Friday, April 5, 2013

Magazetini leo Ijumaa ya 5th April 2013



PICHA ZA MAZISHI YA NYAGA PAUL MAWALLA JIJINI NAIROBI

Mwili wa marehemu Nyaga Paul Mawalla ukiwa katika kanisa la Kilutheri nchini Kenya usharika wa Uhuru Highway kwa ajili ya misa

Mazishi ya Marehemu Nyaga Mawalla, aliyekuwa Mwasisi na Mkurugenzi wa Makampuni ya Mawalla ya Jijini Arusha yamefanyika jana jijini Nairobi Kenya katia Makaburi ya Jumuia ya Langata.

Mapema kabla ya Mazishi hayo yaliyohudhuriwa na Viongozi mbalimbali wa Serikali na familia na marafiki ilifanyika Misa ya kumuombea Marehemu katika Kanisa la KKKK, Uhuru Highway.

Miongoni mwa Viongozi waliohudhuria Mazishi hayo ni Balozi wa Tanzania nchini Kenya, Dk. Batilda Burian, Viongozi wastaafu, Sir. George Kahama, Mwemyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, Wabunge, Mawaziri wanasheria mabalimbali wa ndani na nje ya Tanzania.

Marehemu Nyaga Paul Mawalla alifariki Machi 22, 2013 jijini Nairobi alikokuwaa amelazwa kwa matibabu  Hospitali ya Nairobi.

 Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe,Naibu Waziri wa Utalii na Maliasili Lazaro Nyarandu na Sir George kahama wakiwa kanisani wakishiriki misa ya maziko ya marehemu Nyaga Mawalla.

Picha Zaidi Chini

MTUHUMIWA WA MAUAJI YA PADRI MUSHI AFUTIWA MASHITAKA...DPP -ZANZIBAR ADAI KUWA HANA KOSA

Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) Zanzibar, Ibrahim Mzee Ibrahim, ametupilia mbali uchunguzi wa mauaji ya Padri Evarist Mushi uliofanywa na Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na Maafisa wa Shirika la Upelelezi la Marekani (FBI) na kusema mtuhumiwa hana kesi ya kujibu mahakamani.

Padri Mushi ambaye alikuwa Paroko wa Kanisa Katoliki Minara Miwili aliuawa kwa kupigwa risasi Febuari 17, mwaka huu katika eneo la Beitrasi mjini hapa akiwa ndani ya gari alipokuwa akielekea kuongoza misa ya Jumapili katika Kanisa la Mtakatifu Theresia, mjini Zanzibar.

Baada ya mauaji hayo, Rais Jakaya Kikwete alitoa kibali cha kukaribisha maafisa wa FBI kushirikiana na Jeshi la Polisi kufanya uchunguzi wa mauaji hayo na Machi 17, mwaka huu Jeshi la Polisi lilimkamata Omar Mussa Makame kwa tuhuma za kuhusika na mauaji hayo.

WEMA SEPETU AZIDI KUMPA SHAVU KAJALA MASANJA......



 Muigizaji na Miss Tanzania wa zamani Wema Sepetu amesema licha ya kumsainisha Kajala Masanja kwenye kampuni yake, hategemei kumfanyisha kazi kurudisha shilingi milioni 13 alizomtolea kwenye hukumu yake.

Akiongea kwenye kipindi cha XXL, Wema amesema Kajala atakuwa akifanya kazi zake lakini atakuwa akimlipa kama kawaida. Kwa kuanza Kajala ataigiza kama mhusika mkuu kwenye filamu iitwayo Princess Sasha.
 “Tutaenda kuishoot nje ya Dar, ninataka kuishoot mandhari fulani hivi kama ya kijijini. Ni mtoto wa mfalme, Kajala ndo atakuwa Princess Sasha, she is going to be the main character, “ alisema Wema.
Kajla
 
Kwa upande wake Kajala amesema aliamua kujichora tattoo ya jina la Wema kwasababu anamchukulia kama shujaa.

“Mi naweza kusema nimeichora kuonesha nimeappreciate vipi kitu alichonifanyia , watu wengine wanaichukulia vibaya, wataongea vibaya, lakini mimi najua moyoni mwangu. Sababu nimeona siwezi kumlipa hiyo hela sasa hivi.

Ntamkumbuka siku zote hata chochote kikitokea atabakia kuwa mtu… yaani she is my hero.”