Thursday, January 17, 2013

Push Mobile, Channel Ten kutoa zawadi ya gari Valentine Day

 Meneja Mauzo na Masoko wa Push Media Mobile, Rodney Rugambo akisisitiza jambo wakati wa uzinduzi wa shindano la kampeni maalum ya kuadhimisha sikukuu ya wapendanao ‘ Valentine Day’ iliyoandaliwa kwa kushirikiana na Kampuni ya African Media group (AMG) kupitia kituo cha televisheni cha Channel Ten na Redio Magic FM. Kushoto ni AFISA Masoko na Mauzo wa AMG,  Prosper Vedasto

KAMPUNI ya Push Media Mobile itatoa zawadi ya gari aina ya Vitz lenye thamani ya shs milioni 8 kwa mshindi wa kampeni maalum ya kuadhimisha sikukuu ya wapendanoa “Valentine Day” ikayoa adhimishwa Februari 14

Hayo yalisemwa na Meneja Mauzo na Masoko wa Push Media Mobile, Rodney Rugambo katika uzinduzi wa kampeni hiyi pamoja na Kampuni ya African Media group (AMG) kupitia kituo cha televisheni cha Channel Ten na Redio Magic FM.

MAKAMO MWENYEIKI CCM ZANZIBAR DK. SHEIN, AZUNGUMZA NA VIONGOZI OFISI KUU YA CCM KISIWANDUI


 Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar,na Rais wanZanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akisisitiza jambo alipokua akizungumza na  Viongozi wa Tawi la CCM Afisi Kuu ya CCM Kisiwandui,wakiwemo Viongozi wa  Jumuiya mbali mbali za Chama  hicho katika ukumbi wa Afisi Kuu ya CCM Kisiwandui Mjini Zanzibar jana,Makamo  Mwenyekiti alifanya ziara maalum ya kusalimiana na Viongozi hao ikiwa  ni pamoja na  kuimarisha Chama cha Mapinduzi,(CCM) (kulia) Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Vuai Ali Vuai

Mama Salma Kikwete afunga kongamano la Ulimwengu la afya ya uzazi mjini Arusha

Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisisi ya WAMA , Mama Salma Kikwete akifunga kongamano la Ulimwengu la Afya ya Uzazi la  siku 3 Katika ukumbi wa mikutano ya kimataifa AICC mjini Arusha leo, Kongamano hilo lilewashirikisha wataalamu wa masuala ya afya ya  uzazi wapatao 800 kutoka mataifa mbalimbali ulimwenguni,

SERIKALI YABARIKI FAINALI ZA TAIFA MISS UTALII TANZANIA 2012/13

Serikali ya Jamuhuri ya muungano wa Tanzania, kupitia Baraza la Sanaa la Taifa, limebariki kufanyika kwa Fainali za Taifa za Miss Utalii Tanzania 2012/13 baada ya kuridhishwa na maandalizi yaliyo fanywa na Miss Tourism Tanzania Organisation waandaaji wenye dhima ya kikomo ya kuandaa na kuendesha mashindano hayo kitaifa na kimataifa, pia kwa kuzingatia sheria za nchi, kanuni na Taratibu za mashindano.

Serikali pia imeridhishwa na jinsi Fainali za ngazi za mikoa na kanda zilivyofanyika kwa mafanikio,ambapo kila mkoa umepata washindi wenye sifa za kuwakilisha mkoa husika katika Fainali za Taifa mwaka

36 WACHUKUA FOMU TFF, 18 WAREJESHA

Wakati kesho ndiyo mwisho wa kuchukua na kurejesha fomu za kuwania uongozi kwenye uchaguzi wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) na Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPL Board) waombaji 36 wameshachukua na 18 tayari wamesharejesha.

Idadi hiyo ni kufikia leo mchana (Januari 17 mwaka huu). Pia Kamati ya Uchaguzi ya TFF inasisitiza kuwa wanaorejesha fomu hizo kwa email wanatakiwa kuzituma kwa Katibu Mkuu wa TFF kwa email ya to= tfftz@yahoo.com" target="_blank"> tfftz@yahoo.com na si kwa email binafsi za wajumbe wa Kamati ya Uchaguzi au maofisa wa TFF.

Waombaji wanne walioongezeka katika orodha ni Blassy Kiondo kwa Kanda ya Katavi na Rukwa, Eliud Mvella (Mbeya na Iringa), Geofrey Nyange (Morogoro na Pwani), na Omari Abdulkadir kwa Kanda ya Dar es Salaam.

Orodha kamili ya waombaji ni Athuman Nyamlani, Jamal Malinzi na Omari Mussa Nkwarulo (urais) wakati waombaji wa umakamu wa rais mpaka sasa ni Michael Wambura, Ramadhan Nassib na Wallace Karia.

Magazetini leo Alhamis ya 17thJanuary 2013

















Waziri Simba akabidhi vyerehani kwa wajane

 Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Mhe. Sophia Simba akimsikiliza Gavana wa Lions Ukanda wa Uganda na Tanzania, Joseph Kiwanuka, wakati alipomtembelea leo ofisini kwake akiwa na ujumbe wa watu watano.
 Waziri Simba akiangalia baadhi ya vyerehani viwili viliyotolewa na Lions kwa ajili ya kuwasaidia wanawake wajane. Vyerehani hivyo ni kati ya 100 vitakavyotolewa na Lions kuwawezesha wanawake kujikimu kimaisha.
 Waziri Simba akimkabidhi mmoja wa wafaidi wa vyerehani vilivyotolewa na Lions Bi. Jane Fuiko wakati wa hafla fupi ya kuwakabidhi zilizofanyika leo ofisini kwa Waziri.

WAFANYAKAZI OFISI YA WAZIRI MKUU WATOA MAONI YA KATIBA MPYA

 Mjumbe wa Sekretarieti ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Bi. Hanifa Masaninga (kushoto) akitoa ufafanuzi kuhusu mfumo uandaaji wa maoni ya wananchi katika taarifa rasmi (Hansard) kwa wafanyakazi kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI)wakiongozwa na Kaimu Katibu Mkuu, Bw. Jamanne Sagini (wa pili kushoto) wakati waliotembelea ofisi za Tume hiyo
 Mjumbe wa Sekretarieti ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Bi. Nenelwa Mwihambi (kulia) akitoa maelezo kuhusu mfumo wa uchambuzi wa maoni ya wanachi kwa wafanyakazi kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI)wakiongozwa na Kaimu Katibu Mkuu, Bw. Jamanne Sagini (Kaunda suti nyeupe) wakati waliotembelea ofisi za Tume hiyo