Monday, March 11, 2013

RAIS KIKWETE AMTUMIA SALAMU ZA PONGEZI RAIS MTEULE WA KENYA

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemtumia salamu za pongezi nyingi Rais Mteule wa Jamhuri ya Kenya, Mheshimiwa Uhuru Kenyatta.

Katika salamu hizo zilizotumwa leo, Jumamosi, Machi 9, 2013, saa chache baada ya kuthibitishwa rasmi kuwa Mheshimiwa Kenyatta ameshinda Uchaguzi Mkuu wa Kenya uliofanyika mwanzoni mwa wiki hii Jumatatu, Machi 4, 2013, Rais Kikwete amemwambia Mheshimiwa Uhuru Kenyatta:

“Mpendwa Rais Mteule na Kaka, ilikuwa ni furaha kubwa kwangu kupokea taarifa ya ushindi wako wa kuchaguliwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Kenya. Niruhusu, kwa niaba ya Serikali na Wananchi wa Tanzania, na kwa hakika, kwa niaba yangu binafsi kukupogenza kwa dhati ya moyo wangu kwa mafanikio haya makubwa ya kuchaguliwa kwako.”

UHURU KENYATTA ACHUKUA KITI CHA URAIS NCHINI KENYA

Mchuano  ulikuwa  mkali  kweli  kweli, lakini  hatimaye  Uhuru Kenyatta ameibuka  mshindi wa  kinyang'anyiri  hicho  kwa  asilimia  50.3  ya  kura  zote  zilizopigwa  huku  Raila Odinga  akijipatia  asilimia 43.28  ya  kura zote

RIPOTI  KAMILI.....

MTOTO wa Rais wa kwanza wa Kenya, Marehemu Rais Jomo Kenyatta, ambaye alikuwa anagombea Urais kwa tiketi ya Chama cha TNA, Uhuru Kenyata ameshinda nafasi hiyo baada ya kumwangusha mpinzani wake Raila Odinga.

Mashabiki wapendekeza albam mpya ya Lady Jaydee iitwe ‘Nothing But the Truth’

Lady Jaydee leo aliwaomba mashabiki wake wamchagulie jina la albam yake mpya ambapo aliwataka wachague kati ya The Queen is Back na Nothing But the Truth. Mashabiki wake wengi wamependekeza jina la albam yake liwe Nothing But the Truth.

Wiki hii Lady Jaydee ameachia wimbo wake mpya aliomshirikisha Profesa Jay, Joto, Hasira. Pia March 3, msanii huyo mkongwe nchini alimalizia kushoot video ya wimbo huo huku muongozaji akiwa ni Adam Juma.Tayari Joto, Hasira unapatikana kwenye mtandao wa itunes.