Monday, December 17, 2012

Magazeti ya leo Jumatatu 17th December 2012

Ndege ya Tanapa yaanguka




Ndege ya shirika la hifadhi la taifa (TANAPA) aina ya C182 ikiwa imeanguka katika eneo la nsemulwa mjini Mpanda muda mfupi baada ya kuondoka katika uwanja wa ndege wa Mpanda ikiwa inaendeshwa na rubani Adam kajwa alieumia sehemu ya uso.

Ajali imetokea jioni wakati ndege hiyo ikielekea hifadhi ya taifa ya katavi wilayani mlele mkoa wa katavi ambapo meneja wa uwanja wa ndege wa Mpanda  Mahamud Muhamed  kasema ajali ilitokea jana december 16 2012 saa kumi na dakika 55 jioni.

Ni ndege ya abiria mali ya hifadhi ya taifa ya  TANAPA na una uwezo wa kuchukua abiria wanne na imeanguka umbali wa kilometa moja na nusu kutoka uwanja wa ndege.

Meneja wa uwanja  huo wa ndege  alisema  taarifa za awali   zinaonyesha  chanzo  cha ajali ni injini ya ndege kufeli wakati ikiwa angani.
Rubani wa ndege hiyo alipata msaada kutoka kwa wananchi waliokuwa  shamani mwao ambapo mmoja wao alisema wakati akiwa anafanya shughuli  zake  za kilimo ghafla aliona ndege angani  ikizimika injini na muda mfupi baadae ikaanguka jirani na mti wa mwembe, kazi ya uokoaji ilichukua muda kidogo kutokana na nyuki.
(Taarifa imeandikwa na http://kataviyetu.blogspot.com)

Filikunjombe Anena Mbele Ya Mangula

Viongozi   wa CCM mkoa  Njombe  wakishirikiana na makamu mwenyekiti wa CCM Taifa Phili Mangula ( wa pili kulia ) kuwaongoza  wanachama wapya wa CCM zaidi ya 600 waliojiunga na CCM jana wakati wa mapokezi ya makamu huyo  wa kwanza  kulia ni mbunge wa jimbo la Njombe kusini na spika  wa bunge Anne Makinda  wa tatu kutoka kulia ni mwenyekiti wa CCM mkoa wa Njombe Deo Sanga ambae ni mbunge wa jimbo la Njombe kasikazin na anayefuatia ni katibu wa CCM mkoa wa Njombe Hosea Mpangike

                                                Deo Filikunjombe miongoni mwa wananchi

                               Msafara wa pikipiki kwenye mapokezi ya Mangula Njombe

MBUNGE wa jimbo la Ludewa mkoani Njombe Deo Filikunjombe awakuna wapiga kura wa jimbo la Njombe Kaskazini Linaloongozwa na mbunge wake Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Njombe Deo Sanga Kwa kuwalipua watendaji wabovu serikalini ,mbele ya makamu mwenyekiti wa Chama cha mapinduzi ( CCM) Tanzania bara  Philip Mangula.

Filikunjombe ambea alipewa nafasi ya kusalimia katika mkutano huo mkubwa wa mapokezi ya Mangula mkoani Njombe alisema kuwa masikitiko ya wananchi juu ya serikali ya CCM yanatokana na baadhi ya viongozi wabovu ndani ya Chama na serikalini ambao wamekuwa wakifanya kazi chini ya kiwango na kupelekea wananchi kukichafua Chama tawala.

" Ndugu zangu wananchi wa Makambako na mkoa wa Njombe Chama chetu CCM ni Chama kizuri sana na safu hii ya sasa chini ya Rais Kikwete ,Kinana na Mangula ni safu ya uhakika na itakiwezesha Chama  chetu kuendelea kuaminiwa zaidi na watanzania ...ila tatizo ni viongozi wachache wa serikali wasiowajibika katika nafasi zao"kauli iliyowakuna wananchi na kushindwa kujizuia kushangilia huku wakiimba wewe ni Jembe .

Hata hivyo Filikunjombe alisema kuwa ili Chama kuendelea kupendwa na akina Mangula na Kinana wanapaswa kusaidiwa na watanzania wote kwa kuombewa zaidi ili kuendelea kuifanya kazi hiyo bila woga ndani ya chama.

Kwa Upande wake  Mangula mbali ya kusifu mapokezi makubwa ya kihistoria Katika mji wa Makambako na Njombe mkoani Njombe aliweza kutoa  ya Moyoni kuhusu Kati yake na Rais Jakaya Kikwete kwa Madai kuwa yeye alikuwa hajui chochote juu ya uteuzi wake na kuwa alisitaajabu kupokea simu ya Kikwete kuhusu kusudio la uteuzi wake.

" Kweli Mimi nilikwenda Dodoma katika mkutano mkuu wa CCM Kama mualikwa ila Nikiwa Hotelini nilipokea simu ya mwenyekiti wa CCM Taifa Rais Kikwete akiomba kuniteua kuwa makamu mwenyekiti na baada ya kwenda Ukumbini wajumbe wote walinipa kura zote za ndio...kweli namshukuru sana mwenyekiti wangu na wanachama wote na sasa ni kazi zaidi na sitawaangusha"


Hata hivyo aliwataka wana CCM kufanya vikao bila kuchota na kuwa wasizingizie kukosa ajenda kwani hata kukosa ajenda ndani ya CCM ni ajenda Kukosa agenda pia ni agenda ndani ya CCM pia yaweza kuwa ajenda.

Aidha amehimiza  nidhamu na taratibu ndani ya CCM kuendelea kuzingatiwa ili kukiwezesha Chama kuwa na amani na kuwa iwapo taratibu ndani ya  Chama hazitazingatiwa upo uwezekano wa Amani ndani ya nchi kutoweka.

Alisema kuwa haitapendeza kuona Tanzania inafika mahali inaendeshwa  bila Chama iwapo tutaruhusu wasiopenda Amani kuendelea kuvuruga Amani yetu iliyopo...

Picha na Said Ng'amilo wa Mjengwablog, habari na Francis Godwin

Pinda Ahimiza Mazao Mbadala Ya Biashara

WAZIRI MKUU Mizengo Pinda amewataka wakazi wa wilaya mpya ya Mlele mkoani Katavi walime mazao mbadala ya biashara kama alizeti, karanga na ufuta kwa sababu yanachukua muda mfupi na hivyo kuleta kipato cha haraka.

Ametoa wito huo juzi jioni (Ijumaa, Desemba 14, 2012), wakati akizungumza na wakazi wa kijiji cha Nsenkwa mara baada ya kuweka jiwe la msingi kwenye zahanati ya kijiji hicho akiwa katika siku ya pili ya ziara yake jimboni kwake Katavi wilayani Mlele, mkoani Katavi.

Waziri Mkuu aliwataka wakazi hao kuachana na mazoea ya kulima tumbaku kwa vile inachukua muda mrefu hadi kukomaa na inachangia uharibifu mkubwa wa mazingira kwani inahitaji kuni nyingi wakati wa kukausha.

“Tumbaku hivi sasa haina bei kwa sababu wanaopanga bei ni wakubwa huko nje… tuangalie mazao ya alizeti, ufuta na karanga kwa sababu yanatoa pesa kwa haraka zaidi. Mfano mzuri ni Singida ambao wamekuja juu kiuchumi kwa sababu ya zao la alizeti,” alisisitiza.

Aliwataka wakazi hao waangalie ufugaji nyuki kama fursa ya kipekee kwa sababu mkoa huo umejaliwa kuwa na misitu mingi na unaweza kuongeza kipato cha mkoa wao. “Asali ni dawa, asali ni chakula, asali ni biashara na ina soko hapa nchini hadi nje ya nchi.

Changamkieni fursa  hii, ongezeni uzalishaji wa asali na nta,” aliongeza.Aliwashauri pia waangalie uwezekano wa kulima miembe ya kisasa kwasababu inazaa kwa wingi na katika kipindi kifupi mno. “Hii miembe yenu inazaa maembe 10-20 kwa mwaka lakini ya kisasa inazaa hadi maembe 10,000, ikiwa chinichini tu,” alisema.

Kambi Ya Miss Utalii Kuanza

Huu ni ukumbi ambao utatumika kwa ajili ya Mazoezi   pamoja na shughuli mbalimbali.

Jumla ya warembo Sitini (60)  kutoka nchi nzima na vyuo vikuu  watakao shiriki fainali za Miss Utalii Tanzania 2012/2013 wanatarajia kuanza kambi Rasmi Tarehe 19.12.2012 katika hoteli ya kitalii ya Ikondolelo Lodge iliyopo kibamba Dar es salaam.

Wakiwa katika kambi hiyi ya siku ishirini na moja , warembo hao watashindana kuwania taji la taifa la Miss Utalii Tanzania , na tuzo mbalimbali za kijamii kitalii kitamaduni na kiuchumi. Zikiwemo tuzo za Mazingira, utaluii wa ndani, wanyama pori,hifadhi za Bahari, Mitindo, urembo, maziwa makuu, SADEC, Afrika Mashariki, umoja wa Afrika  Afya ya jamii, Jinsia wanawake na watoto, Rushwa, uwekezaji, Madawa ya kulevya, mazao ya biashara, madini , uchukuzi na Miundombinu mbalimbali ya utalii.

Washiriki pia watajifunza stadi mbalimbali za maiusha , Mbinu za utangazaji utalii na bidhaa mbalimbali za Tanzania, Pia mbinu za kjuhamasisha kampeni dhidi ya uharibufu wa mazingira, tanamaduni kongwe na potefu, kupenda kutumia huduma za Tanzania ( Madre in Tanzania), uvuvi haramu, amna uwindaji haramu.
Washindi wa fainali hizo za taifa watawakirisha fainali mbalimbali za kitaifa na kimataifa yakiwemo ya, Miss Tourism world, Miss Tourism HeritageWorld Miss Tourism University World, Miss Tourism Uniterd Nation,International Miss tourism World, Miss Global International.