Monday, December 17, 2012

Magazeti ya leo Jumatatu 17th December 2012

Ndege ya Tanapa yaanguka




Ndege ya shirika la hifadhi la taifa (TANAPA) aina ya C182 ikiwa imeanguka katika eneo la nsemulwa mjini Mpanda muda mfupi baada ya kuondoka katika uwanja wa ndege wa Mpanda ikiwa inaendeshwa na rubani Adam kajwa alieumia sehemu ya uso.

Ajali imetokea jioni wakati ndege hiyo ikielekea hifadhi ya taifa ya katavi wilayani mlele mkoa wa katavi ambapo meneja wa uwanja wa ndege wa Mpanda  Mahamud Muhamed  kasema ajali ilitokea jana december 16 2012 saa kumi na dakika 55 jioni.

Ni ndege ya abiria mali ya hifadhi ya taifa ya  TANAPA na una uwezo wa kuchukua abiria wanne na imeanguka umbali wa kilometa moja na nusu kutoka uwanja wa ndege.

Meneja wa uwanja  huo wa ndege  alisema  taarifa za awali   zinaonyesha  chanzo  cha ajali ni injini ya ndege kufeli wakati ikiwa angani.
Rubani wa ndege hiyo alipata msaada kutoka kwa wananchi waliokuwa  shamani mwao ambapo mmoja wao alisema wakati akiwa anafanya shughuli  zake  za kilimo ghafla aliona ndege angani  ikizimika injini na muda mfupi baadae ikaanguka jirani na mti wa mwembe, kazi ya uokoaji ilichukua muda kidogo kutokana na nyuki.
(Taarifa imeandikwa na http://kataviyetu.blogspot.com)

Filikunjombe Anena Mbele Ya Mangula

Viongozi   wa CCM mkoa  Njombe  wakishirikiana na makamu mwenyekiti wa CCM Taifa Phili Mangula ( wa pili kulia ) kuwaongoza  wanachama wapya wa CCM zaidi ya 600 waliojiunga na CCM jana wakati wa mapokezi ya makamu huyo  wa kwanza  kulia ni mbunge wa jimbo la Njombe kusini na spika  wa bunge Anne Makinda  wa tatu kutoka kulia ni mwenyekiti wa CCM mkoa wa Njombe Deo Sanga ambae ni mbunge wa jimbo la Njombe kasikazin na anayefuatia ni katibu wa CCM mkoa wa Njombe Hosea Mpangike

                                                Deo Filikunjombe miongoni mwa wananchi

                               Msafara wa pikipiki kwenye mapokezi ya Mangula Njombe

MBUNGE wa jimbo la Ludewa mkoani Njombe Deo Filikunjombe awakuna wapiga kura wa jimbo la Njombe Kaskazini Linaloongozwa na mbunge wake Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Njombe Deo Sanga Kwa kuwalipua watendaji wabovu serikalini ,mbele ya makamu mwenyekiti wa Chama cha mapinduzi ( CCM) Tanzania bara  Philip Mangula.

Filikunjombe ambea alipewa nafasi ya kusalimia katika mkutano huo mkubwa wa mapokezi ya Mangula mkoani Njombe alisema kuwa masikitiko ya wananchi juu ya serikali ya CCM yanatokana na baadhi ya viongozi wabovu ndani ya Chama na serikalini ambao wamekuwa wakifanya kazi chini ya kiwango na kupelekea wananchi kukichafua Chama tawala.

" Ndugu zangu wananchi wa Makambako na mkoa wa Njombe Chama chetu CCM ni Chama kizuri sana na safu hii ya sasa chini ya Rais Kikwete ,Kinana na Mangula ni safu ya uhakika na itakiwezesha Chama  chetu kuendelea kuaminiwa zaidi na watanzania ...ila tatizo ni viongozi wachache wa serikali wasiowajibika katika nafasi zao"kauli iliyowakuna wananchi na kushindwa kujizuia kushangilia huku wakiimba wewe ni Jembe .

Hata hivyo Filikunjombe alisema kuwa ili Chama kuendelea kupendwa na akina Mangula na Kinana wanapaswa kusaidiwa na watanzania wote kwa kuombewa zaidi ili kuendelea kuifanya kazi hiyo bila woga ndani ya chama.

Kwa Upande wake  Mangula mbali ya kusifu mapokezi makubwa ya kihistoria Katika mji wa Makambako na Njombe mkoani Njombe aliweza kutoa  ya Moyoni kuhusu Kati yake na Rais Jakaya Kikwete kwa Madai kuwa yeye alikuwa hajui chochote juu ya uteuzi wake na kuwa alisitaajabu kupokea simu ya Kikwete kuhusu kusudio la uteuzi wake.

" Kweli Mimi nilikwenda Dodoma katika mkutano mkuu wa CCM Kama mualikwa ila Nikiwa Hotelini nilipokea simu ya mwenyekiti wa CCM Taifa Rais Kikwete akiomba kuniteua kuwa makamu mwenyekiti na baada ya kwenda Ukumbini wajumbe wote walinipa kura zote za ndio...kweli namshukuru sana mwenyekiti wangu na wanachama wote na sasa ni kazi zaidi na sitawaangusha"


Hata hivyo aliwataka wana CCM kufanya vikao bila kuchota na kuwa wasizingizie kukosa ajenda kwani hata kukosa ajenda ndani ya CCM ni ajenda Kukosa agenda pia ni agenda ndani ya CCM pia yaweza kuwa ajenda.

Aidha amehimiza  nidhamu na taratibu ndani ya CCM kuendelea kuzingatiwa ili kukiwezesha Chama kuwa na amani na kuwa iwapo taratibu ndani ya  Chama hazitazingatiwa upo uwezekano wa Amani ndani ya nchi kutoweka.

Alisema kuwa haitapendeza kuona Tanzania inafika mahali inaendeshwa  bila Chama iwapo tutaruhusu wasiopenda Amani kuendelea kuvuruga Amani yetu iliyopo...

Picha na Said Ng'amilo wa Mjengwablog, habari na Francis Godwin

Pinda Ahimiza Mazao Mbadala Ya Biashara

WAZIRI MKUU Mizengo Pinda amewataka wakazi wa wilaya mpya ya Mlele mkoani Katavi walime mazao mbadala ya biashara kama alizeti, karanga na ufuta kwa sababu yanachukua muda mfupi na hivyo kuleta kipato cha haraka.

Ametoa wito huo juzi jioni (Ijumaa, Desemba 14, 2012), wakati akizungumza na wakazi wa kijiji cha Nsenkwa mara baada ya kuweka jiwe la msingi kwenye zahanati ya kijiji hicho akiwa katika siku ya pili ya ziara yake jimboni kwake Katavi wilayani Mlele, mkoani Katavi.

Waziri Mkuu aliwataka wakazi hao kuachana na mazoea ya kulima tumbaku kwa vile inachukua muda mrefu hadi kukomaa na inachangia uharibifu mkubwa wa mazingira kwani inahitaji kuni nyingi wakati wa kukausha.

“Tumbaku hivi sasa haina bei kwa sababu wanaopanga bei ni wakubwa huko nje… tuangalie mazao ya alizeti, ufuta na karanga kwa sababu yanatoa pesa kwa haraka zaidi. Mfano mzuri ni Singida ambao wamekuja juu kiuchumi kwa sababu ya zao la alizeti,” alisisitiza.

Aliwataka wakazi hao waangalie ufugaji nyuki kama fursa ya kipekee kwa sababu mkoa huo umejaliwa kuwa na misitu mingi na unaweza kuongeza kipato cha mkoa wao. “Asali ni dawa, asali ni chakula, asali ni biashara na ina soko hapa nchini hadi nje ya nchi.

Changamkieni fursa  hii, ongezeni uzalishaji wa asali na nta,” aliongeza.Aliwashauri pia waangalie uwezekano wa kulima miembe ya kisasa kwasababu inazaa kwa wingi na katika kipindi kifupi mno. “Hii miembe yenu inazaa maembe 10-20 kwa mwaka lakini ya kisasa inazaa hadi maembe 10,000, ikiwa chinichini tu,” alisema.

Kambi Ya Miss Utalii Kuanza

Huu ni ukumbi ambao utatumika kwa ajili ya Mazoezi   pamoja na shughuli mbalimbali.

Jumla ya warembo Sitini (60)  kutoka nchi nzima na vyuo vikuu  watakao shiriki fainali za Miss Utalii Tanzania 2012/2013 wanatarajia kuanza kambi Rasmi Tarehe 19.12.2012 katika hoteli ya kitalii ya Ikondolelo Lodge iliyopo kibamba Dar es salaam.

Wakiwa katika kambi hiyi ya siku ishirini na moja , warembo hao watashindana kuwania taji la taifa la Miss Utalii Tanzania , na tuzo mbalimbali za kijamii kitalii kitamaduni na kiuchumi. Zikiwemo tuzo za Mazingira, utaluii wa ndani, wanyama pori,hifadhi za Bahari, Mitindo, urembo, maziwa makuu, SADEC, Afrika Mashariki, umoja wa Afrika  Afya ya jamii, Jinsia wanawake na watoto, Rushwa, uwekezaji, Madawa ya kulevya, mazao ya biashara, madini , uchukuzi na Miundombinu mbalimbali ya utalii.

Washiriki pia watajifunza stadi mbalimbali za maiusha , Mbinu za utangazaji utalii na bidhaa mbalimbali za Tanzania, Pia mbinu za kjuhamasisha kampeni dhidi ya uharibufu wa mazingira, tanamaduni kongwe na potefu, kupenda kutumia huduma za Tanzania ( Madre in Tanzania), uvuvi haramu, amna uwindaji haramu.
Washindi wa fainali hizo za taifa watawakirisha fainali mbalimbali za kitaifa na kimataifa yakiwemo ya, Miss Tourism world, Miss Tourism HeritageWorld Miss Tourism University World, Miss Tourism Uniterd Nation,International Miss tourism World, Miss Global International.

Friday, December 14, 2012

ODM Kenya Yamkingia Kifua Magufuli

CHAMA cha Orange Democratic Movement (ODM) cha Kenya, kimezungumzia uamuzi wake wa kumwalika Waziri wa Ujenzi, Dk John Magufuli kwenye moja ya mikutano yake ya kampeni nchini humo, uliozua mjadala mkubwa nchini.

Desemba 7 mwaka huu, chama hicho cha upinzani nchini Kenya kilimwalika Dk Magufuli kwenye mkutano wake wa kampeni uliofanyika kwenye Uwanja vya Kasarani ambako pamoja na mambo mengine, alimpigia debe Raila Odinga ili achaguliwe kuwa Rais wa Kenya katika Uchaguzi Mkuu uliopangwa kufanyika Machi mwakani.

Hatua hiyo ya Dk Magufuli ilizua mjadala mkubwa, huku Chadema kikidai kuwa ni makosa kwa nchi moja kuingilia siasa za nchi nyingine na kumtaka waziri huyo aeleze kama alitumwa na Serikali au la.

Chadema pia kilimtaka Rais Jakaya Kikwete atolee kauli hatua hiyo ya waziri wake, vinginevyo nchi itakuwa na uhusiano mbaya na Kenya, endapo Raila hatachaguliwa kuwa Rais. Akizungumza na gazeti hili jana, Katibu Mkuu wa ODM, Profesa Peter Anyang’Nyong’ alisema hakuna haja ya Watanzania kumzonga Waziri Magufuli, kwani ujio wake Kenya, ulitokana na mwaliko wa Odinga.

Profesa Anyang’Nyong’ ambaye chama chake cha ODM kilitangaza kuungana na chama kingine cha Wiper Democratic cha Makamu wa Rais, Kalonzo Musyoka katika uchaguzi huo alisema Odinga alimwalika Magufuli kama rafiki yake wa muda mrefu na rafiki wa ODM.

“Waziri Mkuu wetu Odinga ndiye aliyemwalika Magufuli na alimwalika kama rafiki yake wa karibu. Kuja kwake huku (Kenya) kulikuwa safari binafsi. Hakukuwa (kuja) na uhusiano wowote na wadhifa alio nao Tanzania,” alisema Profesa Onyang’Nyong’.

Alisema ziara ya Magufuli iliratibiwa na Odinga ambaye aligharimia kila kitu na kwamba mwaliko huo ulifanywa kwa kuzingatia ushirikiano wa muda mrefu baina yao.

Profesa Anyang’Nyong’ alisema ODM kumwalika Dk Mafuguli ni mwendelezo wa uhusiano wa wanasiasa wa Tanzania na Kenya uliokuwapo tangu enzi za viongozi; Jomo Kenyatta, Tom Mboya na Mwalimu Julius Nyerere ambao walifanya pamoja kazi ya kudai uhuru.

“Kizazi cha sasa lazima kitambue ushujaa wa viongozi wetu wa zamani ambao walituonyesha namna wanavyoweza kufanya siasa kwa pamoja na kufanikisha malengo yao,” alisema na kuongeza:

“Mambo kama haya lazima tuyatambue kwani sisi sote ni wamoja tena tuna shabaha ya kuwatumikia wananchi wetu. Tunapopata viongozi wenye mitazamo inayofanana kama ile ya waasisi wa mataifa yetu lazima tuwaunge mkono na kuwapa fursa.

“Kwetu sisi Magufuli tunamwona kama shujaa tena mtu ambaye anaweza kutoa idea (mawazo) yanayoweza kukusaidia kusonga mbele kwenye siasa.”Alisema Dk Magufuli ana uzoefu mkubwa na mambo ya siasa na ODM wanatambua umuhimu wake katika siasa zao.

Alipuuza madai kwamba kumwalika Dk Magufuli ni kuingilia siasa za Kenya na huenda hatua hiyo ikadhoofisha uhusiano wa kidiplomasia… “ Kuja kwake hakumaanishi kwamba ameingilia mambo ya Kenya au siasa za taifa hili…. Huyu ni rafiki yetu na alikuwa kama mtu wetu wa karibu.”

Koffi Olomide Atua Dar, Tayari Kwa Onyesho Lake La Jumamosi

 Mwanamuziki nyota wa dansi kutoka nchini DRC-Kongo,Koffi Olomide akiwasalimia baadhi ya mashabiki wake waliofika kumlaki usiku wa kuamkia leo mara baada ya kuwasili akiwa sambamba na skwadi lake zima la Quartier Latin kwenye uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA),tayari kwa onesho lake litakalofanyika siku ya jumamosi ndani ya viwanja vya Lidaz Club,Kinondoni jijini Dar na jumapili jijini Mwanza ndani ya uwanja wa CCM-Kirumba,onesho hilo ambalo limedhaminiwa na kampuni ya bia ya Afrika Masharikia (EABL) kupitia kinywaji chake cha Tusker kiingilio chake kimepangwa kuwa ni shilingi 10,000/= kwa kichwa kama tiketi ikinunuliwa mapema na shilingi 15,000/= getini.Pichani kushoto ni Mwenyeji wake kutoka kampuni ya Prime Time Promotions Ltd,Godfrey Kusaga
Watangazaji wa Clouds FM na Clouds TV pichan shoto ni Millard Ayo na Ben Kinyaiya pichani kulia wakifanya mahojiano mafupi na Mwanamuziki Koffi Olomide mara baada ya kuwasili usiku wa kuamkia leo  kwenye uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA),jijini Dar.Koffi alitanabaisha kuwa yeye amekuja nchini Tanzania kwa mara nyingine tena kuwaburudisha na kuwaonesha vipaji alivyo navyo sasa ndani ya kundi lake la Quartier Latin.