Wednesday, August 8, 2012

Askari Aliyejinyonga Aaacha Ujumbe Mzito

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akutana na Marais wa Maziwa Makuu

 Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete,Rais Paul Kagame wa Rwanda(kushoto),Rais Yoweri Kaguta Museveni wa Uganda(Watatu kulia) na Rais Joseph Kabila wa Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo wakiwa katika mkutano wa viongozi wan chi za Maziwa Makuu unaofanyika jijini Kampala Uganda jana jioni.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete, Rais Paul Kagame wa Rwanda na Rais Yoweri Kaguta Museveni wa Uganda wakifurahia  jambo wakati wa mkutano wa Viongozi wa nchi za Maziwa Makuu unaofanyika jijini Kampala Uganda.

Picha na Freddy Maro-IKULU

Magazeti ya Leo Jumatano 8th August 2012

Godbless Lema Aongoza Mkutano wa Chadema London

   Mbunge wa zamani wa Arusha Kamanda Godbless Lema Akihutubia Mkutano huo jana
                                                    Baadhi washiriki wa mkutano huo
                                                     Baadhi washiriki wa mkutano huo

TSC Mwanza Yarejea Kutoka Ujerumani Na Vikombe Kibao

 Altaf Hirani Rais wa Taasisi ya Tanzania Street Children Sports Academy TSC ya Mwanza akizungumza na waandishi wa habari leo kwenye ofisi za shirikisho la mpira wa miguu nchini Tanzania TFF kulia ni Mkurugenzi wa TCS Mutani Yangwe na kushoto ni Mmoja wa maofisa wa kituo hicho B. Leonard Magomba.
 Viongozi wa kituo hicho wakiwa katika picha ya pamoja na wachezaji wa timu hiyo kutoka TCS Mwanza mara baada ya kuzungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam wakiwa na mataji yao waliyoijishindia na zawadi mbalimbali.
Mkurugenzi wa Taasisi ya Tanzania Street Children Sports Academy TSC ya Mwanza,Mutani Yangwe akizungumza na waandishi wa habari kwenye ofisi za Shirikisho la mpira wa miguu nchini TFF Karume wakati akielezea mafanikio ya timu ya Academy yao waliyoyapata kutoka nchini Ujerumani na kunyakua mataji mbalimbali na zawadi kemkem.
Chanzo: www.fullshangweblog.com

Lazaro Nyarandu: Serikali Kufidia Mifugo Maswa

 Naibu waziri wa Maliasili na Utalii,Lazaro Nyalandu akizungumza na wafanyakazi na viongozi wa pori la akiba Maswa.
 Mbunge wa jimbo la Kisesa wilaya ya Meatu,Mpina akitoa salamu zake kwa wafanyakazi na viongozi wa pori la akiba Maswa.
 Mkuu wa wilaya ya Meatu, Rosemary Kirigini akitoa taarifa yake ya maendeleo ya pori la akiba Maswa kwa naibu Waziri Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu aliyetembelea pori hilo.
Naibu waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu (kulia) akiwa kwenye boti akielekea kukagua hifadhi ya kisiwa cha Saanane jijini Mwanza.

Serikali imeahidi kutoa kiasi cha 6M/- kulipa fidia ya ng’ombe 22 wanaodaiwa kuuawa kwa kupigwa risasi na askari wa wanyamapori wa pori la akiba Maswa wilayani Meatu, mkoani Simiyu.

Inadaiwa ng,ombe hao walipigwa risasi na kuuawa Desemba 2009 baada ya kuingizwa kuchungia ndani ya hifadhi hiyo, kitendo ambacho ni kinyume na sheria zinazolinda hifadhi za wanyama pori .

Ahadi hiyo imetolewa juzi na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu, wakati akizungumza kwenye mkutano wa hadhara uliohudhuriwa na wakazi wa kata ya Sakasaka jimbo la Kisesa.

Alisema lengo la uamuzi huo ni kuimarisha mahusiano mazuri kati ya askari wa wanayamapori na wakazi wa vijiji vinavyozunguka akiba ya pori hilo.

“Pia ni sehemu ya mikakati inayochukuliwa na serikali ya kuhakikisha mgogoro wa muda mrefu kati ya uongozi wa pori la akiba Maswa na wananchi wakazi wa vijiji vinavyozunguka pori hilo,unamalizika na kurejesha amani na utulivu katika eneo hilo,” alisema Nyalandu.

Katika hatua nyingine, Nyalandu ambaye pia ni mbunge wa jimbo la Singida kaskazini, alisema kuwa serikali inatarajia kuunda kamati huru ambayo itashughulikia kutafuta ufumbuzi wa mgogoro uliopo kwa muda mrefu katika akiba ya pori la Maswa.

“Katika kamati hii,kutakuwepo na mwakilishi mmoja kutoka wizara ya mali asili na utalii na wajumbe watakaobaki watakuwa ni watu huru ambao watazitendea haki pande zote mbili. Ni matarajio yetu kwamba taarifa itakayotolewa na kamati hiyo haitaionea au kupendelea upande wo wote, itakuwa timilifu,” alifafanua naibu waziri huyo.

Nyalandu alisema kamati hiyo itatoa taarifa yake wizarani mapema kabla bunge la sasa kuhairishwa.

Katika hatua nyingine, alitumia fursa hiyo kuagiza wananchi waendelee kuelimishwa vya kutosha juu ya sheria zote za hifadhi za wanyama pori ili waweze kuzitii bila ya kushurutishwa.

“Napenda kukumbusha kuwa  marufuku kuchungia,kulima,kuingiza au kufanya shughuli zo zote za kijamii ndani ya hifadhi la wanyama pori. Mfugaji au mtu yeyote atakayevunja sheria halali ailizowekwa atachukuliwa hatua kali za kisheria,” alisema Nyalandu.

Awali Mkuu wa Wilaya ya Meatu, Rosemary Kirigini, alisema hifadhi ya pori la akiba Maswa ipo kwa mujibu wa sheria.

“Kwa hiyo, wananchi kuigiza mifugo yao ndani ya hifadhi hiyo kwa madai ya kutokuwa na maeneo ya malisho ni kuvunja sheria. Tunashauri wananchi wenye mifugo wanaopakana na pori la akiba la Maswa watafute maeneo mengine ya kupeleka makundi yao ya mifugo, au washauriwe kupunguza mifugo yao kwa kuanzisha ufugaji wa kisasa,” alisema DC Kirigini.

Aidha, alisema kuwa wataendelea kutoa elimu ya uhifadhi kwa madai kwamba hifadhi zilizopo, ni hazina kwa vizazi vilivyopo sasa na vya baadaye kwa nchi ya Tanzania na dunia kwa ujumla.

Wakati huo huo, DC Kirigini ameiomba serikali kuangalia uwezekano wa kubadilisha jina la akiba la pori la Maswa na kulipa jina la akiba ya pori la Meatu.

Alisema kuwa kwa vile sasa wilaya ya Maswa imegawanywa na kuwa na wilaya wilaya tatu baada ya kuanzishwa kwa wilaya ya Bariadi na Meatu,akiba ya pori hilo ambalo sehemu kubwa ipo wilaya mpya ya Meatu,hivyo kuna ulazima wa kuitwa pori la akiba la Meatu.

Kwa upande wake Nyalandu alisema ombi hilo la kubadilisha jina la pori hilo linazungumzika.
Chanzo: Nathaniel Limu

CAG Aanza Kuchunguza Madudu Tanesco

MDHIBITI na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Ludovick Utouh amesema ofisi yake imeanza ukaguzi wa tuhuma zinazomkabili Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), William Mhando.

Julai 14 mwaka huu, Bodi ya Wakurugenzi ya Tanesco ilimsimamisha kazi Mhando na Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Huduma za Shirika, Robert Shemhilu, Ofisa Mkuu wa Fedha, Lusekelo Kassanga na Meneja Mwandamizi wa Ununuzi, Harun Mattambo kupisha uchunguzi wa tuhuma za ubadhirifu na matumizi mabaya ya madaraka.

Utouh aliwaambia waandishi wa habari Dar es Salaam jana kwamba ofisi yake imekabidhiwa kazi hiyo na tayari imeshaanza na imefikia pazuri. “Ni kweli suala hilo nimeshakabidhiwa na kazi hii tayari imeshaanza na imefikia pazuri. Kikao cha kwanza kimekaa Jumamosi iliyopita na mimi nimeshafika kuwahakiki maofisa wangu wanaoshughulikia hilo,” alisema Utouh na kuongeza kuwa kazi hiyo inaweza kukamilika ndani ya siku 60 kuanzia sasa.

Tuhuma zilizopo
Tuhuma za ufisadi Tanesco, zilianzia katika ripoti ya CAG ya mwaka huu ambayo ilionyesha gharama za ununuzi ziliongezeka kwa mwaka jana, kutoka Sh300 bilioni hadi 600 bilioni.
Baada ya sakata hilo, Kamati ya Bunge ya Hesabu za Mashirika ya Umma (POAC), ilitaka hatua zichukuliwe dhidi ya Bodi na Watendaji wa Tanesco na kuhoji ongezeko hilo kubwa la gharama za ununuzi.

Lakini wiki mbili kabla ya Bajeti ya Wizara ya Nishati na Madini, bodi hiyo iliitisha kikao cha dharura Julai 13, mwaka huu kujadili tuhuma mbalimbali dhidi ya menejimenti ya shirika hilo na kuamua kwamba tuhuma dhidi ya Mhando ni nzito hivyo ni vyema zifanyiwe uchunguzi huru na wa kina.

“Hivyo, Bodi iliazimia pamoja na mambo mengine kama ifuatavyo: Uchunguzi wa tuhuma hizo uanze mara moja kwa kutumia uchunguzi huru na kumsimamisha kazi Mkurugenzi Mtendaji wa Tanesco, Mhandisi William Mhando ili kupisha uchunguzi huo na kwa kuzingatia matakwa ya sheria za kazi nchini.”
“Pamoja na uamuzi huo, Bodi imechukua hatua stahiki za kuhakikisha kwamba shughuli za utendaji na uendeshaji wa Tanesco zinaendelea kama kawaida,” ilisema taarifa hiyo.

Sakata hilo lilipamba moto bungeni wakati wa mjadala wa Bajeti ya Wizara ya Nishati na Madini, kwa 2012/13. Akiwasilisha Bajeti hiyo, waziri wake, Profesa Sospeter Muhongo alisema mbali ya tuhuma za kupanga mgawo wa umeme kama mkakati na kampuni za mafuta, Mhando pia anadaiwa kuidhinisha zabuni ya kusambaza vifaa vya ofisi kwa kampuni ya mkewe, Eva Mhando. Profesa Muhongo alisema zabuni hiyo ni zaidi ya Sh800 milioni na kwamba, Eva alitumia kampuni ya Santa Clara na Mhando aliidhinisha pasipo kutangaza mgongano wa kimasilahi. Tuhuma hizo na nyingine zilihusisha baadhi ya wabunge na kumfanya Spika, Anne Makinda kuivunja Kamati ya Nishati na Madini baada ya kutuhumiwa kuhusika na vitendo vya rushwa.
Chanzo: http://www.mwananchi.co.tz

NANE NANE LEO

                                               Wakulima wakiwa shambani

NAIBU WAZIRI AFRIKA MASHARIKI APATA AJALI


                                           Wananchi wakitazama gari la naibu waziri wa Afrika Mashariki
                               Gari la Naibu Waziri wa Afrika Mashariki  Lilivyopinduka
Naibu waziri wa Afrika Mashariki Abdullah Juma Saddallah amepata ajali ya gari alilokua akisafiria kwenye eneo la Kongowe Kibaha Pwani akitokea Dodoma kuja Dar es salaam.

Hiyo ajali imetokea leo jioni ambapo Naibu waziri amesema hali yake sio mbaya sana ila dereva ndio ameumia kiasi, bado wanapata matibabu kwenye hospitali ya Tumbi Kibaha Pwani,  chanzo cha ajali amesema ni baada ya dereva wake kukwepa lori lakini hakufanikiwa na gari ikatoka nje ya barabara.

Picha na Francis Godwin wa Matukio.