Saturday, December 8, 2012

SADC Watua Dar Kwa Dharura

 Rais Yoweri Museveni wa Uganda (kulia) akisalimiana na  Makamu wa Rais wa Tanzania Dr. Gharib Bilal  (kushoto)  Dec,7,2012 alipowasili katika Uwanja wa ndege wa kimataifa wa JK ,Nyerere jijini Dar es Salaam kuhudhuria mkutano wa dharura  wa Jumuiya  ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC)

  Rais wa Mozambique Armando Guebuza (kush) akiwa waziri wa mambo ya nje na ushirikiano wa kimataia Membe
 Rais wa Jamhuri yaKidemokrasia ya Congo( DRC) Joseph Kabila (kushoto) akipokelewa na Waziri wa Uvuvi Dkt. David Mathayo Dec,7,2012 katika uwanja wa ndege  wa kimataifa wa Jk . Nyerere jijini Dar es salaam
 Makamu wa Rais wa  Zambia Dkt.Guy Scott (kulia) akifurahia jambo na Waziri wa Uchukuzi Dkt, Harison Mwakyembe (dec,7,2012) wakati wa mapokezi katika uwanja wa ndege wa  kimataifa wa JK Nyerere jijini DSM kwaajili ya kuhudhuria mkutano wa dharura wa SADC
Kikundi cha sanaa ya matarumbeta kinachoongozwa na gwiji wake Mzee Hoza,kikitoa burudani katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa JK, Nyerere Dec,7,2012 wakati wa mapogezi ya Marais na wajumbe mbalimbali wanaohudhuria mkutano wa SADC jijini Dsm.

(Picha na Mwanakombo Jumaa- MAELEZO).

PATA YALIYOJIRI KWENYE SWAHILI FASHION WEEK 2012!










Kutoka Golden Tulip Dar es salaam Tanzania Swahili fashion week ndio inafanyika  mwaka huu ambapo imeanza december 6 na inaisha december 8 2012 yakiwa ni maonyesho ya mavazi Afrika mashariki na kati na huu ni mwaka wa tano, kuna wabunifu 22 kutoka Tanzania na 15 kutoka nje ya Tanzania, kutatolewa tuzo mbalimbali pia.

CUF Yamtumia Ujumbe Maalumu Jaji Warioba

CHAMA cha Wananchi (CUF), kimetoa wito kwa Mwenyekiti wa Tume ya Kuratibu Maoni ya Wananchi juu ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Sinde Warioba kuweka bayana muundo wa Mabaraza ya Katiba ya Wilaya.

Kauli hiyo ya CUF ilitolewa juzi na Katibu Mkuu wake , Maalim Seif Shariff Hamad wakati akizungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara katika Viwanja vya Alabama Miembeni.

Maalim Seif alisema kama Tume hiyo haikuweka bayana muundo wa mabaraza hayo na Chama Cha Mapinduzi (CCM), kinaweza kutumia mwanya huo kuteua wanachama wao ili wapate kulinda sera yao ya muundo wa Muungano uliopo sasa.
“Nasema hivi kwa sababu maraisi wote wawili ni wa CCM kwa hiyo wanaweza kutumia mwanya huu kuteua wafuasi wao ili wapate kutimiza idadi ya wajumbe,” alisema Katibu Mkuu huyo.

Maalim Seif ambaye ni Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar katika Serikali ya Umoja wa Kitaifa, alisema itakuwa jambo zuri sana kama wananchi watawekwa wazi katika kuunda mabaraza hayo.

“Naweka wazi kama kama Mabaraza haya yatakuwa na wanachama wa CCM peke yao hatuwezi kukubali abadani,” alisema Hamad.

“Lazima kuwe na uwazi na wananchi waelezwe Mabaraza hayo yataundwa na wajumbe wepi, ili kuondoa dhana mbaya inayoweza kujengwa na wananchi kuwa wajumbe hao watatoka katika chama kimoja cha siasa,” alisema Maalim Seif.Kutokana na dhana hiyo, Maalim seif aliitaka Tume ya Kukusanya maoni ya Mabadiliko ya Katiba ya Tanzania kuchukua hadhari mapema juu ya suala hilo ambalo linaweza kuharibu mchakato mzima wa maoni hayo.

Sambamba na hilo Maalim Seif alisema hata katika suala la kura ya maoni itakayokuja kufuatia huko mbele, bado kuna masuala mengine ya kujiuliza, kuhusu utaratiubu upi utatumika, wakati wa kura hiyo kwa Wazanzibari wanaoishi Tanzania Bara na watu wa Tanzania Bara wanaoishi Zanzibar.
Alieleza kuwa hofu hiyo inakuja kwa vile sheria ya mabadiliko ya katiba inasema mabadiliko hayo yatapitishwa, iwapo angalau nusu ya wananchi wa kila upande kati ya Tanzania Bara na Zanzibar wataunga mkono mabadiliko hayo, hivyo amehimiza mambo hayo lazima kwanza yawekwe wazi.

 Na: Talib Ussi, Zanzibar

Magazeti ya leo Ijumaa ya 8th December 2012