Thursday, December 13, 2012

Chukua Hii ......Wamependeza









TANZANIA MWENYEJI MKUTANO WA MADOLA

TANZANIA itakuwa mwenyeji wa mkutano wa   Vijana wa Kanda ya Afrika wa Jumuiya ya Madola kuanzia Januari 28 hadi Februari Mosi mwaka huu.

 Hayo yamesemwa (leo)  na  Mkurugenzi  wa Kanda ya Afrika ya Mpango wa Vijana wa  Jumuia ya Madola, James Odit  wakati akizungumza na  Waziri wa Habari, Vijana , Utamaduni na Michezo, Dk. Fenella Mukangara kuhusu  maandalizi ya mkutano  huo.

 Mkurugenzi huyo alisema mkutano utahusisha nchi 22 ambazo ni   wanachama na jumla ya washiriki 60 wanatarajiwa kuhudhuria mkutano huo kutoka katika  wizara zinazohusiana na masuala ya vijana, viogozi wa vijana, viongozi wawakilishi wa Baraza la Vijana, wawakilishi wa kimataifa, viongozi wa kikanda wa maendeleo ya vijana na Jumuiya ya Madola.

Miongoni mwa mambo mengine waliyojadiliana ni utekelezaji wa Sera ya Taifa ya Vijana na jinsi ya kuunda Katiba ya  Baraza la Vijana la Jumuiya ya Madola.

“Mkutano huu utajadili namna ya kuunda Barazala Vijana la Jumuiya ya Madola(CYC) na program za maendeleo ya vijana na jinsi ya kuwawezesha katika shughuli mbalimbali za kimaendeleo,” alisema Odit.

 Kwa Upande wake Waziri wa wizara hiyo, Dk. Mukangara alisema  anaishukuru jumuiya hiyo kwa kuichagua Tanzania kuwa mwejeji wa mkutano huo. Huku akisema suala la uundaji wa Baraza la Taifa la Vijana hivi sasa liko katika hatua ya ngazi za juu.

Waziri huyo alizitaja changamoto za kuendeleza mipago mbalimbali ya maendedeleo ya vijana kuwa ni kukosefu wa fedha za kutosha   mfano vile kuwawezesha vijana katika shughuli za kiuchumi na kimaendeleo, kuwajengea uwezo,  kuwapatia ajira, ujuzi na elimu.

 Akifafanua kuhusu suala hilo  Mkurugenzi huyo alisema atalifikisha  suala hilo  kwa wenzake ili waweze kungalia namna ya kuweza kushirikiana.

Waziri Mukangara alishauri  jumuiya hiyo kuangalia namna ya kuweza kushirikiana katika maeneo mengine  ambayo ni sekta ya Michezo, Utamaduni na Habari.

Magazeti ya leo Alhamisi ya 13th December 2012

KAULI YA FAMILIA YA MAREHEMU SHARO MILIONEA KUHUSU SAUTI YA SHARO KUENDELEA KUTUMIKA KWENYE TANGAZO LA AIRTEL

Ni watu wengi wamehitaji kufahamu kuhusu kauli ya familia ya Marehemu mwigizaji/msanii Sharo Milionea baada ya tangazo la Airtel lenye sauti yake kuendelea kutumiwa na kampuni hiyo wiki kadhaa baada ya Sharo kufariki kwa ajali ya gari iliyotokea novemba 26 2012 Tanga.

Mjomba wa Marehemu ambae ndio msemaji wa familia Shaban Mkiete amethibitisha kwamba wamezungumza na kukubaliana na kampuni ya Airtel na hapa namkariri akisema “ni kweli tumekubaliana, kwa mujibu wa makataba wao lilikua linaisha terehe 31 mwezi huu tumekubaliana kwamba liendelee kwa makubaliano ambayo tumekubaliana nayo sisi kati ya mzee Majuto ambae bado yupo na familia ya Marehemu, mama mzazi wa Sharo Milionea ameridhia hilo hakuna tatizo”

Siku ya msiba millardayo.com ilipopata nafasi ya kuongea na mwakilishi wa Airtel alisema Marehemu Sharo Milionea alifariki ndani ya kipindi cha miezi 6 tu toka asaini dili la kuwa balozi wa Airtel na kufanya matangazo mbalimbali yeye na mzee Majuto.

Sio tu dili la Airtel, imefahamika tayari Sharo Milionea alikua amesaini mikataba mizuri na makampuni mbalimbali wakiwemo Wamarekani waliotengeneza filamu maarufu Afrika kama Yellow Card, Neria na nyingine ambapo kwa sasa Wamarekani hao wako hapa Tanzania na wametengeneza series kadhaa ikiwemo Wahapahapa na Siri ya Mtungi ambayo ndio Sharo Milionea kashiriki ndani na mpaka anafariki tayari alikua ameshaanza kucheza igizo hilo.

Kutoka : millardayo.com

Mwenyekiti Wa Chadema Uk, Chris Lukosi Amevuliwa Madaraka Na Kusitishwa Uanachama


Ikiwa ni takribani miezi minne tangu tawi la CHADEMA UK lifunguliwe rasmi na Mr Godbless Lema, kumekuwepo na maendeleo makubwa ya ujenzi wa tawi hili lakini vile vile kumekuwepo na changa moto mbali mbali kutokana na uelewa wa watu ktk dhana nzima ya M4C. M4C ikiwa na maana ya Movement for Change, ni sharti mtu yeyote anayeingia ktk movement hii kwenye ngazi ya uongozi aelewe haya machache ya msingi:

1) Kwanza aone matatizo yanayomgusa yeye na jamii yake
2) Ajue na kutambua fika chimbuko la matatizo haya
3) Awe tayari kuwa kiini cha mabadiliko ya kweli anayoyataka kwa jamii
4) Aweze kutoa ufumbuzi kwa kukemea maovu, kuelimisha na hata yeye binafsi kuelimika
5) Ili afanikiwe ktk kipengele cha (4) ni sharti ajitambue yeye binafsi ya kwamba ni:
i) Lazima awe safi na mwenye sifa za kukemea waovu
ii) Aweke maslahi ya jamii mbele na si yake binafsi
iii) Awe na sifa za uongozi zinazotakiwa, nidhamu ikiwa nambari moja ktk orodha.
iv) Awe na msimamo wa kiitikadi

Kwa hiyo, uongozi wa CHADEMA UK kwa baraka za watetezi wa haki ya kweli (CHADEMA TZ) unawatangazia umma watanzania kokote mlipo kwamba kuanzia leo

 tarehe 12/12/12, Mr Christopher Lukosi amevuliwa rasmi uongozi na amesitishwa uanachama kutokana na kutokidhi mengi ya yaliyotajwa hapo juu.

Uongozi wa CHADEMA UK unamshukuru sana kwa mchango na ushirikiano wake mkubwa kwa kipindi ambacho matundu ya chujio yalikuwa makubwa. Tutaendelea kumkumbuka na hata kutumia misemo yake yenye maana nzito kwa jamii ya kitanzania, kama vile: -

i) Sisi sote ni ndugu, tatizo ni CCM
ii) Kila kwenye msafara wa mamba na kenge wamo
Uongozi unamwakikishia Mr Christopher Lukosi kwamba mamba wote wa CHADEMA UK kwa kushirikiana na wote wenye kuelewa mageuzi ya kweli
, tutaliondoa tatizo ifikapo 2015. Tunamtakia kila la kheli katika maisha na ni imani yetu tutaendelea kuwa ndugu yake baada ya tatizo kutatuliwa !!!!.

“We fail in most of our endeavours because we too often underestimate People’s Power” [M4C UK, 2012]

Madktari Wanafunzi 300 Kutoka Nchi Mbalimbali Kukutana Arusha Wiki Ijayo

ZAIDI ya wanafunzi 300 wa udaktari kutoka nchi mbalimbali duniani wanatarajiwa kufanya mkutano wa kimataifa utakaojadili jinsi ya kutatua migogoro katika sekta ya Afya kwenye ukanda wa Afrika.

 Hayo yalisemwa na Rais wa Chama cha Wanafunzi wa Udaktari Tanzania(TAMSA)  Francis Tegete wakati akizungumza na waandiishi wa habari jana jijini Dar es salaam.

 Alisema kuwa washiriki wa mkutano huo watajadiliana jinsi ya kuboresha rasilimali watu ,sera za afya na  miundo mbinu ya kutolea huduma ya afya katika nchi zao ili kutimiza malengo ya Melinia .

 Alisema kauli mbiu ya mkutano huo inalenga kujadili migogoro ya afya barani na jinsi ya kuitatua kwa ajili ya kutoa huduma bora kwa wananchi hasa wanaoishi katika mazingira magumu na vijijini.

 Tegete aliongeza kuwa mkutano huo utakuwa muhimu kwa wanafunzi wa udaktari nchini kupata fursa ya kubadilishana uzoefu na wenzao wa jinsi gani wanavyoweza kusaidia katika utoaji wa huduma za afya ikiwemo upunguzaji wa vifo vya watoto na mama wajawazito.

 Alisema kuwa mkutano huo utafunguliwa na Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dkt Hussein Mwinyi siku ya Jumanne tarehe 18 na kumalizika 22 Disemba  mwaka huu  jijini Arusha.

 Baadhi ya washiriki wanatoka Marekani , Uingereza, Lebanon, Sierra Leone , Uganda, Kenya , Rwanda, Burundi, Congo, Korea Kusini, Sudan, Zambia , Ethiopia na Sweden .

Na: Heka Wanna na Shakila Galus-MAELEZO_DAR ES SALAAM    

Ikulu Ilivyowakera Wahariri

•  Wasota kwa saa nne kusubiri mkutano wao na Kikwete

WAHARIRI wa vyombo mbalimbali vya habari nchini, wamelazimika kusota kwa zaidi ya saa nne Ikulu, kusubiri mkutano wao na Rais Jakaya Kikwete.
Hali hiyo ilitokea jana wakati wahariri wakisubiri mkutano wao na Rais Jakaya Kikwete na mgeni wake, Rais Marc Ravalomanana, aliyeondolewa madarakani kwa nguvu nchini Madagascar.

Katika mkutano huo wa dharula ulioitishwa na Rais Kikwete mwenyewe, ulikuwa na lengo la kuzungumzia msimamo wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC ) kuhusu mgogoro wa Madagascar na kutoa fursa kwa Rais Ravalomanana anayeishi uhamishoni nchini Afrika Kusini, kueleza msimamo wake.
Wakati Rais Kikwete akiwa ziarani jijini Dar es Salaam, Ikulu iliwasiliana na wahariri wa vyombo vya habari na kuwataka wafike Ikulu saa sita kwani Rais Kikwete alitaka kufanya mkutano wa dharula na wakuu hao wa vyombo vya habari saa saba.

Wahariri hao walianza kuitikia wito wa kufika Ikulu kuanzia saa sita tayari kwa mkutano huo ambao kwa mujibu wa mawasiliano na Ikulu, ulipangwa kufanyika saa saba baada ya Rais Kikwete kukatisha ziara yake na kisha kuendelea nayo baadaye jioni.

Ilipofika saa saba, hakukuwa na dalili zozote za Rais Kikwete na mgeni wake kufika ukumbini na hakuna taarifa zozote zilizotolewa na watendaji wa Ikulu.
Wanahabari hao waliendelea kusubiri na ilipofika majira ya saa nane mchana, bado hakukuwa na taarifa za muda halisi wa kuanza kwa mkutano huo.

Ilipofika saa tisa, mmoja wa maafisa wa Ikulu, aliwaambia waandishi wa habari hao kwamba mkutano huo ungelianza saa 9.30 na kwamba tayari Rais Kikwete alikuwa amesharejea Ikulu na kujiandaa kukutana nao.

Hata ilipofika saa 9.30, hakukuwa na dalili za kuanza mkutano huo, hali iliyowafanya baadhi ya wahariri kukaa vikundi kuzungumzia adha hiyo, huku wengine wakichapa usingizi.

Rais Ravalomanana aliwasili viwanja vya Ikulu majira ya saa 9.45 na kwenda kukutana na Rais Kikwete kabla ya kuingia ukumbini kuanza mkutano huo.
Majira ya saa 10 jioni, maafisa wa Ikulu na watu wa usalama, walijipanga kujiandaa kuwakaribisha viongozi hao ukumbini, lakini baadaye walirejea kwenye nafasi zao za awali baada ya kuambiwa kwamba ungeaanza saa 10.30 jioni.
Hatimaye ilipofika saa 10.28, Rais Kikwete na mgeni wake waliingia ukumbini na kuanza mkutano huo uliodumu kwa takriban dakika 30.

Wakati mkutano huo unamalizika majira ya saa 11 jioni, Mkurgenzi wa Mawasilino Ikulu, Salva Rweyemamu, aliwashukuru wahariri kwa uvumilivu wao, lakini hakueleza sababu za mkutano huo kuchelewa kuanza saa saba kama ilivyopangwa na badala yake ulianza saa 10.30 jioni.

Uchunguzi wa gazeti hili ulibaini kuwa hakukuwa na mawasiliano sahihi kati ya watendaji wa Ikulu na vyombo vya habari na kusababisha kero hiyo.
Hata hivyo akizungumza katika mkutano huo, Rais Kikwete alisema katika mkutano wa wakuu wa nchi za SADC uliomalizika hivi karibuni jijini Dar es Salaam, umeazimia kuwa Rais Ravalomanana arejee Madagascar bila masharti na kuhakikisha ulinzi na usalama wake.

Alisisitiza kuwa SADC imesisitiza Ravalomanana arejee nchini mwake na kupuuza tishio la wapinzani wake la kumtaka arejee nchini humo baada ya uchaguzi.
Pia alisema wamekubaliana kwamba Rais Ravalomanana na hasimu wake anayeongoza Madagascar kwa sasa, Rais Andry Rajoelina wasigombee urais katika uchaguzi mkuu ujao, unaotarajiwa kufanyika Mei mwakani.

“Ili kudumisha amani nchini Madagascar, viongozi wa SADC wamekubaliana kuwa Rais Rajoelina na Rais Ravalomanana wasigombee urais,” alisema Rais Kikwete.
Kwa upande wake, Ravalomanana alikubali kurejea nchini humo na kuwa raia wa kawaida na kuahidi kutoa ushirikiano katika kuijenga upya Madagascar iliyoathirika kwa kiasi kikubwa kiuchumi.

Alisema pia amekubali kutogombea urais Mei mwakani, lakini anaweza kugombea miaka mitano baadaye kama hali itaruhusu.

Rais Kikwete ambaye ni mwenyekiti wa SADC, alimshukuru Ravalomanana kukubaliana na viongozi wa SADC na kuahidi kuzungumza na Rais Rajoelina.

http://www.freemedia.co.tz/daima/habari.php?id=43437