Wednesday, August 1, 2012

WAKALI WA MAN U MAREKANI NA MAMA OBAMA PAMOJA NA FANS!

 Wachezaji wakongwe wa Manchester United walipokutana na mama Michelle Obama mke wa rais Obama wa Marekani.

HIVI UMEISIKIA KAULI YA GAZETI LA MWANAHALISI BAADA YA KUFUNGIWA NA SERIKALI? NDIO HII..

Siku moja baada ya Serikali kutangaza kulifungia kwa muda usiojulikana gazeti la kila wiki la MWANAHALISI linalochapishwa na kampuni ya Hali Halisi Publishers kutokana na kulituhumu kuandika habari za uchochezi na zinazoleta hofu, Uongozi wa gazeti hilo umezungumza.

Mkurugenzi mtendaji wa kampuni hiyo Said Kubenea amesema kimsingi hawakupokea barua rasmi kutoka Serikalini inayowataka kusitisha zoezi la kuchapisha gazeti hilo na badala yake hizo taarifa wamezipata kupitia vyombo mbalimbali vya habari.

Kubenea amesema hawakubaliani na madai ya serikali kwamba gazeti hilo limekua likiandika habari za uchochezi na kusisistiza kwamba habari yeyote inayoandikwa katika gazeti hilo ni lazima iwe imefanyiwa uchunguzi wa kina na kamwe gazeti hilo halikuwahi kukurupuka na kuandika habari isiyo ya kweli.

Inaaminika kwamba moja kati ya habari za hatari zilizofanya gazeti hilo kufungiwa kwa muda usiojulikana ni ile ya kuchapisha namba za simu za watu waliowasiliana na Dr Ulimboka mara ya mwisho kabla ya kufanyiwa ukatili.

Kwa kusisitiza, Kubenea amesema “hakuna kosa lolote tulilolifanya na tunastahili kupongezwa badala ya kulaumiwa, tulichofanya sisi ni kitu kidogo sana, tuliangalia tu ni nani aliwasiliana na Dr Ulimboka kwa mara ya mwisho… sasa tumepetaje? hizo ni taarifa zetu, kama kuna uchochezi ambao tumeufanya tulipaswa kuwepo Mahakamani lakini mpaka leo hatujaulizwa, hatujahojiwa, hatujaitwa hivyo ina maana hakuna kesi…. mimi kubenea nimefanya uchochezi ni kosa, naweza kufanya kosa kama hilo alafu natembea barabarani? “

"Diamond Hatunae Tena" anasema ndiyo ingekuwa kichwa cha habari leo

DIAMOND HATUNAE TENA...!!!
"Diamond hatunae tena"....hiyo ndo ingekuwa heading na kichwa cha habari cha media na watu wengi kwenye social networks na simu zao za mikononi kwa siku ya jana....Kiukweli hali yangu ilikua ni mbaya sana,nilizidiwa na homa kali ya ghafla iliyosababishwa na kifua kilichonisumbua kwa takribani wiki mbili mfululizo....hadi kupelekwa Heameda Medical Clinic kwa Doctor Hery M. Mwandolela, Specialist wa Heart and Cough kwa uchunguzi na vipimo vikubwa maana hali haikuwa ya kawaida.....namshkuru Mwenyezi Mungu baada ya vipimo vyote iligundulika ni kifua cha kawaida tu ila kilisababishwa na tour na ziara nyingi nilizozifanya mikoa na nchi mbalimbali kwa mfululizo bila mapumziko ya kutosha..
kwa sasa hali yangu si mbaya sana...nawashukuru wote mliokuwa mkiniombea kupitia Blogs, Twitter, Bbm, Facebook...etc, na Media zote niweze recover

Picha toka kwa http://www.thisisdiamond.com

Dah  nimeweka lakini usirudie tena kuweka kichwa cha habari kama hiki........ Poleni kwa mtakaoshtuka si nia yangu.

JLO ASHEREHEKEA BIRTHDAY YAKE KATIKA BOAT NA KING'ASTI WAKE.

                                                                  Akielekea Kwenye boti
                                                  Hakika amependea red is my best
                            Baba shika mama isianguke bana kwa raha zao raha kupendwa Jamani
                                                              Keki ikielekea kwenye boti

Magazeti ya Leo Jumatano August 1st 2012

MABALOZI WA HARAMBEE YA UJENZI WA HOSTELI ZA WASICHANA WA SEKONDARI WAZINDUA KAMPENI YA ELIMU YAO WAJIBU WETU

 Mratibu wa mabalozi wa kampeni ya uchangiaji katika ujenzi wa mabweni Rebeca Gyumi ambaye ni pia ni mtangazaji wa kipindi cha fema akielezea jinsi walivyojipanga kuhakikisha wanachangisha  fedha za kutosha ili lengo la TEA likamilike
 Mabalozi wa kampeni ya TEA katika ujenzi wa hosteli wakiwaomba wananchi kushiriki kampeni hii kwa kuchangia kwa kutuma ujumbe CHANGIA TOFALI kwenda kwenye namba 15564. Katikati ni Mkurugenzi wa uhamasishaji wa TEA Seif Mohamed
 Nancy Sumari ambaye ni Miss Tanzania  2005 na pia mrembo aliyefikia ngazi ya juu katika mashindano hayo ya urembo akielezea jinsi alivyoguswa na kuamua kujitoa kwa asilimia mia moja kusaidia kampeni hizi. Katika kampeni hii TEA inakusudia kuchangisha jumla ya shilingi bilioni 2.3
 Jokate Mwegelo (kulia) akielezea imani yake kwa watanzania  na kuwaomba raia wanaoiombea mema nchi yetu kuguswa kama walivyoguswa wao kujituma katika kuchangia kampeni hii ambapo ujumbe mmoja wa CHANGIA TOFALI ni shilingi 250/=, Kushoto kwake ni Mwanablog maarufu na mwanamitindo Mariam Ndaba
Mabalozi wa kampeni ya kuchangisha fedha kwa ajili ya ujenzi wa mabweni katika picha ya pamoja, kutoka kushoto ni Nancy Sumari (Miss Tanzania 2005) Rebeca Gyumi(Mtangazaji wa kipindi cha FEMA), Mariam Ndaba(Mwana mitindo na mmiliki wa blog)  Jokate Mwegelo(Mshindi wa pili Miss Tanzania 2006) na asiyekuwepo ni Faraja Nyalandu (Miss Tanzania 2004) ambaye alikuwa na udhulu na atakuwepo katika kampeni zinazoendelea.

 Kikundi cha wasichana maarufu watano katika nyanja mbalimbali nchini wameungana kwa pamoja na kuamua kwa hiari kuunga mkono jitihada za Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) za kutafuta kiasi cha shilingi za kitanzania billion 2.3 zitakazotumika kujenga hosteli 30 ambazo zitahudumia wasichana wa shule za sekondari 1,504.

Kikundi hicho cha mabalozi wa kampeni hii kinaundwa na Rebeca Gyumi(Mtangazaji wa kipindi cha FEMA) Faraja Nyalandu (Miss Tanzania 2004), Nancy Sumari (Miss Tanzania 2005) Jokate Mwegelo(Mshindi wa pili Miss Tanzania 2006) na Mariam Ndaba(Mwana mitindo na mmiliki wa blog) kiliguswa kwa namna ya kipekee na na jitihada za TEA na hivyo wakaamua kwa hiari kuungana na TEA katika kuhamasisha watu kujitokeza na kuchangia kampeni hii.

Mabalozi hawa wameiita kampeni yao “Elimu Yao. Wajibu wetu” maana ya usemi huu ni kwa kila mtanzania ana wajibu wa kuhakikisha mtoto wa kike anapewa haki yake ya kuwa na elimu bora. Haki hii ya elimu inajumuisha mazingira mazuri ya kusomea. Hivyo huu ni wito kwa watanzania, wafanyabiashara, wafanyakazi, wanawake watanzania waliofanikiwa na watanzania wa ughaibuni kujitokeza kwa wingi na kuhusika moja kwa moja na jitihada hizi.

Changamoto ambazo mtoto wa kike anakumbana nazo hususani anayetokea nyumbani kwenda shule ni pamoja na kukosa muda wa kujisomea kutokana na kazi za nyumbani ambazo zinapelekea kuathiri maendeleo ya elimu kwa mtoto wa kike, mimba na ndoa za utotoni ni kati ya changamoto kubwa zinazowakumba wale waliopanga karibu na maeneo ya shule, kutokana na hayo, Mabalozi hawa wameamua kujitolea kwa kuweka mpango mkakati utakaosaidia ujenzi wa hosteli tano na kuendelea kati ya hizo 30 ambao TEA imepanga kujenga.

Mpango mkakati huo ni pamoja na kufanya kampeni katika vyomba mbalimbali vya habari nchini na kuandaa  mbio za hisani ambapo hela zitakazopatikana zitapelekwa katika mradi huo. Mabalozi hawa wanaamini kuwa tofali moja kutoka kwa kila mtanzania linaweza kuleta mabadiliko “changia Tofali”. Unaweza kuchangia kwa kutuma neno "Changia Tofali"kwenda namba 15564, na utakuwa umechangia Tshs 250/-. Changia mara nyingi uwezavyo.

Tunakuomba mchango wako wewe mzazi, wadau wa elimu na watanzania kwa ujumla wenu kuchangia katika kampeni hii. Mchango unaweza kuwa ni wa fedha taslimu au vifaa vya ujenzi wa hosteli na samani. Kwa upande wa fedha taslimu unaweza kuweka fedha katika akaunti ya “mfuko wa elimu” benki ya CRDB, namba ya akaunti 01J027639900 au kupitia akaunti ya M-pesa 404040, au tuma ujumbe Changia Tofali kwenda namba 15564. Pia unaweza kuleta mchango wako katika ofisi zetu zilizopo mikocheni barabara ya kambarage au kupitia vituo vya Televisheni vya ITV, Channel 10 na Star TV.
Picha kutoka:8020fashions.blogspot.com