Wednesday, September 5, 2012

Tanzania Yazindua Mpango Wa Mpya Wa Kuboresha Maarifa Ya Utoaji Damu Kwa Wahudumu Wa Afya

 Dr .mohammed mohammed) Mkurugenzi wa Usimamizi Ubora Huduma kutoka Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii akizungumza katika ufunguzi wa mradi unaogharamiwa na serikali ya Marekani.
Sehemu ya washiriki na wakufunzi wa mafunzo ya utoaji damu salama wakisiliza ufunguzi wa kazi inayotarajiwa kupunguza uwezekano wa watoa huduma ya tiba kupata maambukizi kwa njia salama.

Dr Margreth Mhando, Mkurugenzi wa Tiba kutoka Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii akiwa na Dr Mohammed Mohammed wakiwa na mfano wa mkoba wenye vifaa vipya vya kutolea damu kwa njia salamabaada ya uzinduzi wa shughuli hiyo mjini Dar Es Salaam.

Na: Hassan Mhelela

Jumla ya watumishi 500 wa sekta ya afya watanufaika na mafunzo ya mbinu mpya za utoaji damu ya wagonjwa kwa njia salam. Mpango huo mpya ni sehemu ya mradi unaosimamiwa na Wizara ya Afya,
kwa kushirikiana na washirika na wafanyakazi wa sekta ya afya nchini Tanzania.

Kazi hiyo inatekelezwa kwa ushirikiano na Mpango Dharura wa Rais wa Marekani kwa Ajili ya Kupunguza Makali ya UKIMWI (PEPFAR) kupitia taasisi ya udhibiti na kuzuia maradhi (Centers for Disease Control and Prevention - CDC) chini ya Wizara ya Afya ya Marekani na kampuni ya BD (Becton, Dickinson and Company).
Vile vile JHPIEGO, mshirika wa kiufundi wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii ya Tanzania, watashirikiana katika jitihada za kusimamia na kusambaza huduma hizi zilizoongezwa ubora.

Mpango wa Tanzania Initiative for Blood-Drawing Applications (TIBA) , una malengo ya kuboresha huduma za afya na maabira katika vituo vya afya, hasa katika mikoa yenye maambukizi zaidi ya VVU/UKIMWI. Shughuli ya kutoa damu katika mwili wa mgonjwa kupitia mishipa ya damu kwa kutumia sindano ni mojawapo ya njia zinazotumika kwa wingi katika hospitali na zahanati, ingawa njia hii inakabiliwa na hatari nyingi za kiafya.

Utafiti uliofanyika mwaka 2008 katika taasisi za afya 14 ulibaini kulikuwa na asilimia 52.9 ya matukio ya kujichoma kwa sindano na kujimwagia damu ya wagonjwa asilimia 21.7 miongoni mwa wafanyakazi wa
sekta ya afya. Jumla ya wafanyakazi wa huduma ya afya 500 watanufaika na mafunzo hayo kote nchini.

Dkt. Bilal Afungua Mkutano Wa Wakuu Wa Majeshi Ya Polisi Kutoka Nchi Za KusinI Mwa Afrika (SADC)


 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal (katikati) akijumuika kuimba wimbo wa Taifa na wakuu wa Jeshi la Polisi Inspekta Generali, Said Mwema (wa pili kushoto) wakati alipofika kwenye Ukumbi wa Hoteli ya Zanzibar Beach Resort, mjini Zanzibar leo Sept 05, 2012 kwa ajili ya kufungua mkutano wa Wakuu wa Majeshi ya Polisi kutoka Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) wa kujadili uhalifu wa Kimataifa kuhusu madawa ya kulevya na kuimarisha uhusiano kwa nchi za Afrika kiulinzi.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,akisoma hotuba yake ya ufunguzi wa mkutano wa Wakuu wa Majeshi ya Polisi kutoka Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) wa kujadili uhalifu wa Kimataifa kuhusu madawa ya kulevya na kuimarisha uhusiano kwa nchi za Afrika kiulinzi.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,akipokea zawadi kutoka kwa Mkuu wa Jeshi la Plisi, Inspekta Genarali, Saidi Mwema, baada ya kufungua mkutano wa Wakuu wa Majeshi ya Polisi kutoka Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) wa kujadili uhalifu wa Kimataifa kuhusu madawa ya kulevya na kuimarisha uhusiano kwa nchi za Afrika kiulinzi. Kushoto ni Mkuu wa Jeshi la Polisi wa Afrika ya Kusini


                                                       Picha ya Pamoja na Wakuu wa Majeshi

Picha na OMR

Siku Ya Mtanzania



Mahali: Tanzania House, 1232 22Nd Street, N.W. Washington D.C.; 20037Tarehe: SEPTEMBA 15, 2012 Kiingilio: BUREMuda: (Saa 4:00 asubuhi – Saa 12 Jioni)Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Marekani, Washington D.C. unawakaribisha Watanzania wote waishio maeneo ya DMV (District of Columbia, Maryland na Virginia) na vitongoji vyake, kuhudhuria siku ya Mtanzania, ambapo Watanzania watashirikikwenye kuonyesha bidhaa, tamaduni, mila na desturi za Kitanzania kwa wageni (Wamarekani na wa Mataifa mengine) watakaotembelea ubalozini.


Madhumuni makuu ya Ubalozi kuandaa Siku ya Mtanzania kwanza ni kuwaelimisha wenyeji wa Marekani kuhusu Tanzania. Pili kuitangaza zaidi Tanzania kwa kuvutia watalii wengi kutembelea Tanzania. Tatu ni kutambulisha na kutangaza biashara mbalimbali na hudumazitolewazo na Watanzania waishio hapa Marekani.

Ubalozi unaomba Watanzania wenye bidhaa mbambali za Kitanzania, mapishi (wenye leseni),vikundi vya ngoma, muziki, mitindo, na Watanzania wenye kampuni za utalii, kujiandikisha ubalozini kuanzia tarehe 1 hadi 15 Agosti, 2012 kwa maandalizi ya siku hiyo.

Kwa Watanzania watakaopenda kujitolea kushiriki siku hiyo au kuonyesha bidhaa mbalimbali wajiandikishe kwa wafuatao:

Dkt. Suitbert Mkama 202 884 1087 au barua pepe smkama@tanzaniaembassy-us.orgAsia Dachi 202 884 1096 barua pepe adachi@tanzaniaembassy-us.org Rosemary Mziray 202 884 1081 au barua pepe rmziray@tanzaniaembassy-us.org Ubalozi unapenda kuwahamasisha Watanzania kuvaa vazi la Kitanzania.


                                                               Karibuni

Bei Ya Mafuta Yapanda Tena


MAMLAKA ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (Ewura) imetangaza bei kikomo za bidhaa za mafuta ya petroli nchini ambapo bei ya petroli, dizeli na mafuta ya taa zimepanda.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Meneja Uhusiano wa Ewura, Titus Kaguo jana bei mpya zitaanza kutumika kuanzia leo.

"Sambamba na kupanda kwa gharama halisi za uagizaji wa mafuta kutoka kwenye Soko la Dunia, bei za jumla na rejareja kwa mafuta aina zote zimebadilika ikilinganishwa na taarifa iliyopita ya Agosti 1, 2012," ilieleza taarifa hiyo.

Kaguo katika taarifa hiyo alieleza kuwa bei za rejareja kwa Petroli, Dizeli na Mafuta ya Taa zimeongezeka, ambapo Petroli imepanda kwa Sh 291 kwa lita sawa na asilimia 14.50; Dizeli Sh 199 kwa lita sawa na asilimia 10.26; na Mafuta ya Taa Sh 67 kwa sawa na asilimia 3.47.

"Bei za jumla kwa kulinganisha matoleo haya mawili zimebadilika kama ifuatavyo: Petroli imeongezeka kwa Sh 291.54 kwa lita sawa na asilimia 15.07; Dizeli Sh 199.57 kwa lita sawa na asilimia 10.68 na mafuta ya taa kwa Sh 67.29 kwa lita sawa na asilimia 3.63," aliseleza katika taarifa hiyo.

Alisema kampuni za mafuta zipo huru kuuza bidhaa za mafuta ya petroli kwa bei ya ushindani ilimradi bei hizo ziko chini ya bei kikomo kama ilivyokokotolewa na kanuni mpya iliyopitishwa na Ewura na kuchapwa kwenye Gazeti la Serikali Na. 454 la Desemba 23, 2011.

MSG ILIYOTUMWA NA DR SLAA KWA MKUU WA POLISI TANZANIA KABLA YA KIFO CHA MWANDISHI IRINGA.


                                                                Marehemu Daudi.
kiwa ni siku ya pili toka mwandishi wa habari wa Channel Ten Daudi Mwangosi kuuwawa kwa bomu akiwa kwenye mikono ya polisi Iringa, Waziri wa mambo ya ndani Dr Emmanuel Nchimbi ameunda tume huru ya watu watano kwa ajili ya kuchunguza chanzo cha kifo hicho.

Hiyo tume inaongozwa na jaji mstaafu Stephen Kihema na itafanya kazi yake kwa siku 30 ambapo pamoja na mambo mengine, inapaswa kuainisha ukubwa wa nguvu iliyotumika kumuua mwandishi huyo, ichunguze kama upo uhasama kati ya Polisi na waandishi wa habari mkoani Iringa, pia iangaliwe kama kweli ipo orodha ya waandishi wa habari watatu waliopangwa kushughulikiwa na jeshi hilo.

Waziri Nchimbi ameahidi hatua kali zitachukuliwa kwa yeyote atakaebainika kuhusika na kifo hicho bila kujali nafasi aliyonayo.

Kwenye line nyingine, namkariri Nchimbi akisema “kuna maswali kama sita ambayo mimi sina majibu yake na ningependa sana nipate majibu yake, nini chanzo cha kifo cha mwandishi wa habari wa Iringa Daudi Mwangosi? nikiwa Waziri mwenye dhamana ya usalama wa raia kwa sababu hiyo basi naunda kamati ya uchunguzi ya watu watano”

Kuhusu msg iliyotumwa na Dr Slaa kwa Mkuu wa jeshi la Polisi IGP Said Mwema kabla ya mwandishi kuuwawa, naendelea kumkariri Waziri Nchimbi akisema “IGP Mwema alitutumia hiyo msg viongozi wenzake, Dr Slaaa alimuandikia kwamba IGP nasubiri simu yako wajulishe polisi wako waandae risasi za kutosha kutakua na karamu ya mauaji na kisha kusherehekea mjiandae kwenda Mahakamani The Hague”

Kwenye nukuu nyingine Waziri Nchimbi amesmea “nikiona mtu katuma msg ya namna hii kwa IGP alafu bado yuko barabarani anaendelea kutembea, hajahojiwa, hajapelekwa Mahakamani kwa kuandaa vurugu, ni jambo nalishangaa sana… kwa kweli ujumbe wangu ni kwa watu wawili.. IGP namshangaa kwamba aliemtumia msg hiyo yuko barabarani anatembea akiwa huru, pili namshangaa alietuma ujumbe huo ambae ameona vifo vimetokea baada ya ujumbe wake bado hajajisalimisha polisi”

Mwandishi Daudi Mwangosi amezikwa kwao Iringa jana ambapo miongoni mwa waliohudhuria ni katibu mkuu wa Chadema Dr Wilbroad Slaa.

KAULI YA CHADEMA KUHUSU KIFO CHA MWANDISHI IRINGA.


                                                                    Siku ya tukio.

Chama cha Demokrasia na maendeleo (CHADEMA) kimemuomba rais Kikwete kuwasimamisha kazi kamishna wa upelelezi jeshi la Polisi Tanzania Paul Chagonja pamoja na kamanda wa polisi  Iringa Michael Kamuhanda kwa madai kwamba wamekua wakitoa taarifa zisizo sahihi kuhusiana na kifo cha Daudi Mwangosi mwandishi wa habari wa Iringa aliyeuwawa kwa kulipukiwa na bomu akiwa anashikiliwa na polisi.

Mkurugenzi wa habari na uenezi wa Chadema John Mnyika amesema makamanda hao wamekua wakitoa raarifa zinazotofautiana na ushahidi wa picha pamoja na mashahidi waliokuwepo kwenye tukio.

Namkariri akisema “uchunguzi unaopaswa kuendelea unapaswa kuhusu tu ni nani hasa alietoa maagizo kigogo wa juu wa polisi? lakini polisi ambao wamehusika na tukio wanaonekana picha zao, ni askari saba walioko eneo la tukio, jeshi la polisi limekua na kawaida ya kuwakamata raia waliopo kwenye eneo la tukio panapotokea mauaji kwamba ndio washukiwa wa kwanza, ni kwa nini askari wote hawa saba wanaonekana hapa hawajakamatwa? tunataka wakamatwe mara moja kama washukiwa wakuu wa kwanza kabisa wa mauaji, uchunguzi huru kuhusu tu ni nani alihusika vipi kati ya hawa na vigogo gani wa jeshi la Polisi na Serikali walihusika kuwapa maelekezo kufanya kitendo hicho cha mauaji”

Kwenye line nyingine Mnyika amesema chama kimebaini kuwepo kwa mipango ya baadhi ya watu kutaka kukichafulia hadhi ili kionekane ni chama chenye kusababisha vurugu na kuwataka viongozi wote wa chama hicho kuhakikisha wanakua makini na aina hiyo ya watu.

Amesisitiza kwa kusema “wanakusudia kubandikiza silaha kwa hiyo tunatoa tahadhari kwa viongozi wetu kwenye mikutano yote ya Chadema kuchukua tahadhari dhidi ya watu wasiowafahamu ambao wengine watavalishwa mpaka mavazi ya Chadema ili kutekeleza malengo hayo maovu”

Magazeti ya Leo Jumatano 5th September 2012