Saturday, September 1, 2012

DIAMOND AWASILI WASHINGTON TAYARI KWA SHOW USIKU WA LEO


                    Diamond na madansa wake wakiwa Na Miss Temeke mara baada ya kuwasili DC
                                          Picha ya pamoja na Waandaaji wa show Ya Leo

TANAPA Waunda Kikosi Kazi Kupambana Na Ujangili Wa Watalii Na Wanyama

Shirika la hifadhi za taifa(Tanapa) na mamlaka ya hifadhi za Ngorongoro (Ncca) wakishirikiana na Jeshi la Polisi wameunda kikosi kazi katika vita ya kupambana na ujangili na uhalifu kwenye mbuga za Ngorongoro.Manyara,Tarangire na Serengeti katika kudhibiti ongezeko la ujangili haramu kwenye mbuga hizo.

Akizungumza na waandishi wa habari Ofisini kwake Kamanda wa upelelezi mkoa wa Arusha Kamilus Wambura alisema kwamba kama hatutatumia kikamilifu wimbi la vurugu zinazotokea kwa wenzetu wan chi ya jirani na watalii wengi kuhamia nchini kwetu kwa kuweka ulinzi shirikishi kati yetu na mamlaka za hifadhi ya wanyama pori basi badala ya watalii hao kuja watatukimbia hivyo kupoteza mapato kwa taifa letu.

Wambura alisema kuwa watanzania wamejaaliwa kuwa na mbuga nzuri zenye vivutio na wageni wengi sasa wanakuja kutembelea mbuga hizo ukifika kwenye hotel zetu huko mbugani kwa siku hadi wageni 900 wanalala kama hatukuwalinda mali zao na usalama wao watatukimbia.

“Wageni hawa ni wengi sana ndugu waandishi tunatakiwa kuwalinda wao na mali zao ilikuwa mabalozi wazuri wa kuitangaza Tanzania huko kwao na kueleza mazuri ya nchi yetu kuwa ni mahala salama kwao na malizao”alisema Wambura.

Hivyo tumeunda kikosi kazi katika kulinda wanyama wetu na wageni wetu wanaotembelea mbuga zetu ili kuweza kupata wageni zaidi watakao kuja kutembelea mbuga zetu na kuongeza mapato ya taifa kwa ujumla na kuona Tanzania ni mahali salama pa kutambelea.

Tunaomba pia ushirikiano wenu na wananchi wa maeneo yanayozunguka mbuga hizo na nyingine kutoa taarifa za ujangili au kuwepo tetesi zozote za kuwepo majangili na majambazi ilikurahisisha zoezi hili wanyama ni tunu tuliojaaliwa na mungu tunaowajibu wakuilinda.

Hebu fikiri mnyama kama Tembo ukubwa wake halafu anauawawa kwa ajili ya vipembe vidogo tu tuwe na huruma kwa wanyama na mbuga zetu sisi polisi na mamlaka husika tutawalinda kwa nguvu zetu zote.

Pinda - Ashiriki Mazishi Ya Askofu Kikoti Mpanda.

 Waziri Mkuu, Mizengo Pinda kitoa heshima za mwisho kwa marehemu Mhashamu, Askofu Pascal William Kikoti katika ibada ya mazishi iliyofanyika kwenye kanisa kuu katoliki, jimbo la Mpanda, Septemba 1, 2012.
 Mapadri wakiweka kaburini mwili wa aliyekuwa Askofu wa jimbo la Mpanda Mhashamu Pascal William Kikoti kaburini katika mazishi yaliyofanyika kwenye kanisa kuu la jimbo Katoliki la Mpada Mjini Mapanda Septemba 1, 2012

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akitupa mchanga kwenye kaburi la Askofu Pascal William Kikoti katika mazishi yaliyofanyika kwenye Kanisa Kuu la Katoliki jimbo la Mpanda mjini Mpanda Septemba 1, 2012.


Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu

CHADEMA Leo Wako Marekani-Mapokezi

 Mbunge wa Mbeya Mjini(CHADEMA) Mhe. Joseph Mbilinyi a.k.a Mr. II(wa pili Kushoto)akiwa na Uongozi Mzima wa Tawi la Chama Cha Demokrasia na Maendeleo Chadema DMV kwaajili ya mapokezi
 Mbunge wa Hai, na Mwenyekiti wa CHADEMA Mh. Freeman Mbowe(kushoto)akiwa na Mwenyekiti wa Wanawake CHADEMA Maryam Khamis wapili kulia na Katibu wa wanawake Baybe Leila, wa kwanza kushoto wakiwa katika mapokezi ya kumpokea mgeni rasm wa mkutano wa Jumamosi Mh. Freeman Mbowe.
 Mbunge wa Hai, na Mwenyekiti wa CHADEMA Mh. Freeman Mbowe(Wa nne Kulia) pamoja na Mbunge wa Mbeya Mjini(CHADEMA)Mhe. Joseph Mbilinyi(wa tatu kushoto) wakiwa na wa Chadema DMV
 Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Mh. Freeman Mbowe akiwa na baadhi ya viongozi wa Tawi la Chadema DMV aliopowasili siku ya Ijumaa Aug 31, 2012, kwenye uwanja wa kimataifa Dulles Airport, kwaajili ya mkutano utakaofanyika Siku ya Jumamosi Spet 1,2012.
Mkutana huo utaaza rasmi mida ya saa 4:PM (Kumi za Jioni) Wageni rasmi wamkutano huo ni Mhe. Freeman Mbowe na Mhe Joseph Mbilinyi ADDR. Addr: 9670 Baltimore Ave. College Park. MD 20740

Baada ya mapokezi Katibu wa Tawi la Chadema DMV Mhe. Isdori Lyamuya akiongea mpango mzima wa mkutano utakaofanyika Jumamosi Sept 1, 2012 kwenye ukumbi wa Marriott Hotel Addr: 9670 Baltimore Ave. College Park. MD 20740.

Picha Zote na CHADEMA

SACCO - Yapatiwa Mkopo Wa Matrekta Na Benki Ya Raslimali-TIB

 Matrekta 11  yaliyotolewa mkopo kwa wanachama wa Talanta SACCOS ya tarafa ya Kinyangiri wilaya ya Mkalama Mkoani Singida.
 Mkuu wa mkoa wa Singida,Dk.Parseko Kone, akizungumza na wananchi kisha alikabidhi matrekta makubwa 11 kwa wanachama wa Talanta SACCOS ya tarafa ya Kinyangiri wilaya Mkalama, yaliyotolewa mkopo na Benki ya rasilimali (TIB), kwa gharama ya Sh.Milioni 450.5.
 Mwenyekiti wa Talanta SACCOS tarafa ya Kinyangiri Mayasa Salum,akifurahia trekta alilokopeshwa na benki ya rasilimali (TIB), kupitia SACCOS hiyo
MKUU wa mkoa wa Singida Dk.Parseko Kone akikaribishwa na mmoja wa wanachama wa ‘Talanta SACCOS’ katika kijiji cha Iguguno tarafa ya Kinyangiri wilaya ya Mkalama alipoenda kukabidhi matrekta 11 yaliyogharimu Sh. Milioni 450.5.

Wananchi wametakiwa kujiunga katika vikundi ili kunufaika na mikopo inayotolewa nataasisi za vyombo vya kifedha. Mkuu wa mkoa wa Singida,Dk.Kone,alisema hayo wakati wa kukabidhi matrekta makubwa 11 kwa Talanta SACCOS ya tarafa ya Kinyangiri, wilayani Mkalama, yenye thamani ya Sh. Milioni 450.5 kutoka benki ya raslimali (TIB). Dk. Kone alisema kupitia ushirika wakulima na wananchi kwa ujumla watanufaika na mkakati wa kilimo kwanza.Kwa upande wake mwenyekiti wa Talanta SACCOS, Myasa Salum aliishukru benki hiyo ambayo imelenga kumkomboa mkulima wa kawaida kijijini.

Na: Elisante John,Singida

Zoezi La Sensa Kumalizika Tarehe 8 Septemba 2012

 Kamishna wa Sensa wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS)  Hajjat Amina Mrisho Said akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam kuhusu zoezi la Sensa ya watu na makazi 2012  linaloendelea nchi nzima na kutoa wito kwa wananchi ambao bado hawajahesabiwa kutoa taarifa kwa viongozi wa serikali za mitaa.
Waandishi wa habari wakimsikiliza Kamishna wa Sensa wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Hajjat Amina Mrisho Said (hayupo pichani) leo jijini Dar es salaam wakati akitoa taarifa ya kuongezwa kwa muda wa zoezi la Sensa ya watu na makazi litakalomalizika tarehe 8 Septemba 2012.

 Picha na Aron Msigwa - MAELEZO.

Magazeti ya leo Jumamosi 1st September 2012

 

MATOKEO NA WAFUNGAJI WA MECHI YA ATLETICO MADRID VS CHELSEA,