Tuesday, January 1, 2013

Walioteuliwa Kuwania Tunzo Ya Mwasoka Bora Mzalendo.

Kundi A: Kipa Bora

Mwandini Ally- Azam FC, Juma Kaseja- Simba, Shaaban Kado- Mtibwa Sugar, Ally Mustapha-Yanga, Jackson Chove-Coastal Union, Deogratius Munishi- Azam FC

 Kundi B: Beki Bora

 Nassor Said – Simba, Nadir Haroub – Yanga, Agrey Morris- Azam FC, Amir Maftah- Simba, Kelvin Yondan-Yanga  na Shomari Kapombe-Simba.

 Kundi C: Kiungo Bora

Shaban Nditi –Mtibwa, Frank Domayo- Yanga, Mwinyi Kazimoto-Simba, Amri Kiemba-Simba, Chande Mgoja- Mgambo JKT na Abubakar Salum-Azam FC.

 Kundi D: Mshambuliaji Bora

John Bocco – Azam FC, Mrisho Ngassa – Simba, Hussein Javu -Mtibwa FC, Amiry Omary-JKT Oljoro, Simon Msuva-Yanga, Nsa Job-Coastal Union.

 Kundi E: Mchezaji anayechipukia

Mudasir Yahya-Azam FC, Ramadhan Singano-Simba, Edward Christopher-Simba, Manyika Peter Manyika- Mgambo JKT, Miraji Adam-Simba na Chande Mgoja- Mgambo JKT

 Kundi F: Mchezaji Bora wa Kike

Ester Chabruma-Sayari Queens, Mwanahamisi Omar-Mburahati Queens, Mwapewa Mtumwa-Ever Green, Fatuma Mustafa-Sayari Queens, Asha Rashid-Mburahati Queens na Sophia Mwasikili-Luleburgaz Spor Kulubu- Uturuki.

 Kundi H: Mchezaji Bora wa mwaka 2012

Mchezaji atakayetwaa tuzo hii atatoka katika makundi yaliyotajwa hapo juu hii ikiwa na maana kwamba kuanzia kundi A-E. hii ni kumaanisha kuwa wanawake hawataingia kwenye kundi hili wala kwa sababu tayari wanayio tuzo yao tayari kama inavyoonekana katika kipengele F.

 Kundi I: Mchezaji Bora Kigeni

Haruna Niyonzima-Yanga, Kipre Tchetche-Azam FC, Emmanuel Okwi-Simba,  Felix Sunzu-Simba, Hamis Kiiza-Yanga na Jerry Santo-Coastal Union.

 TUZO ZA HESHIMA

Kundi H: Mchezaji bora wa zamani
Madaraka Suleiman – Simba, Edibily Lunyamila-Yanga/Simba/Twiga FC,
Mohamed Mwameja-Simba, Yusuf Macho-Simba/Kagera Sugar, Zamoyoni Mogela-Simba/Yanga na Kenny Mkapa-Yanga.

 Kundi I: Maendeleo soka la Wanawake (tuzo mbili Mwanamke na Mwanaume)
Stephania Kubumba-Sayari, Arafa Tamba-Mburahati Queens, Fatma Makambara-Sayari, Pili Kambangwa- Mchangani, Joha Halfan-Vijana Queens, Amin Bakhresa, Frenk Mchaki na Idd Azan.
 Kundi J:Mwanasiasa wa Afrika aliyesadia maendeleo ya michezo

Benjamin Mkapa-Tanzania, Daniel Arap Moi-Kenya na Joachim Chisano-Msumbiji
 Katika kipengere hiki ni kwamba kilichoangaliwa ni namna gani mwanasiasa mstaafu alivyweza kusaidia michezo kwa ujumla ikiwemo soka. Hapa inaangaliwa ujewekaji wa miundo mbinu, kama ujezi wa viwanja vya michezo, mafanikio katika klabu na  timu za taifa katika nchi ambayo amekuwa akiiongoza.

 Pia kipengere hiki pia kinaangalia katika kipindi kisichozidi miaka 10 ya utawala akiwa kama mkuu wa nchi husika.
 Baada ya kufuatilia kwa takriban mwaka mmoja katika nchi zilizopo jirani na Tanzania, imeonekana wazi kuwa viongozi hao wastaafu ndiyo wenye waliofikia viwango ambavyo kamati ilivihitaji.

UHUSIANO BORA HUUNDWA NA MISINGI IMARA YENYE UKWELI

KIBURI kimejikita kwenye vichwa vya watu wengi, hivyo kufanya hata yale ambayo wapenzi wao hawataki. Mathalan, mtu anaweza kutambua kuwa akivaa nguo za aina fulani, mpenzi wake hawezi kufurahi lakini kwa sababu ya kutokuwa na hofu, anavaa na kuibua ugomvi usio wa lazima.

Mtu anajua fika kwamba mwenzi wake hapendelei tabia ya kutembea usiku lakini kwa sababu ya kiburi, anasaga rumba mpaka usiku wa manane ndiyo anarudi nyumbani. Ni kutafuta shari, hiyo ni tabia ya kutopenda amani na mwenzi wako. Sisemi uogope ila unatakiwa uwe na hofu kutoka moyoni.
Kila jambo linalotokea, hebu jiulize mara mbili mpaka tatu. Ukiona ni zito, jipe muda zaidi wa kutafakari kabla hujapata uamuzi sahihi. Inawezekana ukalichukulia ni dogo, kumbe mwenzako akalitafsiri kwa undani zaidi, mwisho akaona muachane kwa sababu amehisi unamdharau. Zingatia kwamba kufanya jambo la kumkera mpenzi wako kwa makusudi ni dharau.

Kama mchambuzi wa masuala ya mapenzi, nimegundua baada ya utafiti wake kuwa asilimia kubwa ya migogoro kwenye mapenzi hutokea kwa sababu ya wawili wanaoamua kupendana kukosa hofu. Hoja hapa ni kwamba ukiishi kwa kujiamini kupita kiasi mbele ya mwenzi wako ni janga. Ni sawa na kuuweka uhusiano wenu hewani.

Sina maana kuwa watu wasijiamini, mantiki ni kwamba kila mmoja ajipe hofu kwenye matendo yake ili asimkere mwenzake. Ajue kuwa dogo linaweza kuhatarisha mapenzi, kwa hiyo hatakiwi kuthubutu kutenda. Uhusiano wa kimapenzi, huunganisha pande mbili zenye matarajio ya furaha, kwa hiyo ni vizuri kuishi kwa kuheshimu matarajio hayo.

UAMINIFUKifungu hiki kina vifungu vidogo viwili. Mosi: Uaminifu binafsi. Yaani mhusika anakuwa anasukumwa kutorahisi mwili wake kutumika kiholela kutokana na kulinda heshima yake. Hii ina maana ya nidhamu binafsi. Nitoe msisitizo kwamba mwenzi bora wa maisha ni yule anayejitunza kwa nidhamu binafsi. Nidhamu ya woga inasaidia lakini si nzuri sana.

Pili: Ni uaminifu unaotokana na hofu. Mtu anakutana na vishawishi vya hapa na pale lakini anaogopa kuingia kwenye uhusiano wa pili kwa sababu ya hofu aliyonayo kutokana na macho ya jamii inayomzunguka. Anajua watu wakijua watamuona mhuni (malaya), anataka aheshimike, kwa hiyo anabaki na uaminifu wake wa woga.

Katika kipengele hicho cha woga, anaweza pia kuogopa kusaliti kwa sababu anajua za mwizi ni arobaini. Anatambua kwamba ipo siku mwenzi wake atajua na kuanzia hapo penzi litakufa. Naye hataki uhusiano wake ufe, kwa hiyo anajilinda, ingawa ndani yake kunakuwa na msukumo wa kuanzisha figa la pili na tatu. Hata huu nao ni uaminifu.

Ogopa mno mwenzi ambaye haoni cha kupoteza. Huyo anaweza kukufanyia jambo baya wakati wowote. Anaweza kuanzisha uhusiano mwingine katika kipindi ambacho bado unamhitaji. Anaweza kukuacha na asijali maumivu yako. Hivyo basi, tazama uendako, mtathmini mwenzio kama anazo sifa zinazofaa kisha amua kwa faida yako mwenyewe.

HESHIMAUnahitaji mpenzi ambaye anajiheshimu. Weka akilini hilo halafu lifanye kuwa muongozo wa maisha yake ya kimapenzi. Heshima ina matawi mengi lakini muhimu kwako ni kuwa lazima awe anakidhi vipengele vyote. Wengi wanateswa na mapenzi leo hii kwa sababu hawakuzingatia kipengele cha heshima wakati wanaamua kuhusu hatma ya uhusiano wao.

Lazima awe anajiheshimu. Nalisisitiza hilo kwa mara pili kwa sababu kama hana heshima binafsi, maana yake hatakuwa nayo ya kumpa mwingine. Watu wanaojiheshimu ndiyo haohao huwaheshimu na wengine. Nakuomba ulizingatie hili kwa umakini mkubwa kwa sababu huamua furaha ya wapenzi, wachumba na hata wanandoa.

Mtu asiyejiheshimu anaweza kufanya jambo lolote na wakati wowote. Anaweza pia kutoheshimu umuhimu wa mwenzi wake. Tia akilini kuwa mtu asiyejiheshimu huwa hana soni mbele ya macho ya jamii. Anaweza kugombana na watu sehemu yoyote hata ukweni kwake. Anaweza kuvaa nguo za ‘kishenzi’ ambazo zitamuacha kwenye aibu mwenzi wake.

Yeye hawezi kuona aibu, kwani hajiheshimu. Binadamu wengi hujipa mizigo mibaya kwa kuzoa watu ambao hawajui kujistahi, mwisho wanapata tabu kuwarekebisha. Wanasema, samaki mkunje angali mbichi, sasa wazazi wake na familia yake, walishindwa kumuweka sawa, wewe utawezaje wakati ameshakubuhu? Tia akilini.

IPO HAJA YA MFUMO WA UONGOZI KUTUNGIWA SHERIA KATIKA KATIBA MPYA

                                    Mwenyekiti wa Chadema taifa, Freeman Mbowe.

HAKIKA Mungu ni mwema kwani ametufanya tukutane tena leo katika safu hii lakini pia tumshukuru kwa kuweza kutuwezesha kuuona mwaka 2013.
Baada ya kusema hayo nizungumzie kwa ufupi kuhusu  ushauri uliowahi kutolewa na Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe akiishauri serikali kuandaa mfumo na utaratibu wa kikatiba na kisheria utakaoiwezesha nchi kuepuka machafuko na vurugu iwapo chama chochote hasa cha upinzani kitachaguliwa na wananchi kuongoza nchi baada ya  kile kinachotawala kuondolewa madarakani.

Ushauri huo wa Chadema ulitolewa na Mbowe alipokuwa akihutubia mikutano ya wilayani Mbozi, mkoani Mbeya mwishoni mwa mwaka jana.
Alisema kutokana na vuguvugu la siasa za mabadiliko zinazoendelea hapa nchini, ni fursa nzuri na wakati muafaka nchi yetu ikawa na mfumo mzuri wa kikatiba na kisheria kwa ajili ya kusimamia mabadiliko ya uongozi ili yafanyike kwa amani, hivyo kuepusha nchi kuingia katika vurugu na mikanganyiko ya kisiasa.

Kiongozi huyo wa chama hicho alisema, ingawa hiyo inaweza kuonekana kuwa ni dhana mpya, ni vyema Watanzania wakaanza kuitafakari kutokana na umuhimu wake katika mustakabali wa nchi yetu.
Binafsi wazo hilo la Mbowe linafaa kupongezwa bila kujali ni lini chama tofauti na chama tawala kinaweza kupata ushindi katika kuongoza nchi. Nasema tamko hilo linaonekana dhahiri kwa mtu yeyote mwenye mapenzi mema na nchi yetu kwamba limeweka mbele maslahi ya taifa na wananchi wote kuliko kitu kingine chochote.

Hadhari anayotoa kiongozi huyo wa chama kikuu cha upinzani nchini ni kuwa, ni hatari kubwa kwa nchi kama yetu ambayo sasa inapitia kwenye mawimbi ya mabadiliko kutokuwa na mfumo huo ambao huhakikisha mabadiliko ya mpito kutoka serikali moja kwenda nyingine yanafanyika kwa amani na maslahi ya nchi yanalindwa bila kutetereka.

Zanzibar wameanza, wao wameamua katika katiba yao kushirikisha chama cha pili kwa ushindi katika uchaguzi kuunda serikali. Hakika uamuzi ule ni mzuri sana na tumeona jinsi ambavyo umeepusha vurugu za kisiasa kwa sababu haiwezekani chama ambacho kimechaguliwa na wengi na kutofautiana kwa kura chache na kilichoshinda kukiacha bila kukishirikisha katika serikali.

Lakini ipo mifano hai ya jambo hili kwa  mfano nchi ya  Ghana iliyopitia misukosuko kutoka katika utawala wa Rais Jerry Rawlings kwenda kwa chama cha upinzani cha Rais John Kufour kilichoshinda uchaguzi mkuu nchini humo na kuunda serikali, walipata fundisho kiasi kwamba baada ya Rais Kufour kuingia madarakani serikali yake ilitunga sheria ya ‘kipindi cha mpito’ kutoka serikali moja kwenda nyingine.
Ukiangalia mfumo wa Marekani kwa mfano,  inachukua takribani miezi miwili na nusu kwa rais mpya kuapishwa na kukabidhiwa rasmi madaraka ya kuongoza nchi tangu achaguliwe. Hii ni kwa sababu kuna mambo muhimu sana ya kufanyiwa kazi kabla utawala mpya haujakabidhiwa Ikulu.

Tofauti sana na nchi za Kiafrika kwa mfano hapa nchini inachukua saa 48 pekee kwa uongozi mpya kukabidhiwa madaraka baada ya kiongozi wa nchi kuchaguliwa, hivyo ni wazi hali hiyo ni hatari kwa sababu kuna mambo ya msingi ambayo yanahitaji muda wa kutosha katika kufanya makabidhiano.
Nakubaliana na wazo la Mbowe kwa asilimia 100 anapotoa mfano wa wizi wa mabilioni ya fedha za ufisadi katika Akaunti ya Madeni ya Nje (Epa) hapa nchini mwaka 2010 kwamba fedha hizo zilikwapuliwa na mafisadi kirahisi kutokana na kutokuwepo  mfumo na sheria za kusimamia kipindi cha mpito. Hali hiyo ni mbaya na nchi yetu haiwezi kuvumilia tena kuona ikijirudia.
Nakubaliana pia na Mbowe anaposema sasa ni wakati muafaka kwa nchi yetu kuanza kufikiria kuwa na mfumo wa kikatiba na kisheria kuhusu kipindi cha mpito kutoka serikali moja kwenda nyingine kwani usipokuwepo, wakati wa makabidhiano ya madaraka unajitokeza wasiwasi mkubwa ambao hakika unaibua maswali mengi.

Maswali ya msingi ni nani anasimamia kikamilifu rasilimali za umma wakati huo? Nini hatima ya watumishi wa umma, majeshi yetu na nyaraka za siri za serikali, ulinzi na usalama wa nchi yetu? Haiwezekani serikali mpya iingie madarakani kienyeji bila kuwepo muda muafaka wa makabidhiano.
Hiyo ni changamoto kubwa kwa Serikali ya Rais Jakaya Kikwete na pengine kwa Tume ya Marekebisho ya Katiba inayoendelea na kazi yake hivi sasa chini ya uongozi wa Jaji Mstaafu, Joseph Warioba.

Watanzania wote tusiangalie ushauri huu kupitia mboni za kiitikadi, isipokuwa upokelewe na kufanyiwa kazi kwa kuzingatia maslahi ya nchi yetu na watu wake. Ndiyo maana nasema wazi kwamba katiba mpya ni lazima iyazingatie haya.

JK.Azindua Matokeo Ya Sensa Ya Watu Na Makazi 2012.

Rais Jakaya Kikwete akibonyeza kitufe kwenye kompyuta kuzindua matokeo ya Sensa ya Watu na Makazi mwaka 2012  jana jijini Dar es salaam ambapo idadi ya watu Tanzania imefikia milioni 44 929 002.
Rais Jakaya Kikwete akiwa katika picha ya pamoja  kwenye bango linaloonyesha idadi ya watu Tanzania na viongozi na watendaji wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu mara baada ya kutangazwa kwa matokeo ya sensa ya watu na makazi ya mwaka 2012.
Picha na Aron Msigwa -MAELEZO

Magazeti ya leo Jumanne ya 1st january 2013





Happy New Year


Wapenzi wa Tanzania Asilialive Nawatakia Heri ya mwaka mpya wenye mafanikio. tuendelee kulijenga taifa letu.