Monday, July 16, 2012

Patrin Kibello azikwa huko Boston.

Marehemu Patrin Kibelloh aliyefariki ghafla siku ya Jumanne July 10,2012. na kuzikwa Ijumaa july 13 huko kwenye makaburi ya Gardner, West Roxbury Massachussets hapa Marekani.
Baadhi ya ndugu na marafiki waliohudhuria katika msiba huko nyumbani kwake Saugus, Boston Massachussets.
Marehemu Patrin Kibelloh akizikwa. Marehemu alipata mafunzo katika Institute of proffesional & Restaurant mjini Boario nchini ITALY alizaliwa April 25,1963 nchini Tanzania na ameacha mke na watoto wawili akiwa na umri wa miaka 49. Mwenyezi Mungu ailaze roho yake pahala pema peponi Amen. (Picha zote na swahilivilla.blogspot.com)

Mkurugenzi Mkuu Tanesco asimamishwa

Mkurugenzi Mkuu Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), Mhandisi William Mhando amesimamishwa kazi na Bodi ya Wakurugenzi ya shirika hilo kuanzia jana.Kwa  mujibu wa taarifa iliyotolewa na Bodi ya Wakurugenzi  na kusainiwa na Mwenyekiti wake, Jenerali Mstaafu Robert Mboma, Mhando amesimamishwa kazi pamoja na watendaji wakuu wengine wa Tanesco ili kupisha uchunguzi wa tuhuma za ubadhirifu na matumizi mabaya ya madaraka.

Kwa mujibu wa Mwananchi viongozi wengine wa Tanesco waliosimamishwa  kazi ni Naibu Mkurugenzi Mtendaji Huduma za Shirika, Robert Shemhilu, Ofisa Mkuu wa Fedha Lusekelo Kassanga na Meneja Mwandamizi, Manunuzi Harun Mattambo.
Hata hivyo, Mhando alisema kupitia Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC 1) jana kuwa hana taarifa zozote kuhusiana na kusimamishwa kwake.

Ingawa  taarifa hiyo ya Mboma haikueleza nani anakaimu nafasi iliyoachwa wazi na Mhando, lakini habari tulizopata kutoka vyanzo vyetu ndani ya Wizara ya Nishati na Madini na Tanesco zinasema Kaimu Mkurugenzi Mkuu Mtendaji atakuwa Felschami Mramba ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa Masoko na Usambazaji wa Tanesco.Kusoma zaidi bofya

Hatua hiyo imetangazwa jana jijini Dar es Salaam kufuatia  kikao cha dharura cha Bodi ya Wakurugenzi ya Tanesco kilichofanyika  Julai 13 mwaka huu, ambacho kilijadili tuhuma mbalimbali dhidi ya menejimenti ya Tanesco.
Taarifa hiyo fupi imeeleza  kuwa tuhuma dhidi ya Mhandisi Mhando ni nzito hivyo ni vyema zifanyiwe uchunguzi huru na wa kina.

“Hivyo, Bodi  iliazimia pamoja na mambo mengine kama ifuatavyo: Uchunguzi wa tuhuma hizo uanze mara moja kwa kutumia uchunguzi huru na kumsimamisha kazi Mkurugenzi Mtendaji wa Tanesco, Mhandisi William Mhando ili kupisha uchunguzi huo na kwa kuzingatia matakwa ya sheria za kazi nchini,” inaeleza sehemu ya taarifa hiyo.
Mboma alibainisha bodi yake kufanya kikao kingine cha dharura jana Julai 14, na kuamua kuwasimamisha kazi watendaji hao mara moja ili kupisha uchunguzi huo.

“Pamoja na uamuzi huo, Bodi imechukua hatua stahiki za kuhakikisha kwamba shughuli za utendaji na uendeshaji wa Tanesco zinaendelea kama kawaida,” imesema taarifa hiyo.

Awali saa 11 jioni jana waandishi wa habari walijazana katika Ofisi ya Wizara ya Nishati na Madini iliyopo Mtaa wa Ohio, ambapo hawakufanikiwa  kuwaona wakurugenzi hao waliokuwa kwenye kikao huku wakitakiwa kuondoka eneo hilo na kusubiri kwa mbali.

Waandishi hao walilazimika kusubiri kwa takriban saa nzima ndipo alipotokea Ofisa Habari wa Wizara ya Nishati na Madini aliyetambuliwa kwa jina la Fadhili Kileo na kugawa nakala ya taarifa ya kikao hicho huku wakurugenzi hao wakipanda magari yao na kuondoka bila ya kuzungumza  na waandishi hao hali iliyowakera waandishi.

“Jamani naomba mtusamehe sana, hii siyo kawaida yetu, imekuwa ni dharura tu ndiyo maana mnaona wakurugenzi wanaondoka,” alisema Kileo akiwasihi waandishi wa habari waliokuwa wakilalamika.
Wakati hayo yakiendelea, Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Eliakim Maswi naye alikataa kuzungumza na waandishi wa habari akisema kuwa hahusiki.

“Hapana mimi sihusiki, nendeni kwa hao viongozi waliokuwa kwenye kikao,” alisema  Maswi.
Mhando aliteuliwa kuwa Mkurugenzi wa Tanesco kuanzia tarehe 1 Juni, 2010.

Baada ya uteuzi huo, Mhando alisema atahakikisha wateja wote wa Tanesco wanakuwa na mita za Luku.
Kabla ya uteuzi huo, Mhando alikuwa ni Meneja Mkuu Usambazaji Umeme na Masoko katika shirika hilo.
Mhando alichukua nafasi ya aliyekuwa Mkurugenzi wa shirika hilo, Dk Idris Rashid ambaye alimaliza muda wake wa uongozi.

Wasifu wa Mhando
Mhando aliajiriwa na Tanesco mwezi Oktoba mwaka 1987 kama Mhandisi wa Umeme na baadaye alipandishwa na kuwa Mhandisi katika njia za umeme. Mwaka 1990 hadi 1992 aliteuliwa kuwa Meneja wa Tanesco Mkoa wa Singida.

Mwaka 1992 hadi 1994 alikuwa Meneja wa Mkoa wa Tanesco, Mkoa wa Mbeya. Alipandishwa cheo mwaka 1995 na kuwa Mkurugenzi wa Kanda ya Kusini Magharibi hadi mwaka 1999.

Ana elimu ya Shahada ya Uzamili (Masters) katika masuala ya umeme aliyoipata mjini Havana nchini Cuba mwaka 1987, pamoja na mafunzo mengine aliyoyapata katika vyuo mbalimbali ndani na nje ya nchi.

Kwa muda mrefu Tanesco imekuwa katika matatizo mbalimbali ya kiutendaji na utoaji huduma yaliyosababisha taifa kuingia katika mgawo wa umeme na kudhoofisha maendeleo na ukuaji wa uchumi.

Matatizo hayo ni pamoja na uchakavu wa mitambo ya Tanesco, hujuma za miundombinu na kuingiwa kwa mikataba mibovu.

Akijibu maswali ya waandishi wa habari katika mkutano wa kutoa ufafanuzi juu ya taarifa iliyotolewa na Kamati ya Hesabu za Mashirika ya Umma(POAC), kuwa kuna ubadhirifu ndani ya Tanesco  Mei 7, mwaka huu, Mhando alisema ikigundulika kuna ubadhirifu wowote uliofanyika katika shirika hilo kutokana na Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali(CAG) basi atakuwa tayari kujiuzulu.

Taarifa ya POAC ilisema shirika hilo lilifanya ununuzi wa kati ya Sh300 bilioni hadi Sh600 bilioni lakini Mhando alisema kuwa si kweli.

”Kama nimekosea niko tayari kujiuzulu na mwajiri akiamua kunihamisha sina tatizo na ninawaambia mimi sina miaka miwili kazini na shirika linapata hati safi hilo mwelewe na mliseme,” alisema Mhando.

Dlamini – Zuma ampiku Ping Addis Ababa

NKOSAZANA Dlamini-Zuma, kutoka Afrika Kusini, ameshinda uchaguzi mkali kuwa kiongozi mpya wa Tume ya Muungano wa Afrika. Bi Nkosazana Dlamini-Zuma, alimshinda kiongozi wa Tume hiyo anayeondoka Jean Ping wa Gabon, katika uchaguzi mkali uliopigwa mara kadhaa.

“hivi sasa tunaye kiongozi wa Tume ya Muungano wa Afrika Madam Zuma, ambaye sasa ataongoza siku za usoni za taasisi hii,” ndivyo alivyosema Rais wa Benin Thomas Boni Yayi ambaye pia ni mwenyekiti wa Muungano wa Afrika AU.

Dlamini-Zuma, mwenye umri wa miaka 63, ni balozi mwenye ujuzi na alikuwa mstari wa mbele katika kupigania uhuru nchini Afrika Kusini wakati wa Ubaguzi wa rangi. Yeye ni daktari wa mwanadamu na amewahi kuhudumu kama Waziri wa Afya, Maswala ya Nchini na waziri wa Mashauri ya nchi za Kigeni nchini Afrika Kusini.
Zuma ampongezab Dlamini

Mumewe wa zamani, ambaye pia ni kiongozi wa Afrika Kusini, Jacob Nzuma, alikuwa miongoni mwa watu wa kwanza kumpongeza kwa ushindi huo baada ya kura kupigwa katika mji mkuu wa Ethiopia, Addis Ababa.

Rais Zuma alisema; “Ushindi huu ni ufanisi mkubwa kwa Afrika, bara zima, umoja na mafanikio kwa wanawake ni muhimu sana.”

Ushindi wa Dlamini-Zuma umepatikana miezi sita tangu aanze juhudi za kumtimua mwenyekiti wa tume hiyo anayeondoka, Jean Ping. Katika mkutano kama huo kura ilipopigwa hakuna mmoja kati yao aliyepata thuluthi mbili ya kura kumwezesha kunyakua uongozi huo.

Iliamuliwa kuwa Ping aendelee kushikilia cheo hicho hadi usiku wa kuamkia leo aliposhindwa na Dlamini-Zuma. Rais Yoweri Museveni alishangilia kwa kusema: “huyu ni mpiganiaji Uhuru na si balozi wala kiongozi vivi hivi.”

Msemaji wa Ping, Noureddine Mezni, alisema Bwana Ping alimpongeza Madame Dlamini-Zuma na kumtakia kila la heri katika kazi yake mpya.

JACQUELINE ABADILI DINI

MUIGIZAJI nyota wa filamu nchini Jacqueline Massawe ambaye ni maarufu kwa jina la WOLPER amesisitiza kwamba amebadili dini na kwa sasa anajiandaa kwa kuupokea na kufunga mwezi mtukufu wa Ramadhani.

Akizungumza katika chombo kimoja cha habari Luninga WOLPER amesisitiza kwamba yeye hivi sasa ni muislamu na amejitayarisha kufunga na kujizuia kufanya shughuli za kisanii ambazo zitamsababishia kutengua saum yake hivyo kwa kipindi hicho cha muda wa mwezi mmoja atakuwa akijishughulisha na kazi zake zingine.

"Unajua dini ni imani na hii iko ndani ya moyo wangu hivyo nachukizwa kwa kitendo cha baadhi ya ndugu zangu wa karibu kuniita MALAYA na hukumu kwa mambo mbalimbali mimi ndiyo najua na fanya nini katika maisha yangu"alisema.

Aidha amewatupia dongo wale wote wanao mmtupia maneno ya kumdhihaki kwamba hatoweza kufunga na kuswali , "Unajua tumepewa miezi 11 ambayo tuko huru kufanya mambo mbalimbali ya starehe za kidunia kwanini nishindwe kujizuia ndani ya mwezi mmoja tu, mimi nasema hivi  nitasali sitakuwa na makucha , manywele  na mambo mbalimbali ambayo hayapendezi katika ibada "

TAMKO LA CHADEMA KUHUSU VURUGU ZILIZOTOKEA MKOANI SINGIDA JUMAMOSI

 CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO (CHADEMA)
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Tamko Kuhusu Yaliyojiri Katika Mkutano wa Hadhara wa CHADEMA Uliofanyika Kata ya Ndago Siku ya Jumamosi Tarehe 14 Julai 2012

1. Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kiliandaa mikutano ya  hadhara katika Jimbo la Iramba Magharibi. Mikutano hiyo ilitolewa taarifa polisi na jeshi hilo lilitoa baraka zake kama utaratibu wa sheria unavyotaka kwa barua yake ya tarehe 12 Julai 2012 Kumb. Na. KIO/ B1/1/VOL.V/268

2. Mkutano wa kwanza ulipangwa kufanyika katika Kata ya Ndago katika  viwanja vilivyo karibu na kituo cha mabasi ambapo pia ni hatua chache karibu kabisa na Kituo cha Polisi Ndago. Mkutano huu ulipangwa kuanza saa nane mchana.

3. Msafara wa kitaifa unaofanya ziara ya ukaguzi wa chama, katika mkoa  wa Singida chini ya uratibu wa Ofisa wa Sera na Utafiti Makao Makuu, Mwita Mwikwambe Waitara, (ikiwa ni maandalizi ya operesheni nyingine kubwa mkoani humo itakayofanyika baadae), uliwasili katika eneo la  Mkutano majira ya saa tisa na nusu alasiri. Tulikuta wananchi wengi wakiwa wanatusubiri. Kabla ya Mkutano kuanza tulipewa taarifa kwamba kuna kikundi cha vijana kimeandaliwa kuvuruga mkutano wa CHADEMA kwa kufanya fujo, ikiwemo kurusha mawe ili mkutano huo usifanyike. Suala hilo lilielezwa mkutanoni mapema na Mheshimiwa Waitara, mbele ya askari polisi.

4. Wakati tukijiandaa kuanza hotuba, vijana wapatao wanane walianza chokochoko kwa kutoa matusi na punde mawe yakaanza kurushwa kutoka sehemu mbalimbali. Wakati fujo zinaanzishwa na kile kikundi, Mheshimiwa Waitara alikuwa bado anazungumza na wananchi kuwaandaa kusikiliza wazungumzaji wengine. Vurumai hiyo ilizimwa na wananchi wenyewe wa Ndago waliokuwa na hamu ya kusikiliza ujumbe wa viongozi wa kitaifa wa CHADEMA.

5. Kwa kweli tunawashukuru wananchi wengi wa Ndago walioonesha ujasiri  mkubwa kuweza kuwaondoa vijana wale eneo la mkutano, kisha mkutano ukaendelea, huku wananchi wakionesha kila hamasa ya kufurahia hoja kutoka kwa wazungumzaji, akiwemo Mheshimiwa John Mnyika, ambaye aliombwa ahudhurie ziara hiyo kwa nafasi yake ya Mkurugenzi wa Habari na Uenezi wa CHADEMA.

6. Mpaka tunamaliza mkutano huo ambao wananchi waliufurahia sana kwa  namna ulivyohutubiwa kwa amani na utulivu huku wazungumzaji wakijenga hoja juu ya mstakabali wa jimbo na taifa lao kwa ujumla, mamia ya wananchi waliohudhuria walitaka tuendelea kuhutubia, lakini tulibanwa na ratiba ya kuwahi mkutano wa pili, eneo la Kinampanda.

7. Lakini kutokana na vurugu hizo zilizokuwa zikisababishwa na kikundi  cha vijana ambao tayari ilishatolewa taarifa yao kwenye mkutano huo, lakini askari waliokuwepo hawakuthubutu kuchukua hatua, tulilazimika kuomba msaada kutoka kwa OCD na R.P.C, ambapo baadae wakati mkutano unakaribia kuisha tuliona gari la polisi kutoka Mjini Singida likiwa na askari waliojipanga rasmi kwa ajili ya kuzuia vurugu likifika pale eneo la mkutano, lakini wakati huo hali ilishatulia na hotuba zimetolewa vizuri.

8. Kutokana na hali hiyo ya vurugu, zilitolewa taarifa Kituo cha  Polisi cha Ndago, ambapo lilifunguliwa jalada NDG/RB/190/2012. Katika jalada hilo tulitaja baadhi ya majina ya watuhumiwa waliokuwa vinara wa kundi lililokuwa likifanya fujo kwenye mkutano mbele ya askari polisi. Majina hayo ni; 1. Daniel Sima, 2. Tito Nitwa, 3. Bakili Ayubu, 4. Yohana Makala Mpande, 5. Ernest Kadege, 6. Abel John, 7. Athuman Ntimbu, 8. Martin Manase, 9. James Ernest, 10. Simion Makacha, 11. Anton John, 12. Frank Yesaya

9. Kwa hakika askari polisi wa Ndago waliokuwepo mkutanoni mbali ya  kutochukua hatua yoyote dhidi ya fujo tulizofanyiwa ikiwemo kupondwa mawe na kikundi kidogo cha wahuni, fujo zilipozidi askari wote walikimbia eneo la mkutano, akabaki OCS pekee ambaye naye alionekana dhahiri kutotaka kuchukua hatua stahili. Hakuonekana kufanya juhudi zozote za kuhakikisha amani inalindwa na ulinzi unaimarishwa katika eneo la mkutano na hatua zinachukuliwa dhidi ya watu walioonekana kudhamiria kufanya fujo.

 Mtu yeyote makini angeweza kuona kuwa askari wale walikuwepo pale mkutanoni ‘almuradi’ tu lakini kama vile walikuwa na maelekezo maalum ya kuhakikisha hawachukui hatua yoyote katika kuzuia mpango wowote wa kusababisha vurugu na kuvunja amani.

10. Baada ya kumaliza mkutano wa Ndago kwa amani, tulikwenda  Kinampanda ambako tulifanya mkutano mwingine mzuri kwa amani kabisa, ambapo mbali ya wananchi kuwa wametusubiri kwa hamu kubwa na kutusikiliza kwa makini hoja zetu, polisi katika eneo hilo walitupatia ushirikiano mzuri tangu wakati tunafika mpaka tulipomaliza mkutano
huo.

11. Jioni wakati tumerudi hotelini, tukasikia kuna taarifa  zinasambazaa kuwa kuna mtu/watu wamekufa katika eneo la Ndago. Habari hizo zilikuwa zinakanganya kwa sababu zilikuwa zikitaja idadi tofauti tofauti. Lakini kwa vyovyote vile kama ni kweli kuna tukio la mtu kufariki, CHADEMA tunasikitika sana kwa tukio hilo la uhai wa mtu.

12. Tunalaani taarifa zinazozidi kusambazwa ambazo zinawataja polisi  kuwa wanatuhusisha CHADEMA na tukio la mtu aliyefariki. Hii ni ajabu kubwa kwamba tumetoka kwenye mkutano ule kwa amani kabisa mpaka tumemaliza mkutano wa pili kwa amani na polisi wakiwepo sehemu zote mbili, kisha tunasingiziwa masuala ambayo wenyewe hatukuwa na habari nayo tangu mkutano wa kwanza ukiwa unaendelea mpaka mkutano wa mwisho ulipomalizika.

13. Kutokana na habari hiyo ya kifo cha mtu inavyoenezwa kwa  kuihusisha CHADEMA, tumebaini kuwepo kwa mbinu na mikakati ya chama tawala pia vyombo vya dola vikihusika kutaka kuwatisha wananchi waSingida, Watanzania wote wapenda mabadiliko na viongozi wa CHADEMA katika mkoa huu, wasifanye kazi ya kisiasa kwa kuwabambikizia tuhuma na kesi na pia kuwafanya waonekane ni watu wa vurugu.

14. Tunapenda kusema hapa kuwa njama hizo hazitafanikiwa. Zitashindwa  kama zilivyoshindwa njama zingine zote ambazo zimekuwa zikifanywa na vyombo vya dola, viongozi wa serikali na chama tawala dhidi ya CHADEMA na vuguvugu la mabadiliko nchini.

15. Tunawataarifu wananchi kuwa ratiba ya kufanya Operesheni nyingine  kubwa katika Mkoa wa Singida, ikiongozwa na Katibu Mkuu, Dkt. Willibrod Slaa, itafanyika baadae kama ilivyoazimiwa na kikao cha Kamati Kuu.

Ofisa wa Sera na Utafiti CHADEMA Makao Makuu

MKUU WA MKOA WA ARUSHA AWATAKAWANANCHI KUJITOKEZA KATIKA SENSA ILI WACHANGIE MAENDELEO

MKUU wa mkoa wa Arusha Magesa Mulongo amewataka wananchi wa mkoa wa Arusha kuhakikisha kuwa wanajitokeza na kutoa ushirikiano katika zoezi la Sensa kwani sensa ndio chanzo cha Serikali kusaidia jamii
Mulongo aliyasema hayo jijini Arusha leo wakati akifungua mafunzo kwa wakufunzi zaidi ya 100 wazoezi hilo la Sensa  ambalo lintarajiwa kuanza hivi karibuni

Mkuu huyo alisema kuwa kila mwananchi wa mkoa wa Arusha anapaswa kujua na kutambua kuwa zoezi hilo ni muhimu sana kwa ajili ya maendeleo yake na hivyo kamwe wasikubali kupotoshwa na baadhi ya watu

Alisema kuwa mpaka sasa ndani  ya mkoa wa arusha hakuna tetesi zozote ambazo zimejitokeza na kuwasihi watu wasiweze kushiriki katika zoezi hilo la Sensa ya watu na makazi ambalo linatarajiwa kufanyika hivi katibuni

Mbali na hayo aliwataka wadau wa zoezi hilo ambao ni Wakufunzi kuhakikisha kuwa wanatumia uzoefu wa kisasa katika zoezi hilo ili waweze kufikia malengo mbalimbali ambayo yanakusudiwa katika zoezi la Sensa kwa mwaka huu

Alifafanua kuwa zoezi hilo lina umuhimu mkubwa sana na kwa hali hiyo ni vema kama watendaji wakuu wakawa makini kwa kuhakikisha kuwa wanakabiliana na Vikwazo ambavyo vinaweza kutokea wakati  wa zoezi hilo la Sensa ya watu na makazi linaloanza hivi karibuni.

“kama zoezi hili litakwama ni hasara kubwa sana kwa Serikali na hata kwa maendeleo ya jamii sasa nawasihi sana ninyi wadau hakikisheni kuwa mnakuwa makini na kama mdau hanaona kuwa atakuwa moja ya kikwazo cha Sensa ni bora akasema mapema na ajitoe kuliko kuwa chanzo cha kushindwa kufikia malengo”aliongeza Bw Mulongo

Chanzo Fullshangwe - Arusha

CHADEMA WASHINGTON DC YAPATA UONGOZI MPYA

Mwenyekiti mpya wa Chadema Washington Cosmas Wambura akipeana mikono ya pongezi na Katibu mpya Ndugu Isidori Lyamuya.

Tawi la Chadema Washington DC limepata Viongozi wapya walioshika nafasi za waliokuwa Viongozi wa muda. Katika Uchaguzi huo Cosmas Wambura amechaguliwa kuwa Mwenyekiti mpya kuchukua nafasi ya aliyekuwa Mwenyekiti wa Muda Kalley Pandukizi. Nafasi ya Katibu imechukuliwa na Isidori Lyamuya aliyechukua nafasi ya Liberatus Mwang’ombe aliyekuwa Katibu. Nafasi ya Mweka hazina imechukuliwa na Ludigo Mhagama na nafasi ya katibu mwenezi imechukuliwa na Hussein Kauzella. Nafasi nyingine

zilizogombewa ni Wenyeviti na Makatibu wa Mabaraza ya Vijana, Wanawake na Wazee. Pia kulikuwa na nafasi ya Afisa Habari wa Chama. Akiongea baada ya Uchaguzi Mwenyekiti aliyechaguliwa ndugu Cosmas Wambura amesema atatoa ushirikiano mkubwa katika kuendeleza shughuli mbalimbaliza kukijenga Chama. Pia Katibu mpya amesema watashirikiana na Mwenyekiti na wanachama wengine wote kuhakikisha Chama kinzidi kuwa Imara na kupata wanachama zaidi.

SMZ YANDAA MIKAKATI YA KUPAMBANA NA UINGIZAJI WA DAWA ZA KULEVYA ZANZIBAR

Serikali ya Mapinduzi Zanzibar imeandaa mikakati ya kudhibiti dawa za kulevya ili kuweza kupambana na uingizwaji na utumiaji wa dawa hizo nchini .

Akijibu suala la Mhe Ismail Jussa ladhu jimbo la mji mkongwe alietaka kujua hatua gani zinachukuliwa na Serikali kuweza kudhibiti madawa ya kulevya nchini, Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamo wa Kwanza wa Rais ,Fatma  Abdulhabib Fereji  alisema wizara yake itahakikisha mikakati hiyo inafanyakazi ili kuona Zanzibar inakuwa salama na utumiaji wa dawa za kulevya.

Amesema janga la dawa za kulevya halina mipaka na kuathiri mustakbali wa rasilimali na nguvu kazi ya taifa, hivyo juhudi zinahitaji kuchukuliwa katika kuzuiya matumizi ili kuwaepusha vijana kutumbukia katika janga hilo.

Mh. Fatma amesema katika kipindi cha mwaka 2010 kuanzia novembar hadi disemba ni kesi 67 zilizokamatwa na januari 2011 hadi juni 2011 ni kesi 168 na kuanzia julai 2011 hadi juni 2012 ni kesi  104.
Alieleza kuwa katika harakati hizi za kupambana na udhibiti wa dawa  za kulevya na uhalifu kwa ujumla  umepungua kutokana na kuimarisha ulinzi shirikishi na taasisi za  dola  kufanya doria mitaani pamoja na kuandaliwa kikosi maalum kikosi kazi ambacho hufichua maficho ya watumiaji na wauzaji dawa za kulevya .

YUSUF MANJI MWENYEKITI YANGA, MAKAMU WAKE CLEMENT SANGA

Mwenyekiti wa Yanga Yusuph Manjikulia na Makamu mwenyekiti Clement Sanga wakiwa katika uchaguzi huo jana

Yusuf Manji amechaguliwa kuwa mwenyekiti mpya wa klabu ya Young Africans Sports Club, uchaguzi ulioitishwa kujaza nafasi zilizoachwa wazi, kufuatia kujiuzuru kwa baadhi ya wajumbe wa kamati ya utendaji, mwenyekiti na makamu wake.

Akitangaza matokeo hayo, majira ya saa 10:30 alfajiri katika ukumbi wa Diamond Jubilee, Mwenyekiti wa kamati ya uchaguzi wa klabu ya Yanga Jaji John Mkwawa amemtangza Manji kama mishindi wa nafasi ya uenyekiti kufuatia kupata asilimia 97% ya kura zote zilizopigwa katika nafasi hiyo.

Nafasi ya Makamu Mwenyekiti imekwenda kwa Clement Sanga aliyejipatia asilimia 62% ya kura zote zilizopigwa katika nafasi ya u makamu mwenyekiti.
Abdallah Bin Kleb, Moses Katabaro, Aaron Nyanda na George Manyama  wamechaguliwa katika nafasi ya ujumbe wa kamati ya  Utendaji.

Jaji Mkwawa amewashukuru wana Yanga kwa kuwa wastaarabu na watulivu, kitu kilicholekea kufanyika uchaguzi kwa amani na zoezi hilo kumalizika salama pasipo kuwa na rabsha yoyote.
Matokeo kamili ya wagombea ni:

Nafasi ya Mwenyekiti:
Yusuf Manji (kura 1876)  97.0%,  John Jembele (kura 40) 2.6%,  Edgar Chibura (kura 4) 0.24%

Nafasi ya Makamu Mwenyekiti:
Clement Sanga (kura 1948) 62.6%, Yono S Kevela (kura 475) 23%, Ayoub Nyenzi (kura 288) 14%

Nafasi ya Ujumbe:
Abdallah Bin Kleb (kura 1942), Moses Katabaro (kura 1068), Aaron Nyanda (kura 922), Geroge Manyama (kura 682), Beda Tindwa (kura 391), Edgar Fongo (kura 295),  Graticius Ishengoma (kura 247),  Jumanne Mwamenywa (kura 251),  Justine Baruti (610),  Lameck Nyambaya (kura 425),  Omary Ndula (kura 170),  Peter Haule (441),  Ramadhan Said (249),  Yono Kivela (123)

kutokana na matokeo yalivyo hapo juu safu ya viongozi waliochaguliwa ni
Mwenyekiti: Yusuf Manji,
Makamu Mwenyekiti: Clement Sanga
Wajumbe: Abdallah Bin Kleb, Moses Katabaro, Aaaron Nyanda, Geroge Manyama
Habari kwa hisani ya dinaismailblogspot.com

WACHEZAJI WAPYA WA MANCHESTER UNITED WALIYOZAWADIWA MAGARI.

                                                    Shinji Kagawa na Nick Powell
Mjapan Shinji Kagawa amezaliwa miaka 23 iliyopita na club yake ya mwisho kuichezea ni Borussia Dortmund na kaifungia magoli 21 kwa miaka miwili aliyokaa nayo na amezichezea timu za taifa toka mwaka 2006, Powell yeye ameichezea Crew Alexandra kwa miaka miwili na kuondoka na magoli yake 16, Timu za taifa za England amejiunga nazo toka 2009.
                                        Waandishiwa habari wakipata picha

Ebenezer Hair Food Products Registered By Tanzania Food and Drugs Authority (TFDA).

Tunapenda kuwajulisha wateja wote wa nje na ndani ya Tanzania kua Ebenezer Hair Food, Ebenezer Shampoo, Ebenezer Conditioner na Ebenezer 2 in 1 Shampoo Conditioner vyote vimeshasajiliwa na Tanzania Food and Drugs Authority (TFDA).

Tunaahidi kuendelea kuthamini nywele zetu, nywele za Mwafrika kwa kuendelea kukuwezesha kuzipa lishe na matunzo yanayotakiwa.

Usisite kutumia Ebenezer Hair Food kwa nywele zako. Kwa waliopo USA unaweza kununua online at www.ebenezer-arisebeauty.com Kwa waliopo Tanzania jipatie Ebenezer Hair Food toka ARISE Beauty Supply @0714311283.

                                Asanteni na karibuni

Dr Asha Rose Migiro Ateuliwa Kuwa Mjumbe Maalum Wa Katibu Mkuu Umoja Wa Mataifa

Former United Nations Deputy Secretary-General from 2007 to 2012 Dk Asha-Rose Migiro

United Nations Secretary-General Ban Ki-Moon has appointed Asha-Rose Migiro as his Special Envoy for HIV/AIDS in Africa.  “Ms  Migiro’s experience in responding to AIDS as UN Deputy Secretary General, combined with her many years as an advocate for health and social justice in Africa, make her uniquely qualified for this important role,” said  Mr Ban. Ms Migiro served as the United Nations Deputy Secretary-General from 2007 to 2012. In that role, she was integrally involved in promoting the AIDS response globally and within Africa, with special emphasis on reducing the vulnerability of women and girls and ensuring the rights of people living with HIV.

“I am honoured to accept this appointment at this crucial moment in the African AIDS response,” said Ms Migiro. “A decade ago, HIV in Africa was almost entirely an epidemic of despair. Today, we celebrate progress  against AIDS that we never thought possible. Now is the time to take our  efforts to a new level––I am committed to the Secretary-General’s vision  that the beginning of the end of AIDS in Africa starts now.” Ms Migiro served as Tanzania’s Minister of Foreign Affairs and International Cooperation from 2006 to 2007—the first woman to hold that position since the country’s independence.

 She was previously the Minister  for Community Development, Gender and Children for five years. Prior to  Government service, she pursued a career in academia, and, served as a member of Tanzania’s Law Reform Commission in 1997 and as a member of the United Nations Committee on the Elimination of Discrimination against Women in 2000. “I look forward to working closely with Ms Migiro in helping African countries reduce their AIDS dependency and provide universal access to HIV prevention, treatment, care and support services,” said UNAIDS Executive  Director Michel Sidibé. “Her experience and leadership will promote African ownership of the AIDS response at the highest levels and reduce the inequities of people affected by AIDS in the continent.” Africa remains the continent most affected by HIV. In 2010, about 68% of  all people living with HIV resided in sub-Saharan Africa. The region also accounted for 70% of all new HIV infections worldwide.

Kwa Wale Wanaotafuta Ajira Kwenye Database Maalumu Ya Serikali


Kwa wale wanaotafuta Ajira au kuhitaji kuweka CV zao kwenye Database Maalumu ya Serikali basi watembelee  Tovuti hiyo, bado inaendelea na matengenezo madogo madogo lakini utaweza kuweka taarifa na mambo mengine pamoja na kutafuta kazi zinazohusiana na Serikali ya Tanzania. http://www.ajira.go.tz

Magazeti ya leo 16th July 2012


Benki KKKT Yalizwa 250m Kupitia ATM





WATEJA zaidi ya 50 wa Benki ya Uchumi Commercial Bank Ltd (UCB) ya Dayosisi ya Kaskazini ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) wanasakwa na polisi kufuatia wizi wa karibu Sh250 milioni.

Vyanzo vya kuaminika vilidokeza kuwa ingawa taarifa zilizofunguliwa polisi na menejimenti ya UCB zinaonyesha kiasi kilichoibwa ni Sh224 milioni, lakini kinaweza kufikia Sh250 milioni kadri uchunguzi unavyoendelea.

Benki hiyo iliyoanzishwa mwaka 2005 baada ya kupatiwa leseni namba CBA 00031 na Benki kuu ya Tanzania (BoT), inamilikiwa na Watanzania wapatao 330,000 ambao ni waumini wa dayosisi hiyo.

Habari za uhakika zilizolifikia Mwananchi zilisema wizi huo ulifanyika baada ya kuparanganyika kwa mfumo wa kompyuta uliounganishwa na mashine za ATM.

Taarifa nyingine zilisema wizi huo ulitokana na baadhi ya wateja kuusoma mfumo wa kompyuta hiyo na kugundua kuwa kuna nyakati za usiku huchanganyikiwa na kutoa salio lisilo sahihi la wateja.

“Kilichotokea ni kuwa kuna watu walivujisha siri kuwa nyakati za usiku sana ukichomeka kadi kwenye hiyo ATM inatoa pesa hovyo hovyo hata kama hauna salio la kutosha”kilidokeza chanzo chetu.

Uchunguzi wa Mwananchi ulibaini kuwa wateja wa benki hiyo wapatao 50 walijihusisha na wizi wa fedha hizo kupitia ATM hiyo na tayari polisi imeanzisha uchunguzi maalumu wa kuwasaka.

Habari hizo zimedai kuwa baada ya kugundulika kwa dosari katika mfumo huo wa kompyuta za ATM katika benki hiyo, baadhi ya wateja walianzisha kuchukua fedha muda mfumo huo unapoharibika.

“Sio pesa zilizoibwa mara moja hapana yaani unakuta leo anatoa 500,000 kesho hivyo hivyo na ilikuwa ni wateja tofauti tofauti waliokuwa wamegundua siri hiyo”alidokeza mtumishi mmoja wa UCB.

Baadhi ya wanasheria walidai zipo changamoto nyingi katika kesi za aina hiyo hasa katika kuthibitisha kama wakati mtuhumiwa anatoa fedha hizo katika ATM,alikuwa amekula njama ya kutenda kosa hilo.

Meneja mkuu wa Benki hiyo, Angela Moshi alipoulizwa alikiri kuwapo kwa tukio hilo, lakini akasema hakuwa katika nafasi nzuri ya kulielezea kwa vile alikuwa akielekea kanisani kwa ajili ya ibada.

"Naomba uje kesho (leo)tutazugumza vizuri tu juu ya hilo jambo nitakupa taarifa vizuri tu unajua leo ni siku ya ibada na sasa hivi naingia kanisani kwa ajili ya ibada"alisisitiza Meneja mkuu huyo jana.

Kwa upande wake, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro,Robert Boaz alipoulizwa na gazeti hili juzi alisema“ni kweli hilo tukio lipo kwa maana ya wateja ‘wame overdraw’ (wametoa zaidi) kutoka kwenye akaunti zao na uchunguzi wa tukio hilo unaendelea”alisema Kamanda Boaz.
Chanzo:  http://www.mwananchi.co.tz/biashara.