Tuesday, December 11, 2012

JK: Apokea Majengo Mapya Matatu Ya Huduma Za Mama Na Mtoto

 Rais Jakaya Mrisho Kikwete, Mama Salma Kikwete, Mbunge wa Ubungo Mhe John Mnyika na Balozi wa Korea kwa pamoja wakifungua rasmi jengo la Huduma za Mama na Mtoto katika Hospitali ya Sinza Palestine Kinondoni jijini Dar es salaam leo December 12, 2012
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete, Mama Salma Kikwete, Mbunge wa Ubungo Mhe John Mnyika na Balozi wa Korea kwa pamoja wakikata utepe kufungua rasmi jengo la Huduma za Mama na Mtoto katika Hospitali ya Sinza Palestine Kinondoni jijini Dar es salaam leo December 12, 2012
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete, Mama Salma Kikwete na Balozi wa Korea kwa pamoja wakitembelea sehemu ya chumba cha upasuaji mkubwa chenye vifaa vya kisasa baada ya kufungua  rasmi jengo la Huduma za Mama na Mtoto katika Hospitali ya Mnazi Mmoja Ilala ijini Dar es salaam leo December 12, 2012
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete, Mama Salma Kikwete wakimsalimia mzazi aliyejfungua salama alipofanya ziara baada ya kufungua  rasmi jengo la Huduma za Mama na Mtoto katika Hospitali ya Sinza Palestine Kinondoni jijini Dar es salaam leo December 12, 2012
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipewa saluti alipowasili kufungua rasmi jengo la Huduma za Mama na Mtoto katika Hospitali ya Sinza Palestine Kinondoni jijini Dar es salaam leo December 12, 2012
Rais Jakaya Mrisho Kikwete, Mama Salma Kikwete, Mbunge wa Ubungo Mhe John Mnyika na Balozi wa Korea  pamoja na madaktari na wauguzi katika picha ya pamoja  baada ya kufungua rasmi jengo la Huduma za Mama na Mtoto katika Hospitali ya Sinza Palestine Kinondoni jijini Dar es salaam leo December 12, 2012


Rais Jakaya Mrisho Kikwete, Mama Salma Kikwete na Balozi wa Korea kwa pamoja katika picha ya pamoja na madaktari na wauguzi wa Hospitali ya Mnazi mmoja  baada ya kufungua  rasmi jengo la Huduma za Mama na Mtoto katika Hospitali ya Mnazi Mmoja Ilala ijini Dar es salaam leo December 12, 2012

 (PICHA NA IKULU)

UTAJIRI WA MZEE WA UPAKO NI TISHIO

 MCHUNGAJI wa Kanisa la Maombezi (GRC), Anthony Lusekelo, maarufu kwa jina la Mzee wa Upako ametamba kwamba yeye ni tajiri tishio kuliko watumishi wenzake kwani anamiliki magari sita ya kifahari na nyumba ambayo ina kiyoyozi (AC) Mchungaji wa Kanisa la Maombezi (GRC), Anthony Lusekelo 'Mzee wa Upako'.

Akihubiria waumini wake kanisani hapo juzikati, Ubungo- Kibangu, jijini Dar es Salaam na kuoneshwa na Kituo cha Runinga cha C2C na Channel Ten hivi karibuni, Mzee wa Upako alisema magari yake hayo ya kifahari yote yana viyoyozi na si ya kutoka Japan, akimaanisha ya gharama kubwa zaidi.
“Mimi ndiye Mzee wa Upako, nikitoka nje nakuta magari yote sita yapo, nachagua leo niendeshe hili au lile. Najiambia hapana hili nililiendesha jana, nachukua lingine,” alitamba kiongozi huyo.

 Range Rover Vogue.
“Inawezekana vipi mabomu yapigwe madhabahuni halafu wewe kama mtume na nabii usifanye jambo lolote la Kimungu dhidi ya waliofanya kitendo kile madhabahuni?” alihoji Mchungaji Lusekelo.
Alidai kuwa kuna mitume hapa nchini kazi yao ni kugombania ardhi. “Kama kweli wewe ni mtume na nabii halafu unagombania ardhi ya mashamba na Wazaramo, huo ndiyo utume tulioitiwa? Ndiyo maana hata serikali haitutambui,” alisema Mzee wa Upako huku akishangiliwa na waumini wake.
                                                                        Ford Escape.
Wachambuzi wa mambo wameichambua hesabu hiyo na kugundua kwamba mchunga kondoo huyo hutumia zaidi ya shilingi 25,000,000 kwa mwezi kulipia vipindi hivyo.
Kiongozi huyo ana kanisa kubwa la ghorofa Ubungo Kibangu na mabasi makubwa  kadhaa ambayo hutumika kuwasomba waumini bure kutoka Barabara ya Mandela hadi kanisani kwake.
Hivi karibuni Mzee wa Upako amewahi kuwakemea wachungaji wenzake wa makanisa ya kiroho kwa kujitajirisha kwa kujiita manabii na mitume akidai kwamba kufanya hivyo ni kuwatapeli waumini.

                                                    Land Rover Discovery.
“Magari yote nimeandika kwa jina langu ili niyalipie kodi, situmii mwamvuli wa kanisa kwa kukwepa kodi.”
Aliwaambia waumini wake kuwa kazi yake ni kugawa upako wa baraka za utajiri na kwamba kupitia kanisa lake watu wengi wameneemeka kimaisha.
“Nasisitiza kuwa kila mtu anatakiwa kuwa tajiri lakini utajiri wa halali siyo ule wa kudhulumu, ndiyo maana nasimama hapa kutaja mali zangu, magari hayo si mali ya kanisa ni yangu,” alisema.

                                                                      BMW X5.
Pia aliyachambua makanisa kwa kusema: “Makanisa yetu haya ya kiroho ni hovyo, wameingia matapeli na ninayasema haya kwa kuwa ninayajua, nipo ndani, ndiyo maana najua kitu ninachokisema na mtu akitaka tubishane kwa hoja hii hawezi kunishinda.
“Najua hili ninalozungumza ni jambo zito na sasa ninaposema haya maneno ni sauti ya Mungu mwenyewe inatoka kupitia kinywa changu.”
Mzee wa Upako aliwahi kusema kwamba amekuwa akitumia zaidi ya shilingi 300,000,000 kwa mwaka kwa ajili ya kuendesha vipindi vyake katika runinga na fedha hizo huchangisha kupitia akaunti zake, akasisitiza vipindi vya runingani ni mali yake na si kanisa.
                                                                   Mercedes Benz.
Aliyataja magari hayo kuwa ni Mercedes Benz, Land Rover Discovery, Range Rover Sport, BMW X5, Ford Escape na Range Rover Vogue ambayo Uwazi linatafiti bei zake na kuwapelekea wasomaji siku zijazo.
Aidha, mtumishi huyo wa Mungu aliendelea kutamba kuwa nyumbani mwake mna viyoyozi ‘vikali vya kufa mtu’ na kubainisha kwamba huwa akitoka kwenye gari lenye kiyoyozi anaingia katika nyumba yenye kiyoyozi.
“Mimi nasema hayo kwa sababu ni mlipaji mzuri wa kodi za serikali, sioni sababu ya kuficha mali zangu, kwa nini nifiche?” alihoji na kuongeza:

* MAGARI YANAYOONEKANA PICHANI JUU NI MIFANO YA MAGARI ANAYOMILIKI MZEE WA UPAKO.

MAPENZI NI MAISHA, KUISHI KIMAPENZI KUNARAHISISHA MAENDELEO- 3

HAYAKUISHIA hapo, siku moja Mataba alikutana na Idrisa. Bila woga wala aibu, mzee huyo akaanza kumshambulia kwamba amekuwa tajiri hamthamini, wakati yeye ndiye aliwezesha akasoma. Idrisa akiwa anashangaa, Mataba akamwambia: “Mimi nilikuwa namhonga mama yako fedha ili wewe upate karo na nauli ya kwenda shule.”

Hapo utaona kuwa ubinafsi wa mama yake Idrisa, kusaliti ndoa yake na kwenda kutembea na Mataba, inakuwa taadhira kwa mtoto wake. Anatukanwa, anafedheheshwa kwa makosa ambayo si ya kwake. Tafadhali sana, usijifikirie peke yako, fikiria na kizazi chako.

SHINDA UBINAFSI, KOMESHA UCHAFU
Ukivaa mavazi chakavu, machafu, usijifikirie wewe binafsi, fikiria kuwa mwenzi wako utamuaibishaje kwa muonekano wako usio na mvuto. Huwezi kupinga ukweli kwamba mpenzi wako akiwa amevaa ‘malapulapu’, utaona aibu hata kumtambulisha kwa marafiki zako.

Kama inakuwa hivyo, basi nawe jiwekee utaratibu wa kuvaa vizuri kwa lengo la kumlindia heshima mwenzi wako. Usafi wako ni fundisho kwake, vilevile itakuwa rahisi kumrekebisha. Utawezaje kumrekebisha mwenzio kwamba ni mchafu, ikiwa wewe mwenyewe hutamaniki?

Muonekano wako mzuri ni nguo kwa mwenzi wako au familia yako kama tayari wewe ni baba au mama. Kadiri unavyokuwa msafi, ndivyo heshima yako inavyokuwa juu. Usmati ni sanaa inayoweza kumpa hadhi mtu sehemu yoyote ile.

Matapeli wengi mjini ili kuwaibia watu huvaa vizuri. Ukiwaona utadhani ni maofisa fulani kumbe wezi tu. Kama matapeli wanapendeza angalau nao waonekane ni watu wenye heshima zao ni kwa nini wewe mwenye heshima zako usivae vizuri.
Inawezekana nyumbani kwako wewe ni msafi na unazingatia maadili. Hata hivyo, hayo ni matunda ya ndani kwao, nje pia unapaswa kujiweka vizuri, kwani huko ndiko unakoweza kuheshimiwa na kumpa thamani mwenzi wa maisha yako.

Haina maana kwamba nyumbani ndiyo unaruhusiwa kupaacha vululuvululu. Hapana, nako panahitaji umakini wake. Isiwe kama simulizi za Wakongo, kwamba anaweza kupita barabarani ananukia pafyum za bei mbaya, amevaa dhahabu na nguo za gharama, kumbe nyumbani analalia jamvi au boksi.

Siku zote zingatia kwamba heshima ya mwenzi wako itatokana na wewe mwenyewe unavyoonekana mbele za watu. Wakati mwingine uhusiano wa watu wengi unavunjika kwa sababu ndogondogo mno. Pengine mmoja ni mchafu, kwa hiyo mwenzake akashawishika alipomuona msafi.

Ingawa siku zote nimekuwa nikikutaka umjenge mpenzi wako, kwamba kama unaona ni mchafu na we hupendi alivyo, basi fanya jitihada za kumfanya awe na muonekano mzuri mbele yako na kwa wengine. Nenda madukani ukanunue mavazi ambayo unaona yatamfanya apendeze, hivyo kulinda heshima yako.

Kama mpenzi wako ananuka kikwapa, usimuache akachekwa mitaani. Unayo nafasi ya kumlinda kwa kumfanya badala ya kunuka awe ananukia. Hii ni kwa sababu mnapokuwa wawili, ujenzi wa thamani yenu unategemeana. Unamjenga mwenzako naye anakujenga.
Siku zote tambua kwamba jinsi unavyojiweka kistaarabu ndivyo unavyoweza kutoa sura ya namna ambavyo mwenzi wako atachukuliwa na watu wengine. Mapenzi ni sanaa inayohitaji mtu aishi kwa masilahi ya mwenzi wake. Kwa faida yako, nakuomba uanze utekelezaji wa falsafa hii.

Kuna msemo kwamba ukitaka kumjua mtu muangalie rafiki yake. Hivi ndivyo inavyokuwa.

POLISI MWINGINE AUA KWA RISASI

JESHI la polisi nchini limeendelea kuandamwa na mzimu wa mauaji ya raia wasiokuwa na hatia baada askari mmoja kutuhumiwa kumpiga risasi mwananchi na kusababisha kifo.

 Hali hiyo imejitokeza hivi karibuni katika Kituo cha Polisi cha Ushirimbo Wilaya ya Bukombe mkoani Geita, ambapo askari polisi alimpiga risasi na kumuua kijana aliyefahamika kwa jina la Rashidi Juma (23).

Tukio hilo lilisababisha tafrani kubwa baina ya polisi na wananchi wenye hasira kali kwa kuvamia kituo hicho kwa lengo la kulipiza kisasi kwa kukichoma moto na kutaka askari aliyehusika na mauaji hayo naye auawe.

Hata hivyo, askari walilazimika kutumia nguvu nyingi kwa kurusha mabomu ya machozi, risasi za moto na baridi kwa ajili ya kuwatawanya wananchi hao ambao walikuwa wakirusha mawe kwa lengo la kuwajeruhi askari na  kuharibu mali za kituo hicho.

Chanzo chetu kilidai kuwa tukio hilo lilitokana na askari waliokwenda kumkamata mtu ambaye anadaiwa kuwa ni jambazi, aliyesadikiwa alikuwa amejificha katika nyumba ambayo ipo mtaa wa Kilimahewa mjini Ushirombo na wakafanikiwa kumtia mbaroni.

Hata hivyo, baadhi ya wananchi walilizingira gari hilo huku wakitaka mtuhumiwa huyo ashushwe ili auawe ndipo polisi walilazimika kufyatua risasi kuwatawanya na moja ikampata kijana Rashidi aliyekufa papohapo.

Vurugu hizo zilitulizwa na Mbunge wa Bukombe, Profesa Kulikoyela Kahigi aliyekuwa na Diwani wa Kata ya Igulwa, Soud Ntanyagalla baada ya kuwasihi kutulia wananchi na ndugu wa marehemu akiwemo mama yake mzazi, Justina Francis  kwa maelezo kwamba watalishughulikia suala hilo.

Mbunge na diwani walifika katika Hospitali ya Wilaya ya Bukombe na kukutana na Mganga Mkuu wa Wilaya, Dk. Archard Rwezahura ambaye alithibitisha kuwa kijana huyo aliyepigwa risasi na polisi alifia mikononi mwa polisi.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita, (RPC) Lenard Paul alipoulizwa juu ya tukio hilo alikiri kupata taarifa ya kijana huyo kupigwa risasi na kufa, akaahidi kuwa hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi ya askari aliyehusika.

Na Mwandishi Wetu, Bukombe

Magazeti ya leo Jumanne ya 11st December 2012

PICHA ZA RAY C AKIWA NA RAIS KIKWETE IKULU LEO PAMOJA NA TAARIFA.