Wednesday, June 26, 2013

Mzee Mandela afanyiwa maombi maalum

ASKOFU mkuu wa kanisa la kianglikana mjini Cape Town, Afrika Kusini, Thabo Makgoba, amejitolea kufanya maombi kwa niaba ya rais mstaafu Nelson Mandela ambaye anaugua sana hospitalini.

Kasisi huyo anamuombea Mandela aweze kupata nafuu na amewataka wananchi kumshukuru kwa yote aliyowafanyia.Jamaa za Nelson Mandela wamekutana nyumbani kwake huko Kunu, huku hali yake ya afya ikizidi kudorora hospitalini, Pretoria. Afya ya Bwana Mandela ilikuwa mbaya zaidi Jumapili.

Maombi hayo yalitolewa baada ya Askofuu huyo kumtembelea Mandela hospitalini ambako kiongozi huiyo wa zamani amekuwa akilazwa kwa wiki mbili na nusu zilizopita baada ya kuugua mapafu.

Vyombo vya habari nchini humo vinasema kuwa wajukuu wa rais huyo wa zamani wa Afrika kusini wanakutana nyumbani kwake kijijini katika mkoa wa Eastern Cape province, ambako viongozi wa kitamaduni wamealikwa.

Halikopta ya jeshi kadhalika zilionekana zikipaa karibu nyumbani kwa mandela. Afisi ya Rais jacob Zuma ilitangaza jumapili kuwa hali ya mzee Mandela ya afya ilikuwa mbaya sana.

Chanzo: bbcswahili

Magazeti ya leo Jumatano 26th June 2013






Mzee Mandela bado yuko hali mahututi

RAIS mstaafu wa Mandela Nelson Mandela, bado yuko hali mahututi ingawa madaktari wanadhibiti hali yake baada ya afya yake kuzorota mwishoni mwa wiki.Taarifa kutoka ikulu ya rais zinasema kuwa Mandela angali yuko chini ya uchunguzi wa madaktari ambao wameweza kuidhibiti hali yake.

 Anaugua maradhi ya mapafu na amelazwa hospitalini kwa zaidi ya wiki mbili sasa.Mapema leo familia yake ilimtembelea hospitalini, mzee Mandela ambaye anasifika kwa vita alivyopigana dhidi ya utawala wa wazungu nchini Afrika Kusini.

Amekuwa akiugua ugonjwa wa mapafu mara kwa mara na hii ni mara ya tatu kwa Mandela kulazwa hospitalini mwaka huu.Rafiki na jamaa wameendelea kukusanyika katika hospitali alikolazwa Mandela mjini Pretoria kumtakia afya njema mzee Mandela.

Mmoja wa waliomtembelea Mandela , mfanyabiashara Calvin Hugo, aliawachilia huru njiwa weupe, kama heshima yake kwa Mandela anaeyendelea kuugua hospitalini.Alisema kitendo chake kilikuwa ishara ya, hatua ya Mandela kuikwamua nchi ya Afrika Kusini kutoka kwa mkoloni.

Baadhi ya jamaa zake wamekusanyika nyumbani kijijini eneo la Qunu, kujadili kile wanachosema ni habari muhimu sana.

Chanzo: bbcswahili

UCHAGUZI WA ARUSHA WAAHIRISHWA TENA ILI KUIMARISHA HALI YA AMANI NA UTULIVU

TUME ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imeahirisha tena uchaguzi wa madiwani kata nne za Arusha hadi Julai 14 kuruhusu kurejea utulivu baada ya mlipuko wa bomu kwenye mkutano wa kampeni wa Chadema ulioathiri uchaguzi huo wiki iliyopita.

Bomu hilo lilirushwa Juni 15 na mtu asiyejulikana katikati ya mkutano wa Chadema katika viwanja vya Soweto, mjini Arusha na kusababisha vifo vya watu watatu na wengine kujeruhiwa na uchaguzi huo wa Juni 16 kulazimika kuahirishwa.

Baada ya tukio hilo, Msimamizi wa Uchaguzi wa Arusha aliuahirisha hadi Juni 30, lakini jana Mwenyekiti wa NEC, Jaji Damian Lubuva alisema utafanyika Julai.

Kata zinazohusika ni Elerai, Kimandolu, Thani na Kaloleni. Akizungumza na waandishi wa habari, Jaji Lubuva alisema walipotangaza kuwa uchaguzi ungefanyika Juni 30 waliamini kuwa hali ya utulivu na amani ingekuwa imetengemaa.

ULINZI WA RAIS OBAMA JIJINI DAR NI BALAA....MITAMBO MBALIMBALI YA MAWASILIANO IMEFUNGWA UWANJA WA NDEGE WA KIA

Maandalizi ya ujio wa Rais wa Marekani, Barack Obama nchini yanazidi kupamba moto huku maofisa wa usalama wa Marekani wakipiga kambi katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar es Salaam.

Aidha, kutokana na ujio huo, Serikali imeagiza mashirika yote ya ndege kubadili ratiba zao za safari Julai Mosi, siku ambayo Rais huo atatua nchini.

Jana, waandishi wetu walishuhudia pilikapilika za kuimarisha ulinzi katika uwanja huo jambo ambalo uongozi wa uwanja huo jambo wamelieleza kwamba halijawahi kutokea.

Ulinzi haujawahi kutokea

Mkurugenzi wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Moses Malaki alisema jana kwamba ratiba za uwanjani hapo zitabadilika kutokana na uzito wa ugeni huo.

SERIKALI YATOA TAMKO KUHUSU KAULI YA WAZIRI MKUU...YADAI POLISI WANARUHUSIWA KUPIGA NA KUUA KISHERA

Serikali imetoa tamko bungeni kuhusu mauaji ya raia mikononi mwa polisi ikieleza kuwa sheria ya kanuni ya adhabu inaruhusu kutumia nguvu za kadiri hata kiasi cha kusababisha madhara au kifo.

Kauli hiyo imekuja siku chache baada ya Waziri Mkuu, Mizengo Pinda kunukuliwa bungeni akiwataka polisi kuwashughulikia kwa kuwapiga watu wote wanaokaidi kutii sheria.

“…Nasema wapigwe tu, maana tumechoka sasa,” alisema Pinda alipojibu maswali ya papo hapo Alhamisi iliyopita.

Akisoma tamko hilo bungeni jana, Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani, Pereira Ame Silima alisema kuwa kifungu cha 18(B) na 18(C) cha Sheria ya Kanuni ya Adhabu kinatoa uwezo kisheria wa kutumia nguvu za kadiri hata ikibidi kiasi cha kusababisha madhara au kifo katika mazingira ya kisheria.