willy Edward utawekwa kwenye nyumba yake ya milele leo saa 9 alasiri katika kiwanja cha nyumba yao eneo la Molotonga, Mugumu Mjini, wilayani Serengeti , mkoani Mara.

Kwa mujibu wa ratiba ya mazishi iliyotolewa na Msemaji wa Familia, George Ogunde, inaeleza kuwa ibada ya mazishi itaanza saa 5 nyumbani kwa mzee Edward Ogunde, itaongozwa na Askofu wa Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Mara, Hilikia Omindo, Askofu wa Anglikana Dayosisi ya Rorya, John Adiema na Mussa Omboi Mchungaji Msaidizi wa Parishi ya Mugumu.

Baada ya ibada kitakachofuatia ni wananchi kuaga mwili wa mpendwa wetu, marehemu, Willy Edward na hatimaye maziko.

Mkuu wa Mkoa wa Mara ambaye kwa hivi sasa yupo bungeni kushiriki wakati wa kutangazwa kwa Bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu (TAMISEMI), atatuma mwakilishi kwenye mazishi hayo.

Baadhi ya viongozi wengine watakaoshiriki katika mazishi hayo ni Mkuu wa Wilaya ya Magu, Jacquiline Liana, Mwenyekiti wa CCM, Mkoa wa Shinyanga, Hamis Mgeja na wengine wengi.

Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri, Absalom Kibanda aliwasili jana kwenye msiba akitokea Dar es Salaam, akiwa na Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari ya Dar es Salaam, Jane Mihanji, Mhariri wa Gazeti la Matanzania Jumapili, Revocatus Makaranga na Kulwa Karedia ambaye ni Mhariri Mkuu wa gazeti la kila siku la Mtanzania.

Chanzo:  http://richard-mwaikenda.blogspot.com/

Mahakama Kuu Ya Tanzania Yatoa Amri Ya Kusitisha Mgomo Wa Madaktari

Kufuatia Tangazo la Chama cha Madaktari nchini (MAT) la kuanza mgomo siku ya Jumamosi tarehe 23 Juni, 2012, Mahakama Kuu ya Tanzania,Kitengo cha kazi,Dar es Salaam imetoa amri ya kusitisha mgomo huo mpaka hapo pande zote mbili yaani Serikali na Chama cha Madaktari Tanzania (MAT) yatakaposikilizwa na kutolewa uamuzi.

· Amri hiyo ya Mahakama imetolewa kufuatia maombi namba 73 ya 2012 yaliyowasilishwa chini ya hati ya dharura na Mwanasheria Mkuu wa Serikali dhidi ya Chama cha Madaktari Tanzania (MAT).Sababu za msingi amabazo zimepelekea Mahakama kuu kutoa amri hiyo upande mmoja ni pamoja na;

· Iwapo mgomo huo utatokea utakuwa na kuwa amri hii isipotolewa madhara yake ni makubwa isiyoweza kufidiwa kwa namna yoyote ile kama vile kupoteza maisha n.k

· Wajibu maombi,ambao ni MAT, inaundwa na Madaktari ambao wapo katika Sekta ambayo inatoa huduma mahsusi (essential service sector), Aidha Chama cha Madaktari Tanzania kimetangaza mgomo bila kufuatia taratibu zilizoanishwa katika Kifungu cha 76(1 na 2) cha Sheria ya Kazi (Employment and Labour Relations Act No 6 ya 2004.

Masharti hayo ni

· Kuzuia wafanyakazi walio katika Sekta Muhimu kugoma na kama wakigoma, Kuwepo na makubalianao ya pamoja ya kutoa huduma za msingi wakati mgomo ukiendelea. Kwa misingi huu,Mahakama Kuu ya Tanzania, kwa Chama cha Madktari Nchini na wanachama wake kusitisha na kutoshiriki katika mgomo huo.

MAGAZETI YA LEO JUMAMOSI JUN 23


MAMA KANUMBA ANUNUA...


ZIMEKATIKA siku 75 tangu kufariki dunia kwa supastaa wa filamu za Bongo, Steven Charles Kanumba, Aprili 7, 2012. Mama mzazi wa marehemu huyo, Flora Mtegoa mambo yamemnyookea ambapo amenunua jumba kubwa la kifahari, Risasi Jumamosi linakuwa la kwanza kuripoti.

CHANZO CHATEMA NYETI
Kwa mujibu wa chanzo cha uhakika, mjengo huo upo Kimara Temboni jijini Dar es Salaam ambapo mama huyo na familia yake (akiwemo Seth Bosco) wamehamia.

Sanjari na wao, pia magari matatu ya marehemu, Toyota Hiace, Toyota Lexus na Toyota GX 110 yamepiga kambi huko, kila moja likiwa na sehemu yake ya kuegesha.

Kwa mujibu wa chanzo hicho, kwa sasa mama Kanumba hana makazi tena pale Sinza Kijiweni ambako ndiko palipofanyikia msiba wa mwanaye hadi kuhitimisha na arobaini yake.

KUNA USIRI
Chanzo kikadai kuwa kuhama kwa mama huyo na familia yake kutoka Sinza kwenda Temboni kumegubikwa na usiri bila kufafanua siri hiyo inatokana na nini!

MAPAPARAZI WAINGIA MZIGONI KUCHUNGUZA
Baada ya gazeti hili kuzidaka nyeti hizo, Alhamisi ya Juni 21, 2012 lilituma timu ya waandishi wake kwenda kupata uhakika wa madai hayo na kujiridhisha kabla ya gazeti halijakwenda mitamboni.

NJE YA NYUMBA
Ndani ya geti kuu la nyumba hiyo yenye bati la kijani, alikutwa mdogo wa marehemu Kanumba, Seth Bosco akipata chai huku upepo mwanana ukimpuliza. Mama Kanumba alikuwa akiendelea na shughuli zake za kawaida.

Mbali na kuwaona wawili hao, mapaparazi wetu waliendelea na uchunguzi wao ambapo waliipiga raundi nyumba hiyo na kujionea magari yote matatu ya marehemu  yakiwa yamepaki huku jamaa mmoja akiwa juu ya bati kuweka dishi la televisheni la ‘kuangalizia’ Mashindano ya Kombe la Mataifa ya Ulaya ‘Euro’ yanayoendelea kwa sasa nchini Poland na Ukraine.

Makachero wetu walipojiridhisha kuwa mama Kanumba ndiyo kaweka makazi yake mapya, lilipiga picha za kumwaga kisha lilimwendea hewani Seth na kuzungumza naye ili kupata ukweli mwingine.

SAUTI YA SETH KUTOKEA TEMBONI
Paparazi: Mambo Seth?
Seth: Poa tu, nani mwenzangu?
Paparazi: Unaongea na Risasi Jumamosi hapa.
Seth: Enhe, lete habari.

Paparazi: Inasemekana mmehama pale Vatican, mmehamia wapi?
Seth: Aaa, tumehamia Temboni huku.
Paparazi: Ni kweli huko mmenunua nyumba?
Seth: Ni kweli.

Paparazi: Shilingi ngapi?
Seth: Mh! Hilo swali anayeweza kujibu ni mama kwamba ni shilingi ngapi na mambo mengine yote.
Risasi Jumamosi lilipomsaka mama Kanumba kwa kutumia simu yake ya mkononi, hakupatikana hewani siku hiyo.

MJENGO WA BEI MBAYA
Hata hivyo, Risasi Jumamosi lilifanya uchunguzi na kunyaka baadhi ya nyaraka zinazoonesha kuwa mjengo huo umenunuliwa kwa shilingi milioni themanini (80,000,000) za Kibongo.

MASTAA HAWAJUI
Gazeti hili lilijaribu kufanya mawasiliano na baadhi ya mastaa wa filamu Bongo kama wanajua mama yao huyo amehama Sinza lakini kila aliyeulizwa hakuwa anafahamu na kuwa ‘sapraizi’ kwake.
Mwanyekiti wa Klabu ya Bongo Movie, Jacob Steve ‘JB’ alipovutiwa uzi na kuulizwa alisema hajui kama mama Kanumba amehama Sinza.
HII HAPA SAUTI YAKE
“Amehama pale? Duu! Mimi sijui kaka.”

MWAKIFAMBA AKIWA NJIANI KWENDA SINZA
Naye Mwenyekiti wa Shirikisho la Filamu Bongo, Simon Mwakifamba alipopigiwa simu kuulizwa, akajibu anaamini mama huyo bado yupo Sinza, na yeye mwenyewe alipanga kwenda siku hiyo ya Alhamisi jioni ili akamjulie hali. pisha zaidi - globalpulishershttp://www.globalpublishers.

Wolper awindwa alishwe sumu


Imefahamika kuwa kuna kundi la watu linamuwinda kwa udi na uvumba mwigizaji Jacqueline Masawe ‘Wolper’ kwa dhumuni la kumlisha sumu ambayo itakuwa ikimtafuna taratibu hadi imfute juu ya uso wa dunia, Risasi Jumamosi limeinyaka.Akizungumza na mwandishi wetu, rafiki wa karibu wa Wolper aliyeomba hifadhi ya jina lake, alisema kuwa kumekuwa na mazungumzo yanayomhusu staa huyo yanayosikika katika kona mbalimbali kunapokuwa na mastaa wa filamu za Kibongo ambayo yamejaa chuki ndani yake huku kisa kikiwa hakijulikani.

“Ukiniuliza kisa ni nini au kosa la Wolper mpaka sasa siwezi kukwambia kwa sababu sijui ni kitu gani lakini kila kukicha ukikaa mahali na wasanii zitapigwa stori mwisho wataanza kumzungumzia vibaya Wolper.

“Kwa mfano tulipokwenda Moshi na Arusha (wikiendi iliyopita), tukiwa kwenye ndege kuna watu walikuwa wakimsema vibaya sana, tena si kwa sauti ya chini kila mtu alikuwa akisikia, nadhani kuna kitu anatakiwa kukifanya kwa sasa ili ajilinde kwa usalama wake,” alisema rafiki huyo ambaye naye ni muigizaji.

Wolper laivu
Kama ilivyo ada, baada ya kupata maelezo ya chanzo hicho cha habari, Risasi Jumamosi lilimvutia waya Wolper na kumweleza kila kitu ambapo mbali na kukiri kuifahamu ishu hiyo, alikuwa na haya ya kusema:

“Ukweli ni kwamba hali halisi nishaipata kwani kwenye ile ndege waliyopanda, mmoja wa wahudumu ni dada yangu tena wa damu kabisa alikuwa anasikia mazungumzo yote yaliyokuwa yakinihusu.”

Wolper alisema kuwa Waswahili wanasema kuwa jihadhari kabla ya hatari hivyo katika hatua aliyochukua kwa kujihadhari, mojawapo ni hiyo ya kutoacha kinywaji au chakula mezani kisha akakirudia.

“Siwezi kumuamini mtu yeyote katika usalama wangu kwa sasa kwani huwezi kujua moyo wa mtu ni msitu mkubwa sana. Sitathubutu kuacha kinywaji au kitu chochote kinachoingia mdomoni hadharani eti kwa kuwa niliokaa nao ni waigizaji wenzangu, nafanya hivyo kutokana na hali halisi. Inavyoonekana watu wanaumia sana mimi kumiliki BMW X6,” alisema Wolper.

UJERUMANI YATINGA NUSU FAINALI EURO 2012

Beki wa Ujerumani, Philipp Lahm akishangilia pamoja na Jerome Boateng, bao la kwanza aliloifungia timu yake dhidi ya Ugiriki leo wakati wa mechi ya robo fainali ya michuano ya Euro 2012 katika uwanja wa Manispaa jijini Gdansk, Poland. Ujerumani wameshinda 4-2. (Picha zote na Alex Grimm/Getty Images)
Bastian Schweinsteiger wa Ujerumani (kulia) akichuana na mshambuliaji wa Ugiriki, Giorgos Samaras wakati wa mechi ya robo fainali ya michuano ya Euro 2012 katika uwanja wa PGE jijini Gdansk, Poland. Ujerumani wameshinda 4-2. (Picha na REUTERS)

TIMU ya taifa ya Ujerumani imefanikiwa kutinga nusu fainali ya michuano ya Euro 2012 baada ya ushindi wa 4-2 dhidi ya Ugiriki kwenye mchezo wa robo fainali ya michuano ya Euro 2012 katika uwanja wa  PGE jijini Gdansk, Poland. Mabao  ya Ujerumani yamefungwa na Philipp Lahm, Sami Khedira, Miroslav Klose, na Marco Reus.

Lengo la Kuomba Mwongozo - Sakata la Madaktari


 Kwa nini niliomba muongozo-Sakata la Mgomo wa Madaktari

Leo nilitaka kuomba muongozo wa Spika kwa mujibu wa Kanuni 49 (2) baada ya Waziri wa Afya kutoa kauli juu ya utekelezaji wa madai ya madaktari. Kanuni hiyo inataka kauli isiwe ya kuzua mjadala lakini aliyoyaeleza waziri juu ya uboreshaji wa maslahi ya madaktari yanazua mjadala kwa kuwa yanatofautiana na majibu ya Waziri Mkuu, Mizengo Pinda aliyoyatoa bungeni jana, (Juni 21, 2012) na pia hayana uhalisi.

 Mathalani, wakati serikali ikidai imeongeza posho ya kuitwa kazini (on call allowance) toka Februari, 2012 na kutumia bilioni 7.9 kwa miezi michache, imetenga kwa watumishi wa Afya bilioni 18.9 tu kwa mwaka mzima wa 2012/2013 kiwango ambacho hakitoshi.

 Hivyo nilitaka kuomba muongozo Spika awezeshe kauli hiyo ijadiliwe kama ilivyokuwa kwa kauli juu ya fedha za rada. Nakusudia kumuandikia barua Spika kushauri aelekeze kamati ya bunge ya huduma za jamii kauli hiyo ya waziri.

 Pia bunge halipaswi kunyimwa fursa ya kutumia mamlaka yake kwa mujibu wa ibara ya 63 ya kuishauri na kuisimamia serikali kusuluhisha mgogoro na madaktari ili kuepusha mgomo wenye athari kwa nchi na wananchi kwa kisingizio cha kusudio la serikali kupeleka mgogoro mahakama kuu kwa kuwa mpaka leo taarifa iliyotolewa bungeni bado hakuna shauri katika kitengo cha kazi. Hivyo, Spika anapaswa kutoa jukumu kwa kamati husika ya bunge kuendelea na usuluhishi kabla ya serikali kukimbilia mahakamani.

 Wabunge tupewe nakala ya taarifa ya majadiliano ya pande mbili yaliyochukua zaidi ya siku 90 badala ya kupewa hotuba ya nusu saa ya upande mmoja wa serikali pekee.
Hata serikali ikizuia mgomo wa wazi kwa zuio la kimahakama ieleweke kuwa mgomo wa chinichini kwa watumishi wa afya ambao una athari ya muda mrefu kwa maisha ya wananchi nchini.

Mwisho, serikali ipunguze matumizi yasiyo ya lazima na ipanue wigo wa mapato.

                             John John Mnyika.
                     Mbunge Jimbo la Ubungo (CHADEMA)
                               22 Juni, 2012