Tuesday, February 19, 2013

KANISA LACHOMWA MOTO ZANZIBAR

Wakati Watanzania wakiendelea kutafakari tukio la kuuawa kwa kupigwa risasi kwa Padre Evaristus Mushi, wa Kanisa Katoriki Zanzibar, watu wasiojulikana wamelishambulia kwa mawe na baadaye kulichoma moto Kanisa la Walokole la Shaloom lililoko eneo la Kiyanga kwa Sheha mkoa wa Kusini Unguja, Zanzibar.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Kusini Unguja Zanzibar, ACP Augostine Olomi, alisema jana kuwa tukio hilo limetokea majira ya saa 9.30 usiku.

JOHN MNYIKA (MBUNGE) AWAJIBU NAPE NA RIDHIWANI KIKWETE JUU YA ELIMU YAKE

 UTANGULIZI

- Amesoma S/Msingi Mbuyuni (Dar) | Alichaguliwa kwenda Ilboru lakini hakwenda, akaenda Maua Seminary na alipata A tisa | Alisoma A-Level Tambaza | Ana BBA toka UDSM

- Amtaka Ridhiwan aongee na 'mshua' juu ya tatizo la maji Dar!

SASA  ENDELEA>>>>>>>

Nilikuwa katikati ya kazi jimboni nikaambiwa kwamba kuna mwito humu wa Nape na Ridhwan kutaka nieleze elimu yangu. WanaCCM walianza suala hili kwa ari, nguvu na kasi mpya niliposema kwamba nchi imefika hapa ilipo kwa sababu ya udhaifu wa Rais Kikwete, uzembe wa Bunge na upuuzi wa CCM.

Nikapuuza, naona sasa limeibuka tena kwa ari, nguvu na kasi zaidi baada ya yaliyojiri bungeni kuhusu hoja binafsi niliyowasilisha bungeni kuhusu maji na mkutano wa hadhara wa tarehe 10 Februari 2013 na masuala ambayo niliipa Serikali wiki mbili kuyatolea majibu ama sivyo nitaongoza maandamano ya wananchi kwenda Wizara ya Maji kutaka uwajibikaji na hatua za haraka.

HUU NDO WARAKA WA UAMSHO UNAOCHOCHEA MACHAFUKO NA MAUAJI YA WAKRISTU HUKO ZANZIBAR

Huu   ndo waraka uliosambazwa Zanzibar ukichochea  mauaji  ya  wakristu  ambao  wao  wanawaita  "MAKAFIRI"....

Swali  la  kujiuliza  ni JE, SERIKALI  ILILITAMBUA  HILI?..Maana  hizi  ni  dalili  za wazi kwamba  mauaji haya  YALIPANGWA.

NB: Hatutegemei lawama  toka  upande  wowote.Palipo  na  lolote sisi  hufichua  kwa uwazi  ili  kuifahamisha  jamii...

Kuna  haja  gani  ya  kuuficha  ukweli?...Ni bora kuuanika  ili watanzania  wenzetu walioko  zanzibar wachukue  tahadhari  wakisubiri   msimamo  wa serikali.

Chanzo  cha  waraka  huu ni blog ya zanzibar.

"RAIS KIKWETE ANA HASIRA, WANAOSEMA MPOLE HAWAMJUI"...MAMA SALMA

MJUMBE wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCN, Mke wa Rais Mama Salma Kikwete ametoboa siri kwamba mumewe, Rais Jakaya Kikwete pamoja sura yake kujawa haiba ya ucheshi wa mara kwa mara lakini kwa tabia ana hasira.

Amesema, Rais Kikwete hukasirika sana anapoona au kusikia mtu au mtendaji katika Chama au serikali anafanya mambo ya hovyo au ya kizembe hasa katika masuala ya kazi.

Mama Salma Kikwete ametoboa siri hiyo, leo Februari 18, 2013, kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye kijiji cha Kikwetu Kata ya Mbanja akiwa katika ziara ya kukagua, kuimarisha uhai wa chama, kukagua utekelezaji wa ilani ya Chama na kuwashukuru wana-CCM wa Lindi mjini kwa kumchagua kuwa mjumbe wao wa NEC.

"SINA KINYONGO JUU YA PENZI LA DIAMOND NA PENNY"...JOKATE

BAADA ya Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ kupata demu mpya, Penniel Mungilwa ‘Penny’, Jokate Mwegelo ametoa baraka zake kwa jamaa huyo aliyewahi kudaiwa kuwa mpenzi wake akisema haoni tatizo wawili hao kuwa pamoja kama kweli wamependana na kuridhiana.

Akizungumza katika mahojiano maalum alipobanwa kuhusiana na uhusiano wa wapenzi hao huku ikifahamika kuwa Penny alikuwa shosti wake, Jokate ambaye ni Miss Tanzania namba 2, 2006/07 alisema kwamba yeye na mrembo huyo walikuwa washikaji tu na wala hawakuwa na urafiki wa karibu kama baadhi ya watu wanavyoamini.

Jokate ambaye pia ni mtangazaji wa Runinga ya Channel O alifunguka kuwa anawatakia kila la heri na baraka zote Diamond na Penny katika uhusiano wao mpya wa kimapenzi endapo tu watakuwa wamependana na kuridhiana kwa dhati.

“Japokuwa sipendi kumuongelea Diamond lakini ukweli sioni tatizo kwa wao kupendana, mimi naona poa tu,” alifunguka Jokate ambaye pia ni bonge la mwigizaji.

Kabla ya kutoka kimapenzi na Penny ambaye naye ni mtangazaji wa Runinga ya DTV, Diamond aliwahi kuviteka vyombo vya habari akiripotiwa kuwa na Jokate, kabla ya mambo kwenda mrama.
tagazo

"SIPO TAYARI KUKUTANA NA LULU MICHAEL KUTOKANA NA UNYAMA ALIOUFANYA KWA KANUMBA"...MAYA

STAA wa filamu za Kibongo, Mayasa Mrisho ‘Maya’ amefunguka kuwa tangu Elizabeth Michael ‘Lulu’ atolewe gerezani kwa dhamana, moyo wake unakuwa mzito kukutana naye.

Akipiga stori na mwandishi wetu, Maya aliweka plain kuwa kila anapofikiria ukaribu aliokuwa nao na marehemu Steven Kanumba, moyo wake unakuwa mzito kumuona Lulu ambaye alikuwa mpenzi wa marehemu.

“Mh! Kukutana na Lulu ni ngumu sana, sijui hata najisikiaje? Moyo unakuwa mzito sana kukutana naye na sijui kwa nini,” alisema Maya.

Baba Mtakatifu aanza wiki ya kufunga na kutoonekana hadharani.

Baba Mtakatifu Benedict wa 16 ameanza wiki yake ya mafungo ya kiroho ambapo atakuwa haonekani hadharani kwa wiki nzima ikiwa ni mwanzo wa safari yake ya kuelekea kuachia rasmi uongozi wa kanisa Katoliki na kusema kuwa ana matumaini ibada zake zitakuwa na mafanikio.

 Baba mtakatatifu atabakia Vatican na baadhi ya wasaidizi wake wa karibu kwa ajili ya ibada za awali za sikukuu ya Pasaka na atapata mapumziko mafupi kila siku kwa ajili ya kuonana na katibu wake Georg Gaenswein, ili kuyashughulikia masuala ya dharura ya kanisa.

 Baada ya wiki nzima ya ibada, Baba Mtakatifu atakutana na rais wa Italia, Giorgio Napolitano, tarehe 23 Februari kushiriki ibada ya Jumapili yake ya mwisho ifikapo tarehe 24 mwezi huu na kuzungumza hadharani kwa mara ya mwisho mbele ya waumini wapatao 10,000.

Kiongozi huyo wa kanisa Katoliki duniani ataachia uongozi rasmi tarehe 28 mwezi huu na inasemakana kuwa Waziri wa Utamaduni wa Vatican Kadinali Gianfranco Ravasi ndiye anayeonekana mtu mwenye nafasi kubwa ya kuchukua nafasi yake kwa muda mfupi au mrefu.

KAULI ZA SERIKALI YA ZNZ NA MAASKOFU WAKUU KATOLIKI KUHUSU MAUAJI YA PADRE.

 Baada ya kifo cha Padre Evarist Mushi ambae alifariki kwa kupigwa risasi Zanzibar jumapili iliyopita, kanisa Katoliki limewataka waumini wa kanisa hilo na Watanzania wengine kuwa watulivu na kufanya maombi ya amani katika kipindi hiki.

Askofu mkuu wa kanisa hilo Tanzania Muadhama Polycarp Cardinal Pengo amesema kifo cha Padre Mushi ni pigo kwa kanisa na Taifa na ni ishara ya kutoweka kwa amani hivyo hilo swala linatakiwa kufanyiwa kazi kabla ya madhara kuzidi, kwa sababu ukikosekana usalama kwa imani moja, kesho na kesho kutwa haijulikani ni imani gani ikashambuliwa.

Namkariri akisema “vyombo vya usalama vinatakiwa viwe makini, mimi sio mtaalamu wa usalama lakini naona ni jambo ambalo lingeweza kuzuilika na lisitokee kama watu wangesoma ishara za nyakati, wale wanaohusika wazuie kisitokee chochote… kuendeleza moyo wa kisasi hakutasaidia chochote na badala yake kutaleta madhara zaidi”

Magazeti ya leo Jumanne ya 19th February 2013