Monday, September 3, 2012

Jeshi La Polisi Launda Tume Ya Kuchunguza Kifo Cha Daudi Mwangosi

JESHI la Polisi nchini limeunda tume itakayochunguza kifo cha Mwandishi wa Habari wa Kituo cha Channel TEN, Marehemu Daud Mwangosi kilichotokea mjini Iringa wakati Jeshi la Polisi likipambana na wafuasi wa Chadema waliokuwa katika ufunguzi wa tawi la chama hicho katika Kijiji cha Nyololo mjini Iringa.

Kamishna wa Operesheni wa Jeshi la Polisi Paul Chagonja uchunguzi huo utavishirikisha vyombo vya usalama kutoka Jeshi la Polisi pamoja na Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) 'kuwa Jeshi la Polisi limeunda tume  itakayowahusisha Maofisa kutoka Jeshi la Wananchi wa Tanzania JWTZ pamoja Mkurugenzi wa Makosi ya Jinai Robert Manumba, Inspekta Jenerali wa Polisi (IGP), Said Mwema ili kubaini ukweli kuhusu kiliochosababisha kifo cha mwandishi huyo basi tusubiri matokeo ya uchunguzi huo' alisema Chagonja.

Marehemu Mwangosi amefariki dunia jana wakati baada ya kulipukiwa na kitu kinachachodaiwa kuwa ni bomu wakati chama cha Demokrasia na Maendelo (Chadema) kikifungua tawi la chama vchake katika Kijiji cha Nyololo mjini Iringa.

Francis Dande, HabariMseto blog

PICHA ZA TUKIO LA MWANDISHI KUUWAWA IRINGA,


                                       Gari la Chadema lililovunjwa kioo wakati wa vurugu

          Mwandishi David mwenye sweta la rangi ya udongo akipiga picha nusu saa kabla ya kifo chake.
                                   TAHADHARI, kuna picha ya kutisha kwenye Hapa Chini.
                                 Mwili wa Marehemu Daudi ukiwa chini baada ya kulipukiwa na bomu.
                                                       Marehemu Daudi,

REAL MADRID! imemchukua mkali wa soka kutoka Chelsea



                             Essien akiwa na kocha wa Real Madrid Jose Mourinho.
Club ya Real Madrid ya Hispania  imemchukua mkali wa soka kutoka Chelseakwa mkopo wa msimu mmoja Michael Essien ambae ni mzaliwa wa Ghana .

Essien ana miaka 29 tu toka aanze kupumua lakini ana miaka 12 tu toka aanze soka.. alianza kwa kuichezea Bastia kuanzia 2000 – 2003 na kuifungia magoli 11, 2003-2005 akaingia Lyon aliyoifungia magoli 8, 2005akaingia Chelsea aliyoifungia magoli 17 mpaka 2012 ambapo sasa amekwenda Real Madrid kwa mkopo.

PICHA ZA WAZIRI MKUU WA ETHIOPIA MELES ZENAWI UNAAGWA JUMAPILI.












Magazeti ya leo Jumatatu 3rd September 2012