Saturday, July 7, 2012

WEMA SEPETU, JACQUELINE WOLPER HAKUNA MBABE

                                                    Mwamuzi akiamua mpambano uanze.
                                                         Wolper na Wema wakionyeshana ubabe.
Wema akipata mawaidha kutoka kwa mwalimu wake Rashid Matumla.
Waigizaji mahiri wa filamu nchini, Wema Sepetu na Jacqueline Wolper wametoka suruhu katika mpambano wao wa raundi 2 uliofanyika katika Uwanja wa Taifa jijini Dar e Salaam kwenye Tamasha la Usiku wa Matumaini.

SIMBA WAIKANDAMIZA YANGA KWA PENALTI 3-2

Hivi ndivyo hali ilivyokuwa katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam katika mtanange wa watani wa jadi Simba na Yanga (Wabunge) wakati wa TAMASHA LA MATUMAINI ambapo wabunge wapenzi wa timu ya Simba wameibuka kidedea kwa penalti 3-2.  Simba wamefunga penalti 3 wakati Yanga wakifunga 2
                                                           Yanga baada ya kipigo hicho.

BONGO MOVIE WAICHACHAFYA BONGO FLEVA 1 - 0

                                           Bongo Movie wakifurahia ushindi.

SIMBA VS YANGA (WABUNGE) MECHI INAKARIBIA KUANZA

                                             Simba wakiingia uwanjani kupasha misuli.
                             Yanga nao wakiingia uwanjani kwa maandalizi ya mechi.
Yanga wakijichua kwa ajili ya mtanange na watani wao wa jadi Simba.

Mechi ya watani wa jadi inakaribia kuanza muda huu. Timu zote mbili zimejiandaa vyema na kila moja imeahidi kuwashushia kichapo wenzao katika mtanange huu.

WANAMICHEZO WA TANZANIA WANAOKWENDA KUSHIRIKI MICHEZO YA OLYMPIC WAKABIDHIWA BENDERA KUIWAKILISHA NCHI UINGEREZA JULAI 27

Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Amos Makala, akimkabidhi Bendera ya Tanzania Samson Ramadhani, kwa niaba ya wenzake (pichani) wanamichezo wanaokwenda kushiriki mashindano ya Olympic nchini Uingereza inayotarajia kuanza Julai 27 mwaka huu. Kulia ni Meneja Mkazi wa Coca Cola , Demeji Olamiyani

 Naibu Waziri wa Habari, Vijana na Michezo, Amos Makala, akiwa katika picha ya pamoja na wanamichezo hao, baada ya kuwakabidhi Bendera ya Tanzania.NAPE AFUNGUKA KUHUSU MZEE SABODO KUIPIGA JEKI CHADEMA ASEMA MZEE HUYO KUCHANGIA UPINZANI SI TATIZO.

"Kuna watu wengi wanauliza nini maoni yangu juu ya uamuzi wa Mzee Sabodo kusaidia vyama vya upinzani na hasa Chadema.

 Kimsingi sioni tatizo kwa Mzee Sabodo kuamua kusaidia vyama vya upinzani na wakati huohuo akabaki kuwa kada mwaminifu wa CCM.

 Ikumbukwe ni serikali ya CCM ndio iliyobadili sheria kuruhusu uanzishwaji wa mfumo wa vyama vingi! Hata baada ya kuviruhusu vyama vingi bado ikatengeneza utaratibu wa ruzuku kwa vyama vya siasa! Yote haya yamefanywa na serikali ya CCM.

 Sasa kama serikali ya CCM imefanya hivyo, cha ajabu hapa kwa mwanachama wake kufanya hivyo ni nini? Hivi kwanini tunataka kuwafikisha watanzania mahali wasisaidiane kisa siasa!

 Wapo wanaohoji kwanini Mzee Sabodo ametoa visima kwa Chadema?!! Sasa najiuliza visima vitakapoanza kufanya kazi watumiaji wataulizwa itikadi zao au kila mwananchi anauhuru wa kutumia?! Tatizo hapa ni nini?!

 Narudia sioni tatizo kwa Mzee Sabodo kusaidia vyama vya upinzani ili mradi pesa hizo ni zake!!",Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa CCM, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye amesema katika taarifa yake..
Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Idara ya Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye akicheka bila uhasama na viongozi wa Chadema, Mwenyekiti Freeman Mbowe na Katibu Mkuu wa Chama hicho Dk. Wilbrod Slaa hivi karibuni.

Barabara za Kupunguza Msongamano na Bajeti ya Wizara ya Ujenzi

                                       Mbunge wa Jimbo la Ubungo (Chadema), John Mnyika.
Jana usiku tarehe 6 Julai 2012 Bunge limepitisha mapato na matumizi ya Wizara ya Ujenzi kwa mwaka wa fedha 2012/2012. Mtakuwa mmeona wakati bunge lilipokaa kama kamati nilishika mshahara wa Waziri kutaka maelezo ya kisera juu ya mkakati wa serikali katika kupunguza msongamano wa magari katika jiji la Dar es salaam ikiwemo katika barabara ya Morogoro inayopita Jimbo la Ubungo.
Nilitaka maelezo hayo kwa kuwa pamoja na kuunga mkono uwekezaji kwenye upanuzi wa barabara kuu, ujenzi wa miundombinu ya mradi wa mabasi yaendayo haraka na ujenzi wa fly overs, miradi hii kwa ujumla wake inachukua muda wa kati na muda mrefu hivyo kukamilika kwake ni mpaka mwaka 2016 au zaidi.
Nilitaka maelezo ni kwanini Serikali isizingatie vipaumbele vya mwaka wa kwanza wa mpango wa miaka mitano katika kuandaa bajeti ili pamoja na miradi hiyo niliyoitaja iwekeze kwa haraka kwenye barabara za pete/mzunguko (ring roads) za pembezoni ambazo zinaweza kujengwa kwa kiwango cha lami katika kipindi cha mwaka mmoja na hivyo kuchangia kwenye kupunguza foleni katika barabara kuu ifikapo mwaka 2013.


Kufuatia majibu ya Waziri nilihoji tena wakati bunge linapitisha vifungu vya miradi ya maendeleo kwenye kasma ya kuondoa foleni Dar e salaam ambayo imetengewa shilingi bilioni 10.5 tu, wakati ambapo mpango wa taifa wa miaka mitano uliopitishwa umeelekeza kifungu hicho kitengewe jumla ya fedha kwa miaka miwili 2011/2012 na 2012/2013 kiasi cha shilingi bilioni 100.1 Ikumbukwe kwamba mwaka jana serikali ilitenga bilioni 5 tu wakati mpango uliitaka serikali itenge bilioni 68 na nilipohoji wakati huo nilijibiwa kwamba ilikuwa ni kipindi cha mpito hivyo fedha zote zingeunganishwa mwaka huu kitu ambacho hakikufanyika.

Majibu ya kwamba Dar es salaam na Pwani kwa ujumla zimetengewa bilioni zaidi ya 900 yanajumuisha fedha za maendeleo kwa miradi iliyoanza 2010/2011, 2011/2012, 2012/2013 na ni miradi ya muda mrefu ya barabara kuu na madaraja makubwa kwa mikoa yote miwili.

Kwa hiyo bilioni 10.5 imegawanywa kidogo kidogo kwa barabara zifuatazo: Mbezi Luis kupitia Goba mpaka Mbezi Tangi Bovu; Mbezi kwa Yusuph- Msakuzi- Mpiji Magohe mpaka Tegeta/Bunju; Mbezi-Malambamawili-Kinyerezi, Kimara-Mavurunza-Bonyokwa; Kimara-Kilungule-Makoka-Makuburi, Kimara-Matosa-Mbezi; Ubungo-Msewe-Chuo Kikuu na nyingine katika maeneo mengine ya Dar es salaam kama zilivyoelezwa katika hotuba ya Waziri. Kwa kasi hii ndogo, itachukua takribani miaka kumi kuweza kukamilisha ujenzi kwa kiwango cha lami kwa barabara hizo ambazo jumla ya urefu wake ni kilomita 96 tu.

Nashukuru kwamba fedha zimetengwa kumalizia pia barabara ya Ubungo Maziwa- Bus Terminal na pia za kuanza ya kuelekea External, na pia bilioni zaidi ya 240 za mradi wa DART; hata hivyo, tuendelee kuungana katika kuisimamia serikali ili itenge bilioni 100 kujenga kwa kiwango cha lami barabara tajwa za pembezoni za kupunguza msongamano haraka zaidi wakati tukisubiri utekelezaji wa miradi ya muda wa kati na muda mrefu.

Tuendelee kuishauri Tume ya Mipango ambayo Mwenyekiti wake ni Rais kuingiza kwenye Mpango wa Mwaka wa Maendeleo Mwezi Februari 2013 ili hatimaye kiwango hicho cha fedha kiingizwe katika bajeti. Izingatiwe pia kuwa sehemu ya Barabara hizo ni ahadi za Rais alipotembelea Jimbo la Ubungo kabla ya uchaguzi wa mwaka 2010 na kurudia tena ahadi hizo wakati wa kampeni za uchaguzi wa 2010. Tuendelee kushirikiana katika kufuatilia kazi za maendeleo.

Wenu katika uwakilishi wa wananchi,
John Mnyika (Mb)
7/7/2012-Bungeni, Dodoma

http://mnyika.blogspot.com

DILMA ROUSSEF: MWANAMKE WA KWANZA KUWA RAIS BRAZIL

                                                                  Dilma Vana Roussef.
UKWELI ni kwamba mamilioni ya watu duniani wanaifahamu nchi ya Brazil, hususan kutokana na umaarufu wake katika soka. Lakini ni wachache wanaowafahamu marais waliowahi kushika madaraka katika nchi hiyo kwa miaka nenda rudi.

Aidha, ni watu wachache wapenzi wa nchi hiyo ya Kusini mwa Bara la Amerika na ya tano kwa ukubwa wa eneo duniani ikiwa na watu milioni 192, wanafahamu kwamba rais wake wa sasa ni mwanamke.

Ni Dilma Roussef, mama mwenye wajihi na umbo la kuvutia kwa wanaume na wanawake licha ya kuwa na umri wa miaka 64 sasa.

Roussef ambaye majina yake kamili ni Dilma Vana Roussef, aliweka rekodi katika nchi hiyo kwa kuwa mchumi (economist) wa kwanza kushika nafasi hiyo nchini Brazil.

Dilma, aliyezaliwa Desemba 14, 1947 nchini Brazil na akashika wadhifa wa urais Januari 1, 2011, ni rais wa 36 wa nchi hiyo ambayo ilianza kujulikana hivyo mwaka 1500 baada ya Wareno kutoka Ulaya (Portugal) wakiongozwa na Pedro Álvares Cabral kufika huko na kulifanya eneo hilo kuwa koloni.

Rais Roussef ambaye ana mtoto mmoja wa kike aitwaye Paula aliyempata akiwa na mwanasiasa mwenzake, Carlos Araujo, alifanya kazi chini ya Rais Mstaafu, Luiz de Silva (aliyemrithi) akiwa msaidizi mkuu wake (Chief of Staff) ambapo alikuwa ni mtu wa pili mwenye mamlaka zaidi nchini humo.

Vilevile, Dilma, msomi wa Chuo Kikuu cha Shirikisho cha Rio de Grande dol Sul, aliyewahi kuwa waziri wa madini na nishati na aliupata urais huo kupitia Chama cha Wafanyakazi, katika harakati za siasa aliwahi kufungwa 1970 hadi 1972 na kuteswa wakati wa kupinga utawala wa kijeshi nchini humo.

Ni Dilma Roussef, binti wa baba mwenye asili ya Bulgaria ambaye alimwoa mwanamke wa Kibrazil baada ya kukimbia machafuko Ulaya wakati wa Vita Kuu ya Pili ya Dunia na kwenda kuishi Brazil.

Magazeti Ya Leo Jumamosi 7th July


Ziara ya Kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama Washington DC

Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Nje, Ulinzi naUsalama Mhe. Edward Lowassa alimkabidhi Bw. Hayes zawadi kutoka Tanzania ikiwa ni ukumbusho wa ziara yao kwenye taasisi hiyo.
Mjumbe wa Kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama Mhe. KhalifaKhalifa (MB) akifuatilia maelezo ya Mkurugenzi wa Ofisi ya Mambo ya Africa Mashariki ya USAID Bibi Susan Fine, walipokuwa kwenye mkutano na maafisa wa ofisi hiyo ikiwa ni sehemu ya ziara ya wabunge hao mjini Washington DC, Marekani. Picha inayofuata ni ujumbe mzima wa kamati hiyo pamoja na maafisa ubalozi wa Tanzania Washington DC.
Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama Mhe.Edward Lowassa(Mb.) akimkabidhi Bibi Susan Fine zawadi za vinyago vya kuwekea mishumaa baada ya kumaliza mazungumzo yao.
Mjumbe wa Kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama Mhe. RachaelMasishanga Robert (Mb.) akimvalisha afisa wa USAID ushanga uliotengenezwa na wajasiriamali wa Tanzania baada ya kumaliza mkutano.

                                                      Picha ya pamoja.
Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Nje, Ulinzi na Usalama wakiwa na KaimuBalozi wa Tanzania nchini Marekani Mhe. Lilly Munanka kwenye mkutano na Corporate Council on Africa, taasisi ya Marekani inayotoa ushauri wa kibiashara na uwekezaji barani Afrika

Kamati ilikutana Rais wa Taasisi hiyo Bw. Steven Hayes ambaye alielezeafursa nyingi wanazotoa kwa balozi mbalimbali za Afrika hapa Washington DC ili kuvutia wafanyabiashara na wawekezaji wa Kimarekani kwenda nchi hizo za Afrika

Katika mkutano huo Bw. Hayes alisifu jitihada za ubalozi wa Tanzania na Balozi Mwanaidi Maajar kutumia kituo hicho mara kwa mara kwa nia ya kutafuta maeneo ya ushirikiano na kuwahamasisha wawekezaji wa Kimarekani kuwekeza Tanzania.

Theresia Kimaro ndie Redd's Miss Tanga 2012

Redd's Miss Tanga 2012,Theresia Kimaro (katikati) akiwa katika picha ya Pamoja na mshindi wa pili,Beatroce Joseph na wa tatu Johari Harom muda mfupi baada ya kumalizika kwa shindano lao liliilofanyika usiku huu kwenye Uwanja wa Mkwakwani,Jijini Tanga.
                                                        Washiriki walioingia tano Bora.
                                                           Washiriki wote stejini.