Tuesday, April 30, 2013

LULU KURUDIA KAZI YAKE BAADA YA KUSHINDA KESI YAKE!

 HATIMAYE staa wa filamu za Kibongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’ ameingia mzigoni na kufyatua filamu yake mpya baada ya kimya cha muda mrefu, Amani limeinyaka.
 Kwa mujibu wa mtandao wake wa kijamii wa Instagram, Lulu alitupia picha akiwa ‘location’ kuashiria kwamba amerudi kazini baada ya kusimama kuigiza kwa muda mrefu.
Baadhi ya picha hizo zinamuonesha Lulu akiwa na staa mwingine wa filamu Bongo, Hashimu Kambi mbele ya kamera kwa ajili ya kushuti filamu hiyo ambayo jina lake halijapatikana.

TASWIRA ZA SHOW YA DIAMOND JIJINI LONDON



Pichani juu, msanii wa muziki wa kizazi kipya, Naseeb Abdul 'Diamond Platnumz' akifanya makamuzi ndani ya jiji la London wikiendi iliyopita. Msanii huyo bado anaendelea na ziara yake nchini England.

LEMA ASEMA HAYA BAADA YA KUACHIWA MAHAKAMANI KWA DHAMANA

 Mbunge wa jimbo la Arusha mjini Godbless lema ameachiwa huru kwa dhamana na mahakama ya hakimu mkazi baada ya kusota rumande kwenye kituo kikuu cha polisi kwa siku tatu  kwa kosa la kuchochea vurugu chuoni uhasibu huku baada ya kutoka akiwataka wanachama na wapenzi wa chama hicho kumzomea mkuu wa mkoa.

Lema alifikishwa mahakamani hapo majira ya saa Tatu na robo asubuhi akiwa chini ya ulinzi wa polisi na kufikishwa mbele ya hakimu Devotha Msele  na ndipo mwendesha mashtaka Eliang’enyi Njiro alisimama kuanza kumsomewa mashtaka ya uchochezi na kusababisha vurugu na uvunjifu wa amani aliyoyafanya kwenye eneo la chuo cha uhasibu njiro jijini Arusha.

Baada ya kutoka mahakamani hapo alielekea kwenye ofisi za chama hicho na kuzungumza na waandishi wa habari huku akitoa malalamiko na kuwataka wanachama na wapenzi wa chadema kumzomea mkuu wa mkoa iwe kanisani,mskitini,au kwenye sherehe mbali mbali,

“Nawatakeni kumzomea huyo mkuu wa mkoa Magessa Mulongo na kuwa nia ya kumshtaki ipo pale pale ndugu zangu Makamanda wenzangu huyu jamaa awe msikitini kanisani kote tumzome hiyo itakuwa ndiyo salamu yetu kwake”alisema Lema

Katika hali nyingine jeshi la polisi liliimarisha ulinzi tangu nje ya mahakama hadi ndani ya mahakama hiyo kiasi utulivu katika mahakama hiyo ulionekana na shughuli kuendelea bila bughaa.

Hali kwenye mitaa mbali mbali ya viunga vya jiji la Arusha ilionekana kuendelea na mishughuliko ya kila siku kama kawaida kuliko ilivyokuwa ikionekana huko mwanzo kwenye kesi zilizokuwa zikimkabili mbunge huyo kwa wakazi wa jiji hili kuacha shughuli zao na kuelekea mahakamani kufuatilia kesi ya mbunge huyo.

Magazeti ya leo jumanne ya 30th April 2013




BAADA YA GODBLESS LEMA KUKAMATWA AKIHUSISHWA NA UCHOCHEZI WA FUJO WA WANAFUNZI WA UHASIBU ARUSHA BAADA YA MWENZAO KUUAWA KWA KUCHOMWA KISU HATIMAE GODBLESS LEMA AACHIWA HURU KWA DHAMANA YA MILIONI MOJA

 Mbunge wa Arusha Mjini (Chadema), Godbless Lema,ameachiwa kwa dhamana ya shilingi milioni moja katika mahakama kuu kanda ya Arusha.

TUNDU LISSU AHOJIWA NA RADIO TEHRAN KUHUSU SAKATA LA KUKAMATWA MBUNGE LEMA

Nchini Tanzania sakata la kukamatwa na kuwekwa mahabusu Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema (CHADEMA), kwa madai ya uchochezi, limeibua sura mpya baada ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kutajwa kuwa nyuma ya mkakati huo.

Kwa upande wake Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA)kimelaani hatua hiyo na kulilaumu jeshi la polisi mkoani Arusha kwa kukandamiza upinzani.

Chama hicho kimekwenda mbali zaidi na kulituhumu jeshi la polisi Arusha kwamba, limekuwa likitumikia CCM badala ya kutumikia umma.

HUU NDO UNYAMA WALIOTENDEWA WANAFUNZI WA CHUO CHA UHASIBU ARUSHA

                      Marehemu  Henry  katika enzi za uhai wake....

Mwanafunzi  huyo  Alikuwa Masomoni Mida Ya Usiku Na Alipomaliza Aliondoka Na Kuelekea Maeneo Ya Esami. Kabla Hajafika Eneo La Malazi (Hostel) alipigiwa Simu na Mwenzake amsubiri Ili Waende Wote Hostel.
 
Wakati anamsubiri Rafiki Yake Kwenda Hostel, Kuna Bajaj Ilifika Eneo Hilo Na Watu Hao Wasiojulikana Wakataka Pesa Kutoka Kwa Mwanafunzi Huyo...Wakati  wakiendelea  kuzozana, rafiki  yake  naye  alifika.....
Picha  ya  marehemu  Henry Koga  baada  ya  kuchomwa  kisu  na  kufariki  hapo hapo  katika  chuo  cha  uhasibu  Arusha.....

Majibu Ya Wanafunzi Hao Hayakuwafurahisha Watu Hao Na Ndio Walipochomoa Kisu Na Kumchoma Mmoja wa Vijana Hao Tumboni Na Shingoni na Kupoteza Maisha Hapo Hapo....

Mauaji  hayo  yamesababisha  vurugu  kubwa  chuoni  hapo  zilizopelekea  kupigwa  mawe  mkuu wa  mkoa

"UREMBO SIYO KIPAJI NA SI KILA MWANAMKE MZURI ANAWEZA KUIGIZA"...JACKLINE WOLPER

Muigizaji Jacqueline “Jackie” Wolper amewashangaa wanaodhani kuwa urembo wa mwanamke ni mbadala wa kipaji hasa katika sanaa ya maigizo. Alisema urembo ni moja ya sifa ya mwanamke lakini kamwe hauwezi kumfanya asiye na kipaji kuwa nacho.
 “Ukiwa mrembo ni bora zaidi,kwa kuwa itamfanya avutie kwenye movie,lakini pamoja na hayo ni lazima awe na uwezo wa kuigiza kulingana na kipande husika”alisema Wolper.
 Wolper aliendelea kulalama kuwa kila mtu akijona ana sura ya kuvutia na umbo zuri basi anajua anaweza kuigiza ndio maana matokeo yake wanafanya vitu sivyo na mwisho wake wanaacha fani kabisa.
 Alifafanuwa kuwa kuigiza ni zaidi ya urembo hivyo yeyote ambaye anafikiri anaweza kufanya kazi hii kwa uzuri wa sura na umbo ajaribu kama hakuchemka.

Source: Mwananchi

"SIONI TATIZO KWA LULU MICHAEL KUPIGA PICHA NA PENNY....HUO NI UMBEA WA MAGAZETI"..WEMA SEPETU

Hivi  karibuni  zilisambaa  picha  za  Lulu  Michael  akiwa  katika  picha  ya  pamoja  na  Penny....

Picha  hizo  zilizua  utata  mkubwa  miongoni  mwa  watu  huku  kundi  kubwa  likidai  kuwa  picha  hizo  zimepigwa  makusudi  kwa  lengo  la  kumuumiza  Wema  Sepetu...
 Lulu Michael  akiwa  na Penny

Madai  hayo  yaliandikwa  kwa  kina  na  gazeti  moja  la  udaku  hapa  nchini  likisimulia  ugomvi   uliopo  kati  ya Penny  na Wema Sepetu.....

"SIWAOGOPI MATAIRA WANAONIPONDA....MUNGU PEKEE ANAWEZA NA SI HAO TUMBIRI".....HII NI KAULI YA DIAMOND

Watu kadhaa  wamekuwa  wakimponda Diamond  baada ya  kwenda  LONDONI kwa  madai kuwa ni mshamba  wa  jiji  na  limbukeni ....

Madai hayo yamekuja  baada ya msanii huyu kuanza kuyashobokea  magari ya kifahari kwa kupiga nayo  picha na kuzirusha hewani.....

Baada ya kuona  mizengwe  ya watu imekuwa  mingi, Diamond  ameamua kuwajibu  kwa kupost  jumbe  huu

NAWASHUKURU SANA WADAU WANGU.

Hakika nawashukuru sana wote mliokuwa nami katika kipindi hiki cha kuumwa kwangu mungu awaongezee pale mlipotoa kwa ajili yangu.Pamoja na kwamba sikuweza kutupia vitu humu lakini hamkuacha kuperuzi habari. Nawahakikishia kuanzia sasa kila kitu kitakuwa kama kawaida habari za kumwagaaa.Nawapenda sana Asanteni kwa sapoti yenu.