Saturday, June 16, 2012

KIJANA JACKSON THOBIAS A.K.A KUSH ALIYEGONGWA NA TRENI.


Kijana mdogo wa miaka 17, Jackson Thobias aliyekuwa akisoma kidato cha nne ESACS Academy, amefariki kwa kugongwa na treni maeneo ya kwao kipawa, aligongwa akiwa anasikiliza music kwa headphones huku akichati katika simu yake wakati akitembea kwenye reli.

Pamoja na mlio mkubwa wa treni, na juhudi za watu kumpigia kelele kuwa kuna treni inakuja nyuma yake, Jackson hakusikia.

Marehemu Jackson ndio aliye shinda kwenye Tokelezeiyer Inter-School concert iliyoandaliwa na group  ya Friends 4 Friends tarehe 12 may 2012, pia alishinda dougie competition  wakati 5select Event ya EATV ilipotembelea ESACS wiki mbili zilizopita.

Alikuwa ni kijana mwenye kipaji na ndoto nyingi katika umri mdogo wa miaka 17, Mungu aipumzishe roho ya marehemu Jackson Thobias kwa amani, Amen.

SHULE YA SEKONDARI NAURA YADORORA KIELIMU MKOANI ARUSHA.


Mwalimu Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Naura, Ndugu Sunday G. Mshobozi ambaye pia ndiye mwalimu pekee wa somo la Fizikia kuanzia kidato cha kwanza mpaka cha nne.
Mwalimu Mkuu Msaidizi wa Shule ya Sekondari ya Naura, Ndugu Mary Shirima akifanya mahojiano na mwandishi kufahamu changamoto zinazoikabili shule hiyo
Baadhi ya wanafunzi wanaosoma shuleni hapo wakiwa katika muda wa mapumziko

Uchunguzi uliofanywa na Shirika la HakiElimu umegundua kuwa Shule ya Sekondari ya Naura iliyoko katika kata ya Lemara , eneo la Njiro ni miongoni mwa shule zenye maendeleo hafifu ya kielimu ukilinganisha na shule nyingine za serikali na kata zilizoko katika Manispaa ya Wilaya ya Arusha. 

Shule hii iliyoanzishwa mwaka 2008 , inakabiliwa na upungufu mkubwa wa walimu kwani kuna masomo hayajawahi kuwa na walimu toka shule hiyo ianzishwe  mfano masomo ya Chemistry, Mathematics na  Book- Keeping . Pia kuna masomo ambayo yana mwalimu mmoja mmoja mfano English, Commerce,  Literature, na Civics toka kidato cha kwanza mpaka cha nne. 

Tofauti na shule nyingine ambazo hukimbiwa na walimu kutokana na kuwa mazingira magumu shule hii iko eneo zuri na maarufu waishio watu wenye kipato cha juu mkoani Arusha lijulikanalo kama Njiro na kuacha maswali kuwa kama kuna tatizo la uongozi wa shule au kuna tatizo la upangaji wa walimu unaofanywa na serikali , hili hali shule nyingine zikiwa na walimu lukuki. 

Akielezea sababu nyingine za kudorora kitaaluma shuleni hapa Mwalimu Mshobozi alisema kuna mrundikano mkubwa wa wanafunzi kushinda uwezo wa shule akitolea mfano wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza  kwa mwaka huu kufikia 307. Tofauti na malengo ya shule ya kata kusomesha wanafunzi wa maeneo ya karibu ,  wanafunzi wa shule hii wanatoka katika kata zote zilizoko manispaa hii kukiwa na umbali mrefu na kukabiliwa na shida kubwa ya usafiri jambo ambalo pia alilielezea  kuwa ni moja ya sababu za kudorora kitaaluma kwa wanafunzi wa shuleni hapo. 

Kwa upande wake Mwalimu Mkuu msaidizi Bi Mary Shirima alisema sababu za kudodora kitaaluma kwa shule yake ni mwako mdogo wa kielimu kwa wazazi pamoja na watoto wenyewe akisema wengi wa wanafunzi ni kama wamelazimishwa kuja kusoma shuleni hapo na wazazi wao hawajishughulishi na maendeleo ya watoto wao.  “ Historia ya wanafunzi waliomaliza kidato cha nne ni tata kwani kuna waliokuwa wameolewa na wafanyabiashara mara baada ya kumaliza darasa la saba ,ghafla wakasikia wamechaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza na kulazimika kuja shuleni, sasa katika hali hiyo unatarajia nini” aliuliza Mwalimu Shirima.

Katika mtihani wa kidato cha nne wa taifa wa mwaka jana 2011 jumla ya wanafunzi 164 walifanya mtihani  huo ambapo hakuna aliyepata daraja la kwanza wala la pili, wanafunzi 2 walipata daraja la tatu , 24 wakapata daraja la nne na 138 walifeli kwa kupata zero. Shule hii ilishika nafasi ya mwisho kati ya shule 137 zilizofanya mtihani huo katika mkoa wa Arusha. Kitaifa ilishika nafasi ya 2994 kati ya 3108 zilizofanya mtihani huo.

HakiElimu inatoa wito kwa Serikali kupitia mamlaka husika kuangalia upangaji wa walimu na uchaguzi wa wanafunzi shuleni hapo. Wazazi na wakazi wa Njiro nao wanatikiwa kuchukua jitihada za ziada kuhakikisha wanafunzi walioko shuleni hapa wanapata elimu bora na kuelimika .Uongozi wa shule nao ni siri ya mafanikio au kushindwa kufanya vema , hivyo uongozi wa Shule ya Sekondari Naura uongeze jitihada kuhakikisha shule hii inafanya vema kama shule za Kaloleni, Ngarenaro na Arusha Day . 

Mama Salma Kikwete Azindua Kampeni Ya Matibabu Ya Fistula

Afisa Mtendaji Mkuu wa CCBRT, Erwin Telemans akitoa maelezo wakati wa Uzinduzi  wa Kampeni ya Uhamasishaji wa Matibabu ya FISTULA Tanzania, uliofanyika katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar eSalaam. Uzinduzi rasmi umefanywa na Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya WAMA Mama Salma Kikwete. Mradi wa Fistula kwa mwaka inakadiriwa wastani wanawake wapya 2,500 hadi 3000 hupatwa na ugojwa huo wakati wanapojifungua. Kwa sasa wanawake zaidi ya 31,000 inasemekana wanalo tatizo la Fistula hapa nchini, Hivyo Mke wa Rais Mama Salma Kikwete ametoa wito wakina mama wenye matatizo ya Fistula kumuacha kujificha  kwani unatibika .hivyo waende katika matibabu ambayo hupatikana bure ktk  hosp. ya CCBRT jijini DSM na  hosp, ya Kilutheli ya Selian.

Mama Kikwete akihutubia.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete na Mwenyekiti wa Taasisi ya WAMA, akiwa amemshika mtoto mchanga baada ya kukabidhiwa na wazazi wake baada ya ushuhuda walioutoa wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya Uhamasishaji wa Matibabu ya Fistula- Tanzania. Kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya CCBRT, 
Shuhuda wa ugonjwa wa FISTULA, Beatrice Mlunga (kulia) akitoa ushuhuda wa matatizo aliyoyapata ya ugojwa Fistula wakati wa uzinduzi huo. Kushoto ni mume wake,  Hosea Sanga.
 Mke wa Rais NaMwenyekiti wa Taasisi ya WAMA , Mama Salma Kikwete (mwenye miwani ) akiponyeza kitufe kuzindua kampeni hiyo.
Mjomba Mpoto akiwatumbuiza waalikwa wakati wa Uzinduzi.


TAFAKARI?


Leo ni siku ya mtoto wa Afrika ni kweli watoto wanapewa haki zao? JE Jamii, wazazi na walezi umefikiria nini juu ya watoto wanaoishi katika mazingira magumu?TAFAKARI.

KESI YA LULU HADI JUNI 25 MAHAKAMA KUU

 WAKILI mmoja wapo anayemtetea  Elizabeth Michael  Fulgence Massawe akimsalimia ' Lulu' kabbla Jaji Dk. Fauz Twaibu hajaingia Mahakamani leo asubuhi katika Mahaka Kuu ambako kesi hiyo ilipigwa tena kalenda hadi Juni 25 mwaka huu. Pia Jaji Fauz amezitaka pande zote mbili yaani Wakili wa Serikali pamoja na Jopo la Mawakili wanaomtetea  kupeleka vuthibitisho kuhusiana na umri wa Lulu Mahakamani hapo.

Hapa akificha sura aikikwepa picha  pia alisikika akiwaambia waaandishi  wa habari kutoka vyombo mbalimbali vya habari kuwa amechoka kupigwa picha.

Hapa Lulu na Askari  Wanawake wa Jeshi la Magereza wakienda kupanda gari ambako mtuhumiwa amerudishwa rumande.MAHAKAMA Kuu kanda ya Dar es Salaam imewataka mawakili wa utetezi na jamhuri kuwasilisha uthibitisho kuhusu umri wa msanii Elizabeth Michael ‘Lulu’ kabla ya kutoa uamuzi wake Juni 25, 2012.

Agizo la Mahakama hiyo lilitolewa jana na Jaji Dk. Fauz Twaib anayesikiliza madai ya utata wa umri wa msanii huyo nyota wa maigizo nchini.

Kabla ya kuahirisha kesi hiyo Jaji Dk. Twaib alizitaka pande mbili zinazobishana kupeleka vithibitisho vya hati ya kiapo cha cheti cha kuzaliwa ili kujiridhisha umri sahihi wa Lulu.

Kwa upande wake wakili wa mshitakiwa Flugency Massawe alidai mahakamani hapo kwamba hadi Juni 13 atakamilisha vithibitisho hivyo wakati wakili wa serikali Elizabeth Kaganda alidai kazi hiyo ataikamilisha Juni 22 mwaka huu.

Lulu anayetuhumiwa kwa mauaji ya msanii mwenzake Steven Kanumba Aprili 7 mwaka huu anadaiwa kuwa chini ya miaka 18 huku jamhuri wakidai kwamba mshtakiwa huyo ana zaidi ya umri huo.

 Pamoja na Massawe mawakili wengine wanaomtetea msanii huyo ni Jacqueline Dimelo, Kennedy Fungamtama na Maico Kibatala huku Shadrack Kimaro na Kaganda wakiongoza kesi hiyo upande wa jamhuri.

MATILDA MARTIN NDIYE REDDS MISS DAR CITY CENTER

Wema akiwa jaji katika miss Dar city center kazi nzuri dada Nakukubali sana.

HOTUBA YA BAJETI MWAKA 2012/2013 (MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI) HII HAPA

Waziri wa Fedha wa Tanzania,Dr.William Mgimwa,akionyesha briefcase iliyobeba Hotuba Ya Bajeti, Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa Mwaka 2012/13 alipokuwa akiwasili katika viwanja vya Bunge mjini Dodoma tayari kuisoma.



Waziri wa Fedha wa Tanzania,Dr.William Mgimwa akisoma Hotuba Ya Bajeti 2012


I   UTANGULIZI:

1.         Mheshimiwa Spika, naomba kutoa hoja kwamba Bunge lako Tukufu liweze kujadili na kupitisha makadirio ya mapato na matumizi ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2012/2013.  Pamoja na hotuba hii, nimewasilisha vitabu vinne vya Bajeti vinavyoelezea takwimu mbalimbali za Bajeti. Kitabu cha Kwanza kinaelezea makisio ya mapato.   Kitabu cha Pili kinaelezea makisio ya matumizi ya kawaida kwa Wizara, Idara zinazojitegemea; Taasisi na Wakala wa Serikali; cha Tatu kinahusu makisio ya matumizi ya kawaida kwa Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa na cha Nne kinaelezea makadirio ya matumizi ya maendeleo kwa Wizara, Idara zinazojitegemea, Taasisi na Wakala za Serikali; Mikoa na
Mamlaka za Serikali za Mitaa. Aidha, upo Muswada wa Sheria ya Fedha wa mwaka 2012 ambao ni sehemu ya Bajeti hii.

2.  Mheshimiwa Spika, awali ya yote, naomba nitumie fursa hii kumshukuru kwa dhati Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho
Kikwete, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa imani kubwa aliyonayo kwangu kwa kuniteua kuwa Waziri wa Fedha. Naahidi kutekeleza majukumu niliyokabidhiwa kwa umakini na uaminifu mkubwa.
3.         Mheshimiwa Spika, napenda kuwapongeza wafuatao kwa kuteuliwa na Mheshimiwa Rais kuwa mawaziri kama ifuatavyo: Mhe. Prof. Sospeter Mwijarubi Muhongo (Mb); Mhe. Mhandisi Christopher Kajoro Chiza (Mb); Mhe. Dkt. Harrison George Mwakyembe (Mb); Mhe. Dkt. Fenella Ephraim Mukangara (Mb); Mhe. Balozi Khamis Sued Kagasheki (Mb); Mhe. Dkt. Abdallah Omari Kigoda (Mb). Aidha, napenda kuwapongeza wafuatao kwa kuteuliwa kuwa naibu mawaziri katika Wizara mbalimbali, Mhe. Janet Zebedayo Mbene (Mb); Mhe. Saada Mkuya Salum (Mb); Mhe. Dkt. Seif Suleiman Rashid (Mb.); Mhe. George Boniface Simbachawene (Mb.); Mhe.  January Yusuf Makamba (Mb.); Mhe. Dkt. Charles John Tizeba (Mb.); Mhe. Amos Gabriel Makalla (Mb.); Mhe. Angela Jasmine Kairuki (Mb.); Mhe. Stephen Julius Maselle (Mb.); na Mhe. Mhandisi Dkt. Binilith Satano Mahenge (Mb). Kadhalika, nampongeza Mhe. James Mbatia (Mb) kwa kuteuliwa na Mhe. Rais kuwa Mbunge.

4.         Mheshimiwa Spika, nawapongeza pia, Mhe. Alhaji Adam Kimbisa (Mb.); Mhe. Shy Rose Banji (Mb.); Mhe. Abdulah Alli Hassan Mwinyi (Mb); Mhe. Charles Makongoro Nyerere (Mb); Mhe. Dkt Twaha Issa Taslima (Mb); Mhe. Nderkindo Perpetua Kessy (Mb); Mhe. Bernard Musomi Murunyana (Mb); Mhe. Anjela Charles Kizigha (Mb.); Mhe. Maryam Ussi Yahaya (Mb.), ambao wamechaguliwa kutuwakilisha kwenye Bunge la Afrika Mashariki. Ni matumaini yangu watatuwakilisha vyema kwa maslahi na manufaa ya Taifa letu.

5.         Mheshimiwa Spika, maandalizi ya Bajeti hii yamehusisha wadau na Taasisi mbalimbali. Napenda kuwashukuru walioshiriki kwa namna moja au nyingine kufanikisha matayarisho yake. Kwa namna ya pekee, ninaishukuru Kamati ya Bunge ya Fedha na Uchumi chini ya uenyekiti wa Mhe. Mtemi Andrew John Chenge, Mbunge wa Bariadi Magharibi, pamoja na kamati nyingine za kisekta kwa ushauri mzuri waliotoa wakati wakichambua mapendekezo ya Bajeti hii. Aidha, ninawashukuru Waheshimiwa Wabunge wote kwa ushauri na mapendekezo yao ambayo yamezingatiwa katika Bajeti hii.

Read more: BongoCelebrity

 

KUHUSU PREZZO KUJITOA BIG BROTHER.


Ishu ambayo imewashangaza wengi ni pale ambapo mwakilishi wa Kenya kwenye jumba la Big Brother CMB Prezzo kutangaza kwamba amechoka maisha ya kuishi kama mfungwa kwenye jumba hilo.

Mtandao wa Ghafla Kenya umeripoti kwamba hii ishu imetokea wakati Big Brother alipotangaza kupiga marufuku pombe kwa washiriki ndani ya jumba hilo, Prezzo alishikwa hasira na kusema kwamba anaweza kuondoka muda wowote, na anahisi wakati umefika.

Prezzo alimaind mpaka akawa anabishana na washiriki wenzake akiwemo Keita na kutaka mlango ufunguliwe aondoke lakini baadhi ya washiriki wenzake walimsihi asifanye hivyo.

Huu mchongo umetokea siku 30 baada ya Prezzo kuwa trending topic kwa wakenya kutokana na kuchaguliwa kwake kwenda big brother ambapo wengi walikua wanamdiss kwamba haikutakiwa apelekwe BBA.