Wednesday, February 6, 2013

Stars yaichapa Cameroon 1-0


Vivutio saba barani afrika


Sherehe za kutangaza vivutio vya asili vya  bara la  Afrika zinategemea kufanyika katika hoteli ya Mt Meru katika jiji la Arusha Tanzania tarehe 11 February 2013 kuanzia saa nane mchana.

 Kwa mujibu wa taarifa kutoka Bodi ya Utalii Tanzania viongozi mbali mbali wa kitaifa na kimataifa ambazo wanatarajiwa kuhudhuria sherehe hiyo ambayo mgeni rasmi atakuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Mizengo Pinda. Rais wa Taasisi iliyoendesha shindano hilo la kutafuta Maajabu hayo Saba la Seven Natural Wonder Dr Philip Imler kutoka Marekani anatarajiwa kuwasili tarehe 9/2/2013 tayari kabisa kutangaza vivutio Saba vya Asili vya bara la Afrika.

 Tanzania ilikuwa na vivutio vitatu vilivyoingia kwenye kinyanganyiro hicho ambavyo ni Mlima wa Kilimanjaro, Bonde la Ngorongoro  na wanyama wanaohama wa Seregeti. Tanzania imekwisha tajwa kuwa miongoni mwa washindi ambao angalau kivutio kimoja ama zaidi Saba ya Asili Afrika.

Macho na masikio ya watanzania ni kujua ni kivutio au vivutio gani hivyo vya Tanzania vimeweza kushinda.

Kutoka Fullshangweblog

H BABA AMZIBA MDOMO FROLA MVUNGI....."ACHANA NA SHILOLE MKE WANGU"

 MSANII wa miondoko ya bongo fleva H.Baba ameamua kufunguka juu ya malumbano yaliyotokea kwa wasanii wawili wa filamu nchini Shilole na Frola Mvungi,na kuelezea hatua ambazo amezichukua kuhusu malumbano hayo

Akiongea na safu Maisha H.Baba alisema kuwa hatua ambayo ameichukua ni kumshauri mkewake mtarajiwa Flora Mvungi kuachana na malumbano na kuendelea na kazi zake kwani wanamajukumu mazito yanayowakabili

FLAVIAN MATATA ALAMBA SHAVU LA MATANGAZO YA DIESEL + EDUN

Mwanamitindo wa kimataifa kutoka nchini Tanzania Flaviana Matata ameshiriki katika kampeni za matangazo makubwa ya makampuni ya nguo ya DIESELna EDUN.

PENZI LAMTOA MACHOZI CHRIS BROWN...

This is funny or shocking. So Chris Brown and Rihanna were at a club in Hollywood partying and Karrauche showed up with a guy on her arm. Rihanna left and 10 mins later, Chris followed with a watery eye which seems like he was holding back the tears... ...

RAIS KIKWETE ASHIRIKI KATIKA MAADHIMISHO YA SIKU YA SHERIA NCHINI

 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na Mahakimu leo Februari 6, 2013  katika maadhimisho ya Siku ya Sheria nchini nje ya Mahakama Kuu ya Tanzania jijini
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia  leo Februari 6, 2013  katika maadhimisho ya Siku ya Sheria nchini nje ya Mahakama Kuu ya Tanzania jijini

Chadema wamwakia Spika Makinda

                                       Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa

 MWANANCHI

WAKATI Spika wa Bunge, Anne Makinda akitangaza kufutwa kwa hoja zote binafsi za wabunge kutokana na vurugu zilizotokea bungeni juzi na jana, Chadema kimewataka wabunge wao wasiende kwenye Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge hadi pale rufaa zao 10 zitakapotolewa uamuzi. Rufaa hizo ni pamoja na ile ya Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu kulitaka Bunge lisitishe uamuzi wa kupewa ujaji wa Mahakama Kuu, jaji mmoja kwa madai kuwa hana vigezo vya kuwa na nafasi hiyo.

Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa alitoa msimamo huo jana baada ya Spika Makinda kueleza bungeni kuwa Lissu ndiye kinara wa vurugu, huku ikielezwa kuwa Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge itamchukulia hatua za kinidhamu.

JK ana kwa ana na mtikila

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Mchungaji Christopher Mtikila leo Februari 6, 2013 baada ya kuhutubia katika maadhimisho ya Siku ya Sheria nchini nje ya Mahakama Kuu ya Tanzania jijini. Kushoto ni Jaji Mkuu Mhe Mohamed Chande Othman

KAULI YA SPIKA BAADA YA VURUGU BUNGENI FEB 4.

Spika wa bunge Anne Makinda amesema taasisi ya bunge inalaani vurugu zilizojitokeza bungeni february 4 2013 na kusababisha kuahirishwa kwa kikao cha bunge wakati wa mjadala wa mbunge wa Ubungo John Mnyika (Chadema) kuhusu upatikanaji maji katika jiji la Dar es salaam.

Baada ya kipindi cha maswali na majibu february 5 2013 Spika Makinda kasema katika kikao cha dharura cha kamati ya uongozi kilichofanyika feb 4, kimelaani hizo vurugu na kuamua kupeleka hiyo ishu kwenye kamati ya haki, kinga na madaraka ya bunge ili kufanya uchunguzi na kuwasilisha bungeni matokeo ya uchunguzi huo.

Magazeti ya leo Alhamis ya 6th February 2013




"POLISI NILIOWAITA WANISAIDIE WALIAMUA KUNISALITI NA KUNIITIA WAANDISHI WA UDAKU"...LADY JAYDEE

Jana kupitia mtandao wa Twitter mwanadada Lady Jaydee alisimulia kitendo kilimchokera baada ya polisi walioitwa kwenda kumsaidia akiwa kwenye chumba cha hoteli baada ya kuzidiwa ambao waliamua kuwapigia simu waandishi wa habari za udaku waje wapate picha na habari.

“Police mnatumwa kuja kuni rescue mgonjwa Hotel Room, mnaita waandishi waje kuchukua story! Hamjanitendea haki, nimesikitishwa,” alitweet Jaydee.

“Nawaambia I can’t walk wananilazimisha shuka watu watakubeba gari tumepaki nyuma. Kumbe camera ziko chini huko zinangoja.”

Sikia Alichokisema Ridhiwani Kikwete kuhusu Tanzania Loan Society