Monday, May 20, 2013

HII NDIO HOTUBA YA SUGU ILIYOLETA KIZAAZAA BUNGENI LEO

Msemaji Mkuu wa Kambi Rasmi ya Upinzani-Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Joseph Osmund Mbilinyi (Mb).

MSEMAJI MKUU WA KAMBI YA UPINZANI MHESHIMIWA JOSEPH O. MBILINYI (MB) KUHUSU MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI YA WIZARA YA HABARI, VIJANA, UTAMADUNI NA MICHEZO KWA MWAKA WA FEDHA 2013/2014

(Inatolewa chini ya Kanuni ya 99 (9) ya kanuni za Bunge toleo la mwaka 2013)
1. UTANGULIZI

Mheshimiwa Spika,
Dira ya Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo ni “kuwa na taifa lililohabarishwa vizuri, lina vijana wenye uwezo na malezi bora, linathamini utamaduni wake na linakuwa mahiri katika michezo ifikapo mwaka 2025.” Aidha, ‘dhamira’ ya wizara hii ni ‘kuendeleza utambulisho wa taifa kwa kuwezesha upatikanaji mzuri wa habari, kuwawezesha vijana kiuchumi na kukuza utamaduni na michezo kwa umma kwa maendeleo ya kijamii na kiuchumi.’

HII NDO KAULI YA SUGU ILIYOSABABISHA BUNGE LISITISHWE GHAFLA LEO KUOGOPA UCHOCHEZI

Muda mfupi uliopita spika wa bunge, Anna Makinda amelazimika kusitisha shughuli za bunge mwanzoni tu mwa hotuba ya kambi rasmi ya upinzani iliyokuwa ikisomwa na waziri kivuli wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Joseph Mbilinyi aka Sugu.

Kauli kwenye hotuba hiyo iliyobabisha spika wa bunge asitishe shughuli za leo hadi jioni ilisema,

“Tanzania imegeuka chini ya usimamizi wa wizara ya serikali hii ya CCM kuwa taifa linaloteka nyara wanahabari, kuwatesa, kuwangoa kucha na meno, kuwatoboa macho, kuwamwagia tindikali na hata kuwaua.”Spika amesitisha bunge hilo ili kupata muda wa kuipitia hotuba hiyo kuondoa kauli za uchochezi.

HUYU NDO MBUGE ALIYEDONDOKA BUNGENI

MBUNGE wa Viti Maalumu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema),  Mwanamrisho Taratibu Abama  jana asubuhi aliugua  na  kuanguka ghafla katika viwanja vya Bunge na kukimbizwa hospitali....

Tukio hilo lilitokea wakati akienda  kuhudhuria semina ya wabunge kuhusu  Rasimu ya Sera ya Gesi Asilia kabla ya kukosa nguvu   na  kudondoka  na  kisha kusaidiwa na wenzake  kumkimbiza kwenye zahanati ya Bunge.

Baada ya kupatiwa huduma ya kwanza bungeni, gari la wagonjwa lilimkimbiza Hospitali  ya Mkoa wa Dodoma (General) ambako amelazwa.

Kwa mujibu wa waliomshuhudia, mbunge  huyo  alianza kwa kuishiwa nguvu hali ambayo waliokuwa karibu  walimsaidia kumpeleka kwenye zahanati ambako alitundikiwa dripu  kabla ya kupelekwa  hospitalini.

Kaimu Mganga Mkuu wa  Hospitali ya Dodoma,  Zainabu Chaula alikiri kumpokea mbunge huyo.

PICHA BAADHI ZA MBUNGE WA IRINGA ( PETER MSIGWA )BAADA YA KUONGOZA WANANCHI KUFANYA FUJO


 Mbunge  wa  jimbo la Iringa mjini mchungaji Peter Msigwa akiwasili  eneo la vurugu kabla  ya kuanza kwa  vurugu  hizo
 Machinga  wakisukuma gari ya  mbunge Msigwa

"WANAOCHOCHEA VURUGU ZA KIDINI NI WATU WALIOTUMWA NA MATAIFA YA NJE"..... RAIS KIKWETE

Rais Jakaya Kikwete amebainisha kuwa vurugu za kidini na kisiasa zinazotokea nchini, zina uhusiano na watu wa nchi za nje.

Kikwete alitoa kauli hiyo jana kwenye ibada maalumu ya kuwekwa wakfu kwa Askofu Mkuu wa Sitta wa Kanisa Anglikana Tanzania, Dk Jacob Chimeledya.

Rais Kikwete alikuwa mgeni rasmi kwenye ibada hiyo iliyofanyika kwenye Kanisa Kuu la Roho Mtakatifu.

“Wanaohamasisha vurugu hizo ni watu wenye uhusiano ya karibu na watu wa nje ambao mambo yakiharibika nchini watakuwa wa kwanza kupanda ndege, ilhali wakiendelea kutoa matamko ya uchochezi wakiwa nje ya nchi wakati wengine wakiendelea kuumia,” alisema Kikwete.

WANAWAKE JIJINI MBEYA WAMVAA MCHUMBA WA DR. SLAA BAADA YA KUMKASHIFU MKE WA RAIS KIKWETE

UMOJA wa wanawake  wa chama cha Mapinduzi Mkoani Mbeya(UWT) umemshukia Bi.Josephine Mushumbusi ambaye ni mchumba Katibu Mkuu wa chama cha
Demokrasia na maendeleo CHADEMA kufuatia kauli za udhalilishaji dhidiya Mke wa Rais Mama Salma Kikwete.

Hatua hiyo inatokana  na kauli za kiudhalilishaji zilizotolewa mwishoni mwa wiki na mchumba huyo wa Katibu Mkuu wa Chadema kuwa mama Kikwete ameshindwa kumshauri   Rais ambaye ni mume wake  kuiongoza nchi vizuri .

Kauli hiyo imetolewa jana na Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Mkoa wa Mbeya Bi.Priscilla Mbwaga wakati  akitoa Tamko   kwa waandishi wa habari juu ya Matusi ya wazi yaliyotolewa na Bi.Mushumbusi   kwa Mke wa Rais katika mikutano ya hadhara iliyofanyika Wilayani Mbozi Kata ya Vwawa Mkoani hapa.

Magazeti ya leo Jumatatu ya 20th May 2013