Sunday, June 10, 2012

HONGERA TAIFA STARS

 Kikosi cha Taifa Stars kilichoanza mechi ya leo.
Taifa Stars imeilaza Gambia kwa bao 2-1 katika mechi ya kufuzu kucheza Fainali za Kombe la Dunia zitakazofanyika nchini Brazil 2014. Mabao ya Stars yamewekwa kimiani na Shomari Kapombe na Erasto Nyoni. Kwa sasa Stars ina pointi 3 na inashika nafasi ya pili katika kundi C linaloongozwa na Ivory Coast wenye pointi 4.

BOB MAKANI HATUNAYE TENA

Mzee Bob Makani enzi za uhai wake.
Naibu Gavana wa kwanza wa Benki Kuu ya Tanzania na Katibu Mkuu wa kwanza wa Chadema, ambaye pia amewahi kuwa Mwenyekiti wa chama hicho, Bob Makani, amefariki dunia usiku wa kuamkia jana katika Hospitali ya Agakhan jijini Dar es Salaam.
Habari za kifo chake zimetolewa na kuthibitishwa na Mwenyekiti wa Chama hicho, Freeman Mbowe, ambaye amesema kuwa, Bob Makani amefariki dunia, baada ya kuugua kwa muda mrefu, na mwili wake umehamishiwa katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili.
Kufuatia kifo cha mwasisi huyo wa chama hicho, sasa Chadema wamekatisha ziara za kuimarisha uhai wa chama zilizokuwa zikiendelea katika mikoa ya kusini mwa Tanzania.