Thursday, March 28, 2013

BREAKING NEWS:MBUNGE WA CHAMBANI SALIM HEMED KHAMIS AFARIKI


 Mbunge wa chambani Bwana Salim Hemed Khamis baaday ya kuanguka jana ghafla hapo jana jijini Dar katika vikao vya mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa na kukimbizwa hospital ya taifa muimbili kwa matibabu ya haraka.Kwa habari zilizotufikia hivi punde zinaeleza kuwa mbunge huyo amefariki mchana huu.

Taratibu za kuusafirisha mwili wa marehemu kuelekea pemba kwa mazishi zinafanafanyika.Tutazidi kuwafahamisha zaidi.

MUNGU AILAZE ROHO YA MAREHEMU MAHALI PEMA PEPONI. AMINA

Magazeti ya leo Alhamisi ya 28th March 2013






MENEJA WA KAMPUNI YA NDEGE YA FASTJET ATIWA MBARONI

MENEJA wa Wafanyakazi wa Ndani ya Ndege wa Kampuni ya Fastjet Emma Donovan, alifikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Ilala Dar es Salaam kujibu shtaka linalomkabili la kutoa lugha ya matusi.

Emma (40) alipandishwa kizimbani jana na kusomewa shtaka hilo na Wakili wa Serikali Nassoro Katuga, mbele ya Hakimu Joyce Minde.

Katuga alidai Machi 19 mwaka huu Emma alimtolea lugha ya matusi Samson Itinde jambo ambalo ni kinyume cha sheria.Emma alikana shtaka hilo ambapo Katuga alidai upelelezi umekamilika na kuomba kupangiwa tarehe kwa usikilizwaji wa awali.

Hakimu Joyce alisema kuwa dhamana ya mshtakiwa iko wazi lakini kwa kuzingatia vigezo vya dhamana vitakavyotolewa kwa kuwa mshtakiwa ni raia wa kigeni.Alitaja masharti ya dhamana kuwa mshtakiwa anatakiwa kuwasilisha hati yake ya kusafiria au kutoa fedha taslim sh milioni tano na pia awe na wadhamini wawili ambao ni Watanzania.
Kesi hiyo imeahirishwaa hadi Aprili 9 ili kupangwa tarehe ya kuanza kwa usikilizwaji wa awali.

BINTI WA MIAKA 16 ALAZIMISHWA KUNYWA MKOJO NA MAMA YAKE MDOGO HUKO IRINGA

Vituko mjini Iringa haviwezi kuisha kama jamii haitakubali kwa moyo mmoja kupambana na ukatili wa kijinsia. Huyu ni Binti ZAWAD KARIM miaka 16 mkazi wa mshindo nyuma ya banki ya NBC manispaa ya Iringa amepigwa na hatimaye kunyweshwa mkojo na mama yake mdogo aitwaye Ever ubamba.

Tukio lilikuwa hivi:

SHIRIKISHO LA FILAMU TANZANIA LAMMPONGEZA WEMA SEPETU

SHIRIKISHO la Filamu Tanzania (TAFF) limempongeza msanii wa kike Wema Sepetu kwa moyo wa upendo aliouonyesha kwa msanii mwenzie Kajala Masanja kwa kumlipia faini ya sh. milioni 13 alizotozwa na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kutokana na kupatikana na hatia katika kesi ya utakatishaji fedha iliyokuwa inamkabili mahakamani hapo

Akizungumza kwa niaba ya viongozi wengine rais wa shirikisho hilo Simon Mwakifwamba alisema kuwa imani na moyo wa upendo aliokuwa nao msanii Wema ndio uliomsukuma kumlipia kiwango hicho cha fedha bila ya kujiuliza mara mbili kitendo hiko kimeonyesha jinsi gani wanavyohitaji kushirikiana katika matatizo

Alisema kuwa wasanii wanatakiwa kujifunza kutoka kwake kwani wanahitaji kuwa kitu kimoja kujaliana kwenye matatizo na kutambua kuwa wao ni familia moja wanaojenga nyumba moja