Saturday, September 29, 2012

SIMBA vs TANZANIA PRISONS Mechi Inaendelea Jion Hii

Timu za Simba na Tanzania Prisons zinapambana jioni hii Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kuanzia saa 11 kamili jioni. Tayari makocha wa timu zote mbili Jumanne Charles (Tanzania Prisons) na Circo Milovan (Simba) wameshataja vikosi vyao.

Simba:  VS    Tanzania Prisons:
01.Juma Kaseja (c)                        18.David Abdallah
02.Nassoro Masoud                         03.Aziz Sibo
17.Amir Maftah                            05.Laurian Mpalile
15.Shomari Kapombe                        16 .Lugano Mwangama (c)
24.Juma Nyoso                             15.David Mwantika 
14.Mwinyi Kazimoto                        13.Khalid Fupi
28.Amri Kiemba                            07.Misango Magai
08.Ramadhan Chombo                        12.Fred Chudu
19.Edward Christopher                     14.Elias Maguri
10.Felix Sunzu                            17.Peter Michael
16.Mrisho Ngasa                           19.John Matei

Wachezaji wa akiba;
22.Wilbert Mweta                          01.Daudi Mwasongwe
23.Paul Ngalema                           04.Jumanne Elfadhili
20.Jonas Mkude                            09.Sino Augustino
12.Salim Kinje                            22.Julius Kwaga
04.Komanbil Keita                         08.Henry Mwalugala
13.Daniel Akuffor                         11.Hamisi Ally
05.Pascal Ochieng                         23.Jeremiah Juma

Refa: Paul Soleji (Mwanza)
Mwamuzi Msaidizi 1: Jesse Erasmo (Morogoro)
Mwamuzi Msaidizi 2: Mwarabu Mumba (Morogoro)
Mwamuzi wa Akiba: Israel Nkongo (Dar es Sala

RAIS KIKWETE AONANA NA UJUMBE WA MWAPORC IKULU, DAR ES SALAAM, LEO

 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na ujumbe toka kampuni ya Mwambani Port and Railway Corridor Company (MWAPORC) uliomtembelea leo Septemba 29, 2012 Ikulu jijini Dar es salaam kumweleza nia yao ya kutaka kuwekeza katika sekta ya reli.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiuonesha njia za reli katika  ramani ya Tanzania ujumbe toka kampuni ya Mwambani Port and Railway Corridor Company (MWAPORC) uliomtembelea leo Septemba 29, 2012 Ikulu jijini Dar es salaam kumweleza nia yao ya kutaka kuwekeza katika sekta ya reli.

PICHA NA IKULU

KIINGILIO MECHI YA YANGA, SIMBA SH. 5,000, LINE UPS ZA VIKOSI SIMBA NA PRISON

Kiingilio cha chini kwenye mechi ya Yanga (anae kipiga kiungo wa Rwanda Haruna Niyonzima) na Simba (anae chezea kiungo wa Tanzania Mwinyi Kazimoto) itakayochezwa Jumatatu (Oktoba 3 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kitakuwa sh. 5,000 kwa viti vya rangi ya kijani ambavyo ni 19,648 kwenye uwanja huo wenye uwezo wa kuchukua watazamaji 60,000.

Mechi hiyo namba 80 ya Ligi Kuu ya Vodacom itachezwa kwenye uwanja huo kuanzia saa 11 kamili jioni.

Watazamaji watakaotaka kuona mechi hiyo wakiwa wameketi kwenye viti vya rangi ya bluu ambavyo ni 17,045 watalipa sh. 7,000 kwa tiketi moja.

Viingilio vingine kwenye mechi hiyo ni sh. 10,000 kwa viti vya rangi ya chungwa ambavyo viko 11,897 wakati VIP C inayochukua watazamaji 4,060 itakuwa sh. 15,000.

Kwa upande wa VIP B tiketi ni sh. 20,000 na VIP A yenye watazamaji 748 tu kiingilio kitakuwa sh. 30,000.

SIMBA vs TANZANIA PRISONS LINE UPS
Timu za Simba na Tanzania Prisons zinapambana jioni hii Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kuanzia saa 11 kamili jioni. Tayari makocha wa timu zote mbili Jumanne Charles (Tanzania Prisons) na Circo Milovan (Simba) wameshataja vikosi vyao.

Simba:                                        Tanzania Prisons:
01.Juma Kaseja (c)                            18.David Abdallah
02.Nassoro Masoud                             03.Aziz Sibo
17.Amir Maftah                                05.Laurian Mpalile
15.Shomari Kapombe                            16.Lugano Mwangama (c)
24.Juma Nyoso                                 15.David Mwantika
14.Mwinyi Kazimoto                            13.Khalid Fupi
28.Amri Kiemba                                07.Misango Magai
08.Ramadhan Chombo                            12.Fred Chudu
19.Edward Christopher                         14.Elias Maguri
10.Felix Sunzu                                17.Peter Michael
16.Mrisho Ngasa                               19.John Matei

Wachezaji wa akiba;
22.Wilbert Mweta                              01.Daudi Mwasongwe
23.Paul Ngalema                               04.Jumanne Elfadhili
20.Jonas Mkude                                09.Sino Augustino
12.Salim Kinje                                22.Julius Kwaga
04.Komanbil Keita                             08.Henry Mwalugala
13.Daniel Akuffor                             11.Hamisi Ally
05.Pascal Ochieng                             23.Jeremiah Juma

Refa: Paul Soleji (Mwanza)
Mwamuzi Msaidizi 1: Jesse Erasmo (Morogoro)
Mwamuzi Msaidizi 2: Mwarabu Mumba (Morogoro)

Mwamuzi wa Akiba: Israel Nkongo (Dar es Salaam

ERMIE ATAMBULISHWA KUWA KOCHA WA YANGA

                                                Kocha Mpya wa Yanga katika utambulisho

Hatimaye leo hii klabu bingwa ya Afrika mashariki na kati Dar Young Africans imemtambulisha rasmi kocha wake mpya Mholanzi Ernie Brandts.

Kocha huyu ambaye miezi michache iliyopita alikuwa mwalimu wa klabu bingwa ya Rwanda, APR aliwasili jijini Dar es Salaam jana usiku na leo asubuhi ametambulishwa rasmi kwa waandishi wa habari na kusaini mkataba wa mwaka mmoja wa kuifundisha klabu hiyo ya Jangwani.

Brandts ambaye amewahi kuwa mchezaji wa timu ya taifa ya Uholanzi na klabu kubwa ya nchi hiyo PSV Eindhoven akicheza kwenye nafasi ya ulinzi, amekuja Yanga kuchukua nafasi ya mbelgiji Tom Saintfiest aliyetimuliwa wiki iliyopita baada ya kukaa kwenye klabu hiyo kwa siku 81.

SOURCE: Shaffihdauda.com

MAONYESHO YA SARAKASI YA MAMA AFRIKA YAENDELEA KURINDIMA NEW WORLD CINEMA DAR

                         "Karibuni watanzania wote muone sarakasi na utamaduni wa kitanzania".
 Trade Marketing Supervisor wa kampuni ya simu za mkononi ya TIGO ambao ndio wadhamini wakuu wa maonyesho ya 'Sarakasi ya Mama Afrika' yanayoendelea katika viwanja vya New World Cinema Bw. Christopher Mmbando akiwakaribisha wageni waliohudhudhuria onyesho hilo. kushoto ni Afisa Mahusiano wa TIGO.
 




 

 Pichani Juu na Chini ni mfululizo wa maonyesho ya sarakasi ya 'Mama Africa Circus'.

Picha Juu na Chini ni baadhi ya wadau walioshiriki maonyesho hayo wakifurahia.

Magazeti ya Leo Jumamosi 29th September 2012