Tuesday, February 5, 2013

PREZZO NA GOLDIE KUFUNGA PINGU ZA MAISHA FEBRUARI 9

 Kwa mujibu wa mitandao mbalimbali nchini Nigeria, rapper Jackson Makini aka Prezzo anatarajia kufunga ndoa na mwanamuziki wa Nigeria Goldie February 9.

Habari hiyo pia imeandikwa na website ya Big Brother Africa. Harusi hiyo itafanyika jijini Lagos, Nigeria.

Katika hatua nyingine mwakilishi wa mwaka jana wa Nigeria kwenye shindano la Big Brother Africa, anatarajia kuanzisha Reality TV show yake.Goldie anaanzisha show hiyo iitwayo ‘Tru Friendship’. ‘Tru Friendship’ itaonesha maisha ya kila siku ya muimbaji huyo wa Skibobo, Goldie, yote kama mtu maarufu na kama Susan Harvey.

Show hiyo itaanza kuonekana mwishoni mwa mwezi huu.

"JAPO KUNA WATU WANANIPONDA, LAKINI BIG BROTHER LAZIMA NITASHIRIKI"....T.ID

Nia ya Khalid Mohamed aka Top in Dar kutaka kushiriki shindano la Big Brother Africa mwaka huu iko pale pale licha ya kuwepo watu walionza kumkatisha tamaa.

Kupitia Facebook TID ameandika, “A Bad Company always corrupt a good character…I wont accept that, I WILL Be in a Big Brother Superstarz.”

Mwandishi wa ripoti hii  amempigia simu TID kutaka kupewa ufafanuzi wa alichokiandika ambapo amesema alimaanisha kuwa tangu Bongo5 imtaje kuwa miongoni mwa mastaa wanaoweza kuwa wawakilishi wazuri wa Tanzania katisha shindano hilo mwaka huu na watu wengi kumuunga mkono, kumetokea watu wachache wanaosema hatoweza.

TID amesema maneno hayo hayamkatishi tamaa na kwamba msimamo wake wa kuchukua fomu kujaribu bahati yake uko pale pale ambapo anatarajia kuichukua wiki hii.

“Hey bro! jst trust in urself go there n bliv t or not u gonna do smthng splendid,i adore u as wel as im ur fan so i bliv u wil do smthng so splendid and we as tanzanians we bliv in t…wsh ya ol da best, ” aliandika shabiki wake mmoja.

“As i have been buying ur albums,listening to your music,watching your videoz,come to ur show’z and many more……my positive support by VOTING alooooooooooooo……t for U@Tid Tid Topband,” aliandika mwingine.

MAMA STEVEN KANUMBA AJA NA FILAMU YA "WITHOUT DADDY."

 MAMA Mzazi wa msanii nyota Tanzania marehemu Steven Kanumba ‘Kanumba’ Frola Mtegoa ameigiza filamu katika muendelezo wa kipaji cha mwanaye baada ya kuigiza katika filamu ya Without Daddy akishirikiana na watoto waliokuwa wakiigiza na marehemu Kanumba kama Patrick na Jamila, katika filamu hiyo mama Kanumba kaigiza katika kiwango cha juu.

HALI YA MSANII "MATUMAINI BADO NI MBAYA...ZOEZI LA KUMRUDISHA NYUMBANI TOKA MSUMBIJI BADO HALIJAFANIKIWA

 Waigizaji zaidi ya 30 ambao jumapili february 3 2013 walijitokeza kumpokea mwigizaji mwenzao mgonjwa Matumaini, walirudi mikono mitupu baada ya mwigizaji huyo aliekua anatarajiwa kuwasili Tanzania akitokea Msumbiji kushindwa kufanya hivyo chanzo kikiwa ni hati yake ya kusafiria ambayo akiwa uwanja wa ndege aliagizwa kuishughulikia kwenye ofisi za uhamiaji ambazo zipo mbali na uwanja wa ndege.
.
Matumaini amekua Msumbiji kwa wiki kadhaa alikokwenda kufanya show lakini muda mfupi baadae mambo yakageuka na kuanza kuumwa miguu, mwigizaji huyu anatarajiwa kuwasili Dar jumanne au jumatano na tayari umoja wa waigizaji umepanga kumpeleka hospitalini moja kwa moja.
                                                                Waigizaji waliokwenda kumpokea.

BINTI WA MIAKA 13 AFANYIWA KITCHEN PARTY.....POLISI AINGILIA KATI

 Tukio hilo la kusikitisha na kuhuzunisha limetokea Jumatano ya wiki iliyopita ambapo Gpl ilikuta Rafia akiwa katika sherehe hizo huku ndoa yake ikitarajiwa kufungwa leo Februari 2.

Hakuna lugha nyepesi unayoweza kuzungumza zaidi ya kusema haya ni maajabu ya mwaka 2013, kwani familia ya Masoud Kassim wa Karakata Ukonga Dar imejikuta ikiingia kwenye mgogoro wa kisheria baada ya kuamua kumfanyia ‘kitchen party’  mtoto wao wa miaka 13 aitwaye Rafia Masoud, tayari kwa ndoa.
 akiingizwa kwenye gari ambapo alipelekwa Kituo cha Polisi, Stakishari kwa mahojiano zaidi.




  Binti huyo (kushoto) akiwa chini ya ulinzi wa polisi akitolewa ndani na kuingizwa kwenye gari

 Akina mama walikokuwa katika sherehe hiyo wakitahamaki baada ya kachero wa polisi kujitambulisha

WOLPER AFICHUA SIRI YA UREMBO WAKE


Msanii wa filamu Tanzania Jackline Wolper hatimaye amefichua siri ya urembo wake kitu kinachomfanya aendelee kuonekana kuwa  mrembo na kubaki na mvuto wake wa asiri

Akizungumza na Pro-24 ,Wolper alijikuta akiweka wazi anachokifanya ili kuendelea kubaki na urembo huo huku akisisitiza kuwa mazoezi ya viungo vya mwili na kutokunywa bia ni siri kubwa ya urembo wake

Wolper hakusita kuweka wazi kuwa yeye ni mtu wa kula mbogamboga,samaki, maziwa na matunda kwa wingi huku akipata muda wa kupumzika ili kujenga mwili wake bila ya kusahau kunywa maji kwa wingi kwani hayo yanamfanya ngozi yake iendelee kuwa yenye mvuto

Wolper alisisitiza kuwa katika maisha yake hutumia kula nyama nyeupe na kuepuka nyama nyekundu ili aendelee kubaki hivyo alivyo na kuepuka kuwa mnene na kutoka kitambi kama baadhi ya wanawake wengine wanavyokuwa

WEMA SEPETU ACHUKUA FORM YA KUSHIRIKI BIG BROTHER AFRICA





Taarifa kutoka ofisi za DSTV jijini Dar es Salaam zinadai kuwa aliyekuwa Miss Tanzania mwaka 2006 na muigizaji wa filamu Wema Sepetu alikuwa katika ofisi hizo kuchukua fomu za kushiriki shindano la Big Brother Africa mwaka huu.

Wema ni miongoni mwa mastaa nchini wanaopendekezwa zaidi kuiwakilisha Tanzania mwaka huu. Mwingine anayependekezwa zaidi ni Khaleed Mohamed aka TID



NIMEMALIZA KWA LULU NAHAMIA KWA KAJALA"..DK. CHENI

STAA aliyekuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha msanii wa filamu Elizabeth Michael ‘Lulu’ anapata dhamana, Mahsein Awadh ‘Dk. Cheni’ amefunguka kuwa baada ya kufanikiwa kwa Lulu sasa anahamia kwa msanii mwingine, Kajala Masanja.    

Akizungumza nje ya Mahakama Kuu jijini Dar baada ya Lulu kuachiwa, Dk. Cheni alisema kwa sasa anaanza mchakato wa kumsaidia Kajala mpaka ajue hatima ya kesi  inayomkabili.

“Unajua Lulu siyo mtu wa kwanza kumsaidia na mama yake ndiye aliniomba, nilishawasaidia wengi.

Hata Cloud alipofungwa nilifuatilia mimi na Dude mpaka mwisho, hatukukata tamaa na kwa Kajala nitafanya hivyo kwa sababu ni mwenzetu jamani, naamini Mungu anaweza sana na atafanikisha kila kitu,” alisema Dk. Cheni.

Kajala anasota Segerea akikabiliwa na kesi ya kuuza nyumba iliyokuwa imewekwa bondi na serikali kutokana na mumewe kutakatisha fedha haramu.

magazeti ya leo Jumanne ya 5th February 2013



Hoja binafsi ya Mh.Mnyika iliyoleta balaa bungeni


Mheshimiwa Spika;
Awali ya yote niungane na wote wenye mapenzi mapema katika kuomba ulinzi wa Mwenyezi Mungu wakati tukitimiza wajibu wa kibunge kwa mujibu wa ibara ya 63 ya Katiba ya Jamhuri wa Muungano wa Tanzania wa kuwawakilisha wananchi, kuisimamia serikali, kuidhinisha mipango na kutunga sheria.

Mheshimiwa Spika;
Aidha, kwa namna ya pekee ni kushukuru wewe binafsi na uongozi mzima wa Bunge kwa kunipa fursa hii adimu na adhimu ya kuwasilisha hoja binafsi kwa mujibu wa kanuni ya 54 fasili ya (1) ya kupendekeza bunge lijadili na kupitisha maazimio ya hatua za haraka zaidi za kuboresha upatikanaji wa maji safi na ushughulikiaji wa maji taka katika Jiji la Dar es salaam.