Thursday, November 8, 2012

Ikulu: Hatuwezi Kumzuia Lissu Kumshtaki Rais

SIKU moja baada ya Mnadhimu wa Kambi ya Upinzani Bungeni, Tundu Lissu kusema atawasilisha hoja ya kumshtaki Rais Jakaya Kikwete iwapo atashindwa kuwaondoa kazini majaji wasio na sifa aliowateua, Ikulu imemwambia aendelee na mchakato wake.

 Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu, Salva Rweyemamu alisema jana kuwa hakuna anayemzuia Lissu kushtaki kama anaona kuna sababu za kufanya hivyo.“Lissu ni Mbunge na ana haki zake za msingi na kama amefikia hatua hiyo anaweza kufanya hivyo... hakuna mtu ambaye anaweza kumkataza. Nani mwenye uwezo wa kuingilia uhuru wa mtu?”

 Akizungumza na waandishi wa habari katika Ofisi za Bunge jana, Lissu alisema amechukua uamuzi huo baada ya kuona Bunge limeikalia ripoti ya Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge iliyomhoji kuhusu kauli yake ya kuwatuhumu majaji kuwa baadhi yao hawana sifa.

 Alisema ameamua kuchukua hatua hiyo baada ya kuona Rais Kikwete ambaye ana mamlaka ya kuteua majaji, ameshindwa kuwaondoa kazini majaji hao wasiokuwa na sifa.

Lissu alisema atawasilisha hoja yake hiyo kwa kutumia Kanuni ya Bunge sehemu ya 11, Ibara ya 121, 122, 123, 124, 125 na 126 na pia kwa kutumia Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Ibara ya 146 A. Sehemu ya 11 ya Kanuni ya Bunge, Ibara ya 121 inaeleza kuwa mbunge yeyote anaweza kuwasilisha kwa Spika taarifa ya hoja ya kumshtaki Rais kwa madhumuni ya kumuondoa Rais madarakani kupitia azimio la Bunge kwa mujibu wa Ibara ya 46 A ya Katiba ikiwa inadaiwa kwamba Rais; ametenda vitendo ambavyo kwa ujumla vinavunja katiba au sheria ya maadili ya viongozi wa umma.

 Lissu alisema atakusanya saini za wabunge kuunga mkono hoja yake ambayo ni asilimia 20 kwa mujibu wa Kanuni za Bunge. Wabunge wote kikatiba ni 357. Julai 13, mwaka huu wakati akitoa maoni ya kambi ya upinzani katika Wizara ya Katiba na Sheria bungeni, Lissu alisema uteuzi wa majaji umegubikwa na ukiukwaji wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano.

 Alisema baadhi ya majaji walioteuliwa hawana sifa, uwezo na kwamba hawakufaa kufanya kazi hiyo. Kauli hiyo ilisababisha Bunge kuiagiza Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge inayoongozwa na Mbunge wa Mlalo (CCM), Hassan Ngwilizi kumhoji ili athibitishe kauli yake.

 Alisema wakati akihojiwa na kamati hiyo, pamoja na nyaraka nyingine, aliwasilisha nakala ya ripoti ya kikosi kazi kilichoundwa mwaka 2008 na aliyekuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Johnson Mwanyika na aliyekuwa Katibu Mkuu Kiongozi, Philemon Luhanjo kuchunguza uteuzi wa majaji nchini.

 Alisema ripoti ya kikosi kazi hicho kilibaini kuwapo majaji ambao hawana sifa ya kufanya kazi hiyo, lakini Rais Kikwete ameshindwa kuwaondoa kazini. Lissu ambaye pia ni Mbunge wa Singida Mashariki kwa tiketi ya Chadema, alisema hali ya Mahakama ni mbaya, kwani kuna majaji wawili ambao waliwahi kukamatwa kwa rushwa wakiwa mawakili, lakini wakateuliwa kufanya kazi hiyo.

 Alisema baadhi ya majaji hawana uwezo hata wa kuandika hukumu kutokana na kutojua vyema lugha ya Kiingereza ambayo ndiyo inayotumika katika Mahakama Kuu na Mahakama ya Rufani.

 Alisema ili mtu aweze kuchaguliwa kuwa Jaji wa Mahakama Kuu lazima awe na elimu ya shahada ya kwanza ya sheria, awe ametumikia miaka 10 mahakamani na anayechaguliwa kuwa jaji wa Mahakama ya Rufani lazima awe ametumikia miaka 15 mahakamani.

 Mbali ya kueleza hayo, Lissu alisema kwamba alitoa pia katika kamati hiyo, ushahidi unaoonyesha kuwa kuna jaji mmoja wa Mahakama Kuu ambaye hawezi hata kuandika sentensi moja ya Kiingereza ilinyooka... “Kama jaji hawezi kuandika hata sentensi moja ya Kiingereza ilinyooka, tunaweza vipi kuwa na Mahakama inayotenda haki?”

Alisema kuna jaji mwingine ambaye ameongezewa mkataba wa kufanya kazi mara ya tatu kitu ambacho ni kinyume cha sheria. Alisema kwa mujibu wa Tume ya Mahakama, hakuna jaji ambaye anaweza kufanya kazi kwa mkataba kwa vipindi vitatu.

 Kama Lissu atachukua hatua hiyo, itakuwa ni mara ya pili kwa mbunge kuwasilisha bungeni hoja ya kutaka kumwajibisha kiongozi wa juu serikalini. Mara ya kwanza alikuwa Mbunge wa Kigoma Kaskazini (Chadema), Zitto Kabwe katika Bunge lililopita alipokusanya saini za wabunge kutaka kupiga kura ya kutokuwa na imani na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akitaka awawajibishe baadhi ya mawaziri waliokuwa wametajwa kuhusika katika matumizi mabaya ya madaraka katika Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG).

 Hata hivyo, Rais Kikwete alifanya mabadiliko makubwa katika Baraza lake la Mawaziri hivyo kuzima hoja hiyo ya Zitto.

    Chanzo: http://www.mwananchi.co.tz/habari

Viongozi Uamsho Wakosa Dhamana Tena

Na Maelezo Zanzibar 08/11/2012

Kesi inayomkabili Shekh Farid Hadi Ahmed na wenzake sita wa Jumuiya ya UAMSHO na Mihadhara ya Kiislam imeakhirishwa leo hadi terehe 20 mwezi huu.

Akitoa maamuzi hayo Mrajisi wa Mahakama kuu Zanzibar iliyopo Vuga George Kazi amesema kuwa uamuzi huo umetokana na kuwa upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika.

Kwa upande wa Wanasheria wa watuhumiwa walielezea juu ya haki ya washitakiwa wao kupatiwa dhamana lakini dhamana hiyo hawakupatiwa na kurejeshwa Rumande hadi tarehe 20 mwezi huu.

Washitakiwa hao ni Farid Had Ahmed (41) wa mkazi wa Mbuyuni, Mselem Ali Mselem(52)wa Kwamtipura, Mussa Juma Issa (37) wa Makadara, Azan Khalid Hamdan (43) wa Mfenesini, Suleiman Juma Suleiman (66) wa Makadara,Khamis Ali Suleiman (59) anayeishi Mwanakwerekwe pamoja na Hassan Bakar Suleiman (39) mkaazi wa Tomondo.

Watuhumiwa wote walishitakiwa kwa kosa la uchochezi wa kufanya fujo kinyume na kifungu cha 45 (a) (b) cha sheria namba 6/2004 sheria za Zanzibar.

Ilifahamishwa kuwa Agosti 17 mwaka huu majira ya saa 11:00 za jioni huko Magogoni Msumbiji Wilaya ya Magharibi Unguja, wakiwa ni Wahadhiri kutoka Jumuiya ya UAMSHO na Mihadhara ya Kiisalam, walitoa matamko ya uchochezi yanayoashiria uvunjaji wa Amani na kusababisha fujo,maafa mbalimbali na mtafaruku kwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

IMETOLEWA NA MAELEZO ZANZIBAR

JK: Azindua Ujenzi Wa Bomba La Gesi Asilia Kutoka Mtwara-Dar es salaam

 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na ujumbe wa kampuni inayojenga bomba la gesi asilia kutoka Mtwata hadi Dar es salaam, Benki ya Exim ya China na viongozi waandamizi wa serikali alipowakaribisha Ikulu kwa mazungumzo baada ya uzinduzi rasmi wa ujenzi wa bomba hilo maeneo ya Kinyerezi jijini Dar es salaam
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Makamu wa Rais Dkt Mohamed Ghalib Bilali na viongozi wengine wakimsikiliza  Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo miundombinu ya  bomba la gesi asilia toka Mtwara hadi Dar es salaam leo Novemba 8, 2012 maeneno ya Kinyerezi njijini Dar es salaam. Nyuma yake ni Makamu wa Rais Dkt Mohamed Ghalib Bilali.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akizindua rasmi ujenzi wa bomba la gesi asilia toka Mtwara hadi Dar es salaam leo Novemba 8, 2012 maeneno ya Kinyerezi njijini Dar es salaam. Nyuma yake ni Makamu wa Rais Dkt Mohamed Ghalib Bilali.

Mashirika 64 Yaliyobinafsishwa Hayafanyi Kazi

Ndugu zangu,
Mara nyingi Watanzania wamekuwa wakipigia kelele kuhusu suala la ubinafsishaji lililoanza mwanzoni mwa miaka ya 1990 kwamba halikwenda sawa.

Kwamba, pamoja na shinikizo la Benki ya Dunia na IMF kutekeleza Sera ya Ubinafsishaji kwa mashirika yaliyokuwa mzigo kwa serikali, lakini viongozi wetu waliyabinafsishaji hata yale yaliyokuwa na uwezo wa kujiendesha, mengi wakajiuzia wao.

Sasa inasikitisha tunapoasikia leo kwamba, mashirika 64 kati ya yaliyobinafsishwa mpaka sasa hayafanyi kazi tena.

Tujiulize, mashirika hayo ni yetu hasa; kabla ya kubinafsishwa hali ilikuwaje; sasa yamebinafsishwa kwa akina nani; na kwa nini mpaka sasa serikali inawaangalia tu wawekezaji hao ambao wameshindwa kutekeleza masharti ya mkataba?

Ikumbukwe kwamba, mpaka yanabinafsishwa, kulikuwa na wafanyakazi, ambao walikuwa na familia zilizotegemea kazi wanazofanya kwenye mashirika hayo, na kubinafsishwa kwa mashirika maana yake kumewafanya wengi wakose kazi, wengine wamepoteza maisha kutokana na ugumu wa maisha kwani kiinua mgongo walicholipwa hakikutosha.

Tuijadili zaidi, lakini isome pia hapa...wp-content/uploads/2012/11/Janet-Mbene.jpg

Kutoka kwa: Mbega Mnyama,

Obama Tears Up While Addressing Campaign Staff

Before heading back to the White House on Wednesday, President Obama made a stop at campaign headquarters in Chicago to address his campaign staff after Tuesday night's big victory.
The president gave an emotional thanks to the staff, tearing up as he expressed his gratitude for their support and dedication to the reelection effort.
"I'm really proud of all of you," Obama said. "What you guys accomplished will go on in the annals of history."
               Source: http://www.huffingtonpost.com

kesi ya lema yahairishwa tena

RUFAA ya aliyekuwa Mbunge  wa Arusha Mjini kupitia Chadema, Godbless Lema imeponea chupuchupu kutupiliwa mbali baada ya Mahakama ya Rufani, kukubali hoja moja ya pingamizi la makada wa CCM dhidi ya rufaa hiyo.

Mahakama hiyo ilikubali hoja ya wajibu rufaa kuwa rufaa hiyo ilikuwa  na dosari kutokana na tofauti ya vifungu vya sheria vilivyotumika katika hukumu iliyomvua ubunge na vilivyotumika katika hati ya kukaza hukumu, iliyowasilishwa mahakamani sambamba na rufaa hiyo.

Hata hivyo, kilichomwokoa Lema ni kifungu cha 111 cha Kanuni za Mahakama, ambapo mahakama hiyo ilisema kuwa chini ya kanuni hiyo dosari hizo zinaweza kurekebishwa.

Chini ya kanuni hiyo, Mahakama ya Rufani ilimwamuru Lema kupitia kwa mawakili wake, Tundu Lissu na Method Kimomogoro, kufanya marekebisho ya dosari hizo zilizobainika na kisha kuwasilisha upya rufaa yake ndani ya siku 14 kutoka jana.

Lema alivuliwa wadhifa huo na Mahakama Kuu Kanda ya Arusha, Aprili 5, 2012 kutokana na kesi iliyofunguliwa na wanachama watatu  wa CCM, Mussa Mkanga, Happy Kivuyo na Agnes Mollel, wakipinga ushindi wake katika Uchaguzi Mkuu mwaka 2010.

Lakini baadaye alikata rufaa Mahakama ya Rufani, kupitia kwa wakili wake, Method Kimomogoro kupinga hukumu ya Mahakama Kuu, huku akitoa hoja 18 za kupinga hukumu hiyo.

Tarehe ambayo rufaa hiyo ilipangwa kusikilizwa na jopo la  majaji watatu Mahakama ya Rufani; Salum Massati, Natalia Kimaro  na  Jaji Mkuu, Mohamed Othman Chande (kiongozi wa jopo), wakili wa wajibu rufaa, Alute Mughwai, aliweka pingamizi la awali.

Katika pingamizi hilo,wakili Mghwai aliiomba Mahakama hiyo iitupilie mbali rufaa hiyo, akidai kuwa ina kasoro za kisheria na za kikanuni huku akibainisha hoja tatu za kuunga mkono pingamizi hilo.

Hoja hizo za pingamizi la awali zilikuwa ni pamoja na kuchanganywa au kutofautiana kwa vifungu vya Sheria ya Uchaguzi ya Mwaka 2010, kati ya hukumu iliyomvua ubunge na hati ya kukaza hukumu hiyo.

Pia hoja nyingine ni kwamba hati ya kukaza hukumu hiyo haikuwa na mhuri wa Jaji aliyeitoa wala tarehe ambayo  hati hiyo ya kukaza hukumu ilitolewa.

Hoja ya tatu ilikuwa ni mtindo wa kuandika hati ya kukaza hukumu, kwa kutokuandika maneno, “imetolewa kwa mkono wangu na mhuri wa mahakama.”

Hata hivyo, katika uamuzi wake jana, Mahakama ya Rufani ilikubaliana na hoja moja ya pingamizi hilo, kuwa tofauti au kuchanganywa kwa vifungu hivyo vya sheria ni dosari ambayo inaifanya hati hiyo isiwe halali na ikatupilia mbali hoja nyingine mbili kuwa hazina msingi.

Uamuzi huo ulioandikwa na Jaji Nathalie Kimaro kwa niaba ya jopo hilo, ulisomwa na Naibu Msajili wa Mahakama ya Rufani, Zahra Maruma.

DIRECTOR WA FILAMU ILIYOKASHIFU UISLAMU AHUKUMIWA.

The man behind an anti-Muslim film that led to violence in the Middle East has been sentenced to one year in prison.

Mark Basseley Youssef, 55, was sentenced on Wednesday for violating probation stemming from a 2010 bank fraud conviction.

US District Court Judge Christina Snyder handed down the sentence after Youssef admitted four of eight alleged violations including obtaining a fraudulent California driver’s licence.

Youssef served most of a 21-month prison term in the bank fraud case. Federal authorities wanted Youssef to serve two years for the violations.

After he was released from prison, Youssef was barred from using computers or the Internet for five years without approval from his probation officer.

None of the violations had to do with the content of “Innocence of Muslims,” a film that depicts Mohammad as a religious fraud, pedophile and a womaniser.

The movie sparked violence in Libya and other parts of the Middle East, killing dozens. Enraged Muslims had demanded severe punishment for him, with a Pakistani cabinet minister even offering $100,000 to anyone who kills him.

Federal authorities have said they believe Youssef is responsible for the film, but they have not said whether he was the person who posted it online.

He also was not supposed to use any name other than his true legal name without the prior written approval of his probation officer.

At least three names have been associated with Youssef since the film trailer surfaced – Sam Bacile, Nakoula Basseley Nakoula and Youssef. Bacile was the name attached to the YouTube account that posted the video.

Court documents show Youssef legally changed his name from Nakoula in 2002, though when he was tried, he identified himself as Nakoula. He wanted the name change because he believed Nakoula sounded like a girl’s name, according to court documents.

Magazeti ya leo Alhamisi ya 8th November 2012