Saturday, August 4, 2012

Breking News, Seacliff yaungua Moto

Kwa habari za sasa ni kwamba sea cliff ya jijini dar es salaam inaungua moto nitaendelea kuwaletea picha na habari kamili.

ROMA APATA AJALI MBAYA NA GARI LEO,

                                                            Gari Lilivyoharibika
 Msanii wa Bongo fleva Roma Mkatoliki amepata ajali mbaya ya gari Morogoro road ambapo kwa mujibu wa Roma ni kwamba tairi la mbele lilipopasuka na gari likaacha njia na kugongana uso kwa uso na fuso ambalo lilikuwa upande wa pili na gari hilo dogo alilokuwa akiendesha na kurudi lilipotokea.

Roma amesema kwamba anaelekea hospital kwa check up zaidi ila aliokuwa nao kwenye gari hakuna aliyeumia wote ni wazima.
Roma amepata ajali hii leo ikiwa ni siku 18 tu toka msanii mwingine wa bongofleva Chege kupata ajali ya gari yake kwa kumgonga mtu wa pikipiki alieingia barabarani ghafla na kusababisha gari kuharibika

MAMA MARIA NYERERE AKABIDHI MATREKTA KUMI KWA WAKULIMA WA KATA YA KWADELO, KONDOA

 Mjane wa Baba wa Taifa, Mwalimu Nyerere, Maria Nyerere, akimkaribisha, diwani wa Kata ya Kwadelo, wilaya ya KLondoa mkoa wa Dodoma, Alhaj Omar Kariati, wakati diwani huyo na ujumbe wake wa wakulima kumi, walipofika nyumbani kwa Mama Nyerere kwa ajili ya kukabidhiwa trekta kumi kwa wakulima hao, katika sherehe iliyofanyika nyumbani kwa Mama Maria Nyerere, Msasani jijini Dar es Salaam, leo.
                           Kariati akizungumza neno la kufungua shughuli. Kulia ni Mama Nyerere
Kisha Kariati akamkabidhi zawadi ya Kitenge Mama Nyerere kama shukurani ya wananchi wa Kwadelo kujengewa kisima cha maji na baba wa Taifa Mwalimu mwaka 1961 ambacho hadi sasa kipo.
                         Halafu akamkabidhi mkoba wa safari kama akitaka kwenda Butiama
Mama Nyerere akapata fursa ya kuzungumza mambo mbalimbali kabla ya kukabidhi trekta kwa wakulima hao, ambao pichani wamekaa kushoto.
       Mama Maria Nyerere na Kariati wakaongozana na wakulima kwenda eneo la makabidhiano ya trekta
                     "Trekta zenyewe ndiyo hizi" akasema Kariati kumwambia Mama maria Nyerere
 Mama Maria akimkabidhia funguo za trekta moja kati ya kumi aliyokabidhi, mmoja wa wakulima hao Sheikh Hamis Haji ambaye pia ni Sheikh wa Kata ya Kwadelo.
                       Baadha ya Sheikh akamkabidhi pia mkulima Maulidi Msema funguo za trekta
                     Baada ya Mama Nyerere kukabidhi trekta kumi, Kariati akamshukuru
     Kisha Mama Nyerere na diwani Kariati na Wakulima wakapigwa picha ya pamoja kuhitimisha shughuli

RAIS KIKWETE KWENYE WARSHA KUHUSU MFUMO WA KUSIMAMIA UTEKELEZAJI WA MIPANGO YA MAENDELEO

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akifungua warsha kuhusu mfumo wa kusimamia utekelezaji wa mipango ya maendeleo kwa mawaziri, makatibu wakuu na wakuu wa taasisi za serikali leo Agosti 4, 2012 katika ukumbi wa St Gaspar mjini Dodoma
 Washiriki wakimsikiliza Rais Jakaya Mrisho Kikwete wakati akifungua warsha kuhusu mfumo wa kusimamia utekelezaji wa mipango ya maendeleo kwa mawaziri, makatibu wakuu na wakuu wa taasisi za serikali leo Agosti 4, 2012 katika ukumbi wa St Gaspar mjini Dodoma
 Rais Kikwete, Makamu wa Rais Dk. Muhammed Gahrib Bilal, Waziri Mkuu Mizengo Pinda, Spika wa Bunge Anna Makinda na viongozi wengine waliohudhuria warsha hiyo, wakiwa katika picha ya pamoja

NBS YATOA TAARIFA YA HALI YA UCHUMI NCHINI.


Mkurugenzi wa Takwimu za Uchumi wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Bw. Morrice Oyuke akiongea na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam kuelezea hali ya Ukuaji wa Pato la Taifa kwa 7.1% katika kipindi cha robo mwaka 2012.

Picha na Aron Msigwa - MAELEZO.

Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) imetoa taarifa ya hali ya uchumi nchini na kufafanua kuwa  pato la taifa  la Tanzania limekua kwa  asilimia 7.1 katika kipindi cha robo ya mwaka 2012  ikilinganishwa  na asilimia 6.1  za mwaka jana.

Ukuaji huo wa asilimia 7.1 unatokana na ongezeko la uzalishaji katika shughuli mbalimbali za kiuchumi zikiwemo za kilimo, Uvuvi, Viwanda, Ujenzi na zile za utoaji wa huduma mbalimbali za jamii.

Akitoa taarifa hiyo jana jijini Dar es salaam Mkurugenzi wa Takwimu za Uchumi wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Bw. Morrice Oyuke amesema kuwa lengo la  utoaji wa taarifa hizo kwa vipindi vifupi vya vya  robo mwaka unalenga kuwapatia wadau wa Takwimu za Pato la Taifa uwezo wa kutathmini mabadiliko ya ukuaji wa uchumi nchini.

Amesema kuwa jumla ya thamani ya pato la Taifa katika kipindi cha robo ya mwaka 2012 ni shilingi 4,220,535 milioni ikilinganishwa na kiasi cha shilingi milioni 3,940,261 za mwaka 2011.

Amefafanua kuwa ukuaji wa shughuli uzalishaji katika shughuli za kilimo nchini ulifikia asilimia 1.4 katika kipindi cha robo ya kwanza ya mwaka 2012 zikilinganishwa na asilimia 1.2 katika kipindi hicho kwa mwaka 2011 kutokana na upatikanaji wa mvua za kutosha nchini katika mikoa inayozalisha mazao kwa wingi.

 Amesema ukuaji katika shughuli za uvuvi ulikua  asilimia 2.6 katika robo ya kwanza ya mwaka 2012 huku shughuli za uchumi katika sekta ya viwanda na Ujenzi ambayo inahusisha uchimbaji wa madini na kokoto ikikua kwa asilimia 14.3 ikilinganishwa na 0.8% za mwaka 2011.

Bw. Oyuke ameongeza kuwa ongezeko hilo  la uzalishaji wa madini ya dhahabu linatokana na uzalishaji wa wa madini ya dhahabu kutoka kilo 8,140 kwa mwaka 2011 hadi kufikia kilo 16,736 kwa mwaka 2012.

Pia amebainisha kuwa  shughuli za utoaji wa huduma za biashara za jumla na rejareja, ukarabati wa magari na pikipiki na vifaa vingine vya majumbani katika kipindi hicho zilifikia asilimia 9.0 huku shughuli za upangishaji nyumba na biashara zikiwa 8.2 %, uchukuzi na mawasiliano 16.4%, hoteli na migahawa 3.8%, Benki asilimia 15 shughuli za uendeshaji  serikali 6.4%, Elimu 6.1% na utoaji wa huduma za Afya nchini zikikua kwa kasi ya asilimia 5.1.

BONDIA FLOYD MAYWEATHER ATOKA JELA MWEZI MMOJA KABLA YA KUMALIZA KIFUNGO

             FLOYD MAYWEATHER KATIKATI AKIFURAIA WAKATI WA KUTOKA JELA
        MAYWEATHER AKILAKIWA NA NDUGU ZAKE WA KARIBU WAKATI AKITOKA JELA
    MAYWETHEA AKIWAPA AI WATU WALIOKUWA MBELE YAKE WAKATI AKITOKA JELA


 Boxing superstar Floyd Mayweather walked free from a Las Vegas jail early on Friday morning after serving two months for battering his ex-girlfriend in front of their children.The undefeated five-division champion was greeted by 20 family and friends, including rapper 50 Cent, as he emerged from Clark County Detention Centre just after midnight.The 35-year-old remained silent as, in the darkness, he got into a blue Bentley sedan and drove himself away the three months jail time he was handed for a hair-pulling, arm-twisting attack on former lover Josie Harris as two of their three children watched.And he is now free to resume a boxing career his lawyers warned in court documents might be at risk because jail food and water did not meet his dietary needs.They also said his lack of exercise space in a cramped cell of fewer than 98sq ft threatened his health and fitness.

A lot has happened in Mayweather's world since he was jailed June 1. With no television in his solo cell, he could not see arch rival Manny Pacquiao lose his WBO welterweight title on June 9 to Timothy Bradley. Mayweather, who goes by the nickname 'Money', was also not around to celebrate last month when Forbes magazine named him the world's highest-paid athlete for 2011.

And he missed fiancee Shantel Jackson's private birthday bash last week at a Las Vegas steakhouse with friends.Las Vegas Review-Journal celebrity columnist Norm Clark noted that Mayweather sent diamonds. But Mayweather is now a free man, even if his next opponent is not immediately clear. Mayweather's manager Leonard Ellerbe did not respond this week to repeated messages from The Associated Press. Promoters for Mayweather's main rival, Philippine boxer Manny Pacquiao, are planning a fight for November 10 at the MGM Grand Garden arena in Las Vegas, Nevada Athletic Commission executive Keith Kizer said. Pacquiao's opponent has not been named but Mayweather was not believed to be on the list.

Pacquiao, who earned $62million in fights and endorsements last year, ranked second on the Forbes richest athletes list behind Mayweather and his $85million in fight earnings. To fight in Las Vegas, Mayweather will need a new license from the Nevada Athletic Commission, Kizer said yesterday.His last license, for the May 5 bout against Miguel Cotto, was for one fight only. If Mayweather applies, commission Chairman Raymond 'Skip' Avansino Jr could decide to grant approval administratively or summon Mayweather before the panel for a public hearing, Kizer said. Mayweather received about 30 days off his 90-day jail sentence for work time and good behaviour.Nevada state law allows inmates to receive up to 10 days off per month for co-operating with jailers and working or being willing to work. Las Vegas police administer the jail, and a department spokesman said Mayweather was not required to work and did not misbehave behind bars.

The plea deal allowed him to avoid trial on felony charges that could have gotten Mayweather up to 34 years in prison if he was convicted. Harris and the children have since moved to the Los Angeles area.As a high-profile inmate, police say Mayweather was kept separate for his protection from the other 3,200 inmates in the downtown Las Vegas facility.

Las Vegas Justice of the Peace Melissa Saragosa rejected arguments that Mayweather's accommodations were cruel and unusual. The judge ruled June 13 that while Mayweather may not have liked the regimen, he had sufficient space and time for physical activity and the only reason he was not eating properly was because he was refusing to eat the meals he was given. The judge earlier gave Mayweather a break - allowing him to remain free long enough to make the Cinco de Mayo fight against Cotto at the MGM Grand Garden arena in Las Vegas.Mayweather won to run his record to 43-0 with 26 knockouts. Cotto lost for just the second time in 38 fights

MANENO ALIYOZUNGUMZA TAMEKA RAYMOND KWA MARA YA KWANZA TOKA UTOKEEE MSIBA WA MWANAE NDIO HAYA.

                                                       Usher Raymond naTameka Raymond
                                                     Marehemu Kile na mama mzazi Tameka.
Zikiwa hata wiki mbili hazijaisha toka mke wa zamani wa mwimbaji Usher Raymond na Tameka Raymond kumzika mwanae kipenzi Kile aliefariki dunia kwenye ajali iliyotokana na pikipiki zinazoendeshwa kwenye maji, Mama huyu wa watoto watano ametoa kauli ya kwanza toka msiba utokee.

Tameka ambae kwa kipindi kirefu amekua mahakamani kutokana na kesi ya kugawana watoto yeye na mumewe wa zamani Usher Raymond, amesema hii statement haijaandikwa na timu yake, msaidizi wake wala yeyote bali ni maneno ambayo ameyaandika kutoka moyoni mwake.

Ripoti yake inasema hivi “Kwa majonzi makubwa nimejikuta nikilazimika kujibu waraka wa mahakama unaonitaka nifike Mahakamani kwenye kesi ambayo sio mimi niliyeianzisha, sikumshitaki mtu yeyote kwenye hii kesi ya January 2011 japo niliridhika na maamuzi ya  ya kugawana majukumu kuwalea watoto”

“Kinachonisikitisha ni kulazimika kwenda Mahakamani katika kipindi ambacho naomboleza kifo cha mwanangu, hata hivyo sitozuia Mahakama kufanya kazi yake, nitaendelea na yale yote nitakayolazimika kuyafanya huku nikiwa na matumaini kuwa hali hii ngumu itanisaidia kupambana na hali nyingine ngumu zaidi ya majonzi ya mwanangu” – Tameka

Kwenye line ya mwisho, Tameka mwenye umri wa miaka 41 amesema “naisihi jamii yote kutoamini yale yote yanayosikika kwenye vyombo vya habari na pia jamii isiwe nyepesi ya kuhukumu, wanangu ndio ulimwengu wangu na nitapambana kufa na kupona kuwalinda na kuwa nao maisha yangu yote”

Hiyo ni taarifa kupitia mtandao wa Global Grind, Hallo Beautiful wameripoti kwamba Usher Raymond hakutoa ushirikiano wowote kipindi cha msiba na hakuwahi kuongea na Tameka wala familia yake, pia alikwenda kumzika Kile kwa sababu tu tayari anajulikana kwamba ni mtoto wake wa kufikia na vyombo vya habari na watu wengine walitegemea kuona angefanyaje kwenye maziko ya mtoto wa mke wake wa zamani.

HBL wameripoti zaidi kwamba taarifa zilizopo ni kwamba wakati wote wa msiba Usher alikua hapokei simu za Tameka wakati alipohitajika kutoa msaada wa pesa kwa ajili ya matibabu ya Kile alipokua kalazwa.

MWALIMU AFUKUZWA KAZI KWA KUONGEA "KISWAHILI" - ARUSHA


Mwalimu Daniel Urioh.
Ninaomba WIZARA YA ELIMU iwe makini na wawekezaji katika secta ya elimu, hasa kwenye shule ambazo zinatoa msaada kwa watoto wakitanzania ambao familia zao hazina uwezo wa kifedha, kwa mfano ninaomba mmiliki wa shule ya St Jude apate muda wa kusikiliza kilio cha wafanyakazi wake wakitanzania kwani kimsingi wamekuwa wakiteswa, kukandamizwa na kupuuzwa wanapodai haki na maslahi bora kazini kwao.


Shule hii utumia picha za wafanyakazi kuzalisha kiasi kikubwa cha fedha kuendesha shule, kwa wafanyakazi na wanafunzi hupigwa picha mara kwa mara na kulazimishwa kuleta picha za familia zao kila mwaka bila shule kuweka wazi kwa mfanyakazi kuwa anawafadhili wangapi, wafadhili  huchangia kiasi gani cha fedha, kukatazwa kuwasiliana na mfadhili, kuruhusiwa kuhoji lolote kuhusu pato na matumizi ya uzalishwaji wa fedha kupitia wewe na familia yako? Hata hivyo picha za familia zinazalisha fedha kwaajili ya uendeshaji wa shule ilihali familia haifaidiki kwa uuzaji huo wa sura zao ughaibuni? Kinachosikitisha zidi ni pale mfanyakazi anapoachishwa ,shule inaendelea kitumia picha za wafanya kazi na familia zao kuzalisha fedha nyingi za kigeni bila ridhaa wala fedha hizo kuwafaidisha wenye picha, na kutojali kuwa kitendo hicho kinyume na sheria.

Pia picha hizo zimekuwa mara kadhaa zikidhalilisha utu na uhuru wa muafrika, kwani sura za watanzania zimekuwa bidhaa ya kuzalisha fedha zisizojulikana ni kiasi gani na kwa faida ya nani? tena ulazimisha vitendo visivyo halisi na maisha yetu mfano unalazimishwa kucheka ukichukuliwa picha ilihali mapato uzalishayo hujui na ukikataa kutekeleza unatishiwa kufukuzwa kazi, wanafunzi ushikishwa zawadi zisikuwa zao na kupigwa picha na uzalisha kiasi cha fedha bila ridhaa wafunzi wanapohoji  hupewa adhabu au kutishiwa kufukuzwa.

Kama hiyo aitoshi shule hii imekuwa mara kadhaa ikipuuza sheria za nchi bila sababu za msingi mfano wamekuwa wakiajiri familia za ughaibuni kinyume na sheria za nchi mfano wanaajiri baba, mama na mtoto wa familia moja tena kwenye nafasi za juu na kutoweka wazi taaluma zao wakiwaaminisha kuwa ukiwa mzungu basi we msomi wa kila kitu, kinyume na sheria ya ajira nchini, pia shule imekuwa mara kadhaa haieshimu sikukuu za kitaifa bila sababu za lazima na kutojali wala kuthamini mchango wa waasisi na wazalendo waliopoteza maisha kujenga utaifa, amani na umoja wa Tanzania, cha kushangaza shule ujiamulia siku za mapumziko ya wafanyakazi na wanafunzi watakavyo wao, huwa najiuliza  hivi  shida inaweza tulazimisha kufuata sheria za wawekezaji na kupuuza sheria za nchi yetu Tanzania?

Linalosikitisha zaidi shule hii imekuwa hodari wa kupiga vita ya matumizi ya lugha ya kishwahili kwa wanafunzi na wafanyakazi hata kudiriki kuwaadhibu kwa kuwarudisha wanafunzi nyumbani kwa kosa la kuzunguza kishwahili, hata kufika mbali zaidi na kufukuza mwalimu mwenye shahada ya ualimu kwa kosa ni kuzungumza kishwahili na wanafunzi, huu ni uvunjaji wa sheria za nchi usiovumilika.
Hata hivyo nataka wao wajue kuwa lugha ya taifa Kiswahili imekuwa mhimili mkubwa wa kujenga umoja na amani. Kiasi cha kuwa wekeza kupata mafanikio, kama awa amini wakajaribu kuwekeza Somalia na kuwasaidie watoto wa Somalia wenye shida kubwa ya elimu, ilo linge ondoa jeuri yao ya kupuuza sheria za Tanzania.
Kitendo cha shule hii kuwatumia watanzania kama bidhaa na utaratibu wao wa fukuza fukuza waliyonayo hasa kwa watanzania.  Shule hii huwatumia viongozi wazalendo kuwanyanyasa wenzao na kusaidia shule kuendelea na  dharau na kupuuza sheria za nchi zenye maslahi kwa wazalendo, wale wote watakaonyesha uzalendo kama mimi wakuonyesha kukerwa na kuchukua hatua ya kuhoji na kutetea sheria za nchi na watanzania dhidi ya upuuzwaji wa uzalendo, haki, utu, lugha ya taifa, maslahi ya kiwango cha utumikishwaji, niliishia kufukuzwa kwa kosa la kuongea kishahili na wanafunzi.

Ushauri wangu kwa wizara ya elimu.
Kwanza kupandisha mshahara na mazingira ya kazi serikalini ilikuvutia waalimu wote toka shule binafsi kwani wangi wamechoshwa ni manyanyaso ya waajiri.
Pili kufanya ukagua si wa taaluma tu bali pia mfumo wa uajiri na maslahi ya watanzania waajiriwa kwenye shule zinazomilikiwa binafsi kwa misaada ya watu toka ughaibuni.
Tatu iwe na utaratibu wa ufuatiliaji wa mapato na matumizi ya shule zinazopata fedha toka kwa wafadhili kwani shida za  watanzania zimekuwa zikinufaisha wachache na kutengeneza ajira ya watu wasiona sifa za kufanya kazi ughaibuni na kuja kufanya kazi ambazo wazalendo wanaweza kuzifanya.
Nne kusisitiza hasa shule binafsi nchini kuthamini lugha ya kishwahili, kuheshimu sheria za ajira, kuheshimu sikukuu za kitaifa na kuheshimu, kulinda tamaduni  na vipaji vya watanzania kwa manufaa ya Tanzania.

Ni kweli tar 15/06/2012 nimefukuzwa kazi ya kufundisha (ualimu) St-Jude-Arusha kwa kosa la kuzungumza Kiswahili.

Uzalendo gharama nimeamua kujitoa kwa kutetea nchi yangu Tanzania.

Mwalimu Daniel Urioh. Kwa undani zaidi piga :+255 755 379 737.

CHANZO NA kajunason.

Magazeti ya leo Jumamosi 4th August 2012