Saturday, August 11, 2012

Taarifa Kwa Umma Kutoka Benki Kuu Ya Tanzania

Katika Gazeti la Business Times toleo nambari 1248 la Ijumaa, tarehe 10 Agosti 2012, ziliandikwa habari zenye kichwa cha habari chenye maana kuwa “Operesheni za NBC zawekwa chini ya usimamizi wa Benki Kuu”. Katika habari hiyo ilielezwa kuwa Benki Kuu imechukua hatua hiyo kufuatia ripoti za tuhuma kadhaa zihusuzo udhaifu katika uendeshaji wa benki na utawala bora.

Benki Kuu inapenda kuchukua fursa hii kuueleza umma kuwa haijaweka operesheni/shughuli za NBC chini yake. Benki hiyo inajiendesha yenyewe kwa kufuata utaratibu wa Sheria za Makampuni, 2002, Sheria ya Mabenki na Taasisi za Fedha 2006 na miongozo itolewayo na Benki Kuu kama zilivyo benki zingine. Wateja wa NBC na Umma kwa ujumla wanashauriwa kuendelea kufanya biashara na benki hii kama kawaida.

IMETOLEWA NA BENKI KUU YA TANZANIA11AUGUST 2012

Magazeti ya Leo Ijumaa 11st August 2012

Ajali Ya Gari Yaua Raia 11 Wa Kenya Eneo La Wami Mkoa Wa Pwani

 Basi lililokuwa limewabeba raia wa Kenya waliokuwa wakielekea jijini Dar es salaam kwa ajili ya mikutano ya injili  likiwa limetumbukia katika korongo jirani na Mto Wami na kuua watu 11 katika Kijiji cha Makole Mkoa wa Pwani.

Baadhi ya abiria walionusurika wakiwa katika eneo la tukio kabla ya kupata msaada.

WATU 11 wanaoaminika kuwa raia wa Kenya wamefariki dunia papo hapo, huku wengine saba wakiwa mahututi baada ya mabasi waliyokuwa wakisafiria kutoka Nairobi kwenda Dar es Salaam kupata ajali katika Mto Wami mkoani Pwani.Mbali na vifo hivyo, ajali hiyo pia ilisababisha majeruhi 25 na saba kati yao waliripotiwa kuwa mahututi na walipelekwa katika Hospitali ya Tumbi, Kibaha kwa matibabu.

Ajali hiyo ilitokea katika Kijiji cha Makole, wilayani Bagamoyo wakati abiria hao ambao ni wanakwaya walipokuwa wakisafiri kutoka Kenya kwenda Dar es Salaam kushiriki katika tamasha la uimbaji.

Ajali hiyo ilitokea jana saa 11 alfajiri ikihusisha magari manne, mawili kati yake yakiwa ni mabasi hayo yakitokea Kenya na malori mawili ya hapa nchini.Tukio hilo pia lilifunga Barabara Kuu ya Chalinze - Segera kwa zaidi ya saa nane hivyo abiria waliokuwa wakisafiri kuelekea na kutoka mikoa ya Kaskazini ikiwamo nchi ya Kenya kwenda na kutoka Dar es Salaam kukwama.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Ernest Mangu alisema raia hao wa Kenya ni waumini wa Kikristo na walikuwa wakielekea Dar es Salaam kwenye tamasha la kwaya.

JK: Ahudhuria Mazishi Ya Aliyekuwa Rais Ghana John Atta Mills

 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisaini kitabu cha maombolezo wakati shughuli ya mazishi ya Rais John Evans Atta Mills wa Ghana katika ukumbi wa Mikutano wa Ghana jijini Accr.
                                        Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na viongozi wenzie
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akitoa heshima za mwisho kwa aliyekuwa Rais wa Ghana Marehemu Profesa John Evans Atta Mills katika ukumbi wa Mikutano wa Ghana jijini Accra Jana.
 Jukwaa kuu katika uwanja wa Independende Square wakati wa Shughuli mbalimbali za mazishi za aliyekuwa Rais wa Ghana Profesa John Evans Atta Mills katika uwanja wa Independence Square jijini Accra.


 Shughuli mbalimbali za mazishi za aliyekuwa Rais wa Ghana Profesa John Evans Atta Mills katika uwanja wa  Independence Square jijini Accra jana.