Sunday, January 13, 2013

BONDIA MTANZANIA THOMAS MSALI ALIVYOMKOROGA BERNARD MACKOLIECH WA KENYA

 Bondia Mtanzania Thomas Mashali kushoto akiwa amemgalagaza bondiaBernad Mackoliech na kwenda chini akimsubili ili amwendelezee kipondo wakati wa mchezo wao wa kugombania ubingwa wa Afrika Mashariki uliofanyika katika ukumbi wa Friends Conner, Manzese jijini Dar es Salaam na Mashali kuibuka na ushindi wa K,O katika raundi ya sita
  Bondia Bernad Mackoliech wa kenya na Mtanzania Thomas Mashali wakioneshana ufundi wa kutupiana makonde wakati wa mchezo wao wa ubingwa wa Afrika Mashariki Mashali alishinda kwa K,O raundi ya sita
 Baadhi ya mashabiki waliojitokeza katika mpambano huo wa ubingwa wa Afrika Mashariki




Refarii Mark Hatia akimwesabia Bondia Bernad Mackoliech huku akimuamuluThomas Mashalikwenda katika kona nyeupe baada ya kumtwanga konde zito lililomsababisha kulamba sakafu wakati wa mpambano wao wa ubingwa wa Afrika Mashariki

 Kamanda wa polisi mkoa wa Kipolisi wa kinondoni Charles Kenyela akimvisha ubingwa wa Afrika Mashariki bondia Thomas Mashali baada ya kumpiga Bernad Mackoliech wa Kenya kwa K,O Raundi ya 6

Refarii Mark Hatia akimwesabia Bondia Bernad Mackoliech huku akimuamuluThomas Mashalikwenda katika kona nyeupe baada ya kumtwanga konde zito lililomsababisha kulamba sakafu wakati wa mpambano wao wa ubingwa wa Afrika Mashariki. Picha zote na www.superdboxingcoach.blogspot.com

ARSENAL YASHIKWA, YALALA 2-0 KWA MAN CITY





Edin Dzeko wa Manchester City akishangilia baada ya kuifungia timu yake bao la pili na kufanya matokeo kuwa 2-0.



Jack Wilshere wa Arsenal (kushoto) akijaribu kumtoka David Silva wa Manchester City wakati wa mpambano wao uliomalizika kwa Man City kuibuka kidedea kwa bao 2-0.
James Milner wa Manchester City (kulia) akishangilia bao lake la kwanza dhidi ya Arsenal katika mchezo wao uliopigwa kwenye Uwanja wa Emirates jijini London leo. Man City wameshinda 2-0. Kushoto ni Lukas Podolski wa Arsenal.

(PICHA KWA HISANI YA EPA NA REUTERS)

MAN UTD 2, LIVERPOOL 1

Mshambuliaji wa Manchester United, Robin van Persie akishangilia baada ya kuifungia timu yake bao la kuongoza dhidi ya Liverpool leo katika mechi iliyopigwa kwenye Uwanja wa Old Trafford.
          Daniel Sturridge akiifungia Liverpool bao na kufanya matokeo yawe 2-1.

Joe Allen wa Liverpool (kushoto) akichuana na Tom Cleverley wa Manchester United wakati wa mtanange wao uliomalizika kwa Man Utd kuibuka kidedea kwa bao 2-1.

(PICHA: AP, GETTY IMAGES NA REUTERS)

Baruti zauzwa jirani na Ikulu Dar

BARUTI zilizotengenezwa maalumu kwa ajili ya kulipua miamba, sasa zimezagaa katika Soko la Samaki la Kimataifa, lililopo Feri jijini Dar es Salaam, jirani na Ikulu ya Rais Jakaya Kikwete, zikiuzwa kwa ajili ya kutekeleza uvuvi haramu wa samaki katika Bahari ya Hindi.

Biashara hiyo inadaiwa kufanywa na baadhi ya askari wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ), wanaowatumia mawakala, ambao huziuza kwa watu wanaofanya uvuvi haramu sokoni hapo na kutoka maeneo mengine.

Uchunguzi wa gazeti hili, umebaini kuwa biashara hiyo haramu imekuwa ikifanyika zaidi nyakati za usiku na alfajiri kwa takriban mwaka mmoja sasa.
Kwa mujibu wa uchunguzi huo, baruti hizo huuzwa kati ya Sh20,000 hadi 30,000 pamoja na nyaya zake, ambazo huuzwa Sh5,000.

Kitaalamu baruti hutumika katika miradi ya ujenzi wa barabara, migodi ya madini pamoja na jeshini kwa ajili ya kulipulia miamba ya mawe.

Magazeti ya leo Jumapili ya 13th January 2013



Tumechoka mgombea urais kuchaguliwa Dodoma

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), Zanzibar, kimeeleza nia yake ya kutaka kuachiwa mamlaka ya kumchagua mgombea urais wa visiwa hivyo, badala ya utaratibu wa sasa unaoshirikisha wenzao wa Tanzania Bara. Pamoja na hatua hiyo, chama hicho pia kinafikiria kurejea mtindo wa kupokezana kiti cha urais wa Tanzania kati ya bara na visiwani kama ilivyokuwa awali, ili kuweka usawa katika Muungano.

Hatua hiyo inaelezwa kuwa huenda ikazua mpasuko na malumbano mapya kuhusu suala la urais ndani ya CCM, ambako harakati za baadhi ya wanachama wake wameanza kupiga mbio za kuutaka urais katika uchaguzi mkuu wa 2015.

Akizungumza katika mahojiano maalumu visiwani humo, Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Zanzibar), Vuai Ali Vuai, alisema kwa sasa suala hilo linajadiliwa na kwamba ana matumaini kuwa litapatiwa ufumbuzi.

Aliyepiga picha na Lema jela miaka minne

MTU aliyepiga picha na Mbunge wa Arusha mjini, Godbless Lema akiwa amevalia sare za Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), amehukumiwa kifungo cha miaka minne jela. Abubakari Kikulu (29), alipiga picha na mbunge huyo Desemba 23 mwaka jana, baada ya Lema kumaliza kuhutubia mkutano wa hadhara eneo la Mererani, ikiwa ni sehemu ya mikutano aliyoifanya kutokana na Mahakama ya Rufani Tanzania kumrejeshea ubunge wake.

Mbali na kupiga picha hiyo na Lema pamoja na Mbunge wa Arumeru Mashariki Joshua Nassari, kijana huyo alionekana katika picha hiyo akionyesha vidole viwili, ambayo ni alama ya Chadema.

Hata hivyo, baada ya picha hiyo, JWTZ lilimtilia shaka kijana huyo na kutangaza rasmi kumsaka, ili lijiridhishe kama ni mmoja wa wanajeshi wake.
Baada ya kumsaka kwa takriban siku 12, kijana huyo alikamatwa Januari 13, katika Mji wa Bomang’ombe wilayani Hai na baada ya kupekuliwa alikutwa na sare hizo.


Jana, Kikulu alifikishwa mahakamani mjini Moshi, akiwa chini ya ulinzi wa polisi na kusomewa mashtaka mawili, ambayo yote alikiri kuyafanya kama ilivyodaiwa mahakamani.
Baada ya kukiri kosa hilo Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Mkoa wa Kilimanjaro, alimhukumu kifungo cha miaka minne jela, ili iwe fundisho wa wakosaji wengine wa aina hiyo.

Kabla ya hukumu hiyo, Wakili wa Serikali, Ignas Mwinuka alimsomea mshtakiwa huyo mashitaka yake mawili, likiwamo la kujifanya Ofisa wa Jeshi, wakati akijua ni uongo.
Wakili huyo alidai mahakamani kuwa Januari 3, mwaka huu katika eneo la Bomang’ombe wilayani Hai, mtuhumiwa huyo alijitambulisha kama mtumishi wa umma.

Katika shtaka la pili, wakili huyo alidai siku hiyo hiyo katika Mtaa wa Msikitini, eneo hilo la Bomang’ombe, mtuhumiwa alipatikana na sare za JWTZ kinyume cha sheria.

Sare hizo ni pamoja na suruali moja, mashati mawili na kofia mbili, vyote vikiwa na alama za Jeshi la Wananchi wa Tanzania la Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Baada ya Hakimu Kobelo kumuuliza mshtakiwa kama ni kweli alitenda makosa anayoshitakiwa, mshtakiwa huyo alikiri makosa yake katika hali ambayo haikutarajiwa.

Kutokana na kukiri kwake makosa hayo, Hakimu Kobelo alimhukumu kifungo cha miaka miwili kwa kosa la kwanza la kujifanya Ofisa wa JWTZ na miaka mingine miwili kwa kosa la pili.
Hata hivyo, Hakimu Kobelo alisema kuwa kwa kuwa adhabu hizo zinakwenda kwa pamoja (concurrent), mshtakiwa huyo atatumikia kifungo cha miaka miwili jela.

Kwa mujibu wa hakimu huyo, kosa alilolifanya mtuhumiwa huyo ni baya na linastahili adhabu kali, ili iwe fundisho kwa watu wengine wanaotumia vibaya sare za majeshi nchini.

 MWANANCHI.