Monday, June 25, 2012

BAJETI YA OFISI YA WAZIRI MKUU

 Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akisoma Hotuba ya Bajeti ya Ofisi yake , Bungeni Mjini, Dodoma Juni  25, 2012

Mke wa Waziri Mkuu, Mama Tunu Pinda  akisalimiana na  Mbunge wa Lindi Mjini , Salum Baluany kwnye viwanja vya Bunge Mjini Dodoma Juni 25,2012. Kulia ni Mtoto wa Waziri Mkuu, George Bush.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda  akizungumza na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala  za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Hawa Ghasia  (kulia) na Katibu Mkuu katika Ofisi ya Waziri Mkuu, Peniel Lymo kwenye viwanja vya Bunge Mjini Dodoma Juni 25, 2012.

MLIPUKO WA BOMU ULIOTOKEA MOMBASA KENYA.


Idadi ya waliopoteza maisha kutokana na bomu lililolipuka kwenye baa moja Mombasa Kenya imefikia watatu kwa mujibu wa shirika la msalaba mwekundu ambapo wawili walifariki dunia wakiwa hospitali.

Mlupuko huo umetokea Jericho Beer Garden umbali wa kilomita saba kutoka kwenye mji wa Mombasa siku moja tu baada ya ubalozi wa Marekani Kenya kuonya kutokea kwa mlipuko huo, Standard Media Kenya wameripoti kwamba wengi wa watu hao walikua wanatazama mechi ya England na Italy.

Msemaji wa polisi amesema mlipuko ulitokea kwenye mida ya saa nne usiku wa kuamkia leo ambapo wengi wa waliojeruhiwa walikua nje ya baa hiyo huku shuhuda wa tukio hilo akisema mmoja wa waliofariki alikua kwenye dancing floor.

Inaaminika shambulio hilo linaweza kuwa limefanywa na kikundi cha wanamgambo cha Al Shabaab cha Somalia toka Kenya ilipotangaza nacho vita october mwaka jana.

Tawi la Chadema Washington DC limepokea Mwanachama Mpya Ambae Pia Amezawadia Tawi Hilo Zawadi ya Gari ili Kufanikisha Shuhuli za Chama Hicho

Mwenyeketi wa tawi la Tawi la Chama Cha Demokrasia CHADEMA Washington DC Mhe. Kalley Pandukizi, pamoja na katibu wake Mhe. Libe Mwang'ombe wakimkabidhi rasmi Hussein Kauzel Msabaha kadi ya uwanachama.
Hussein Kauzel Msabaha akiwa na kadi ya Chadema
 Wanachama wa tawi la chadema Washington DC wakipata picha ya pamoja
Hussein Kauzel Msabaha akimkabidhi funguo za gari Mwenyeketi wa Tawi la Chama Cha Demokrasia CHADEMA Washington DC Mhe. Kalley Pandukizi
Mwenyeketi wa Tawi la Chama Cha Demokrasia CHADEMA Washington DC Mhe. Kalley Pandukizi akionyesha funguo za gari ya aina ya Chevy Suburban walilokabidhiwa na Hussein Kauzel Msabaha
 Gari ya aina ya Chevy Suburban walilozawadiwa  Chadema na Hussein Kauzel Msabaha

Tawi la Chama Cha Demokrasia CHADEMA Washington DC lapokea zawadi ya gari aina ya Chevy Suburban kutoka kwa Hussein Kauzel Msabaha, baada ya kukabidhiwa rasmi kadi ya uwanachama mpya wa chama hicho jijini Washington DC

kiongea katika hafla hiyo Mwenyekiti wa Chadema Washington DC Ndugu Kalley Pandukizi amemshukuru sana mwanachama wao huyo mpya na kusema gari hilo litawasidia katika kueneza Sera za Chama kwa Watanzania Wanaoishi Majimbo mengine ya Marekani.

Naye mwanachama huyo mpya amesema amejitolea gari lake hilo litumike kwa kazi za chama kwa Ridhaa yake si kwa kushawishiwa na mtu yeyote kutokana na kukubali Sera za Chadema. Mwenyekiti wa Chadema aliongeza kwa kusema anawaomba Watanzania wote wenye kutaka Mabadiliko waige mfano wa Ndugu Hussein Kauzela kwa kukisaidia Chama kwa hali na mali ili waweze kuzidi kukijenga Chama ambacho Wanachama wake ndio washika Dau wakuu kwenye kukijenga Chama.Picha na Habari na Mdau SwahiliVilla
Mbio za Mt. Kilimanjaro Zatimua Vumbi Mjini MoshiMcheza sinema maarufu kutoka Marekani Deidre Lorenz leo amezipamba mbio za Mt. Kilimanjaro Marathon zilizotimua vumbi kuanzia saa mbili za asubuhi kutoka klabu maarufu ya Moshi hadi Rau madukani. Lorenz alikuwa mmoja wa wakimbiaji zaidi ya 200 kutoka katika nchi za Marekani, Canada, Uingereza, India, Australia, Brazil na Tanzania.

Kushiriki kwa mcheza sinema huyo maarufu wa sinema za Santorini Blue (ambayo ilitegenezwa kwenye fukwe za mahaba za kisiwa cha Santorini nchini Ugiriki), Perfect Strangers, The Big Fight na nyingije nyingi imezifanya mbio za Mt. Kilimanjaro Marathon kuwa na hadhi ya kipekee katika mbio za marathon hapa Afrika.

Mbio hizi zilizoanzishwa na Marie Frances kutoka katika jiji la matajiri la Bethesda nje kidogo ya jiji la Maryland kule Marekani zimetimiza miaka 22 toka zianzishwe mwaka 1991. Mt. Kilimanjaro Marathon zilizishwa baada ya balozi wa zamani wa Tanzania nchini Misri kumwomba Marie Frances kuja Tanzania na kuanzisha mbio zenye hadhi ya kimataifa. Mt. Kilimanjaro Marahon zimeshawahi kushinda tuzo mbalimbaliza kimataifa zilizotolewa na Wonders of the World Magazine ambalo lina wasomaji zaidi ya miloioni 5 na kuzipa nafasi ya pili na wakati gazeti maarufu duniani la Forbes lilizipa nafasi ya kwanza kati ya mbio zinazojulikana kama Seven Continental Races.

Kutokana na kuutangaza mji wa Moshi kwa kiwango kikubwa kimataifa Manispaa ya Moshi ilimpa barabara inayojulikana kama Marie Frances Boulevard pamoja na funguo za Manispaa ya Moshi na Cheti ya ukazi wa kudumu.

Mkimbiaji kutoka jiji la Arusha Getuni Tsekewey aliibuka kidedea wa mbio za kilometa 42 kwa kukimbia kwa saa 2 na dakika 26 nukta 30 wakati Nicodemus Hiiti kutoka Kilimanjaro alikuwa wa 2 kwa kukimbia saa 2 na dakika 38 nukta 20 naye Shauri Habiye kutoka Arusha alikuwa wa tatu kwa kukimbia saa 2 na dakika 38 nukta 24.

Wengine ni Samwel Lucian kutoka Kilimanjaro aliyenyakua nafasi ya 4 kwa kukimbia kwa saa 2 dakika 38 nukta 47 wakati Petro Gimanya wa Kilimanjaro alitimka kwa saa 2 dakika 57 nukta 18 na kushika nafasi ya 5.

Katika mbio za Marathon upande wa wanawake Banuelia Brighton alitimua vumbi na kushika nafasi ya kwanza kwa saa 3 dakika 06 nukta 01 wakati Flora Yada alimfuatia kwa mbali kwa kukimbia kwa saa 3 dakika 38 nukta 08.

Kwa upande wa mbio za nusu marathon wanariadha kutoka Arusha walinyakua nafasi zote. Peter Sule alikimbia kwa saa 1 dakika 07 nukta 42 na kuwa wa kwanza, Mohamed Duley alishika namba mbili kwa kikimbia kwa saa 1 dakika 07 sekunde 98 wakati Said Hassan alitimka kwa saa 1 dakika 10 sekunde 25 na kuwa wa tatu.

Nusu marathon kwa wanawake kulikuwa na mkimbiaji mmoja tu ambapo Farida Guse wa Arusha alikimbia kwa saa 3 dakika 22 sekunde 22.

Mbio za kilometa 10 (10K) ziliwashirikisha wageni tu ambapo kwa upande wa wanaume Sander Markos kutoka Marekani alishika nafasi ya kwanza kwa kukimbia kwa saa 1 dakika 01 sekunde 20 na Malcom Frazer pia kutoka Marekani alikimbia kwa saa 1 dakika 20 sekunde 22 na kuwa wa pili.

Kwa upande wa wanawake mbio za kilometa 10 (10K) kwa wageni Cindy Johanson kutoka Kanada alikuwa wa kwanza kwa kukimbia kwa saa 1 dakika 12 sekunde 22, Marika Johson alishika nafasi ya pili kwa kukimbia kwa saa 1 dakika 20 sekunde 48, Talia Peter kutoka Marekani alikuwa wa tatu kwa kukimbia kwa saa 1 dakika 26 sekunde 04.

Naye mcheza sinema maarufu kutoka Marekani Deidre Lorenz alimaliza mbio za kilomita 42 na kufanya kuwa mbio za tatu za marathon alizowahi kukimbia baada ya zile za New York Marathon mwaka 2010 na 2011.

Lorenz aliondoka na ndege ya shirika la Ethiopia Airlines kurudi kwake "The Big Apple" kama linavyojulikana jiji la New York la Marekani ambapo hufanya shughuli zake za kucheza sinema.

Rais Jakaya Kikwete Alivyompokea Rais wa Jamhuri ya Kiarabu ya Sahrawi, Mohamed Abdelaziz

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimpokea Rais wa Jamhuri ya Kiarabu ya Sahrawi Mhe, Mohamed Abdelaziz katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam jioni ya jana Jumapili Juni 24, 2012
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akibadilishana Mawazo na  Rais wa Jamhuri ya Kiarabu ya Sahrawi Mhe, Mohamed Abdelaziz muda mfupi baada ya kumpokea katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam jioni ya jana Jumapili Juni 25, 2012 ambapo gwaride la Kijeshi na ngoma za utamaduni zilimlaki kwa nderemo.Picha na IKULU

OMOTOLA JALADE NDANI YA BONGO-TANZANIA

Mchezaji wa Filamu kutoka nchini Naigeria Omotola Jalade katikati akiwa katika picha ya pamoja na mwigizaji Wema Sepetu kushoto na Khadija Mwanamboka pamoja na watoto yatima wa kituo cha Tanzania Mitindo House cha jijini Dar es salaam Omotola amekuja nchini maalum kwa ajili ya uzinduzi wa filamu ya Wema Sepetu Super Star ambayo imezinduliwa jana kwenye hoteli ya Hyyat Kilimanjaro jijini Dar es salaam PICHA KWA HISANI YA 8020FASHION

Mohammed Mursi Aibuka Kidedea Uchaguzi Wa Misri

Mursi ameshinda kura kwa asili mia 51.7% akimshinda mpinzani wake wa karibu Ahmed Shafik kwa mujibu wa tangazo la tume ya uchaguzi wa juu wa Rais.

Mkuu wa jopo la Majaji, Farouq Sultan, amesema kua wamezingatia malalamiko 466 kutoka kwa wagombea, ingawa matokeo ya uchaguzi hayatobalika.

Tangazo hilo lilifuatiwa na shangwe na vigelegele katikakati ya medani ya Tahrir mjini Cairo ambako wafuasi wengi wa Bw.Mursi walikua wamekuanyika.

Wafuasi hao wamekaa kwenye medani hio kwa siku kadhaa wakionyesha msimamo wao wa kuchukia sheria kadhaa zilizotangazwa na Baraza la juu la utawala wa majeshi ambayo wanadai zimeundwa ili kupunguza mamlaka ya Rais na kuelekeza uwezo mkubwa kwa majeshi.


Wafuasi wa Bw.Shafiq nao waliweka kambi yao katika eneo la kaskazini mwa mji ambako kuna makao makuu ya Tume ya uchaguzi huko Nasser City.

Akitangaza matokeo ya uchaguzi Jaji Sultan alianza kwa kunena kua tangazo la matokeo ya uchaguzi yalikua yamezongwa na shinikizo pamoja na hali ya wasiwasi.

Tume ya uchaguzi ilizingatia sheria ilipochunguza visanduku vya kupigia kura, na Jaji.Sultan alisema hakuna kilicho juu ya sheria.

Jaji huyo akaongezea kukanusha madai mawili nyeti kuhusu njama za kuibia uchaguzi, kwamba baadhi ya karatasi za kupigia kura ziliwekwa ndani ya visanduku tayari zikiwa na majina ya mgombea wanayemtaka ashinde.

Hatimaye Jaji Sultan akamtangaza mshindi kua ni Bw.Mursi ambaye ni Mwenyekiti wa chama cha Muslim Brotherhood cha Freedom and Justice, Bw.Mursi.

Baada ya dakika kadhaa akitangaza marekebisho kuhusu matokeo madomadogo ya kura ndipo akamtangaza Bw.Mursi kua mshindi kwa kuzoa kura 13,230,131, na Bw.Shafiq akiweza kuzoa 12,347,380, sawa na asili mia 48.27%.
Chanzo: bbc swahili.  http://www.bbc.co.uk/swahili/habari

Magazeti Leo Jumatatu


Magazeti ya leo Jumatatu