Friday, June 14, 2013

RATIBA YA MAZISHI YA MSANII LANGA KILEO ALIYEFARIKI JANA

Ratiba ya mazishi ya ndugu yetu Langa Kileo itakuwa kama ifuatavyo, msiba upo nyumbani kwa wazazi wa Langa maeneo ya Mikocheni nyuma ya Hospitali ya AAR zamani kulikuwa na ofisi za Benchmark Production.

 Mwili wa marehemu utaagwa siku ya Jumatatu majira ya saa 7 mchana na baada ya hapo mwili utaelekea makaburi ya Kinondoni kwa mazishi majira ya saa kumi alasiri.

KINANA AMBURUZA KORTINI MBUNGE MSIGWA BAADA YA KUMWUITA JANGILI

KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Abdul-rahman Kinana amemfungulia kesi Mbunge wa Iringa Mjini, Peter Msigwa (Chadema), kutokana na kumtuhumu anajihusisha na ujangili na biashara haramu ya pembe za ndovu.

Kinana amefungua kesi hiyo katika Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam kutokana na kitendo cha Mbunge huyo kutoa tuhuma hizo dhidi yake kwa nyakati tofauti nje na ndani ya Bunge, pia alikataa kuzikanusha na kumuomba radhi.

Inadaiwa kuwa Aprili 21 mwaka huu Msigwa ambaye ni Waziri Kivuli wa Maliasili na Utalii alitoa tuhuma hizo kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika Shule ya Msingi Mbuguni wilayani Nyamagana mkoani Mwanza.

KILICHOSEMWA NA HOSPITALI YA MUHIMBILI KUHUSU KIFO CHA MSANII LANGA

Aminiel Aligaesha ambae ni Afisa Uhusiano wa hospitali ya Taifa Muhimbili amethibitisha kwamba msanii Langa amefariki dunia June 13 2013 saa kumi na moja jioni baada ya kufikishwa hospitalini hapo toka juzi jioni ambapo kutokana na sababu za kimaadili kwenye tiba, Muhimbili hospitali hawawezi kusema rapper huyu alikua anaumwa nini bali ndugu ndio wenye mamlaka ya kufanya hivyo.

Kwenye maelezo aliyoyatoa kwa millardayo,  Aminiel amesema Marehemu Langa alipokelewa kwenye idara ya wagonjwa wa magonjwa ya dharura usiku wa kuamkia jana na kupatiwa huduma ambapo June 13 2013 ndio alihamishiwa kwenye chumba cha wagonjwa Mahututi na baadae kufariki dunia.

 MillardAyo

MSANII LANGA AFARIKI DUNIA

                                               Langa Kileo (msanii wa Hip Hop Tanzania, pichani)
Habari zilizotufikia hivi punde ni kwamba msanii Langa amefariki dunia..
Habari zinadai  kuwa , Msanii huyu alikumbwa na Malaria kali sana hali iliyopelekea kukimbizwa Hospitali ya Muhimbili jana.

LADY JAYDEE NA MWANAFA KESHO HAPATOSHI....SUGU AMPA SHAVU LADY JAYDEE NA ZITTO KABWE KALALA KWA MWANAFA

Ile the Big Square 1, show za magwiji wa muziki Tanzania mwana FA ‘The Finest’ na Lady Jay Dee ‘Miaka 13 ya Lady Jay Dee’ zitapigwa kesho June 14, huku presha ikiwa inaongezeka hasa kwa fans wanaotamani kuhudhuria show walioichagua na kuona ukubwa wa show kama walivyotarajia.

Show hizi kubwa zina nguvu sana kutokana na ukubwa wa majina ya wasanii husika. Kwa mujibu wa lady Jay Dee timu anaconda kesho itaungwa mkono na mheshimiwa Joseph Mbilinyi a.k.a Sugu.

Jide ambae hivi karibuni ameachia wimbo mpya unaopatikana kwenye album yake ‘Nothing but the truth’ inayoitwa Yahaya, amepost kupitia kupitia ukurasa wake wa facebook na pia katika akaunti yake ya Twitter kuonesha list ya wasanii watakaopanda jukwaani, na pia uwepo wa Sugu.