Sunday, October 14, 2012

Magazeti ya Leo Jumapili 14th October 2012


JK. Atembelea Makanisa Yaliyoharibiwa Katika Vurugu Za Waislamu Mbagala

 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiangalia uharibifu mkubwa ulkiofanywa katika kanisa la Pentekoste la Mbagala jijini Dar es salaam wakati wa vurugu za Waislamu Ijumaa iliyopita kufuatia habari kuwa kuna mtoto amekojolea Msahafu
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akioneshwa na Katibu wa Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Dar es salaam Bw. M Mkosimonga  uharibifu mkubwa uliofanywa kwenye kanisa hilo huko  Mbagala jijini Dar es salaam wakati wa vurugu za Waislamu Ijumaa iliyopita kufuatia habari kuwa kuna mtoto amekojolea Msahafu

 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akitoa pole kwa baadhi ya waumini wa  Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Dar es salaam kufuatia uharibifu mkubwa uliofanywa kwenye kanisa hilo huko  Mbagala jijini Dar es salaam wakati wa vurugu za Waislamu Ijumaa iliyopita kufuatia habari kuwa kuna mtoto amekojolea Msahafu
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akioneshwa na Mchungaji Alkwin Mbawi uharibifu mkubwa uliofanywa kwenye kanisa la Pentekoste la Mbagala jijini Dar es salaam wakati wa vurugu za Waislamu Ijumaa iliyopita kufuatia habari kuwa kuna mtoto amekojolea Msahafu

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akioneshwa na Mchungaji Alkwin Mbawi uharibifu mkubwa uliofanywa kwenye kanisa la Pentekoste la Mbagala jijini Dar es salaam wakati wa vurugu za Waislamu Ijumaa iliyopita kufuatia habari kuwa kuna mtoto amekojolea Msahafu

PICHA NA MUHIDIN MICHUZI

Hatimaye Mkuu Wa Wilaya Temeke Afika Eneo La Matukio Mbagala

            Mkuu wa wilaya ya temeke akiwa kanaisa lililoharibiwa kwenye vurugu  za waislamu jana

                                                                                FFU
                                                          Kamanda wa mkoa wa Temeke
 Akijibu hoja za waamini.wameomba wapewe ulinzi na serikali iwajibike kujenga kanisa kwani polisi walizembea kuzuia waislamu waliokuwa wakifanya vurugu kwa awamu tatu bila polisi kudhibiti hali hiyo
                                                                     Yupo kazini

Madabida Ambwaga Guninita Dar

PATASHIKA ya uchaguzi imeendelea ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa kuchagua wenyeviti wa mikoa, huku baadhi ya wenyeviti wa zamani wakiangushwa, sura mpya kuibuka na wengine wakitetea nafasi zao. Jijini Dar es Salaam, kada wa siku nyingi wa chama hicho, Ramadhani Madabida ameibuka mshindi wa nafasi ya uenyekiti wa CCM, Mkoa wa Dar es Salaam baada ya kumbwaga John Guninita aliyekuwa akishikilia nafasi hiyo.

 Madabida ameshinda kwa kupata kura 310 akimng'oa John Guninita aliyekuwa mwenyekiti, ambaye alipata kura 214 huku Madison Chizii akipata kura 52. Katika uchaguzi huo wajumbe walianza kuingia ukumbini hapo saa 2.00 asubuhi na kuanza kupiga kura saa sita mchana. Awali Madabida alijikuta katika wakati mgumu wakati akijinadi baada ya mjumbe mmoja kumuuliza swali kuhusiana na kiwanda chake kudaiwa kutengeneza dawa bandia za kupunguza makali ya Virusi vya Ukimwi za ARV.

 Hata hivyo, Msimamizi wa uchaguzi huo, Assa Simba alimzuia Madabida kujibu swali hilo akisema kwamba haukuwa wakati wake. Awali, akifungua mkutano wa uchaguzi huo, Makamu wa Rais, Dk Gharib Bilal alisema kuwa chama hicho kimelenga kurudisha majimbo yake yote yaliyochukuliwa na wapinzani katika Uchaguzi Mkuu wa 2015.

“Natumaini uchaguzi utakuwa wa haki bila vurugu zozote, nawaomba msiwe na wasiwasi kwani chama chenu kipo imara kuwakabili wapinzani,” alisema Dk Bilal. Kambi ya Sitta yapeta Habari kutoka mkoani Tabora, zinaeleza kuwa kambi ya Samuel Sitta imeibuka mshindi mkoani humo baada ya mtu anayetajwa kuwa mgombea wake katika nafasi ya uenyekiti wa CCM mkoani humo, Hassan Wakasuvi kuchaguliwa kukiongoza chama hicho.

 Wakasuvi alichaguliwa katika nafasi hiyo kwa mara ya pili, alipata kura 921 kati ya kura 1012 zilizopigwa, huku Mwamba Z mwamba akiambulia kura 75, ambapo kura 16 ziliharibika. Kimbisa ambwaga Kusila Mzizi wa fitina ndani ya CCM, mkoani Dodoma ulikatwa juzi baada ya Mbunge wa Afrika Mashariki, Alhaj Adam Kimbisa kushinda kiti cha uenyekiti wa chama hicho mkoani humo kwa kumbwaga Mwenyekiti wa zamani, William Kusila.

Baada ya kutangazwa mshindi wa kiti hicho, Kimbisa alisema kuwa bado kuna watu wanaoendeleza siasa za ukabila na kuongeza kuwa jambo hilo ni hatari kwa siasa hasa mkoani Dodoma. Wagombea watatu waliwania kiti hicho, ambapo Kimbisa aliibuka na ushindi wa kimbunga kwa kupata kura 948 katika kura 1198 zilizopigwa akiwaacha Kusila aliyepata kura 216 na Denis Bendera aliyeambulia kura 30.

Ushindi wa Kimbisa ulianza kuonekana mapema juzi asubuhi, baada ya mkutano huo kuanza ambapo wajumbe kutoka wilaya zote saba za Mkoa wa Dodoma walipokuwa wakiingia walikuwa wakiimba wimbo wa kumsifu Kimbisa. Baada ya aliyekuwa msimamizi wa uchaguzi huo, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dk Rehema Nchimbi kumtangaza Kimbisa kuwa ndiye mshindi ukumbi mzima ulilipuka kwa nderemo na shangwe.

Serikali Yafikishwa Mahakama Ya The Hague

KITUO cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), kimeipeleka Serikali ya Tanzania katika Mahakama ya Kimataifa ya Makosa ya Jinai (ICC), kutokana na matukio 24 ya mauaji yanayokiuka haki za binadamu yaliyotokea nchini kati ya Januari na Septemba mwaka huu.

Mbali na hilo, LHRC kimepeleka taarifa hizo kwa Mjumbe Maalumu wa Umoja wa Kimataifa, anayeshughulika na masuala ya mauaji ya raia yanayofanywa na vyombo vya dola.

Hatua hiyo ya LHRC inatokana na ripoti tatu zilizotolewa hivi karibuni kuchunguza kifo cha aliyekuwa Mwandishi wa Habari wa Kituo cha Televisheni cha Channel Ten, Daudi Mwangosi kilichotokea katika Kijiji cha Nyololo, Mkoa wa Iringa, Septemba 2 mwaka huu.

Ripoti hizo ni ile ya Kamati ya Kuchunguza Mauaji hayo iliyoundwa na Waziri wa Mambo ya Ndani, Dk Emmanuel Nchimbi iliyokuwa chini ya Jaji Steven Ihema; Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora iliyokuwa chini ya Jaji Kiongozi Mstaafu, Amir Manento na ile ya Baraza la Habari Tanzania (MCT) na Jukwaa la Wahariri Tanzania (Tef), iliyoongozwa na John Mirenyi.

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Mkurugenzi Mtendaji wa LHRC, Dk Helen Kijo-Bisimba alisema kuanzia Januari hadi Septemba mwaka huu, jumla ya watu 24 wameuawa na watendaji wa vyombo vya ulinzi na usalama.

 “Tumepeleka mashtaka 24 ICC tangu Septemba 28 mwaka huu, ambayo yanahitajika kufanyiwa uchunguzi na kuchukua hatua kali dhidi ya Serikali ya Tanzania ambayo imekuwa ikiwalinda viongozi wake wanaokiuka haki za binadamu,” alisema Dk Bisimba.

Alisema taarifa hizo pia wamezipeleka kwenye Tume ya Afrika ya Haki za Binadamu katika kikao kinachoendelea huko Ivory Coast, lengo likiwa ni kuchunguza na kuchukua hatua katika Mahakama ya Afrika.

“Tunatarajia kuona uwajibikaji wa viongozi wote wa Serikali na vyombo vya dola waliohusika kwa njia yoyote ile. Hatua hizo au uwajibikaji huo ni pamoja na kujiuzulu, kuachishwa kazi na kufikishwa Mahakamani, ” alisema.

 Aliitaka Serikali kuacha propaganda zinazotaka kuchochea vurugu katika taifa huku akisema inapaswa itambue kuwa hivi sasa nchi iko katika zama za vyama vingi vya siasa na kuacha kutumia vyombo vya dola kuleta chuki na mafarakano.

 Dk Bisimba alisema baada ya kupitia taarifa zote tatu, LHRC kimesikitishwa na taarifa ya Kamati ya Dk Nchimbi... “LHRC hakijashangazwa sana pale taarifa hiyo ilipoonyesha wazi nia ya kuwalinda watuhumiwa kwa kuwa Serikali yetu bado haijajenga mfumo wa kujichunguza na kujiwajibisha yenyewe.”

Askofu Malasusa Awatuliza Wakristo Mbagala

 Askofu mkuu wa KKKT Alex Malasusa akiwaasa wakristu kuwa watulivu wakati huu wakati mamlaka za dola zikishughulikia swala hili,wakati huu wadumu katika maombi na wawasamehe ndugu zao waislamu. na kuwaombea.Mungu atawapigania



 Mchungaji wa TAGP akiongoza maombi wakristo wakiwaombea waislamu.Mpaka muda huu hakuna kiongozi yeyote wa serikali ameshafika eneo la matukio na uongozi wa kanisa unawasubiria viongozi wa kiserikali
                                waumini wakiwa katika maombi na huyu akilia kwa uchungu