Tuesday, May 7, 2013

PINDA ATEMBELEA KANISA LA OLASITI NA KUZUNGUMZA NA WAUMINI NA VIONGOZI WA KANISA KATOLIKI

 Waziri Mkuu, Mizengo Pinda  akizungumza na Viongozi na Waumini wa Kanisa Katoliki la Olasiti Jijini Arusha  May 7,2013 alikokwenda kutoa pole kufuatia mlipuko wa bomu la kutupwa kwa mkono uliotokea kanisani hapo May 5,2013 na kusababisha vifo na majeruhi.


 Paroko wa Kanisa Katoliki la Olasiti la Arusha Peddy Castelino akiomba wakati Waziri  Mkuu, Mizengo Pinda alipotembelea kanisa hilo May 7,2013 kutoa pole kufuatia mlipuko wa bomu la kutupwa kwa mkono uliotokea kanisani hapo May 6,2013 na kusabisha vifo na majeruhi.

Magazeti ya leo Jumanne ya 7th May 2013



VICTOR AMBROSE NDIYE ALIRUSHA BOMU KANISANI...

DEREVA wa pikipiki maarufu kama bodaboda, Victor Ambrose, anatuhumiwa kurusha bomu katika Kanisa Katoliki la Mtakatifu Joseph Mfanyakazi, Parokia ya Olasiti jijini Arusha, lililosababisha vifo vya watu wawili na wengine karibu 70 kujeruhiwa.

Ambrose mwenye umri wa miaka 20 na mkazi wa Kwa Mrombo, Arusha, anashikiliwa pamoja na watuhumiwa wengine tisa, wakiwemo raia wanne wa Saudi Arabia kwa mahojiano zaidi ya kuhusika na tukio hilo.

Taarifa zilizopatikana jana jioni, zilieleza kuwa raia hao wa Saudi Arabia, waliingia nchini Jumamosi usiku kwa ndege kupitia Uwanja wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA), na baada ya tukio Jumapili, waliondoka nchini kupitia mpaka wa Tanzania na Kenya, Namanga.

Serikali kupitia kwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi, ilitoa taarifa hiyo jana bungeni na kueleza namna uhalifu huo ulivyotendeka kanisani hapo juzi, muda mfupi baada ya ibada kuanza.

Kwa mujibu wa Waziri Nchimbi, uchunguzi wa awali unaonesha kuwa mlipuko huo ni bomu. Hata hivyo uchunguzi wa kubaini aina ya bomu lililotumika, unaendelea kufanywa na Polisi na wataalamu wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ).

“Hadi sasa watuhumiwa sita wanashikiliwa na Jeshi la Polisi. Miongoni mwao ni Victor Ambrose mwenye umri wa miaka 20 dereva wa bodaboda...ambaye anatuhumiwa kurusha bomu hilo. “Watuhumiwa wengine watano waliokamatwa ni raia wa kigeni na Mtanzania mmoja ambao wanashikiliwa kwa mahojiano,” alisema Dk Nchimbi.