Friday, August 10, 2012

TAFF YATOA TAMKO JUU YA MAHARAMIA WA FILAMU

SHIRIKISHO la Filamu nchini(TAFF) kwa kushirikiana na Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA) pamoja Kampuni za usambazaji wa filamu na kazi za wasanii ‘wameapa’ kupambana na maharamia wote wa kazi hizo ili kulinda maslahi ya wasanii.

Wakizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Jijini Dar es salaam jana, umoja huo kwa pamoja ulisema umefika wakati tatizo la wizi wa kazi za wasanii lishughulikiwe kikamilifu ili kuzima mianya yote ambayo ni kero kwa muda mrefu.

Rais wa Shirikisho hilo Simon Mwakifwamba, mbali na mikakati hiyo pia aliiomba Serikali kutekeleza ahadi yake ya kuwasaidia wasanii kwa kupambana na maharamia hao aliodai kuwa wapo kila pembe ya nchi hii huku wakijiamini kwa kuendelea na kazi hiyo.

“Umefika wakati kwa Serikali kusikia kilio hiki cha wasanii na kuweka mbinu kali zitakazosaidia kuokoa maisha ya wasanii wanaoendelea kuwa masikini kila kukicha kutokana na uwepo wa watu wachache wanaoiba kazi zao”
“Tuna imani kuwa kama kazi za wasanii zitasimamiwa vizuri, tutaweza kuongeza pato la Taifa kwa kiwango kikubwa ikizingatiwa kuwa sanaa hii kwa sasa hapa nchini imeonyesha mafanikio isipokuwa kuna watu wachache ndiyo wananufaika nayo” alisema Mwakifwamba.

Naye Mwenyekiti wa Bongomuvi Jacobo Steven ‘JB’ alisema sanaa inaweza kuwa na nafasi ya tatu kwa kuchangia pato la Taifa ukiacha pato linalochangiwa na sekta za madini maliasili pamoja na utalii.

Alisema Serikali inapswa kuonyesha makali yake kwa kuwakamata wahusika wote wa wizi wa kazi hizo ili kuendeleza nguvu za wasanii wa hapa nchini walioamua kujitoa mughanga kufanya kazi zao.

Kwa upande wake Meneja usimamizi kutoka TRA Msafiri Ndimbo alisema Mamlaka hiyo imejipanga kudhibiti wizi wa kazi hizo kuanzia Januari Mwakani hasa baada ya Serikali kupitia Bunge lake kukubaliana kuweka mikakati ya kupamba na suala hilo.

Ambapo wasanii na wasambazaji wa kazi zao wameungana pamoja kwa ajili ya kuhakikisha kazi zao zinakwenda kwa haki ili wasanii na kazi zao

Tume ya Huduma za Bunge la Malawi yakutana na Spika wa Bunge la Tanzania mjini Dodoma

 Spika wa Bunge la Tanzania Mhe. Anne Makinda (kushoto) na Naibu Spika Mhe. Job Ndugai (Mb) kwa pamoja wakiwa na mazungumzo ya kina leo na ujumbe wa Tume ya Huduma za Bunge la Malawi ulioko nchini hivi sasa, ambapo pamoja na mambo mengine walizungumzia uhusiano mzuri wa mabunge ya nchi mbili hizi. Kushoto kwa Mhe. Ndugai ni Naibu Spika wa Bunge la Malawi Mhe.Juliana Mpande (Mb) ambaye ni mkuu wa msafara. Wengine ni Kamishna  Alfred Mwechumu (Mb) na Kamishna Christina Chiwowo (Mb).
Spika wa Bunge la Tanzania akiwa na mazungumzo na Uongozi wa Serikali ya Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam waliofika ofisini kwake Dodoma leo. Spika Makinda amewataka na kuwaasa kuwa na uzalendo kwa nchi yao.

Picha na Prosper Minja - Bunge

CHAMA CHA WALIMU CWT CHATOA TAMKO LAKE KWA SERIKALI


 Rais wa Chama Cha walimu Tanzania Bw. Gratian Mukoba (Kushoto) akiongea na waandishi wa habari leo katika makao makuu ya Chama hicho jijini Dar es Salaam kuhusiana na Tamko lao  kwa serikali kutaka iwarudishie madaraka wakuu wote waliovuliwa nyadhifa zao kwakuwa ni viongozi wa (CWT) ndio waliohamasisha mgomo.

Vilevile chama hicho kimeitaka serikali  kufuta nia yake ya kuwashitaki walimu zaidi ya 180,000 walioshiriki mgomo kati ya walimu 233,440 walioko nchini kwani kwa kufanya hivyo watoto wa maskini wanaotegemea walimu hao kufundisha watakosa haki yao ya kufundishwa.Kulia na Kaimu katibu mkuu wa chama hicho Bw, Ezekiel Olotu.

(PICHA NA PHILEMON SOLOMON WA FULLSHANGWE)

Hali ya uuzaji wa madawa ya binadamu kiholela jijini Dar Es Salaam inatisha

Matokeo haya yametokana na utafuti ulifanywa na YITA Novemba 2011 na ulihusisha watafitit waliofanya ziara siri (mystery shoppers) 126 katika maduka 64 ya wilaya zote tatu za Dar es salaam. Jina la muhtasari wenye matokeo hayo ni “Ununuzi wa dawa jijini Dar es Salaam-Je, maduka ya dawa yanazingatia kanuni?” . Pamoja na mengine watafiti waliweza kuhoji yafuatayo;

    Je, dawa zinaweza kutufanya wagonjwa? Je, zinatolewa ipasavyo? Na je, mfumo wa kuwalinda wananchi kutokana na madhara ya matumizi mabaya ya dawa unafanya kazi vizuri?

    Ikumbukwe mamlaka ya dawa na chakula Tanzania imetamka wazi kwenye  Kifungu cha 31:3 ya viwango vya biashara ya dawa nchini ya mwaka 2006 (Pharmaceutical Business Standards Regulations) kuwa;

    “Hakuna mtoaji dawa yeyote atakayetoa dawa ambazo matumizi yake yanapaswa kuwa kwa maagizo ya daktari tu isipokuwa kwa agizo la matumizi ya dawa husika lililotolewa na mfanyakazi wa afya, mganga wa meno au wa mifugo au mtu mwingine yeyote aliyeidhinishwa kuagiza matumizi ya dawa”.

    Utaafiti imedhihirisha ukiukwaji mkubwa wa kanuni za Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA).Ni wazi madhara yafuatayo yataliandama Taifa kama hatua za dhati hazitachukuliwa haraka;

WENGI WAZIDI KUNUFAIKA NA PROMOSHENI YA "JENGA MAISHA YAKO NA NMB"


 Meneja wa Benki ya NMB, Kanda ya Dar es Salaam, Salie Mlay (kushoto) akibofya kwenye kompyuta kuwapata washindi wa promosheni ya 'Jenga Maisha Yako na NMB' katika droo iliyofanyika, Dar es Salaam jana, ambapo baadhi ya washindi watazawadia mabati, saruji, ada ya shule, mteja kuongezewa amana maradufu na zawadi nyingine lukuki. Wanaoshuhudia ni Mratibu wa Miradi wa Selcom Wireless, Everline Simpilu (kulia) na Sadiki Elimsu ambaye ni Mkaguzi Mwandamizi wa Bodi ya Kusimamia Michezo ya Kubahatisha (GBT)
 Meneja wa Benki ya NMB, Kanda ya Dar es Salaam, Salie Mlay (kushoto) akibofya kwenye kompyuta kuwapata washindi wa promosheni ya 'Jenga Maisha Yako na NMB' katika droo iliyofanyika, Dar es Salaam leo.

Meneja wa Benki ya NMB, Kanda ya Dar es Salaam, Salie Mlay (kushoto) akibofya kwenye kompyuta kuwapata washindi wa promosheni ya 'Jenga Maisha Yako na NMB' katika droo iliyofanyika, Dar es Salaam jana, ambapo baadhi ya washindi watazawadia mabati, saruji ada ya shule, mteja kuongezewa amana maradufu na zawadi nyingine lukuki. Wanaoshuhudia ni Mratibu wa Miradi wa Selcom Wireless, Everline Simpilu

 PICHA ZOTE NA KAMANDA MWAIKENDA

"Hujafa Hujaumbika" Duniani matezo na raha zote za wanadamu aliyeguswa toa kwa moyo leo kwake kesho kwetu Naamini watanzania tunaweza na moyo tunao...

Beatrice Shimende Kantimbo (48) anaomba msaada wa pesa kwa ajiri ya matibabu ya maradhi ambayo vipimo vya kitabibu vimegundua kuwa ni matende (elephantiasis), ili kufanikisha safari yake kwenda India kwa matibabu.

Kantimbo anasumbuliwa na maradhi hayo kwa takribani miaka 12, kwahivi sasa yamemtoa kwenye mstari wa maisha yake ya kujitegemea na kumfanya awe tegemezi kwa watoto wake na mumewe ambao hata hivyo kipato chao si cha uhakika.

Kabla ya hapo alikuwa ni mama 'mchakarikaji' kweli, aliendesha maisha yake kwa biashara kadhaa ikiwemo biashara ya duka, grosari na saluni ya ususi wa nywele ambapo yeye mwenywe ni msusi mzuri wa nywele na kwa ucheshi wake na kujiamini pia alikuwa akifanya kazi za ushereheshaji (MC) kwenye sherehe kadhaa akifahamika kama MC Kimbaumbau.

Ila kwa sasa, tofauti na hapo awali alipoitwa MC na mama mchakariji, Kantimbo hawezi kufanya lolote amebakia ni mama wa kukaa mahali pamoja tu kuanzia asubuhi hadi jioni.

Kwa uchungu anasimulia namna alivyoanza kuugua…"Nakumbuka mwaka 1998 nikiwa kwenye biashara zangu pale Ubungo, kuna kitu kilinichoma hapa (anaonyesh pajani) maumivu yake yalikuwa mithiri ya sindano, hata hivyo hayakudumu sana wala hapakuwa na alama yoyote.

"Baada ya dakika chache nikajihisi homa kali. nikaanza kutetemeka mwili mzima, nikaamua kwenda hospitali ya Neema, hospili ya karibu na mahali nilipokuwa nikiishi pale Ubungo. Daktari akanipima, akagundua nilikuwa na malaria.

"Wakati huo mguu haukuonyesha dalili zozote za maumivu wala jeraha. Malaria ilkuwa kali, nikalazwa kwa muda wa wiki mbili pale hospitali. Nikaruhusiwa, nikarudi nyumbani na hapo ndipo nilipoanza kuona mguu unavimba. Kaadri siku zilivyozidi kwenda ndivyo mguu nau unavimba"


Kuanzia mwaka 2010 mguu umezidi kuongezeka  kuvimba na maumivu makali yaliyotokana na kidonda kikubwa kilichosababishwa na kuondolewa kwa sehemu ya nyama ya mguu wake wa kuume iliyokuwa imeoza. Anasema:

"Baadhi ya madaktari wa Muhimbili walinishauri nikubali kukatwa mguu. Wanasema ya nyama imeoza na mfupa wa mguu umeharibika. Mimi sikukukubaliana na ushauri wao kwa sababu baada ya kupigwa X-ray 2007 iligunduliwa tatizo kubwa lilikuwa matatizo kwenye mishipa ya kupitisha maji kutokana na nyama kuharibika. Sio mfupa.

"Nilikataa kwa imani kuwa nitapona tu. Nikijiangalia nina uwezo wa kusimama na kutembea isipokuwa tu kinachonipa taabu kwa sasa ni nyama za mguu zimekua sana kiasi kwamba nikitembea zinagusa mguu wa kushoto" alisema.

Kwa mawasiliano namna ya kumsaidia piga simu namba 0716 850350, 0784 861031.

RAIS JAKAYA KIKWETE AWASILI ACCRA KUSHIRIKI MAZISHI YA RAIS WA GHANA JOHN EVANS ATTA MILLS


Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwasili jana Agosti 9, 2012 katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Kotoko jijini Accra, Ghana, kuhudhuria mazishi ya aliyekuwa rais wa nchi hiyo Marehemu John Evans Atta Mills anayetarajiwa kuzikwa leo Ijumaa Agosti 10, 2012.


PICHA NA IKULU

Mkazi wa Silent Inn afariki baada ya kugongwa na gari.

MKAZI mmoja wa eneo la Silent Inn aliyefahamika kwa jina la Bakari Sefu (35) amekufa baada ya kugongwa na gari .

Kamanda wa polisi mkoani hapa, Liberatus Sabas alisema kuwa tukio hilo limetokea wiki iliyopita  katika eneo la stand ndogo karibu na cafe la Aziz .

Alisema kuwa, chanzo cha ajali hiyo ni gari aina ya Nissan Caravan lenye namba za usajili T 278 BXD lililokuwa linaendeshwa na dereva ambaye bado hajafahamika jina lake baada ya dereva huyo kuondoa gari hilo kwa kasi.

Alisema kuwa, dereva huyo aliondoa gari hilo lililokuwa limeegeshwa likisubiri abiria ndipo lilipomgonga kondakta huyo ambaye alikuwa amesimama mbele ya gari hilo akiita abiria.

Sabas aliongeza kuwa, baada ya kusababisha ajali hiyo dereva huyo alikimbia na jeshi la polisi linaendelea kumsaka dereva huyo , huku mwili wa marehemu ukiwa umehifadhiwa katika hospitali ya mkoa ya Mount Meru.

NGORONGORO HEROES YAWASILI NCHINI NIGERIA


Ngorongoro Heroes, timu ya Taifa ya vijana wenye umri chini ya miaka 20 imewasili asubuhi hii (Agosti 10 mwaka huu) kwa ndege ya Overland Airways kwenye mji wa Ilorin, Jimbo la Kwara lililo Kusini mwa Nigeria tayari kwa mechi ya marudiano dhidi ya wenyeji Flying Eagles itakayochezwa Jumapili.

Mechi hiyo ya raundi ya pili ya michuano ya U20 ya Afrika itachezwa kwenye Uwanja wa Township kuanzia saa 10 kamili jioni kwa saa hapa ambapo Tanzania itakuwa ni saa 12 kamili jioni. Ngorongoro Heroes ilitua jana (Agosti 9 mwaka huu) jijini Lagos ambapo ililala kabla ya kuja hapa.

Msafara wa Ngorongoro Heroes wenye watu 27 ukiongozwa na mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Mtwara (MTWAREFA) ulipokea na Ofisa Ubalozi wa Tanzania nchini Nigeria, Jones Mndeme na viongozi wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Nigeria (NFF) umefikia hoteli ya Kingstone Grand Suites.

Kwa mujibu wa Kocha wa Ngorongoro Heroes, Jakob Michelsen, timu itafanya mazoezi leo jioni (Agosti 10 mwaka huu) wakati mazoezi ya mwisho yatakuwa kesho jioni (Agosti 11 mwaka huu) kwenye uwanja ambao utatumika kwa mechi ya Jumapili.

WAKAZI WA KIBAMBA WAKIMBIA NYUMBA ZAO

WAKAZI wa Kibamba, Kinondoni, Dar es Salaam, usiku wa kuamkia leo, wamezikimbia nyumba zao baada ya kutokea kishindo kikubwa cha milipuko katika Kambi ya Jeshi la Vifaru ilyoko Mloganzila,Kisarawe, Pwani.

Tukio hilo limetokea kati ya saa tano na 7:04 usiku ambapo milipuko hiyo ilikuwa mitano, ikiambatana na kukatika kwa umeme, mawasiliano ya simu pia kukiwa na mvua kubwa.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti na Fullshangweblog, wakazi hao walisema tukio hilo limewashtua kwasababu halijawahi kutokea katika miaka zaidi ya saba walioshi kwenye neo hilo.

Walisema waliamua kukimbia na kuelekea kusikojulikana kwa ajili ya kuokoa maisha yao.

Mmoja wa wakazi hao Mhando Yahaya alisema Wakazi wote wa Kibamba walikimbilia kwenye kijiji kidogo cha Kibwegele ambapo waliamua kuacha nyumba pamoja na mali zao bila kujali.

“Ujuwe serikali inabidi itowe angalizo kabla na siyo kufanya siri kwa kuwa matokeo ya siri ndiyo kama haya wananchi tunatishika na kukimbia hovyo usiku huu, mvua na giza vikituandama ”alisema Yahaya.

Naye Egnes Habiyu, alisema milipuko kama hiyo, imesababisha baadhi ya wagonjwa wa moyo kushtuka hadi kufikia hatua ya kuishiwa nguvu na kuanguka kwenye maji ya mvua ilyokuwa ikinyesha.

Alipotakiwa kutoa ufafanuzi kuhusu tukio hilo, Msemaji wa Jeshi hilo, Kanali, Kapambala Mgawe alisema hayo yalikuwa mazoezi ya kawaida na hayana uhusiano wowote wa kivita.

Vilevile aliwatoa wasiwasi wananchi kuwa milipuko hiyo haina madhara bali ni moja ya mazoezi ya kawaida hivyo wawewatulivu.

Kanali, Mgawe alisema taarifa zilitolewa kwa wakazi wanaoishi jirani na kambi hiyo, bali kwakuwa yalifanyika usiku kukiwa kumetulia kumesababisha sauti ya milipuko hiyo kusikika mbali.

Magazeti ya Leo Ijumaa 10th August 2012

Mwenge Wa Uhuru Waingia Arusha Jana

 waongoza mwenge wakielekea ndani ya viwanja vya chuo cha ufundi cha Arusha.



Picha kwa hisani ya http://www.wazalendo25.blogspot.com

JK: Awaapisha Watendaji Wakuu Wa Mahakama Ikulu Jijini Dar Jana

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dk. Jakaya Mrisho Kikwete akimuapisha Mhe.Hussein Kattanga kuwa Mtendaji Mkuu wa Mahakama, kabla ya uteuzi wake,Mhe. Kattanga alikuwa Katibu Mkuu TAMISEMI.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
 Mhe.Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akimuapisha, Mhe. Ignas Paul Kitusi kuwa Msajili Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, kabla ya uteuzi wake Mhe. Kitusi alikuwa Msajili wa Mahakama Kuu.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
 Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akimuapisha Mhe. Panterine Kente kuwa Msajili wa Mahakama ya Rufani. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.  
Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na Watendaji Wakuu wapya wa Mahakama ya Tanzania, mara baada ya kuwaapisha Ikulu jijini Dar es Salaam, kutoka kushoto ni Katibu Mkuu Kiongozi, Mhe. Ombeni Sefue, Mhe. Hussein Kattanga, Mtendaji Mkuu wa Mahakama, Mhe. Ignas Paul Kitusi, Msajili Mkuu wa Mahakama na Mhe. Panterine Kente, Msajili wa Makahama ya Rufani.
                                 
 Picha na Ikulu.