Saturday, June 30, 2012

WINFRIDA DOMINIC NDIYE MISS UNIVERSE TANZANIA 2012

Miss Universe Tanzania 2012, Winfrida Dominic(katikati) akiwa na mshindi wa pili,Bahati Chando(kushoto) na Dorice Mollel(kulia)-Picha kwa hisani ya Taji Liundi

Shindano la kumtafuta Miss Universe Tanzania 2012, limemalizika hapa jijini Dar-es-salaam na Winfrida Dominic,mshiriki kutoka Dar-es-salaam,ameibuka mshindi.


Picha kwa hisani ya Taji Liundi

Dk. Steven Ulimboka nakumbuka kila kitu

NI juu ya kilichompata alipotekwa na watu wasiojulikana, muda mfupi baada ya kuokotwa akiwa taabani, mwenyekiti wa Jumuiya ya Madaktari nchini, Dk. Steven Ulimboka amefunguka kuwa alinusa kifo.

Akisimulia tukio hilo, Dk. Ulimboka alisema kuwa alipigiwa simu na mtu aliyejitambulusha kwake kuwa anaitwa Hemed, aliyemwambia kuwa anahitaji kuongea naye, ndipo walipopanga kuonana kwenye Viwanja vya Leaders Kinondoni, Dar.

Dk. Ulimboka aliyekuwa akizungumza kwa tabu, alisimulia kuwa wakati akiongea na mtu huyo anayekiri kuwa alikuwa wakifahamiana naye kabla, alikuwa na wasiwasi kwani kila mara mtu huyo alikuwa akipokea simu na kuwasiliana na watu wengine ambao hawakuwapo eneo hilo.

Dk. Ulimboka alisema kuwa baada ya muda alishangaa kuona wanaongezeka watu wengine watano wakiwa na silaha, kisha wakamwambia kuwa anahitajika kituo cha polisi na kumvuta na kumuangusha barabarani kabla ya kumuingiza katika gari lenye rangi nyeusi na kuondoka naye.

Dk. Ulimboka alisema kuwa, wakiwa njiani walimpiga na kumfikisha katika Msitu wa Pande na kuendelea kumpiga mpaka alipopoteza fahamu.

Ilielezwa kuwa jamaa hao walimwacha na kuondoka wakiwa na uhakika kuwa amekufa kumbe alikuwa amepoteza fahamu tu hadi alipookotwa asubuhi.

Irine Sizari ndiye Redds Miss Ubungo 2012

Redds Miss Ubungo 2012, Irine Sizari, akipunga mkono kwa furaha mara baada ya kutangazwa kuwa mshindi wa shindano hilo na kuwabwaga warembo wengine 14 usiku huu katika Ukumbi wa Land Mark Hotel jijini Dar es Salaam.
Redds Miss Ubungo 2012, Irine Sizari (katikati) akipunga mono baada ya kuvukwa taji hilo na kupata tiketi ya kushiriki Miss Kinondoni 2012. Kushoto ni Mshindi wa Pili, Mwantumu Mustafa na kulia ni Mshindi wa tatu, Antonia Nyaragwinda. Shindano hilo limefanyika Juni 29, 2012 kuamkia Juni 30.
Baadhi ya warembo wa miss Ubungo wakipita jukwaani na vazi la ubunifu

PICHA KWA HISANI YA BLOGU YA FATHER KIDEVU

MAGAZETI YA LEO JUMAMOSI JUNE 30


WAZIRI FENELLA MUKANGARA APATA AJALI YA GARI

                     Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dkt. Fenella Mukangara.

Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dkt. Fenella Mukangara amepata ajali ya gari wakati akielekea jijini Mwanza Jana. Waziri Mukangara amepata ajali hiyo mkoani Tabora wakati akielekea jijini Mwanza kwenye Ufunguzi wa Mashindano ya Taifa ya Mchezo wa Vishale (Darts). Gari la Mukangara limegongana na basi la Green Star na waziri huyo amelazwa kwa matibabu.

DEIDRE LORENZ KUITANGAZA TANZANIA

Deidre Lorenz akihojiwa na waandishi wa habari mjini Moshi.…
Deidre Lorenz akimkabidhi picha ya Ground Zero (New York) Rais wa Mt. Kili Marathon 1991, Onesmo Ngowi baada ya kukimbia mbio hizo.

Mcheza sinema maarufu wa Marekani Deidre Lorenz ameahidi kuleta wacheza sinema wenzake na kushiriki kwenye mbio za mwaka kesho za mt. Kilimanjaro Marathon zitakazokuwa zinatimiza miaka 23 tangu zianzishwe mwaka 1991.

Lorenz aliyekimbia mbio za mwaka huu ambazo zilipewa jina la “mbio za kutimiza miaka 50 ya uhuru wa Tanganyika” na Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) amesema kuwa atakuja na timu yake ya wapiga picha ili kupiga picha vivutio kadhaa vya Tanzania ikiwa ni pamoja na mlima Kilimanjaro. Gwiji hili la sinema za Santorini Blue, The Great Fight, Perfect Strangers na nyingine nyingi ameelezea kuipenda sana Tanzania.

“Sikutegemea kuikuta nchi nzuri kama hii” alisema mcheza sinema huyo ambaye ameshawahi kuchaguliwa zaidi ya mara 4 kugombea tuzo maarufu za Oscar. “Sasa nimeamini kuwa mlima Kilimanjaro ni mali ya Tanzania na nitautangaza katika sinema zangu zote”aliendelea kusema Deidre Lorenz.

Mcheza sinema huyu ambaye ameingia kwenye mkataba na kampuni kubwa ya Google hivi karibuni ili kuuza sinema zake katika mtandao aliielezea Tanzania kama nchi nzuri na yenye watu wakarimu sana.

Mbio za Mount Kilimanjaro Marathon zilianzishwa mwaka 1991 na Marie Frances anayetoka katika jiji la matajiri la Bethesda nchini Marekani baada ya kuombwa na balozi wa zamani wa Tanzania nchini Misri. Tangu kuanzishwa kwake mbio hizi zimekuwa zinaleta watalii matajiri katika mji wa Moshi kupanda mlima Kilimanjaro na kukimbia mbio hizi zinazojulikana kama Seven Continental Races.

Hakuna masharti yote ya kukimbia mbio hizi na watanzania wanaoshiriki katika mbio hizi huwa hawatozwi pesa za kiingilio.

Kwa kutambua mchango wake katika uchumi wake Manispaa ya Moshi iliibadilisha jina barabara ya zamani ya Bustani Ale na kuiita Marie Frances Boulevard ili kumuenzi mama huyu aliyejitolea maisha yake kuutangaza mlima Kilimanjaro.

“Kila siku napokea ujumbe kutoka nchi mbalimbali niende huko kuanzisha mbio za marathon lakini kwa sasa basi” alisema mama huyo aliyekuwa mtayarishaji wa vipindi vya televisheni ya ABC kabla ya kunzisha Mt. Kilimanjaro Marathon.

Alisema kuwa mwaka jana yeye na Rais wa klabu ya Mt. Kilimanjaro Marathon Mtanzania Onesmo Ngowi walifanya makubaliano ya Ethiopia Airlines (ET) jijini Addis Ababa kuzifanya mbio hizo kuwa za kimataifa zaidi. “ET walikubali kutoa ufadhili kwetu na pia kugharamia kushiriki kwetu katika mbio za New York Marathon, Boston Marathon na Los Angelos Maratthon ili kuitangaza vyema Tanznaia” alibainisha Frances.

Katika makubaliano hayo, Ngowi na Frances pia wataanzisha mbio za “King Solomon Marathon” zitakazofanyika katika jiji la Addis Ababa nchini Ethiopia.

Deidee Lorenz amefungua pazia kwa watu mashuhuri kushiriki katika mbio za marathon nchini Tanzania na ni jukumu la Watanzania kuchangamkia fursa zinazoletwa na ujio wao.

Imetumwa na:

Grace Soka

Afisa Uhusiano

MT. KILIMANJARO MARATHON 1991