Wednesday, January 16, 2013

Chadema sasa waanza kulipuana


KATIKA kuonyesha hali si shwari ndani ya Chadema, Makamu Mwenyekiti wa Baraza la Vijana (Bavicha) wa chama hicho, Juliana Shonza amesema ameamua kumshtaki Mwenyekiti wake, John Heche kwa kumuita kuwa ni msaliti wa chama na kwamba anatumiwa na CCM na kuamua kumfukuza nafasi yake bila kutoa nafasi ya kusikilizwa.

Pia, amemlipua Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk Willibrod Slaa akidai kuwa amefanya ufisadi ndani ya chama kwa kujikopesha Sh140 milioni ambazo hajazilipa hadi sasa.

Mbali na hilo, amemshukia Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe kwa kudai kuwa anatoa kauli za kukurupuka ambazo zinakiyumbisha chama hicho kikuu cha upinzani nchini.

Shonza alitoa kauli hizo jana wakati akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam juu ya tuhuma zilizotolewa na mwenyekiti wa Bavicha na kuhusu kufukuzwa kwake ndani ya chama akiwa na wenzake Mtela Mwampamba na Habibu Mchange.

Bus la champion lamgonga mtembea kwa miguu na kusababisha kifo

YAH: TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA DODOMA KWA VYOMBO VYA
HABARI TAREHE 15/01/2013

Mtu mmoja amefariki Dunia Mkoani Dodoma katika tukio la ajali ya gari kumgonga mtembea kwa miguu na kusababisha kifo.

Tukio hilo  limetokea tarehe 14/01/2013 majira ya saa 09:30 alasiri katika kijiji cha Kelema  Wilaya ya Chemba barabara ya DODOMA -KONDOA baada ya  gari lenye namba za usajili T. 769 BNP aina ya Scania  Bus mali ya  Kampuni ya Champion  likendeshwa na dereva aliyefahamika kwa jina la  George s/o Maiko Kwayu likitokea Dodoma kuelekea Kondoa kumgonga mtembea kwa miguu na  kumsababishia kifo chake papo hapo.

MKE WA RAIS MAMA SALMA KIKWETE AWAFANYIA SHERRY PARTY WENZA WA MABALOZI


                                                   Mama salma akisoma hotuba

                                          Wake wa Mabalozi katika hafla hiyokatika viwanja vya Ikulu

Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiongea kwenye hafla  maalumu ya kuwakaribisha wake wa Balozi nchini kwa  mwaka mpya 2013, Hafla hiyo imefanyika  katika viwanja vya Ikulu jijini Dar- es Salaam , Jan 15,2013,

JK: Uvumilivu sasa basi

SERIKALI imesema haitavumilia kwa namna yeyote ile vurugu za kidini, kikanda na ukabila ambazo baadhi yake zilitaka kulitia doa taifa mwaka jana. Pia imesisitiza kwamba haitawavumilia wanasiasa wanaotumia rasilimali za taifa kujitafutia umaarufu kwa gharama za kuligawa taifa.

Akizungumza na mabalozi kwa nyakati tofauti Ikulu, Dar es Salaam; kwanza katika sherehe ya kuukaribisha Mwaka Mpya iliyofanyika juzi na alipokuwa akiagana na Balozi wa Uingereza nchini, Dianne Corner jana, Rais Jakaya Kikwete alisema vurugu zilizotaka kujitokeza mwaka jana zinatosha.

“Serikali haitavumilia vurugu wala ukabila kwa namna yoyote ile…. Mwaka 2012 vurugu zenye sura ya kidini zilianza kujitokeza ila sasa nasema kwamba hatutazivumilia kwa namna yeyote ile, inatosha,” alisema Rais Kikwete.

MZEE MKAPA NA MZEE MSUYA WATOA MAONI LEO

 Rais Mstaafu Mhe. Benjamin Mkapa (kulia) akiongea na Wajumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Jaji Mkuu Mstaafu Augustino Ramadhani (katikati) na Dkt. Salim Ahmed Salim. Wajumbe wa Tume walikutana na Rais huyo Mstaafu leo (Jumatano, Jan 16, 2013) jijini Dar es Salaam ili kupata maoni na uzoefu wake katika uandishi wa Katiba Mpya.
                                 Rais Mstaafu Mhe. Benjamin Mkapa akiwa na wageni wake

JK: AZINDUA AWAMU YA KWANZA YA JENGO JIPYA LA HOSPITALI YA SHREE HINDU MANDAL JIJINI DAR ES SALAAM

 Rais Dk. Jakaya Mrisho Kikwete akiwasha mshumaa kama ishara ya uzinduzi wa Awamu ya Kwanza ya jengo jipya na Awamu ya pili ya Hospitali ya Shree Hindu Mandal ya jijini Dar es salaam leo katika Mtaa wa Nyanza, ambapo huduma hiyo itapunguza msongamano wa wagonjwa katika hospitali jijini na kuongeza wigo wa utoaji huduma n kuongeza vitanda vya kulaza wagonjwa, Hospitali ya Shree Hindu Mandalilianzishwa mwaka 1931 ikianza na Zahanati anayeshuhudiatukio hilowa pili katikati ni Mwenyekiti wa hospitali hiyo Bw Ramesh Patel.
Rais Jakaya Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na Uongozi , Madaktari , Wauguzi pamoja na wafanyakazi wa hospitali ya Shree Hindu Mandal mara baada ya kuzindua rasmi leo
 Rais Dk. Jakaya Kikwete akikata utepe wakati wa uzinduzi wa hoapitali hiyo uliofanyika leo jijini Dar es salaam.

Manumba mahututi, alazwa Aga Khan

Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai wa Jeshi la Polisi (DCI), Kamishna Robert Manumba

HALI ya Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai wa Jeshi la Polisi (DCI), Kamishna Robert Manumba ni mbaya na amelazwa katika Chumba cha Wagonjwa Mahututi (ICU), Hospitali ya Aga Khan, Dar es Salaam.Habari zilizopatikana jana zilieleza kuwa Manumba amelazwa hospitalini hapo baada ya kusumbuliwa na maradhi kadhaa, ikiwamo figo.

Taarifa za ndani kutoka Jeshi la Polisi zilisema jana kuwa tangu juzi, Manumba alikuwa hajitambui baada ya kuugua malaria ghafla na hali hiyo ilisababisha pia figo zake zote mbili kushindwa kufanya kazi.

“Alitakiwa kupelekwa nje ya nchi kwa matibabu, lakini ilishindikana kwa sababu hajitambui, wakajaribu kumzindua, ikashindikana,” kilieleza chanzo hicho cha habari ndani ya jeshi hilo.

Yaliyojiri leo Magazetini Jumatano ya 16th January 2013