Wednesday, August 29, 2012

Mechi Ya leo Simba 2 JKT Oljoro 1 Mchezo uliochezwa Mjini Arusha



Couple of the day


Mtoto Azaliwa Na Vichwa Viwili Mkoani Mara

Mtoto azaliwa na vichwa viwili katika hospital ya DDH Bunda Mara mtoto huyu alikaa kwa saa moja ni kisha kufariki dunia picha imepigwa na Berensi Alikadi mshiriki wa mafunzo ya Online Journalism yanayoendelea Mkoani  Mara.

UMEVUNJWA MOYO KIMAPENZI? ZINGATIA HAYA


Mada iliyopo mezani wiki hii ni mambo ya kuzingatia inapotokea kwamba umeumizwa na kuvunjwa moyo na yule uliyekuwa umempenda na kumpa nafasi ndani ya moyo wako.

Ni ukweli usiopingika kuwa hivi sasa vitendo vya kusalitiana na kuumizana mioyo, vimeongezeka maradufu kutokana na maendeleo ya sayansi na teknolojia. Simu za mkononi, mitandao ya kijamii kama Facebook, Twitter na mambo mengine kama hayo, yamerahisisha sana usaliti. Licha ya kuongezeka kwa usaliti, ni wachache sana wanaoelewa nini cha kufanya pale wanapoanguka kimapenzi. Zifuatazo ni dondoo zitakazokusaidia usiumie zaidi baada ya kutokewa na tukio baya.

BADILISHA MAZINGIRA/ MARAFIKI
Baada ya kuumizwa na mwandani wako, mbinu ya kubadilisha mazingira na marafiki husaidia sana kukupa nguvu ya kukabiliana na msongo unaoweza kukusababishia madhara makubwa.

Unaweza kubadilisha mazingira kwa kusafiri, kubadilisha mpangilio wa chumba chako cha kulala na kuondoa vitu vyote vinavyoweza kukukumbusha hisia chungu za maumivu. Taratibu utaona akili yako ikianza kusahau maumivu.

Yawezekana pia kuwa mpenzi wako ulishamtambulisha kwa marafiki zako nao wakamuona kama sehemu ya familia. Ukiendelea kujumuika na marafiki hao, watakuwa wanakukumbusha hisia chungu zitakazoendelea kukutesa, jiweke karibu na marafiki wapya wasiojua historia yako ya mapenzi, watakuwa sehemu ya faraja kwako.

JIPENDE, JITHAMINI
Utafiti wa kisaikolojia umebaini kuwa baada ya kutendwa kimapenzi, watu wengi hujishusha thamani na kudhani huenda wana upungufu au udhaifu fulani ndiyo maana wapenzi wao wakawasaliti na kutoka kimapenzi na watu wengine.

Kama ni mwanamke, muda wote atashinda kwenye kioo akijikagua kama ana kasoro kwenye sura na mwonekano wake. Mwanaume vivyo hivyo, atashinda akijiuliza kuhusu uwezo wake wa kumfurahisha mwenza wake faragha au uwezo wake wa kifedha.

Kuyabadili maumivu haya kuwa furaha, jitazame kwa jicho la tatu na kujiambia kuwa wewe ni mzuri, una umbo zuri, unajua kukidhi haja za mwenzako mkiwa faragha na kwamba hauna kasoro yoyote. Jipe nafasi ya kushughulikia maisha yako ya baadaye na suala la mapenzi achana nalo kwa muda mpaka utakapokuwa umetulia.

Kujipenda na kujithamini kuenda sambamba na kuboresha mwonekano wako, hakikisha muda wote unakuwa msafi na mazingira unayoishi pia yanakuwa masafi.

SITISHA MAWASILIANO
Unapokuwa na maumivu ndani ya moyo wako, jambo la busara ni kukaa mbali na kusitisha mawasiliano ya aina yoyote na yule aliyekusababishia maumivu hayo. Wengi hufikia hatua ya kubadili namba zao za simu ili kupata muda wa kutafakari mustakabali wa uhusiano wao.

Kama alikuwa rafiki yako kwenye Facebook au Twitter, ‘block’ mawasiliano naye, kama ni kwenye simu sitisha kumtumia ujumbe mfupi au kumpigiapigia simu, iache akili yako ndiyo iamue kama bado unahitaji kuendelea kuwa naye au la.

Hata kama njia uliyokuwa unapita kwenda kwenye shughuli zako za kila siku ilikuwa inakufanya ukutane naye, badilisha njia na ratiba yako kwa jumla.

USITAFUTE WA KUZIBA PENGO
Kosa ambalo wengi hulifanya baada ya kutendwa na wapenzi wao, ni kukurupuka na kuanzisha uhusiano wa kimapenzi na watu wengine muda mfupi baada ya kuumizwa. Badala ya kupunguza maumivu, utajikuta ukiongeza ‘stress’ kichwani kwani huyo unayedhani atafaa kuziba pengo, anaweza kuwa na maovu kushinda hata huyo aliyekuumiza.

Jipe nafasi ya kukaa mwenyewe na kufikiria maisha yako ya baadaye, amini kwamba maisha yanawezekana hata ukiwa peke yako, kubaliana na kilichotokea na jiambie kuwa hutaki kurudia makosa kwa kuanzisha uhusiano na mtu atakayeuchezea moyo wako.

JIPE ZAWADI 
Huenda wengi wakashangaa kwamba inawezekanaje kujipa zawadi mwenyewe? Inawezekana. Tembelea duka linalouza zawadi za kimapenzi kama maua, kadi nzuri, midoli au chocolate na jichagulie unayoipenda zaidi. Jiambie kuwa hakuna anayekupenda zaidi ya jinsi unavyojipenda mwenyewe, jipongeze kwani maumivu hayatajirudia tena.

True story - tafadhali soma Imetumwa na Mwanafamilia wa Asilialive


Here comes the story part I. 

Jana 21.08.2012 nlipotoka job, wife alinipa taarifa kuwa mdogo wangu wa kike (mwenye salon ya kike kimanga) alimpigia simu kuwa amepata msichana na atakuja nae home jioni akifunga saluni.

Ikabidi nimpigie simu mdogo wangu ili anipe full information.

Mdogo wangu akanimbia majira ya jioni uyo msichana alifika Saluni kwake akidai anatafuta kazi za ndani. Uyo msichana akasema yeye alikuwa anfanya kazi morogoro but ametoroka kwani alikuwa anateswa na mama mwenye nyumba.uyo msichana akizidi kuongeza kuwa yeye hana mawasiliano ya ndugu yeyote ila baba yake anishi mwanza but hanjui mama yake. Basi mdogo wangu akamuonea huruma akamkaribisha saluni ilia je nae home jioni na nifanye nae mahojiano ya kina.

Jana majira ya saa 3 usiku baada ya wao kurejea home na kula chakula ikabidi nianze kumhoji yule binti.

Akanitajia jina lake na umri wake 15yrs, na nia yake ni kufanya kazi za ndani na akipata pesa ataenda kwao kusalimia then angerudi tena kuendelea na kazi yake.

Ni binti mdogo na nilitamani kumsaidia.

Baada ya kupata maelezo kutoka kwake; nilimuambia kwa sababu hatumfahamu ni lazima tukatoe report kwa balozi/mjumbe kabla hajaenda kulala na alikubali.

Nikaenda kwa mjumbe akawa ameshalala; ikabidi nimwambie wife kesho asubuhi (yaani leo) wakiamka waende kwa balozi/mjumbe kutoa taarifa na kuandikishana.

Leo asubuhi najiandaa kwenda kazini; kumbe yule binti ametoroka mapema asubuhi after mlango na geti kufunguliwa.

Majirani wakasema walimuona katoka na viatu mkononi wakazani anaenda kutupa taka coz alikuwa anafagiafagia nje. Kuangalia vitu sebuleni na chumbani kwa kina dada ikaonekana everything is OK.

Basi nikawmambia mdogo wangu na kijana flani wa jirani wamfuatilie then mimi nikaondoka zangu kuelekea job.

Here comes the story part II. 
Majira ya saa 4 asubuhi nikiwa job nilimpigia simu mdogo wangu anitaarifu yaliyojiri:

Akaniambia yule binti walimuona na akakimbilia nursery school flani karibia na barakuda na kwa msaada wa raia wengine walimkamata.

Walimpiga kidogo na kumsachi. Walimkuta na elfu 90 na alikiri kuwa aliziiba ktk wallet ya mdogo wangu.

Ikabidi mdogo wangu achukue bodaboda wakaenda nae hadi saluni kwake kimanga ili akamhoji zaidi.

Yule binti akasema kuwa alitudanganya hajatokea morogoro but anaishi na bibi ake mbagala na ule ndo mchezo wake yeye na bibi yake.

Akasema kuwa bib ake ni mchawi na huwa anamtumaga kwa nyumba za watu kwa mbinu ya kuomba kazi but baadae wanaiba na kuchukua watoto wadogo kimazingara.

Akaongeza kuwa hao watoto wadogo huwa wanawachukua misukule na wengine wakiwa wakubwa wanatumwa kama alivyotumwa yeye.

Yote hayo aliyasema bila woga huku watu wakiwa wamemzunguka pale saluni.

Akasema kuwa jana alipoingia getini bibi ake alikuja kimazingara but ghafla macho yake yalianza kumuwasha na hakuwa na amani. Kuona vile bibi ake akaondoka.

Ilipofika muda wa kulala alienda kuoga but aliporudi chumbani alimkuta mdogo wangu anasali ndipo alipigwa na miale ya blue na nyekundu akakimbia kurudi sebuleni.

Aliporudi sebuleni alimkuta wife anachek TV nae wife akashtuka kumuona yule binti hana amani.

Baade yule binti akaenda kulala ndipo wife akachukua maji ya Baraka akanyunyiza pale mlangoni na sebuleni kisha akaenda kulala.

Yule binti akazidi kuelezea kuwa usiku hakulala kwani aliteseka sana na kuweweseka na bibi ake alipokuja kimazingara hawakuweza kuchukua watoto ikabidi aondoke na kumuacha yule binti kwani alikuwa kaishiwa nguvu.

Akasema tangu aanze iyo kazi hajawahi kukamatwa na akmeshangaa sisi tumeweza kumkamata na kueleza siri zake. Akasema bibi ake alimjia kimazingara na akamwambia asirudi kwake kwani ametoa siri.

Alionesha CHALI alizochanjwa na bibi ake kama kinga na alipokuwa anapigwa hakusikia maumivu yoyote.

Alielezea mambo mengi ambayo mdogo wangu hakuweza kunielezea ktk simu kwani nae alikuwa anatetemeka kutoamini yaliyoukuwa yanatokea. Walimuachia akaondoka zake.

I felt so sorry for my twins but I thank GOD wamebaki salama.

Tuwe makini sana na wasichana wa kazi ndugu zangu; you may share it to your relatives and beloved.

Vuta Nikuvute Baina Ya Polisi Na Chadema Imehamia Iringa

VUTA nikuvute baina ya Polisi na Chadema imehamia Iringa, ambako jeshihilo limezuia maandamano na mikutano yote ya chama hicho iliyokuwa imepangwa kufanyika kwa siku nane kuanzia jana.
Amri hiyo ya polisi imekuja siku moja baada ya kutokea vurugu kubwa mjini Morogoro, baina ya wafuasi wa chama hicho na polisi na kusababisha kifo cha mtu mmoja na wawili kujeruhiwa.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa, Michael Kamhanda alisema jana kuwa wameamua kuzuia maandamano na mikutano ya Chadema iliyopangwa kuanza jana kutokana na Sensa ya Watu na Makazi.

“Kutokana na hali halisi ya Sensa, tumeamua kuzuia maandamano na mikutano yote ya vyama vya kisiasa mkoani Iringa wakiwamo hawa watu wa Chadema,” alisema.

Alisema kabla ya kuwazuia, walikutana na viongozi wa chama hicho Wilaya ya Iringa na kuwataka wazuie mikutano yao, jambo ambalo alisema walilikubali kwa ‘mbinde’.

Dk Slaa: Wametuomba
Awali, akiwa Mjini Morogoro, Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa alisema polisi wamekiomba chama hicho kusitisha maandamano na mikutano yake iliyopangwa kufanyika mkoani Iringa kupisha Sensa ya Watu na Makazi.
Alisema Chadema imekubali ombi hilo lililotolewa na Mkuu wa Polisi, IGP Said Mwema hivyo kuamua kusitisha mkutano wake uliopangwa kufanyika katika Viwanja vya Mwembetogwa, Iringa jana.

“Juzi Agosti 27, 1:00 usiku tulipata barua kutoka Jeshi la Polisi Iringa iliyokubali Chadema kufanya maandamano wakiwa ndani ya magari na si matembezi ya miguu, lakini baadaye saa 3:00 usiku, tulipigiwa simu na OCD wa Iringa akitujulisha kuwa maandamano yao yamebatilishwa na kutengua mambo yote tuliyoafikiana mwanzo,” alisema Dk Slaa na kuongeza:

“Asubuhi ya leo (jana) tulipigiwa simu na RPC (wa Iringa) na kudai kuwa wanataka kuonana na viongozi wa Chadema, huku wakiwa na hoja kuwa tuahirishe kufanya mkutano kutokana na Sensa.
Hoja nyingine ambayo mimi naona ni ya upuuzi ni ile ya kusema kwamba wananchi wa Iringa watakuwa wameathirika na kifo cha kijana aliyekufa Morogoro,” alisema Dk Slaa.

Alisema baada ya kutokubaliana na hoja hizo, alipigiwa simu na IGP Mwema akimwomba asitishe mkutano na maandamano ya mkoani Iringa kwa kuwa hiyo ni amri kwa vyama vyote vya siasa na si Chadema pekee.
“Nimeongea na IGP leo kwa dakika zaidi ya 40 akisema Dk Slaa sijawahi kukuomba hata siku moja, naomba nikuombe na usinikatalie kati ya siku nne hadi tano kuanzia sasa tumezuia vyama vya siasa kufanya mikutano ya hadhara kutokana na kuwapo kwa Sensa naomba tuelewane,” alisema Dk Slaa akimnukuu IGP Mwema.

Vurugu za Morogoro
Juzi, chama hicho kikuu cha upinzani kilifanya maandamano mjini Morogoro na kuzua taharuki, baada ya kutokea vurugu wakati polisi walipoamua kuyasambaratisha na kusababisha mauaji ya mtu mmoja, Ally Zona (38) mkazi wa Kihonda

Akizungumzia kifo hicho, Dk Slaa alisema chama chake kitashiriki kikamilifu katika mazishi ya kijana huyo kulingana na ratiba ya ndugu wa marehemu.
“Endapo familia itaamua kusoma dua hapa Morogoro na kuzika hapa, tutashiriki kikamilifu. Tumejadiliana na wanafamilia kuna mambo ya msingi tumekubaliana na walichoomba ni kusaidia kusafirisha mwili. Hatutajali itikadi aliyokuwa nayo marehemu,” alisema.

Chanzo: http://www.mwananchi.co.tz/habari

WATANZANIA TUNAWEZA,TUMSAPPORT MREMBO WA KITANZANIA ANAESHINDANIA MISS EAST AFRICA BELGIUM

Jina lake ni Juliana Pierre mtanzania ambae yuko kwenye list ya warembo wanaolitaka taji la Miss East Africa Belgium 2012 ( representing Tanzania), mwenye nguvu ya kumuweka kwenye nafasi ya ushindi ni wewe pekee kwa kulike page yake ya facebook… please tumsupport mtu wetu kwa kukopi na kulike hiyo page yake ya facebook hapo chini, mimi nimeshalike tayari….

http://www.facebook.com/JulianaPierreFinalisteMissEastAfricaBelgium2012

Magazeti ya Loe Jumatano 29th August 2012