Friday, March 15, 2013

TCRA YAKATAA KURUDISHIA MFUMO WA ZAMANI WA ANALOGIA....

 Dar es Salaam. Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imesema haitarudi nyuma kwenye suala la kutumia mfumo wa matangazo kupitia njia ya dijitali na kwamba mfumo huo utaendelea kutumika.

Kauli ya TCRA imekuja siku moja baada ya wamiliki wa vituo vya utangazaji vya televisheni nchini kutishia kusitisha kurusha matangazo ndani ya mwezi mmoja kuanzia sasa kutokana na kushindwa kumudu gharama za uendeshaji.

Mwenyekiti wa Chama cha Wamiliki wa Vyombo vya Habari Tanzania (Moat), Reginald Mengi juzi alisema hakuna haja ya kurusha matangazo kwa hasara kwani watangazaji wamesitisha kutoa matangazo kwa sababu wananchi wengi hawana ving’amuzi. Licha ya Moat kutoa kauli hiyo juzi, Mkurugenzi wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Profesa John Nkoma alisisitiza kwamba TCRA haiwezi kurudi nyuma katika suala hilo kwani mfumo huo utaendelea kutumika.

WAGANGA 12 WAJITOKEZA KUPAMBANA NA "JINI MAHABA" LINALOMSUMBUA LADY JAYDEE

WAGANGA wanaodai kuwa ni wataalam na wana uzoefu wa kupambana na jini mahaba linalomsumbua Mwanamuziki Judith Wambura ‘Lady Jaydee’, wamejitokeza huku kila mmoja akiomba apewe nafasi ya kumtibu bure.

Mmoja wa wataalam hao aliyejitambulisha kwa jina la Jumaa wa Magomeni, Dar alisema: “Nimesoma habari kuhusu Jide, mimi naweza kumtibu tena bure, mpe namba yangu na mwambie anipigie.”

Mwingine ambaye hakupenda jina lake liandikwe alisema: “Nimesikitika sana kusoma hii habari ya huyu msanii Lady Jaydee, kwa kifupi naweza kumtibia free of charge.”

Kufuatia maombi ya wataalam hao, mwandishi wetu alijitahidi kumtafuta Jide bila mafanikio lakini juzikati kupitia kipindi chake cha Diary ya Lady Jaydee alionekana akipewa matibabu na ustaadhi mmoja, mazingira yanayoashiria kuwa huenda mambo yametulia.

BENARD MEMBE AGEUKA MBOGO BAADA YA KUHUSISHWA NA UTEKAJI WA ABSALOM KIBANDA

 Ifuatayo ni kauli iliyotolewa na Waziri wa mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa Bernard Membe kuhusu kilichoandikwa na gazeti la Mtanzania march 13 2013 toleo namba 7255.
 “SAKATA LA KUTESWA KWA KIBANDA: Membe atajwa” na kwamba eti mimi ninahusika na vitendo vya kikatili na unyama alivyofanyiwa Mhariri Mtendaji Mkuu wa kampuni ya New Habari, Bw. Absalom Kibanda”

“Nimeshangazwa na kusikitishwa sana na habari hizo na ningependa kuwahakikishia Watanzania wenzangu kwamba sijahusika, sihusiki na sina sababu ya kuhusika kwa namna yoyote ile. Sina nia, genge wala fedha za kufanya shughuli kama hiyo.

 Katika maisha yangu yote, sijawahi kugombana naye na hajawahi kunifanyia ubaya wowote. Kwa kifupi, sina uhasama na Bw. Absalom KIbanda”
.

"VIDEO YA LWAKATARE NI FEKI,,," HII NI KAULI YA DR. SLAA

  KATIBU  Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Wilbroad Slaa amezungumzia video aliyorekodiwa Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa Chama hicho, Wilfred Lwakatare na kusema ni ya kutungwa na vyombo vya dola.

Dk. Slaa pia amelituhumu Jeshi la Polisi kufanya mchezo mchafu kwa maslahi ya kisiasa.

Alikuwa akizungumza na waandishi wa habari Makao makuu ya chama hicho kufafanua suala la kushikiliwa kwa Lwakatare.

CHADEMA WALITAKA JESHI LA POLISI LIMCHUNGUZE LWAKATARE BILA UPENDELEO

Chama cha Demokrasia na Maendeleo kimesema kilikuwa na taarifa za mapema juu ya uwepo wa mkakati unaoratibiwa na kufanikishwa na maafisa wa ngazi za juu wa usalama wa taifa wa kukihusisha chama hicho na njama za kumdhuru mwenyekiti wa jukwa la wahariri Absalom Kibanda ili kukidhofisha chama hicho kisiasa.

Magazeti ya leo Ijumaa ya 14th March 2013

                  
                                                

DIAMOND AMTIA MIMBA PENNY NA KUAMUA KUMZAWADIA GARI LA MILIONI15

 Kupitia segment ya U Heard ya XXL Clouds FM na Soudy Brown, mwimbaji Diamond Platnums ambae aliongoza kwa kuwa msanii wa bongo alieandikwa sana kwenye internet mwaka 2012 amethibitisha kumnunulia mkoko mama watoto wake mtarajiwa.

Soudy Brown alimuuliza kuhusu fununu za kutumia Milioni 15 kununua gari la mke wake mtarajiwa mtangazaji Penny ambae kwa sasa ni mjamzito.

Diamond amekiri kwamba ni kweli kamnunulia Penny gari kwa sababu anaelekea kuwa mama watoto ambapo namkariri akisema “nilimuuliza gari gani anapenda, nimemuagizia iko njiani inakuja kwa hiyo sasa hivi anatumia la muda wakati akisubiria gari lake”

Alipoulizwa kuhusu kumuoa na kama mtoto atazaliwa nje ya ndoa, Diamond amejibu “siwezi kusema lini ila Mwenyenzi Mungu ndio anajua inaweza ikawa harusi ila kuna time inafika inabidi utulie, siwezi kusema chochote kwa sababu inawezekana mtoto akazaliwa ndani ya ndoa pia “