Tuesday, May 21, 2013

Magazeti ya leo Jumanne ya 21st May 2013




HII NDIO KUMBUKUMBU YA MIAKA 17 YA AJARI YA MELI YA MV BUKOBA ILIYOZAMA TAREHE 21 MAY

  Makaburi ya Igoma ambako ndugu zetu waliokuwa wakisafiri kwa meli ya MV Bukoba walizikwa.
                             MV Bukoba ikiwa inazama ilikuwa ni tarehe 21 mei 1996

" MATOKEO YA KIDATO CHA SITA".....SIFURI KIBAO ZAFUTWA KIMYA KIMYA

MPANGILIO wa alama mpya za kufaulu kwa wahitimu wa kidato cha sita waliohitimu mwaka jana, ambao matokeo ya mitihani yao yanaweza kutangazwa wakati wowote kuanzia sasa, unadaiwa kuzua aibu na kama si uamuzi uliotajwa bungeni wa matumizi ya alama za ufaulu za zamani, matokeo hayo yangeibua aibu kama ilivyojitokeza kwa kidato cha nne, 2012.

Kwa mujibu wa vyanzo vyetu vya habari kutoka Baraza la Taifa la Mitihani (NECTA) ambalo linaendelea kupanga matokeo hayo ya kidato cha sita kwa kuzingatia alama za zamani kama ambavyo taarifa ya awali ya Tume iliyoundwa na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, ilivyosomwa bungeni hivi karibuni, hali ingekuwa mbaya zaidi katika ufaulu kwa wanafunzi wa kidato cha sita kiasi cha kuweza kutishia uhai wa vyuo vikuu nchini kukosa wanafunzi wa kutosha.

“Hali ilikuwa mbaya sana kama alama za kufaulu zingeachwa zitumike zile mpya na si za zamani. Vyuo vikuu nchini visingeweza kupata wanafunzi wa kutosha.

SPIKA WA BUNGE AAMURU KUFUTWA KWA HOTUBA YA SUGU ILIYOSABABISHA BUNGE LISITISHWE ASUBUHI

Spika wa Bunge la Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, Mh Anne Makinda, ameamuru kambi ya upinzani kuyaondoa maneno yote yaliyomo kuanzia ukurasa wa kwanza mpaka wa 14 katika hotuba rasmi ya Kambi ya upinzani iliyosmwa na mbunge wa Mbeya Mjini, Mh. Joseph Mbilinyi ‘Sugu,’ ambaye ni Waziri Kivuli wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo.

Mh. Makinda ametoa amri hiyo baada ya Kamati ya Kanuni ya Bunge kujadili hotuba hiyo na kubaini kuwa ina kauli za uchochezi; na kusema kuwa kuwa Bunge sio sehemu kugombanisha wananchi, hivyo maneno yote ya uchochezi hayaruhusiwi.

Katika hotuba hiyo, Mh. Mbilinyi aliishutumu serikali kuhusika na kuteka nyara waandishi wa habari, kauli iliyopelekea Spika Makinda kuahirisha Bunge.

MAHAKAMA YAMWACHIA HURU MSIGWA KWA DHAMANA.....

WATUHUMIWA 60 wa vurugu kati ya machinga na polisi mjini Iringa akiwemo Mbunge  wa  Jimbo  hilo, Mchungaji Peter Msigwa, kwa sasa  wanafanyiwa  utaratibu  wa  dhamana  baada ya mahakama  kukubali  kupewa  dhamana.

 Awali watuhumiwa  walisomewa mashitaka matatu  huku mbunge  akisomewa shitaka la  kushawishi  watuhumiwa hao kufanya  vurugu.
 
Watuhumiwa  wote  wamekana mashitaka  dhidi yao na kwa  sasa utaratibu  wa dhamana  unafanyika mbele  ya mahakama ya  hakimu mkazi  wa wilaya ya  Iringa, Mheshimiwa  Godfrey Isaya.

Mashitaka waliyosomewa watuhumiwa ni pamoja na shitaka la kwanza la mbunge ambalo ni kushawishi kufanya vurugu, huku  wengine  wote  makosa yao yakiwa ni kufanya mkutano bila kibali, kuharibu mali kinyume na sheria ni  kufanya  vurugu.

RAIS KIKWETE AMWAGIA SIFA LOWASSA......AMEDAI KWAMBA LOWASSA NI "JEMBE"

Rais Jakaya Kikwete amemwagia sifa Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa hatua ambayo inaweza kutafsiri mengi katika medani ya siasa nchini.

 Akizungumza na wabunge wa CCM kwenye Ukumbi wa White House Dodoma juzi, Rais Kikwete ambaye pia mwenyekiti wa chama hicho, alisema nguvu za Lowassa pekee zinatosha kushinda uchaguzi mdogo wa kiti cha udiwani Kata ya Makuyuni kilichoko wilayani Monduli.

Kata ya Makuyuni iko wilayani Monduli, ambako Lowassa amekuwa mbunge wake tangu mwaka 1995.

Habari za kutoka ndani ya kikao hicho zinaeleza kuwa Rais Kikwete alitoa kauli hiyo kuhusu kampeni za uchaguzi huo wa Makuyuni, baada ya kuwa ametoa ruksa kwa makada wa chama hicho wanaotaka urais kuanza kujipitisha pitisha miongoni mwa wanachama wa chama hicho.

Lowassa anatajwa kuwa miongoni mwa wanaCCM wanaotaka kumrithi Rais Kikwete kwenye Uchaguzi Mkuu mwaka 2010.

“Sina tatizo na pale Makuyuni, najua muscles (misuli) za Mzee Lowassa zinatosha kutupa ushindi; au vipi mzee?” alidokeza mmoja wa wabunge wa CCM akimnukuu Rais Kikwete.