Wednesday, May 22, 2013

NYUMBA YA MWANDISHI WA HABARI WA TBC YACHOMWA MOTO HUKU MABOMU YAKIRINDIMA HUKO MTWARA

Hali imezidi kuwa mbaya katika Mji wa Mtwara na hivi punde watu wanaendelea kufanya uharibifu katika maeneo mbalimbali ya mji huo.

Jengo moja ambalo linadaiwa kumilikuwa na CCM limechomwa moto katika eneo la Majengo na daraja linalounganisha Lindi na Mtwara limevunjwa.

Mbali na hayo pia nyumba ya mwandishi wa habari wa Shirika la Utangazaji la Tanzania (TBC)imechomwa moto.

Katika Mji wa Mtwara milio ya mabomu na risasi ndio inayosikika kila kona. Jeshi la Polisi linajaribu kuwadhibiti vijana  na watu wengine ambao wanafanya vurugu hizo.

VURUGU ZA MTWARA ZASABABISHA BUNGE LIAHIRISHWE....

Spika wa bunge , Anne Makinda ameahirisha Bunge kutokana na hali ya Mtwara na ameiagiza serikali kuwa kesho wawasilishe taarifa bungeni kuhusiana na hali hiyo.

Makinda ameitisha kamati ya uongozi ili kuona kama wanaweza kutuma kamati ya Bunge kesho kwenda huko.

HALI NI MBAYA MKOANI MTWARA....MABOMU NA RISASI VIMETAWALA, HUDUMA ZA KIJAMII ZIMESTISHWA

Hali ni tete na hakuna amani, mabomu ya machozi yanarindima muda huu na huduma zote za kijamii zimefunngwa hakuna usafiri, masoko, maduka na bar zote zimefungwa, daladala, Taxi na Bodaboda hazifanyi kazi. 

Kwa ujumla kinachoendelea ni mapambano makali kati ya Jeshi la polisi na wananchi wenye hasira wanaopinga vikali kuendelea kwa mchakato wa gesi ilihali nchi ikiwa haina sera inayosimamia nishati hiyo.

Kufuatia Kambi ya Upinzani kuukataa mpango wa serikali wa ujenzi wa bomba la gesi kutoka Mtwara Mpaka Dar es salaam ilihali Waziri wa Nishati akisoma hotuba yake kwa hisia kali na mbwembwe na kusema bomba la gesi linajengwa kutoka Mtwara kwenda Dar es salaam Wananchi wa Mtwara walicharuka!

 Daraja la Mikindani limevunjwa hakuna mawasiliano Mtwara na Dar es salaam.

Baadhi ya Wananchi wamepora Silaha na wanazitumia kujibu mashambulizi ya Jeshi la Polisi (habari haijathibitishwa rasmi)

 Jengo la Ofisi ya CCM saba saba limechomwa moto.
Lodge/Hotel (Shengena) inayoaminika kwamba ndiyo waliyofikia Askari wa Jeshi la Polisi (FFU) kutoka mikoa ya jirani kwaajili ya operation inayoendelea imechomwa moto.
 

Washirika sita wa ‘polisi wa bangi’ wakamatwa wakiwa na magunia 30

                 Kamanda wa Polisi mkoani Arusha Leberatus Sabas akionyesha bangi iliyokamatwa 

“Siku za karibuni tulipata taarifa kutoka kwa raia wema kwamba kuna mtandao wa wahalifu wanaoshirikiana na baadhi ya polisi wasiyo waaminifu,” alisema Kamanda Sabas.

Arusha. Polisi mkoani Arusha, imekamata magunia mengine 30 ya dawa za kulevya aina ya bangi kwa watu sita ambao inadaiwa ni washirika wa polisi wawili, waliokamatwa na magunia 18 ya bangi katika maeneo ya Himo mkoani Kilimanjaro.

Kamanda wa Polisi mkoani Arusha, Liberatus Sabas akizungumza na waandishi wa habari jana, alisema watuhumiwa hao, walikamatwa Mei 19 saa 10 jioni katika Kijiji cha Kisimiri juu, Kata ya Ngaramtoni wilayani Arumeru.

BREAKING NEWS: GESI YA MTWARA KIMENUKA

 Habari zilizotufikia kutoka Mtwara zinaeleza kuwa kumeibuka vurugu ambazo zimepelekea mabomu ya machozi na risasi za moto kutumika baada ya Bajeti ya Wizara ya Nishati na Madini kusomwa bungeni na kueleza kuwa mradi wa gesi Mtwara utatekelezwa bila kutaja faida za moja kwa moja watakazozipata wananchi hao. Inadaiwa kuwa kwa sasa kauli mbiu ya wananchi walio katika maeneo hayo ni  "Gesi haitoki hata kwa bomba la peni". Inaelezwa kuwa kituo cha mafuta cha Total kimechomwa moto wakati wa vurugu hizo. Katika kukabiliana na vurugu hizo, inadaiwa polisi kutoka Masasi na Lindi wapo eneo hilo kuongeza nguvu. Taarifa zaidi zitawajia hivi punde

Magazeti ya leo Jumatano y 22nd May 2013




GODBLESS LEMA AUMBUKA....VODACOM WADAI KWAMBA ULE UJUMBE WA VITISHO HAUKUTOKA KWA MKUU WA MKOA

KAMANDA wa Polisi wa Mkoa wa Arusha, Liberatus Sabas, amedai kuwa uchunguzi wa awali kuhusu ujumbe unaodaiwa kutumwa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Magesa Mulongo, umetumwa na mtandao wa simu wa nje ya nchi.

Kamanda alisema katika ujumbe huo ambao Lema anadai uliandikwa na Mkuu wa Mkoa Mulongo na kutumwa kwenye simu yake Aprili mwaka huu, uchunguzi wa polisi umeonyesha kwamba haukutumwa kupitia kampuni moja wapo ya simu za mikononi ya hapa nchini.

“Katika kipindi cha mwishoni mwa Aprili mwaka huu, vyombo vingi vya habari vikiwemo radio, magazeti na mitandao ya kijamii viliandika na kutangaza habari iliyoelezea shutuma zilizotolewa na Mbunge Lema kuwa aliandikiwa ujumbe wa vitisho kwa njia ya simu na Mkuu wa Mkoa Mulongo na ulisomeka:

TUNDU LISSU NA ANNE KILANGO NUSURA WACHAPANE MAKOFI BUNGENI

Baada ya Bunge kuahirishwa jana, nje ya ukumbi hali haikuwa nzuri baina ya Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu na Mbunge wa Same Mashariki (CCM), Anne Kilango Malecela.

Mtafaruku huo uliibuka baada ya Kilango kusikika akimtuhumu Lissu kwa uchochezi, akisema kwamba amekuwa mbunge pekee anayeongoza kwa vurugu.

Maneno hayo hayakumfurahisha Lissu ambaye alishindwa kuvumilia na kumgeukia Kilango kwa nguvu huku baadhi ya wabunge wakishuhudia na wengine wakimzuia Lissu.

UJIO WA RAIS OBAMA NCHINI TANZANIA

Rais wa Marekani Bw. Baraka Obama na Mkewe wanatarajia kufanya ziara ya nchi tatu barani Afrika itakayojumuisha nchi za Senegal, Afrika ya Kusini na Tanzania, Kuanzia tarehe 26 Juni hadi tarehe 3 Julai.

Katika ziara yake hiyo, Rais atawekea mkazo umuhimu ambao Marekani inauweka katika ushirikiano wetu wa kina na unaoendelea kuimarika na nchi za Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara kupitia mipango mbalimbali ikiwemo ile ya kuimarisha ukuaji wa uchumi, uwekezaji na biashara, uimarishaji wa taasisi za kidemokrasia na uwekezaji katika kizazi kipya cha viongozi wa Kiafrika.

Rais atakutana na viongozi mbalimbali wa kiserikali, sekta binafsi na jumuiya huru ya kiraia ikiwemo vijana ili kujadili ubia wetu wa kimkakati katika ushirikano wetu rasmi na masuala mengine ya kimataifa.

Ziara hii itadhihirisha dhamira ya dhati ya Rais ya kupanua na kuimarisha ushirikiano kati ya Marekani na watu wa nchi za Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara katika kuimarisha amani na ustawi katika kanda hii na duniani kote kwa ujumla

PROFESA JAY AJIUNGA NA CHADEMA TAYARI KWA KUENDELEZA MAPAMBANO YA KISIASA KAMA MKONGWE SUGU

 Rapper mkongwe nchini, Joseph Haule aka Profesa Jay amejiunga rasmi na Chama cha Demokrasia na Maendeleo, CHADEMA.
Profesa amekabidhiwa kadi ya uanachama wa CHADEMA na mbunge wa Mbeya mjini, Joseph Mbilinyi aka Sugu.

Kujiunga rasmi kwa Profesa kwenye chama hicho kunaashiria kuwa huenda akawa na nia ya kugombea ubunge kwa tiketi ya chama hicho mwaka 2015.
Profesa ameamua kuweka wazi uamuzi wake baada ya watu wengi kuanza kumuuliza maswali. “Mmeniuliza sana kwamba mimi ni CHAMA gani jibu litapatikana Muda sio mrefu!! Still in Dodoma STAY TUNED,” alitweet.

Rapper huyo anayejulikana kama mchawi wa rhymes yupo Dodoma pamoja na wasanii wengine akiwemo Lady Jaydee kwa mwaliko wa Sugu